Kisa cha Shariff Abdallah Attas na mwalimu Julius Nyerere ofisi ya TANU baada ya uhuru

Ngamiani hilo jina unalojinasibu nalo huna kun'yya nalo kabisa wenyewe wazaliwa wa ngamiani tumekaa kimya!!
 
Haiwezekani, lah uswahiba umekufa au haujali yanayojiri kwa swahiba
Platozoom,
Nimerejea tena.
Uzee una starehe zake na kunwa ni mbili unaweza sana kulala na kusema.
Katika minhaji hii hapo ''kusema,'' weka ''kuandika.''

Hebu nisome huku ukitembea katikakati ya mistari yangu na huku ukiwasikiza
wanasiasa wenyewe:
Mohamed Said: MHESHIMIWA KATANI AHMED KATANI (CUF) MBUNGE KIJANA WA TANDAHIMBA (UKURASA WA NYONGEZA)

MHESHIMIWA KATANI AHMED KATANI (CUF) MBUNGE KIJANA WA TANDAHIMBA (UKURASA WA NYONGEZA)

Inawezekana kabisa kuwa hata kwa mbali au hata kwa ndoto mbaya ya kutisha ya jinamizi Mh. Ahmed Katani alipatapo kufikiri kuwa itatokea siku yeye atasoma tamko la uamuzi wa kumfukuza Prof. Ibrahim Haruna Lipumba kutoka CUF. Kama wasemavyo wanasiasa wenyewe, siku ni muda mrefu sana katika siasa. Mwandishi alikutana na Mh. Katani siku chache zilizopita alipofika nyumbani kwake akiongozana na Mh. Riziki Shahari Mbubge wa Mafia Viti Maalum wakitokea Bungeni Dodoma. Mazungumzo aliyofanya na Mwandishi kwa muda mfupi kama ungewasikiliza utadhani wawili hawa walikuwa wanajuana kwa muda mrefu. Msomaji anaweza kusoma utangulizi hapo chini wa ukurasa ambao Mwandishi aliandika kama ufunguzi wa matumaini kuwa iko siku Mh. Katani atakuja na historia ya maisha yake katika siasa za upinzani. Mh. Katani Ahmed Katani tayari keshaingia katika jedwali la historia kwa kusoma tamko la kumfukuza Prof. Lipumba kutoka CUF.

Hivi yawezekana kwa Prof. Lipumba kumtazama usoni kijana wake Mh. Katani na akasema maneno aliyosema Julius Caesar, ''Et tu Brute?''

Msikikilize Mh. Katani hapo chini:


Utangulizi
Mheshimiwa Katani Mbunge wa Tandahimba ni kijana kwa maana halisi ya neno lenyewe. Katika muda mfupi wa kuzungumza nae kwa mara ya kwanza akisubiri kikombe cha kahawa alipopita nyumbani kwa Mwandishi, Mwandishi amegundua kuwa Mh. Katani amekalia kitabu ambacho ikiwa atakiandika kinatosha kuwa rejea ya kueleza adha za siasa za upinzani khasa wakati wa uchaguzi mkuu. Ukurasa huu umefunguliwa rasmi kumsubiri Mh. Katani afunguke kwa faida ya wapenda demokrasia...

bjQYGjSVTSTkfcINPXQ_FUEcj6-3CDKAijIcP7V18Fp5lWLxAuRlH5isb0TeCKF7XqK_QngqR3NiNINM7BWrZhVIN3g4o4z4EOxgGKyOfkoNKKnyay6Kqj1I0dHu7R-glM63J-HIvQw_xHhJftvfI4kP9pZim0YgpbPtpxIpyIjOFjLSQ9xwIuNyN9winiHDaNY4tkknn-qzaBT25XzuAdfzkSew03OPHOzg-1Xjhk0mxizj9izWvclfndx9xG1rZ_LeD3iFamnkxMbbGu2HwQhfCHbm7ne8u9JOPcTBS3-d_EAmA3chMLkqJxJU2AuwU-fW6OKihWfABx7hejwW4je-iK2K2oYxco7wNMNYDBFd2AtByg08FwZPTOU5JDzPhnqyxT01r1vDnVI8SaqvQlklE-hknw3efBGg3ZmAoSvHWuw1jvlySNhO4GdJD4g8zgyjjUK5YDZ6nh8aeUxgG1xXSVk4d4VYrqGeWy_pbIaQLtWjgkcNQQG4YfYEMnkvLIQJyssdc-pwubTKTaZV7U4pc0YlD8nbABnF7HJO7ZBIIIxWJ2doU-VPPOjTR3kBqwAWvwAvzC6DyJ98fOiqwiB4hYY7uSxVQcCPVMw_GI7mJAhk0A=w876-h657-no

Mheshimiwa Katani Mbunge wa Tandahimba
 
Bukyanagandi,
Mzee Chihota
alikuwa Meneja wa Arnatouglo Hall nadhani alipotoka yeye
ndiye akaja Denis Phombeah, Mnyasa.

Mzee Chihota alikwenda masomoni Uingereza na huko mauti yakamfika na
alizikwa huko huko.

Hii ilikuwa miaka ya mwanzoni 1950s.
Kuna mtaa Temeke unaitwa, ''Chihota,'' kwa heshima yake.

Kulikuwa na Norman Chihota bingwa wa 100 metres na Raymond kaka
yake.

Hawa walitoka Rhodesia.

Gershom Chihota nilisomanae St. Joseph's School na tukicheza mpira sote
na kupiga muziki yeye akipiga bass guitar.

Baada ya uhuru kupatikana walirudi kwao na huko Raymond alifariki.
Huyu alisoma Urusi na alioa Mrusi.

Raymond alipomaliza shule Aga Khan alifanyakazi TBC kama mtangazaji na
allikuwa na kipindi, ''Teenagers Time,'' akipiga pop music akina Cliff Richard,
Helen Shapiro, Elvis Presly, Beatles, Rolling Stones etc.

Ray kama alivyokuwa akijulikana alikuwa mmoja wa ''Chipukizi,'' na akina Henin
Seif, Abdul Nanji, Badrin,
Salum Hirizi, Yusuf Ramia, Hussein Shebe, Cuthbert Sabuni,
Sauda Mohamed, Maryam Zialor
na vijana wengi wa Dar es Salaam.

Salim Hirizi akijulikana kama Sammy Davis.

Ray alikuwa mwimbaji mzuri wa nyimbo za Kizungu na Chipukizi na yeye kwa
msaada wa David Wakati wakaanzisha kipindi RTD, ''Chipukizi Club.''

w4vW4gv7SxJyr6Q7ucMTdZj6fP0N48FfKXc9DSgzcMeq-xPH3XvE0BsfKT_FciVts0m9gwjqliWGSqU=w1280-h800-no

Kulia Raymond Chihota, Henin Seif, Hussein Shebe
Nyuma ya Hussein Shebe Mbaraka Bata, Nyuma ya Henin Seif Hussein


Kipindi hiki kilipendwa sana na vijana hadi pale kilipokuja kupigwa marufuku na
Regiional Commissioner wa Dar es Salaam, Mustafa Songambele kwa sabau ati
kinatukuza utamaduni wa nje.

Songambele hakupendezewa na zile nyimbo za Kizungu bendi ile ya Chipukizi
walizokuwa wakipiga.

Chipukizi walikuwa wakipiga pamoja na vijana wa Kigoa wakijiita ''The Blue Diamonds.''
Walikuwa na wapiga magitaa hodari sana.

Hii ilikuwa 1963/64.

Ray
na Yusuf Baruti wakaenda kusoma Urusi na ''members,'' wengi wa Chipukizi wakaondoka kwenda
nje.

Hussein Shebe akaenda Nairobi kujiunga na Ashantis kama muimbaji na kwa kweli
aliipaisha ile bendi na hawakukaa sana Nairobi wakenda Addis Ababa wakawa
wanapiga Wabe Shebelle Hotel, hotel kubwa sana wakati ule.

Sal Davis ndiye aliyemchukua Hussein kumpeleka Nairobi.

