Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,857
- 30,205
- Thread starter
- #161
Sineno,Mtanganyika ana hasira sana, anaweza hata kuua! Dah
Kaghadhibishwa na kitu gani?
Maana kataka picha nimeweka.
Kataka historia yangu nimeweka.
Kipi kilichomuudhi?
Labda ndugu zanguni Wana Barza muulizeni.
Unajua mie nimesomeshwa mlango wa mnakasha
na Maalim Haruna.
Kanifunza mengi ambayo kwa kweli ndiyo yanayonisaidia
katika kila mjadala hapa.
Kwanza Maalim alikuwa anasema ili kushinda mjadala lazima
ulijue somo lako vizuri.
Kisha akatufunza kuwa adabu ni muhimu.
Usimkejeli mwenzio wala usimtukane.
Akatufunza kuwa ukiona mtu anakuja na lugha si za kiistaarabu,
Maalim akikusudia matusi na vitisho, ujue hamna kitu.
Ukiona hizo dalili basi sitisha mjadala kwani hauna tija.
Mwenye ilm hatukani kamwe wala hatishi watu.
Akisema kuwa madhumuni ya mjadala ni kusomesha na kuongeza
elimu.
Huwezi kusomesha wala kusoma katika matusi na vitisho.