Kisa cha Shariff Abdallah Attas na mwalimu Julius Nyerere ofisi ya TANU baada ya uhuru

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,912
30,253
er3bQjXjUA-gIjirvYPZ7req0Qq9Vy1t9K3kKNqRFoltAKW2HjRaPgHuGfv7enUhi6x4K7Xj5GSVjw2IZb2hYfKanrQQmgaeG5-2ABlbQohvXjPYctrAhbvqMdKRO9kp0MLlAt5vt7zFKZal73DKMUpZEILcLU_6ANrk8kQaOdROeypele2WR7vaXsOhM1iXfSCdqKiJGdVIpUXf73td0aPDHkPQPIG6oNyhxXDYIuBOJkQ_iVlNTMUbIAXPFD9QDHaJez37AjexF3uwb4MWXblYp_C0q5aKQyid3Qo8UA4kNfDrdwgRNA92bCS08qSFgLmNZ5oluK8H66I1Y4sEeajSaW0EgSyUNfcrURvEfpb2cxOygCbl5GQvf_YAiVfb6hY6Vnv59m4TVVkJupd4l_M4kL99Hur8fH0pea2fEbTTtCeTnSK_Nrg8RkvfMYmMoSqIcqTZ4CAQMv8IDCv2NTwg_YVHi827JxcUuTmQtPwcFXYCtU_OPID59dP4zIwiKyhc307YfgRy3X9pvyHMt7z6ebwsgMefyJpLIMictYmeCo12RWtCMWmYLd0Ew6YqePFyFniOi8GH_gMKLve-kLioOq3CGv2hGbK54EOlPdehcZaa=w493-h657-no

Shariff Abdalla Attas
(Picha kwa hisani ya Bwana Shomari)

Sie wengine tumekuja kumjua Shariff Abdallah Attas katika utu uzima wake akikaa Mtaa wa Twiga na Sikukuu nyumba yake mkabala na Msikiti wa Shadhili Dar es Salaam.Katika miaka ya 1950 Shariff Attas alikuwa akifanyakazi Soko la Karikaoo kama dalali wa soko. Market Master akiwa Abdulwahid Sykes. Sifa kubwa ya Shariff Attas ni ubingwa wake katika hesabu. Yeye alikuwa na uwezo wa kukokotoa hesabu ndefu kichwani bila ya kutumia ‘’calculator.’’

Kisa chake hiki ninachokieleza nimekisikia kwa masikio yangu mwenyewe miaka kadhaa nyuma takriban zaidi ya 25 hivi sasa..

Ilikuwa siku ya Eid El Fitr mimi na Kleist, mtoto wa Abdul Sykes tumekwenda kusali Eid Msikiti wa Kitumbini. Kleist ana uhusiano mkubwa sana na msikiti huu kwani hapo katika miaka ya 1930 babu yake alikuwa akienda kuswali hapo huku kafatana wa wanae Abdul, Ali na Abbas.

Habari hii kanihadithia Ali Mwinyi Tambwe. Mzee Ali Mwinyi alikuwa kaniita nyumbani kwake Kinondoni Block 41 ili asahihishe baadhi ya mambo ambayo alikuwa kasoma katika mswada wa kitabu cha Abdul Sykes, mswada ambao mwane mmoja Abdulrahman Mbamba alikuwa kamwonyesha. Kabla ya kuanza mazungumzo yetu akanambia, ‘’Mimi Abdul hanipati kabisa mimi nikimuona akija kuswali na baba yake pale Kitumbini mtoto mdogo kashikwa mkono. Si huu msikiti unaouna hii leo, msikiti ule wa zamani.’’

Msikiti huu ndipo baba yake Kleist, Abdulwahid Sykes alipofanyiwa sala ya jeneza kabla hajakwenda kuzikwa Mkaburi ya Kisutu. Kwa hiyo sikushangaa Kleist aliponiambia tukasali Eid Kitumbini. Nakumbuka wakati ule Kleist alikuwa na Mercedes Benz nyekundu, gari ya kupendeza sana. Nami nikawa sishi kumtia tashtiti kuwa kafuata nyayo za baba yake kwa kuwa baba yake amekufa gari yake ikiwa Mercedes Benz. Nikimpiga vijembe hivi yeye kazi ilikuwa kucheka tu.

Baada ya kumaliza kuswali na kupeana mikono na wazee wetu…Kleist hapo yeye ndipo alikuwa anakutana na rafiki wa marehemu baba yake na sasa ni watu wazima sana yeye akawa kila akitoa mkono anaufumba anamwachia kitu mzee wake. Tulipomaliza akanambia, ‘’Mohamed sasa twende kwa Shariff Attas.’’ Tulipofika kwa Shariff Attas tukakuta veranda yake imejaa ‘’who’s who’’ katika wazee maarufu wa Dar es Salaam, mmoja wapo marehemu Bwana Hamida Tuli, muungwana wa Kizaramo kutoka Masaki. Bwana Tuli akiishi Mtaa wa Matumbi hapo jirani. Mikeka ya rangi nzuri nzuri imetandikwa na udi unatoa riha nzuri, sinia zimejaa maakuli - kaimati, maandazi, visheti, vitumbua, tambi, katlesi, kababu, sambusa nk. Tumewakuta wazee wetu wanafuturu. Shariff kumuona Kleist kafurahi sana kupita kiasi anamwashiria aje akae ubavuni kwake. Mara tumeletewa sahani na vikombe tunakaribishwa chai.

Mara Bwana Hamida Tuli kasimama anaomba ruksa kwa niaba ya wenzake anasema, ‘’Shariff tunaomba ruksa tuondoke kwa kuwa tumealikwa chai Ikulu kwa Rais Ali Hassan Mwinyi.’’

Basi ikapigwa fatha ikaombwa dua wazee wakapeana mikono na Shariff Attas hao wakatimka kwenda Ikulu kunywa chai na rais. Ukumbi ukabaki mtupu tuko sie watatu tu - Shariff Attas, Klesit na mimi. Kleist akaangua kicheko kile cha kejeli. Shariff Attas yeye ni babu yake anamtania na kumuogelea atakavyo. Hizi ndizo mila zetu watu wa pwani.

‘’Duu, Shariff wenzako wote wanaalikwa Ikulu kwa rais, wewe uko hapa huna akujuaye!’’ Kleist anaangua kicheko. Shariff Attas hakuwa mdogo hivyo ni mtu maarufu kwa watu maarufu wa mjini na wenye majina ya kutajika.

Shariff Attas yuko kimya kaagemea ukuta anamtazama kwa jicho la deko hasemi kitu. Kleist kamaliza kumcheka Shariff. Mkono unakwenda kwenye sambusa, kababu, kaimati.

‘’Kleist sikiza bwana. Mimi kama kuingia Ikulu ningeliingia enzi za Nyerere yeye ndiye alikuwa mwenzangu. Mimi Mwinyi atanijulia wapi?’’ Shariff Attas akaanza.

Mimi masikio yangu yashakuwa walu namtazama Shariff usoni. Picha ninayoiona siyo ile ya dakika mbili zilizopita. Namuona Shariff ghafla amebadilika anaacha maskhara anataka kusema jambo.

‘’Sikiza Kleist, hiyo ni 1954/55 Nyerere anakaa kwa baba yako pale Stanley ndiyo TANU inakuja juu. Nyerere kesha acha ualimu. Anakuja ofisini kwa baba yako pale Kariakoo Market. Ikifika mchana Abdul ananiita ananiambia nifatane na Nyerere nyumbani kwa ajili ya chakula cha mchana. Mimi na Nyerere mguu kwa mguu, tunaingia Swahili, Narung’ombe, Gogo, Mchikichi, Sikukuu hadi Stanley kwa mama yako Mama Daisy. Njia nzima mimi na Nyerere tunazungunza. Wakati ule hakuna anaemjua. Tunafika nyumbani kwa baba yako chakula kipo mezani tunakula tukimaliza tunarudi ofisini pale kwa baba yako pale sokoni. Yeye alikuwa hatoki anaendelea na kazi. Nyerere alikuwa mwenzangu na mzungumzaji wangu sana wakati ule.

Basi miaka ikenda hadi tukapata uhuru na Nyerere akawa Waziri Mkuu.

Siku hiyo mimi niko ofisi ya TANU ghafla Nyerere anaingia watu hamkani wamesimama na Nyerere anaanza kupeana mikono na watu walioko pale hadi akafika kwangu nami nikampa mkono. Nyerere akanitazama nami nikamtazama tukawa sote tunatazamana usoni. Nyerere akasema,‘’Mzee tumepata kukutana?’’ Mimi nikamjibu, ‘’Hapana hatufahamiani.’’

Basi akapita kusalimiana na watu wengine. Sasa Kleist mimi ilikuwa niingie Ikulu enzi za Nyerere rafiki yangu lakini bahati mbaya kanisahau.’’

Shariff Attas alikuwa mtu wa tasnifa sana.

Akajinyoosha kaegemea ukuta anamtazama Kleist kwa mtazamo wa jicho la pembeni huku uso umejaa tabasamu kama vile anamwambia mjukuu wake Kleist, ‘’Nimekukomesha kwa kutaka kwako kunicheka ati sijaalikwa Ikulu.''

Mimi nilishusha pumzi kwani nilikuwa nimechoka kwa kisa kile kilichokuwa kimetokea kwa wakati ule zaidi ya miaka arobaini nyuma.

Kleist akaomba ruksa na Shariff akaturuhusu baada ya kupiga fatha. Kleist wakati tunatoka akaingia jikoni kwa mke wa Shariff Attas kwenda kuaga.

Tulipokuwa sasa tunatoka nje Shariff Attas akampigai kelele Kleist, ‘’Kleist bibi yako umempa shilingi ngapi?’’

Kleist akacheka akamjibu Shairff, ‘’Nenda kamuulize mwenyewe.’’
Shariff akawa anacheka kwa ndani ya nyumba na sisi tunacheka hapo nje.

iQl-N4u7N12cUVPdLGb_jw_LjTkiTjxz9DJ7wHC6LjOzHWmEPeflA3S8U20FOZFzuCwEV8lcuEQ=w469-h657-no

Gazeti hili ndilo lililochapa kisa cha Shariff Attas na Nyerere mwaka wa 2006
Nakala ya gazeti hili nimekuta katika Nyaraka za Ally Sykes miaka mitatu baada ya kifo chake

2016%2B-%2B1

Hiyo hapo juu kulia katika gazeti ndiyo ilikuwa nyumba ya Abdul Sykes aliyosihi na Nyerere 1954
Nyumba hii ilikuwa Mtaa wa Stanley na Sikukuu
 
Sidhani Sharifu alimaanisha kuwa Mwal. Nyerere alimpuuza yeye ama kumdharau....swali lile lililenga ama kujaa masikhara makubwa sanaaa kati yao, mwandishi wa makala hiyo gazetini na pengine Sheikh Said mnauona ukweli bayana ila kwa makusudi hamtaki kukiri kuwa Mwal. Nyerere alikuwa binadamu aliyeishi kibinadamu zaidi. Sasa hakuhitaji utambulisho wa wengine kwanini alimuuliza Sheikh Sharifu? Nafurahi kuona Sheikh Said ametoa picha nyingi za stori kwa kila mtu kuipambanua na kuilewa kwa picha aionayo. All in all nimefurahia historia hii na namna ulivoileta. Mungu wetu daima ni mkarimu, Sheikh wangu dumisha UKARIMU
 
Asiyejua maana hastahili kuambiwa maana..!

Mkuu endelea tu nakutoelewa kwako
tatizo kisa majina yote yana ubini wa mudi basi kwako faraja kweli ila mleta maada amelete hii stori kama kejeli kwa marehem mwl julius nyerere.....ila weewe endelea kukuna matako kwa unafki wenu malipo ni hpa hapa dunian
 
Unaiga kukariri kuwa kila kitu kejeli

Matusi hayakusaidii ...
 
tatizo kisa majina yote yana ubini wa mudi basi kwako faraja kweli ila mleta maada amelete hii stori kama kejeli kwa marehem mwl julius nyerere.....ila weewe endelea kukuna matako kwa unafki wenu malipo ni hpa hapa dunian
Ngamiani,
Sijaileta stori hii kama kejeli.

Historia ya TANU na nyakati zile ina mengi ambayo nilikutananayo
katika utafiti.

Hebu sikiliza kisa hiki.

Baada ya uhuru pakatokea waandishi wakawa wanamkejeli marehemu
Abdul Sykes kuhusu TAA wakikiita chama cha ''starehe,'' na majina
mengi ya dharau na kejeli.

Hawakuishia hapo wakawa hata kuwa Abdul kaunda TANU wakaifuta na
kumvisha Nyerere taji lile.

Haikupita muda ikawa Abdul Sykes hatajwi kabisa katika kundi la wazalendo
walioasisi TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ajabu ni kuwa hili halikubalika hata siku ile alipofariki magazeti hayakuandika
chochote kuhusu mchango wake katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kilichondikiwa ilikuwa kutoa taarifa kuwa Nyerere kahudhuria maziko ya Abdul
Sykes.

Hiki ndicho kipindi Shariff Attas alipokutana na Nyerere pale TANU Office.
Kwa bahati mbaya sana ikawa Nyerere hakumkumbuka Shariff.

Bahati mbaya zaidi Shariff Attas yeye akaamua iwe hawakupatapo kujuana.
Sikuleta kejeli kwani hakuna tija katika hilo.

Nia yangu ilikuwa kuonyesha TANU ilikuwa imetoka wapi na vipi kwa kuacha
kuandika historia ile nchi imepoteza hadhi za mashujaa wake.

Laiti nisingeandika kitabu cha maisha yake wengi hapa JF mngebaki kizani.

Abdul Sykes na Julius Nyerere marafiki wakubwa wakati wa kuunda TANU
leo wote ni marehemu.

Tunataja majina yao katika historia ya Tanganyika kwa ajili ya kuhifadhi heshima
na kumbukumbu zao.

Mimi nasikitika kuwa mkasa wa Shariff Attas umekuchoma kiasi umefika kutukana.
Hii ni bahati mbaya.

Miaka kama 30 iliyopita wakati naanza utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes sikufikiria
haya kwa mbali kuwa kitabu hiki kitaleta msisimko katika historia ya Tanganyika.
 
There we go again!
Sooth,
Katika miaka ya 1960 kulikuwa na kundi la vijana wakijiita, ''Chipukizi Club,''
wakipiga muziki wa ''pop.''

Alikuwapo Hussein Shebe, Raymond Chihota, Cuthbert Sabuni, Chico,
Nanji, Badrin, Henin Seif, Mariam, Sauda
na wengineo wakiungana na
vijana wa Kigoa na band yao, ''The Blue Diamonds.''

Walikuwa na kipindi Radio Tanzania kila Jumamosi mchana kikiitwa ''Chipukizi
Club.''

Kipindi hiki walikuwa wakikifungua na nyimbo inaitwa, ''Here We Go Luubiluu.''

Hii ndiyo ilikuwa ''signature tune'' ya kipindi hicho.

ewpqn4-FaFMKjGmhSafT_UMcz8t-FyKsVV-2-Gg-QAc38mavJQyD20ScvJZkaqjLwP4vrt1VS0H-ElKU5V0uQyasw5BXoXFnRRJoReaWRTHmFmtgBKBRwlz7LThkgWqYS2KKC_B0Uc_6D6MGknvogomi8Ul9MU7obw406TfhOX1NA7Zg90DoAPyOMYt7qWb_OzAnc_Lin9Qzr7jrYNx0dZTrzGO7EaeulcnIGP_Id5eEy1Abvjq8_kw2N-HHUuUDlxi6w5NXpOIYNLxuUptE94kO4WptOJrzbjg0alqNmLBP8rBZDt7BtkRFN7sdgGHuZXrsU-Xtg4blOiEDtzp7R33S_Q327ywJvJP0TNssrb9rOt2iryFXL3CuCxhBwD8BBIWHBRQgCypnJJXHmb0f8NnfdFYTn4-R76I3vWKwRJctndYu20yMAP70HOtMSeh4dCqdzMsj1UQSxhS298cXfUiQffQwRu0i0wnrChRkc7nTc0hDP-1zaZIrz7dCVNE017hU0WOo8-FYvBYrbVMTaE_Rk8ktHdw3VNAdg_CwlLj8vN1DDu-NPcWVz9jfExkl4eRbU9u23jfz6eb2sLAyS1RCRnk6CxalgpmafqkpiODigqScLQ=w670-h526-no

Miaka hiyo mimi ndiye huyo hapo Mnazi Mmoja na nyuma yangu ni barabara
ambayo baadae ikajapewa jina Titi Street na hizo nyumba ni Soko la Kisutu.
 
Sooth,
Katika miaka ya 1960 kulikuwa na kundi la vijana wakijiita, ''Chipukizi Club,''
wakipiga muziki wa ''pop.''

Alikuwapo Hussein Shebe, Raymond Chihota, Cuthbert Sabuni, Chico,
Nanji, Badrin, Henin Seif, Mariam, Sauda
na wengineo wakiungana na
vijana wa Kigoa na band yao, ''The Blue Diamonds.''

Walikuwa na kipindi Jumamosi mchana kikiitwa ''Chipukizi Club.''

Nimekuelewa vizuri Mzee Mohamed Said. "Here we go again"!
 
Daaaah ! Mambo kweli hubadirika.. ! Mie kijana wa 90 naona mji nmeshaumaliza... Kumbe silolote sichochote.. !
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom