Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,256
Kwa maoni yangu, yote sahihi mkuu... kazi iliyobaki ni ku-practice pahala pa kuyatumia tu hivi sasa... lol
John Mnyika said:Mosi, sipendezwi na neno upinzani maana lina maana nyingi na wengine hulichukulia tofauti. Mimi napenda zaidi kutumia vyama mbadala. Na wachache hutumia neno vyama vya ushindani. Jina lina mantiki sana katika kutanabahisha dhima. Wengine jina upinzani wanalichukulia ni kupinga tuuu!!!! Nitatumia neno mbadala.
JK afanya kweli
2008-08-09 14:52:15
Na Mwandishi Wetu, Songea
Tahadhari ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Jakaya Kikwete kuwa Serikali yake haitakuwa na msamaha kwa viongozi na watumishi watakaofanya ufisadi kwa kutumia pesa za umma kwa manufaa yao binafsi, imeanza kuliza vigogo baada ya vijana wa kazi kufanya kweli na kumsweka jela kigogo mmoja.
Hatua hiyo imekuja baada ya vijana wa JK kuvalia njuga sakata la kigogo huyo, hadi kupata ushahidi wa kutosha juu ya namna jamaa huyo alivyolamba mapesa ya umma.
Kigogo huyo aliyeswekwa jela ni Mhasibu wa Shule ya Sekondari Mbinga mkoani hapa aitwaye Omari Millanzi, 56.
Mapesa hayo yaliangukia mikononi mwa kigogo huyo baada ya kutumwa na ofisi ya Hazina ili yafanye kazi ya kuboresha elimu.
Hata hivyo kigogo huyo alizinyaka pesa hizo na kuzikandamizia kwenye mambo yake mwenyewe hadi aliposhtukiwa na kuburuzwa kortini.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Ruvuma, Baptist Mhelela ndiye aliyesikiliza kesi juu ya sakata hilo na baadaye kumuona Millanzi ana hatia katika makosa 60 aliyoshtakiwa.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mhelela alisema kuwa kwa kuzingatia ombi la Mwendesha Mashtaka aliyetaka adhabu kali itolewe kwa mshtakiwa, na kwa kuzingatia vilevile kuwa mshtakiwa amekutwa na hatia ya makosa hayo yote, mahakama imeamua kumfunga jela mshtakiwa huyo kwa miaka mitatu kwa kila kosa, katika mashtaka 30 ya awali, hivyo kutakiwa atumikie jela kwa miaka 90.
Aidha, Hakimu Mhelela akasema kwa makosa mengine 30, kila kosa litampasa mshtakiwa atumikie jela kwa miaka mitano, hivyo jumla kuwa miaka mingine 150.
Jumla kuu ya kipindi cha adhabu za mshtakiwa huyo kilipaswa kuwa miaka 240 jela.
Hata hivyo Hakimu Mhelela alisema kwakuwa adhabu zote zitatumikiwa kwa pamoja, mshtakiwa atakwenda jela miaka mitano.
Pia Hakimu huyo akaamuru mshtakiwa alipe kiasi chote cha pesa alizoiba kwa mwajiri wake ambazo ni Sh. Milioni 24.1, mara tu baada ya kumaliza adhabu yake ya kifungo.
Kabla ya hukumu hiyo, upande wa mashtaka ukioongozwa na Inspekta George Omary, ulidai kuwa katika kipindi cha mwezi Januari na Julai mwaka 1998, mshtakiwa Millanzi aligushi nyaraka mbalimbali za Serikali na kuiba pesa hizo, kaisi cha Sh. Milioni 24.1.
Alipotakiwa kujitetea, ndipo mshtakiwa Millanzi alipomlilia hakimu na kumtaka ampunguzie adhabu akidai kuwa ana umri mkubwa na kuwa vilevile, ana familia inayomtegemea.
Mara kwa mara, Rais Kikwete amekuwa akisisitiza juu ya nidhamu ya matumizi mazuri ya pesa za umma na kuonya kuwa yeyote atakayekiuka taratibu, atachukuliwa hatua kali za kisheria.
SOURCE: Alasiri
Hawa wanaostahili kuitwa vigogo watafungwa lini na miaka mingapi???
Nafikiri vyombo vya habari, hasa reporter huyu kaweka kichwa cha habari kikubwa kuliko habari yenyewe, sijui wenzangu mnaonaje??
...Labda akienda huko lupango atajifunza tabia njema.
You are mistaken doug unachoona ni Visitor messages!Unless na mimi nimechanganyikiwa!
Actually I have left a visitor message for you in your profile.Ila what I believe PM that is Private Message is strictly between the sender and receiver!
You are mistaken doug unachoona ni Visitor messages!Unless na mimi nimechanganyikiwa!
Actually I have left a visitor message for you in your profile.Ila what I believe PM that is Private Message is strictly between the sender and receiver!