Sal alikuja Dar es Salaam na alifanya show moja na Chipukizi Radio Tanzania na hapo
ndipo alipomsikia Hussein akiimba.

Badrin na Nanji wao walikwenda America.

Sabuni na bendi yake, ''The Flaming Stars,'' akiwa na Peter Kondowe (Peco) na
George Mzinga wao wakaenda Mombasa.

Miaka mingi baadae nilifika Addis Ababa na nilikaa Wabe Shebelle lakini hoteli ilikuwa
taaban, imechoka.

Nakumbuka nililetewa Coke lakini sikuweza kuitambua chupa jinsi ilivyokuwa imesagika.

Hii ilikuwa 1989 enzi ya Mengitsu Haile Mariam na Hussein Shebe na Ashanti
wamekimbia wanapiga muziki wao Italy.

Nakumbuka Ray aliporudi alikaribishwa Radio Tanzania English Service kwa mahojiano
katika kipindi cha muziki.

katika nyimbo alizochagua apigiwe moja naikumbuka kwa kuwa nami nikiipenda,
''Let The Good Times Roll,'' ya Ray Charles.

Mwaka wa 1993 nilikwenda Harare na nilimtafuta Gershom na Norman na bahati
nzuri nilikutananao.

Nina picha nikizipata nitaziweka hapa In Shaallah.

Baada ya miaka mingi sana nilikutana na Hussein Shebe kwenye boat tunakuja Dar es
Salaam kutoka Zanzibar nilikuwa na rafiki yangu Tamim Faraj.

Tulikumbusha mengi na akanipa cassette yake na Ashanti.

Hivi sasa Hussein amepumzika muziki na akiwa na nafasi hupita nyumbani kwangu
kunijulia hali kila anapokuja kutoka Zurich anakoishi na mkewe Mswiss na wanae na kila
siku ananikaribisha Switzerland.

Ingia You Tube ustaladhi na muziki wa Hussein Shebe.

Katika mahojiano nliyofanya na Hussein ananambia kuwa siku alipomwabia Meneja wake
kuwa yeye muziki basi alishtuka na akambembeleza sana.

Hussein hajatazama nyuma.
Mke wake anasema, ''Huyu Hussein toka amerudi kwenye Uislam wake...''

Siku moja nafanya mahojiano na Hussein.
Ghafla ananyanyuka ananambia, ''Mohamed Maghrib sasa tuswali kwanza...''

Machozi yalinilengalenga...
Tulikuwa nyumbani kwa rafiki yake toka udogo wao - Henin Seif.

Kakutana na mke wangu msikitini Maamur anamwambia, ''Mohamed si rafiki
yangu ni ndugu yangu...''

Ingia hapo chini kuangalia picha:
Mohamed Said: KUTOKA JF: CHIPUKIZI CLUB WATOTO WA MJINI DAR ES SALAAM 1964

Dah, hao waliotajwa na hao kwenye picha nawaona hivi machozi. Maalim ulipomtaja Bi Mariam Zialor na Sauda nikahisi utamtaja na Bi Eshe Sururu.

Nnazikumbuka kumbuka enzi za Mariam na Hussein Shebe.
 
Ahlaan Wasaalan Maalim Faiza...
Kumekucha.

Huu ukimya wako naamini Wanabarza wengi tulikuwa tunajiuliza kulikoni?
Majlis ilipooza.

Asalaam Alaikum.

AlhamduliLlah nipo Alama, ni majukumu ya hapa na pale na hii holiday season iliyopita nilirundikiwa wajukuu wote basi ikawa hata muda wa kuchangia humu sina, si unajuwa hawa wanetu siku hizi wakikuwachia watoto zao wanakupa na time table, aah sisi wao tuliwalea kwa time table za kichwani. Na kama hukufata time table waliokuachia basi una kesi ya kujibu.

Nakusoma Maalim, umenitajia kaka na Dada zangu wa karibu kabisa. Akina Hennin, Hussein, Chico, na Da Mariam. Bila kumsahau Salum Hiriz. Aah nilitamani nimsome na Ali Bobo, Abdallah Awadh, Abby Sykes, Salmin Tamim, Marehem Ali Ghafur (mabichwa).

Aah, ni mambo adhyim na Adim hayo.

Juu huko nimemsoma Mzee Tuli, jee huyo ni baba yake Dr. Mohamed Tuli?
 
Asalaam Alaikum.

AlhamduliLlah nipo Alama, ni majukumu ya hapa na pale na hii holiday season iliyopita nilirundikiwa wajukuu wote basi ikawa hata muda wa kuchangia humu sina, si unajuwa hawa wanetu siku hizi wakikuwachia watoto zao wanakupa na time table, aah sisi wao tuliwalea kwa time table za kichwani. Na kama hukufata time table waliokuachia basi una kesi ya kujibu.

Nakusoma Maalim, umenitajia kaka na Dada zangu wa karibu kabisa. Akina Hennin, Hussein, Chico, na Da Mariam. Bila kumsahau Salum Hiriz. Aah nilitamani nimsome na Ali Bobo, Abdallah Awadh, Abby Sykes, Salmin Tamim, Marehem Ali Ghafur (mabichwa).

Aah, ni mambo adhyim na Adim hayo.

Juu huko nimemsoma Mzee Tuli, jee huyo ni baba yake Dr. Mohamed Tuli?
Maalim Faiza,
Nimefurahi sana kukusikia.
Allah atukuzie wajukuu zetu.

Amin.
Hakika najua jukumu ulilonalo.

Katika hao wajukuu unao waume zako na mawifi na najua hutaki kujiharibia kwa hawa
waume kwani ni ghali na adimu hivi sasa hapa mjini wanasakwa kwa udi na uvumba.

Ukiwafurahisha mawifi na kaka zao wanafurahi, ''and they will be looking forward to go
to their heartthrob next holiday.''

Wajukuu ni watamu kuliko watoto kiasi unataka Allah angetupa kwanza wajukuu kisha
wafuatie wana.

Ali Bob na Abdallah Awadh watu muhimu sana katika mji wa Dar es Salaam na wataacha
historia nzuri In Shaallah.

Watu waungwana, wastaarabu.
Kila shughuli wao hutaka kuwatumikia watu tu, kuwaandalia chakula na nini.

Siku moja nilimuuliza Ali Bob, ''Kaka iweje wewe na Abdallah Awadh siku zote nyie ni
waandazi?''

Ali Bob
akanijibu kuwa wakati mwingine wao hualikwa shughuli kama watu wengine lakini
wanachelea shughuli kuharibika ndipo husimama kuandalia.

Akaongeza na kusema wao wanawajua watu wengi wa Dar es Salaam na anapompokea mtu
anajua amkalishe na nani.

Anawajua kuwa nani hali nyama, nani hali pilau kwa hiyo anawatengea jamvi lao maalum na
hivyo taklif huondoka.

Nami umenipeleka mbali.
Siku hizi shughuli hatuli tena katika sinia tumekizunguka chakula kama ilivyo ada.

''Catering is taking over.''
Kila mtu na kisahani chake mkonini, ''already packed.''

Maalim Faiza huu ni msiba.

Nakutakeni radhi Wanabarza huenda wengine wasielewe lakini hii ndiyo ilikuwa Dar es Salaam
tuliolelewa sisi miaka hiyo.

Dr. Tulli ni mtoto wa Madhehebi Tulli.
 
Maalim Faiza,
Nimefurahi sana kukusikia.
Allah atukuzie wajukuu zetu.

Amin.
Hakika najua jukumu ulilonalo.

Katika hao wajukuu unao waume zako na mawifi na najua hutaki kujiharibia kwa hawa
waume kwani ni ghali na adimu hivi sasa hapa mjini wanasakwa kwa udi na uvumba.

Ukiwafurahisha mawifi na kaka zao wanafurahi, ''and they will be looking forward to go
to their heartthrob next holiday.''

Wajukuu ni watamu kuliko watoto kiasi unataka Allah angetupa kwanza wajukuu kisha
wafuatie wana.

Ali Bob na Abdallah Awadh watu muhimu sana katika mji wa Dar es Salaam na wataacha
historia nzuri In Shaallah.

Watu waungwana, wastaarabu.
Kila shughuli wao hutaka kuwatumikia watu tu, kuwaandalia chakula na nini.

Siku moja nilimuuliza Ali Bob, ''Kaka iweje wewe na Abdallah Awadh siku zote nyie ni
waandazi?''

Ali Bob
akanijibu kuwa wakati mwingine wao hualikwa shughuli kama watu wengine lakini
wanachelea shughuli kuharibika ndipo husimama kuandalia.

Akaongeza na kusema wao wanawajua watu wengi wa Dar es Salaam na anapompokea mtu
anajua amkalishe na nani.

Anawajua kuwa nani hali nyama, nani hali pilau kwa hiyo anawatengea jamvi lao maalum na
hivyo taklif huondoka.

Nami umenipeleka mbali.
Siku hizi shughuli hatuli tena katika sinia tumekizunguka chakula kama ilivyo ada.

''Catering is taking over.''
Kila mtu na kisahani chake mkonini, ''already packed.''

Maalim Faiza huu ni msiba.

Nakutakeni radhi Wanabarza huenda wengine wasielewe lakini hii ndiyo ilikuwa Dar es Salaam
tuliolelewa sisi miaka hiyo.

sasa kwa porojo kama hizi kweli tutafikia nchi ya viwanda????
"et na wewe msomi na hivi ndo vitu unavyojinasibu navyo"

wewe ni mwandishi 'mwanasesere'
 
sasa kwa porojo kama hizi kweli tutafikia nchi ya viwanda????
"et na wewe msomi na hivi ndo vitu unavyojinasibu navyo"

wewe ni mwandishi 'mwanasesere'

"Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba".

Nnauhakika hujaelewa kinachoongelewa. Hayo ya Dar za enzi hizo tuwachie sisi, Alama Mohamed Said kishawaomba radhi wana jamvi.

Jee, umewahi kumsikia Mshume Kiyate?
 
sasa kwa porojo kama hizi kweli tutafikia nchi ya viwanda????
"et na wewe msomi na hivi ndo vitu unavyojinasibu navyo"

wewe ni mwandishi 'mwanasesere'
Mtanganyika...
Ndugu yangu mimi si lolote wala si chochote kaka.
Sina moja nilijualo mie kwa hiyo unistahamilie tu ndugu yangu.

Mwanasesere mbona ana afueni?
Mimi ni Karagosi.

Huyu Karagosi ni mwanasesere zuzu tukimwangalia vituko
vyake pale Mnazi Mmoja siku za Eid.

Aliyekuwa akimcheza (puppet on a string) alikuwa mtu mmoja
anaitwa Juma Mlevi lakini jina lake khasa ni Juma Sulemani.

Huyu Juma Mlevi alikuwa katika TANU mstari wa mbele katika
vijana na alihudhuria Mkutano wa Kura Tatu Tabora, 1958.

Sasa mimi ni mbumbu na Waarabu wana msemo, ''Sababu huondoa
ajabu.''

Ukishakubali kuwa mimi ni mbumbu utakuwa huna tena sababu ya
kuja hapa barazani kunitukana maana tayari mimi ni maadhura.

Maana yake nishasamehewa kwa kuwa punguani.
Kama kweli nilitegemewa mimi kuendeleza viwanda....
 
Mkuu Mohammed Said kwa maoni yangu ulitakiwa uwe part time lecture for African/East African history hususan kwenye hizi East African colleges and universities
Waonekana una hazina kubwa sana kwenye historia Ya nchi hii. Kutokushare hiyo rich history uliokuwa nayo Ni kutotutendea haki sote wenye kiu Ya kutaka kufahamu na kujifunza historia Ya nchi hii
Ni ombi langu binafsi tu
 
wacha kuleta ngonjera zako;suala liko palepale kwa uandishi huu kweli tutafika nchi ya viwanda????
kila ukija habar za vijiwe vya kahawa ooohh mara fulani kafanyaje,
hizo hadithi unajaza server bure,

maandiko yako lazima yawe na mchango kwa taifa sio utengano unaoleta kwa kujivika udini!
Mtanganyika...

Hapana mimi sijapata kulalamikiwa ''udini,'' na wasomi wakubwa waliofanya
''review,'' ya kitabu changu cha Abdul Sykes na paper nyingine nilizowasilisha
katika vyuo kadhaa Afrika, Ulaya na Marekani ila hapa JF na watu mfano
wako.

Lakini kila ninapoomba ushahidi wa hilo wanashindwa kutoa na wengine kama
wewe huishia matusi.

Yawezekana ndugu yangu unahangaishwa na wivu na hasad na haya ni maradhi
mabaya ya nafsi na husababisha kensa mwilini madaktari wamethibitisha hili.

Hapa JF kuna wengi wanapenda kunisoma.

Ama hilo la ''porojo'' Allah hakunijalia kipaji hicho na ndiyo maana nimeweza
kuchapwa na Oxford University Press (East Africa) na New York.

Ndiyo maana pia kitabu changu kilipotoka 1998 mabingwa wa African History
John Iliffe na Jonathon Glassman wakanifanyia ''review,'' katika Cambridge
Journal of African History.

Ndiyo maana naalikwa kwingi ndani na nje ya nchi kuhadhiri.

Huu ndiyo mchango wangu kwa taifa hili kwa kuihifadhi historia ambayo tayari
ilikuwa imeshapotea.

Hapo chini niko VOA Washington wamenialika kwa mahojiano waliposikia nipo
mjini.

JqBQlGOMIgS3lqD9NQFj5UnBSQEiO3nzVyuHVhHbhCD2R2OLw7LrXZgGfi0bSlbTYY8Juo8Y1B27MxVgh4rN80phy_aLOpLCzvG6cbf7Bd5B6sky8ZrGiJlqYI5ehYv6h6K9mNZAj5pwRwDVS2Nzc8FJTfWXb5X_A0FpnNu8xPczst0Kfs3U8YVdGwvBisrYZN8JHoraMlBUir2eAmAXRwIggn4XUtopWbETMbr_Pk4BhJq2cgMntgM8DRcfyKIGFc4g3QLaFv23NvlmtcWFD3quKW8IheqzLUVzmP45mzmVDzsWkxybWetgjBf8x29dMCEsBNR6a-Yp2doivaL6nJW_-feWejrnpHFbi4VhRW3ldNGenXnFnmtaJD6W9gi0zG3G3rFetvHAfpw17VoGWf1s_4XC0OZVocT6iJNZPYhFrGu3Fu3NtMbCN4hhmyQpogauwVXZwR6fI-cgpUYkkBKPdJ1IzmyXrMe3zJmnMe3Z1mrt9HlaocZMBiXS-E4lS7mGfjzRSIxgeaK7zZj4DggKN7x_sHNoZaCa_i5rdHeHPkFAiLwzMLvP1IjSA5bP6JIeAdPu7fJ6mglpW_5MhUd5U1DnfEUq25WGmjM4uJJkAmN8=w571-h657-no
 
Mkuu Mohammed Said kwa maoni yangu ulitakiwa uwe part time lecture for African/East African history hususan kwenye hizi East African colleges and universities
Waonekana una hazina kubwa sana kwenye historia Ya nchi hii. Kutokushare hiyo rich history uliokuwa nayo Ni kutotutendea haki sote wenye kiu Ya kutaka kufahamu na kujifunza historia Ya nchi hii
Ni ombi langu binafsi tu
Sheriff,
Ahsante kwa kuniwazia makubwa.
Nimejitahidi kuandika mengi ninayoyajua.
 
Obviously yote uyajuayo hujayamaliza yote na I have a feeling that unayo Mengi sana ambayo hayajachapishwa wala kuelezwa
Tafadhali funguka
Sheriff...
Ni kweli huwezi kuandika yote.

Inawezekana ninayo mengi ambayo sijasema kwa sababu hii au ile au
kwa sababu ya kusema haipo.

In Shaallah tusibiri ikitokea fursa nitazungumza.
 
Jackline,
Hilo ulosema ni kweli kabisa mchango wa Nyerere ulikuwa mkubwa sana.

Yeye ndiye aliyepanda jukwaani na kwa kinywa kipana kuwaambia watu
tudai nchi yetu.

Kabla yake moto wa uhuru ulikuwa ukiwaka chini kwa chini.

Kwenye kitabu cha Abdul Sykes nimesema mambo yalikwenda kwa kasi
ya ajabu baada ya TANU kuundwa na Nyerere akiwa kiongozi wake.

Hakuna mtu atakaeweza kupuuza mchango wa Mwalimu hata kidogo.
Lakini sasa kuna kitu muhimu sana katika juhudi hizi za Mwalimu Nyerere.

Nyerere hakufanya haya peke yake na asingefanikiwa kama asingeungwa
mkono na viongozi wenzake katika TANU.

Kulikuwa na Baraza la Wazee wa TANU chini ya uenyekiti wa Sheikh Suleiman
Takadir
akifahamika kwa jina lake la siasa ''Makarios.''

Hili Baraza ndilo lilompeleka Mwalimu Nyerere UNO.

Nitakuwekea ''link'' hapa usome historia nzima ya safari hii na mchango wa Iddi
Faiz Mafungo
katika kukusanya fedha za safari.

Hii safari ya UNO ndiyo iliyomdhihirishia Nyerere kuwa ana watu wa kuaminika
na ndiyo iliyomfanya asiwe na wasiwasi wa kuacha kazi ya ualimu.

Lakini kubwa kulikuwa na ngome ya Kanisa Southern Province ambayo ilikuwa
ikiwatisha watu kujiunga na TANU wakiwaambia hizi ni fitna za Waislam wanataka
kuitumbikiza Tanganyika kwenye vita na Waingereza kama walivyofanya kwa
Wajerumani katika Maji Maji.

44221_471855816182358_1465711726_n.jpg

Askari wa Maji Maji baada ya kushindwa vita

Hii ilikuwa bugdha kwa chama kwani wengi walitishika.

Nitakuwekea link In Shaallah uwasome Yusuf Chembera, Salum Mpunga,
Suleiman
Mnonji
na Sheikh Yusuf Badi juhudi gani walifanya kuwaunganisha wananchi
kuwa kitu kimoja kumkabili Mwingereza.

Hii ilikuwa 1956 baada ya safari ya UNO.

Hii ni mifano michache katika mingi ya wazalendo waliopigania uhuru wa
Tanganyika ambao sijui kwa sababu gani hadi leo hawajaenziwa.

Tatizo ni pale historia ya mashujaa hawa ilopofutwa likabakishwa jina la
Nyerere peke yake.

8lS-bGcfJLi-US4KM0clKL332ZwGi0MysIEH5ffaAkw=w680-h510-no

Wa Kwanza Kushoto ni Idd Faiz Mafongo Mwekahazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi
Tanganyika na Mwekahazina wa TANU. Wanaofuatia ni: Sheikh Mohamed Ramiya wa Bagamoyo,
Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu Picha Hii Ilipigwa
Dodoma Railway Station Mwaka 1956 Wakati wa Kueneza TANU Katika Majimbo

Mohamed Said: Idd Faiz Mafongo Mweka Hazina wa Safari ya Nyerere UNO 1955

Mohamed Said: TANU Ilivyovunja Ngome ya Kanisa Katoliki Jimbo la Kusini, 1955 Sehemu ya Sita
Mohamed, unakosea unaposema historia ya hao wazee ilifutwa. Labda mchango wao ulipuuzwa lakini historia yao haikufutwa. Huwezi kufuta historia. Haiwezekani.
 
Mzee Said kuna watu wengi ktk TAA ambao nimewasoma kwa mara kwanza ktk bandiko lako.

Kitabu chako hicho kinaitwaje na kinapatikana wapi? Nadhani nikikipata nitaongeza elimu na ufahamu wangu kuhysu historia ya Tanganyika.


Vv
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom