KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

Undermine = -tekua, kwa mujibu wa kamusiProject

.

One of those words we don't use.Thanks for the education.

The Kamusi Project is really slow most of the time, and moving from host to host.
 
So ?

"The Kamusi Project is really slow," and it returns big Kiswahili words.

So what Pundit?

I was trying to find out from the Kamusi Project, and it did not let me.I was merely pointing out the technical difficulty associated with that charitable organization.This is an open discussion forum and one never know what sharing of a simple observation like that could bring.

Others could appreciate more the effort of our fellow who might have tried several times to get the meaning of the words.

Others could start an initiative to contribute towards the Kamusi Project (They accept donations you know)

Better yet, others could start another initiative towards a Swahili dictionary.

It was an open ended observation, totally unrelated to the narrow scope of the thread, on which I thanked the contributor from obtaining a rarely used word from the most authoritative source online.

If I may ask, what was the "So?" motivated by?
 
...hii thread members wengine mme-iundermine sana kwa kutoisoma mapema!!! :)

tafsiri ya: 'members should not undermine the efforts of the administration'

"wanachama wasidhoofishe ((kwa)makusudi) jitihada za uongozi"
 
sasa neno kudhoofisha ni sawa na kupunguza nguvu (to weaken). Mtu ambaye ni dhaifu (which is the root word ya neno dhoofu) inahusiana na hali ya kuchoka nguvu, kupungua nguvu n.k

Nilitaka tutumie lile neno "tekua" alilolisema memba hapo nyuma.
 
sasa neno kudhoofisha ni sawa na kupunguza nguvu (to weaken). Mtu ambaye ni dhaifu (which is the root word ya neno dhoofu) inahusiana na hali ya kuchoka nguvu, kupungua nguvu n.k

Nilitaka tutumie lile neno "tekua" alilolisema memba hapo nyuma.


Weaken ni katika synonyms za undermine. Tekua ni neno zuri lenye maana halisi ya undermine, ila nahofia hadhira yako kuweza kuling'amua mara moja. Kama unaandaa sheria ndogo ndogo tumia lugha rahisi iwezekanavyo.
 
"he was undermining her efforts to succeed" = Alikuwa anahafifisha jitihada/juhudi zake za kufanikiwa
 
mpaka sasa neno "komputer" ni msamiati sahihi wa kiswahili. ni neno ambalo limetoholewa/ kukopwa kutoka katika kiingereza kama maneno mengine kama vile shati-(shirt), trekta-(tractor). kutohoa au kukopa maneno kutoka lugha nyingine, ni jambo la kawaida na katika lugha zilizo nyingi duniani zimetumia njia hii kujiongezea msamiati wake.
 
Nitasaidia kama ninavyoweza kama ifuatavyo:
*Vukiza/Fukiza ni maneno yenye maana sawa,yaani kuweka kwenye mazingira ya moshi,iwe wa kuni au maVumba kwa nia ya kukausha kwa maana ya kuhifadhi au kufanya takatifu.
*Vundika au Vumbika:Haya ni maneno yenye maana sawa.Yaani kufanya ive au ioze:
*Compyuta:Hili sio neno la kiswahili,ila ni neno lililoazimwa kutoka kwenye kiingereza.
*Ingawa:Hili ni neno linalo halalisha udhuru.Kwa mfano,'ingawa sikwenda lakini mambo yatakwenda vizuri.'
*Msanii:Maana halisi ya msanii ni mstareheshaji,ingawa siku hizi msanii anaelezwa pia kama mtu asiye mkweli.
*Puchu:Hali ya kutokuwa na manyoya.
*Mkwara:kumkosoa mtu katika hali ya kukasirika.
*mwake:mazingira yanayomilikiwa na mtu husika.
Chuna:Toa ngozi.
Mbongo:Sina hakika sana ya neno hili,lakini nimesikia watu wengine wakilitumia wakimaanisha akili nyingi.

Fukiza ni kwa Moshi, Vukiza ni kwa Mvuke hivyo ukisema yana maana sawa si kweli ila yanakaribiana kimaana kwa kiasi.
Vundika ni neno mnyumbuliko wa Neno VUNDA
Vumbika linatokana na mnyumbulisho wa VUMBA/VUMBI
kwa hayo mengine sitofautiani sana nawe.
 
Shukrani kwa wote waliochangia katika kudadavua maneno yaliyoulizwa. Ningependa kuongeza tu kwamba Baraza la Kiswahili la Taifa (Tanzania) limeridhia kutohoa neno "Computer" na kuwa kiswahili bali linaandikwa kwa silabi za kiswahili yaani "Kompyuta".
 
Back
Top Bottom