Mtaa wa Ali Mwinyi Tambwe

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,266
MTAA WA ALI MWINYI TAMBWE

Mtaa huu uko Kinondoni Block 41.
Nani huyu Ally Mwinyi Tambwe?

Ana mchango gani katika historia ya Tanzania?

Ally Mwinyi picha yake ya zamani kabisa katika picha zake chache katika historia ya Tanganyika ni picha iliyokuwa katika Maktaba ya Picha ya Sykes.

Picha hii ilitolewa hadharani mara ya kwanza mwaka wa 1997 ili iwe sehemu ya picha katika kitabu cha Abdul Sykes.

Katika picha hii yuko Ali Mwinyi Tambwe, Kleist Sykes, Maalim Muhammad Mattar na Abdul Sykes akiwa mtoto mdogo pengine hajavuka miaka 10.

Maalim Mattar ni wa kwanza kushoto kwa waliosimama nyuma.

Nilipata kufanya mahojiano na Ali Mwinyi Tambwe hapo nyumbani kwake Kinondoni B Block 41 na aliniambia, "Abdul na Ali wadogo sana kwangu.

Mimi nimewaona wale watoto wadogo wanakuja kusali Msikiti wa Kitumbini wameshikwa mkono na baba yao.

Mimi niko pale msikitini nina akili zangu."

Wakati ananieleza haya nilikuwa picha hii bado sijaiona.

Picha hii imepigwa ndani ya ua wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika, Mtaa wa New Street na Stanley katika miaka ya mwanzo 1930s.

Ali Mwinyi Tambwe alichukua nafasi ya Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika badala ya Kleist Sykes kulazimishwa kujiuzulu.

Hii ni historia inayohitaji muda kuelezwa.

Ally Mwinyi alishiriki katika mazungumzo ya mwaka 1953 nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio Ukerewe akiwa na Abdul Sykes agenda kuu ikiwa vipi wamwingize Julius Nyerere katika TAA na kumchagua awe President.

Ali Mwinyi akiwa Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na Abdul Sykes akiwa Secretary wa TAA na Act. President.

Kisa hiki nimekieleza mara nyingi hapana haja ya kukirudia.

Ali Mwinyi ana mengi sana lakini kwa sasa tutosheke na haya.
 
Hawana maana zaidi ya kukuzwa na mjukuu wao ambaye kila siku anapayuka juu ya umuhimu wao katka nchi yetu ilihali hana lolote la maana zaidi ya kuvaa makubazi.
Washapewa mashavu sana
Ila naona kizazi chao walichokiacha
Wameshindwa kuendeleza walichoanzisha wazee wao

Ova
 
Ali Mwinyi alimfanya Julius Nyerere kuwa rais, halafu Julius Nyerere akamfanya Ally Mwinyi kuwa rais.
 
Hawana maana zaidi ya kukuzwa na mjukuu wao ambaye kila siku anapayuka juu ya umuhimu wao katka nchi yetu ilihali hana lolote la maana zaidi ya kuvaa makubazi.
Unasumbuliwa UAK (upungufu wa akili kichwani maana hujui hata kwa nini tunajifunza historia.
 
Picha zikowap
Ndege...
Samahani sana.
Picha hizi hapo chini:

1713952113409.png

1713951708148.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom