Kisa Cha Idi Amin Na Mwandishi Wa Kitanzania!

Status
Not open for further replies.
Maggid, Tatizo lililopo nitakueleza kwa kifupi sana na hakuna
vinginevyo zaidi ya hivyo pia Tatizo hilo lipo kwa serikali na
wananchi wa kawaida ni hivi-:

TUMEKUWA TUNAPENDA KUSIKIA TUNACHOTAKA KUSIKIA
HATUPENDI KUSIKIA TUNACHOTAKIWA KUSIKIA.

CCM imetukifu watz tulio wengi! Mkuu, acha tubadishe wimbo
 
Yeye naye kama yule mwana wa Malecela........akizidiwa hoja ataanza ''unajua nilipokuwa Sweden'' as if sisi wengine hatujatembea....huu ulimbukeni wa kufika ulaya unapotosha sana watu wengi

Si anajua hatuwezi kwenda kuuliza kwa vile ni mbali? Chezea, Maggid wewe!
 
Maggid

Safari zako zinafadhiliwa ma magamba nini ?

za Usubuhi huku kushakucha...

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Ndugu zangu,

Nilikuwa kibaruani mpaka muda huu. Nimeingia humu JF na kupitia comments zote kwenye thread yangu ya asubuhi kuhusi nilichokiona na kukisikia kule Nyololo. Kuna waliotoa maoni yaliyojaa chuki na mashambulizi binafsi. Hakika naliona hili la chuki kutawala humu JF.

Ukweli, kuna wanaonekana kuandika maoni yao yaliyojaa chuki badala ya hoja. Wakati mwingine najiuliza; hivi hawa ni Watanzania? Maana, Watanzania hatuna hulka ya chuki za namna hii. Kuna mwingine akiliona jina langu tu anatanguliza chuki. Na kila sentesi yangu niliyoandika anatafuta ni wapi nimeteleza ili anishambulie. Kuna ambao hawaoni hata moja jema la kwangu.

Inanikumbusha kisa cha Idi Amin na mwandishi wa Kitanzania.

Inasemekama makachero wa Idi Amin walimnasa mwandishi wa Kitanzania ndani ya mpaka wa Uganda. Mwandishi yule akafikishwa mpaka kwa Idi Amin mwenyewe.

Alipofika kwa Amin, mwandishi yule wa Kitanzania akaamini kuwa amekwisha, kuwa atauawa. Idi Amin akamkaribisha kiti na soda anywe. Kisha akamwuliza; " Hivi nyinyi waandishi wa Tanzania mnaandika mabaya tu kuhusu mimi. Nikuulize, unadhani hakuna hata jambo moja zuri ambalo Idi Amin amelifanya?"

Mwandishi yule Mtanzania akajibu; " Ni mengi tu mazuri umefanya Mheshimiwa Rais!"

Idi Amin akatamka; " Kama ni hivyo, basi, rudi nyumbani Tanzania na huende ukaandike jambo moja tu zuri kuhusu Idi Amin!"

Mwandishi yule Mtanzania hakuamini masikio yake kuwa Idi Amin amemwachia huru!

Usiku Mwema.

Maggid,
Iringa.

Ndio Bw. Maggid, twambie huyo Mwandishi alipokuja Tz aliandika zuri lipi la Idd Amin? Au alisimulia tu hiyo habari ya kuachiwa na Idd Amin!? Kwako tu au gazetini? Kama aliandika gazetini, lilikuwa gazeti gani na la lini? Ni hadithi nzuri hiyo, tusimulie zaidi maana hapa umetupa nusu nusu kama ulivyotupatia habari ya Nyololo. Uwe unakamilisha habari, vingivevyo watu hawatakoma kukushambulia mnyalukolo wangu Maggid.
 
Mkuu Narubongo,
Hivi ni Media gani ipo huru (isiyoegemea upande wowote) kwa sasa hivi Tanzania?

hahahahaaaaa mkuu kwa sasa soma same story kutoka media tofauti tofauti then use below formula to get balanced news

[Free Media + Uhuru + Mwanahalisi + Clouds + MCL + habari leo ] / 6
 
Last edited by a moderator:
Hahahahaaaaa Mkuu kwa sasa soma same story kutoka media tofauti tofauti then use below formula to get balanced news

[Free Media + Uhuru + Mwanahalisi + Clouds + MCL + habari leo ] / 6

Formula yako nzuri ila inakuwaje kwa mfano umekuta Story ime appear kwenye gazeti moja tu. Mfano unakuta gazeti la Sauti Huru limeandika "Slaa, Mbowe wachapana Makonde". Au gazeti la HOJA limeandika "Uingereza na Ujerumani yamwaga Mabilioni CHADEMA".

Na wakati huo huo unakuta Tanzania daima limeandika "Vigogo waficha Mabilioni Uswiss". Huku MwanaHalisi likiandika "Aliyemteka Ulimboka huyu hapa. Ni Ramadhani Ighondu wa Usalama wa Taifa". Hivi hapo unafanyaje Mkuu wangu? Nieleweshe na mimi nianze kutumia hiyo formula yako.

Nakala: Matola, Kimbunga, Candid Scope nk.

TUMBIRI (PhD in Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form Six National Exams),
tumbiri@jamiiforums.com
 
mimi huwa napenda sana kufuatilia media zisizo egemea upande wowote na ndio maana huwa sisomi habari za free media, uhuru, mwanahalisi, clouds etc miaka ya nyuma nilikuwa nikiamini maggid ni mwanahabari huru lakini ilipokaribia october 2010 nilianza kutafakari nilichokuwa nikiamini. Bila kuuzunguka mbuyu tatizo la maggid ni chuki ya kibinadamu aliyonayo kwa cdm lakini kwa vyama vingine na matukio mengine ya kijamii bado yupo fair, kwahiyo unatakiwa kuwa mwangalifu unaposoma habari zake zinazoigusa cdm.

Swala jingine maggid ni msomi lakini anapenda udini vibaya sana, kwenye blog yake huwa analeta habari fulani za kuchokoza nyuki and the likes of malaria sugu, zomba wanaingia kichwa kichwa na anapublish comment zao zote lakini kwa upande wa pili anaziminya hata kama ni za busara that's why utakuta katika comment 30 alizopublish 25+ ni zenye mitazamo ya kina MS.

Kitu cha pekee ninachokipenda kwa maggid ni kuuma na kupuliza

Msomi hawezi kuweka "urban legend" kama habari bwana, usimpandishe cheo bila uchunguzi.
 
Formula yako nzuri ila inakuwaje kwa mfano umekuta Story ime appear kwenye gazeti moja tu. Mfano unakuta gazeti la Sauti Huru limeandika "Slaa, Mbowe wachapana Makonde". Au gazeti la HOJA limeandika "Uingereza na Ujerumani yamwaga Mabilioni CHADEMA".

Na wakati huo huo unakuta Tanzania daima limeandika "Vigogo waficha Mabilioni Uswiss". Huku MwanaHalisi likiandika "Aliyemteka Ulimboka huyu hapa. Ni Ramadhani Ighondu wa Usalama wa Taifa". Hivi hapo unafanyaje Mkuu wangu? Nieleweshe na mimi nianze kutumia hiyo formula yako.

Nakala: Matola, Kimbunga, Candid Scope nk.

TUMBIRI (PhD in Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form Six National Exams),
tumbiri@jamiiforums.com

mkuu sidhani kama mtu makini anaweza kusoma gazeti la Sauti Huru, hoja, dira, jamhuri, jambo leo. Unaposoma MwanaHalisi na tz daima unatakiwa kutafakari mstari baada ya mstari mfano mwanahalisi huwa wanaweka majina ya watu, namba za simu na muda wa maongezi tu! lakini hawaelezi nini kilichoongelewa kati ya pande mbili, tz daima kidogo hawana msimamo mkali kama ule wa mwanahalisi lakini tegemea kukuta habari za kuibeba cdm na mabaya ya ccm... tz daima linaaminika kwa 65%.

-usitegemee kukuta habari nzuri za 6, mwakymbe habari leo corp
-usitegemee sana kukuta habari nzuri za kabwela mwanahalisi, tz daima
-usitegemee kukuta habari nzuri za EL dira, jamhuri, mwanahalisi

ITV na star TV wameanzisha mtindo wa kusoma maoni ya watazamaji kupitia facebook na hivyo unaweza uka_conclude mtazamo wa watz kupitia maoni yao kwa habari husika, lakini kwa upande wangu nimekuwa na kawaida ya kuingia kwenye page zao ili kujiridhisha na kilichosomwa kwenye screen,
huko nimegundua maoni yanayosomwa ni yale yenye muelekeo wakuibeba serikali tu.
 
Msomi hawezi kuweka "urban legend" kama habari bwana, usimpandishe cheo bila uchunguzi.

msomi si lazima aelimike.. baada ya kutandikwa za uso sasa hivi ameshika adabu kiasi fulani anasubiri msahau tena
 
Mkuu sidhani kama mtu makini anaweza kusoma gazeti la Sauti Huru, Hoja, Dira, Jamhuri, jambo leo.

Mkuu lakini na yenyewe ni magazeti kama yalivyo magazeti mengine na yana mlengo flani ambao si wa kupuuza na kama ulivyosema ni muhimu ku cover yote kwenye formula yako ili kupata average story. Je inapotekea Sauti Huru au MwanaHalisi yanatoka na kichwa cha Habari cha kipekee huoni kwamba average ya story itakuwa ni the same story? Je hiyo same story ni sahihi kuiita balanced news?

Naona formula yako ina Limitations / Critiques
 
Iddy alijitahidi sana kujenga uchumi wa Uganda kwa wakati ule lazima tumpe sifa zake ingawa baada ya kupinduliwa mambo yakaanza kuwa hovyo tena
 
Ni sawa na Ramadhani Semtawa wa Mwananchi usitalajie ashuke na habari ya kumsema vibaya Zitto Kabwe. Am sick & tired na hawa waandishi uchwara sasa napata ushahidi na ukweli ni kwa nini Mkapa alikuwa anawadharau hawa waandishi wetu.
 
Iddy alijitahidi sana kujenga uchumi wa Uganda kwa wakati ule lazima tumpe sifa zake ingawa baada ya kupinduliwa mambo yakaanza kuwa hovyo tena
 
Mkuu lakini na yenyewe ni magazeti kama yalivyo magazeti mengine na yana mlengo flani ambao si wa kupuuza na kama ulivyosema ni muhimu ku cover yote kwenye formula yako ili kupata average story. Je inapotekea Sauti Huru au MwanaHalisi yanatoka na kichwa cha Habari cha kipekee huoni kwamba average ya story itakuwa ni the same story? Je hiyo same story ni sahihi kuiita balanced news?

Naona formula yako ina Limitations / Critiques

Kila mmoja ana kichwa chenye nywele, lakini kuna kuzidiana mwenye nyingi na chache, hata hivyo wote hawa hakuna anayejisikia kuzidiwa na mwenzake kwani hata mwenye kubakiwa na chache za karibu na masikio zilobaki kushikisha miwani anaamua kupitisha kiwembe. Nataka kumwonea huruma mwenye kupitisha kiwembe kwani nilikuwa na maoni ya kumshauri atumie kofia kuwa ziada ya upungufu wa nywele zake. Kazi kweli kweli.

TUMBIRI nikujibu kama ifuatavyo
Mtu akipotea njia nani wa kumwuliza ili ampe maelekezo sahihi?

  1. Kibaka atamhakikishia njia ya kufika salama aendako?
  2. Polisi doria atamsaidia mwenye mfuko wa dhahabu njia ya usalama kutoka bandari ya salama?
  3. Changudoa anayehaha kupata mshiko kwa siku nzima?
  4. Mfanya biashara kwa vile njaa yake ni wateja ili amtangaze huko aendako?
  5. Mwanasiasa kwa vile atafikisha ujumbe wake kwa atakakofikia kuongeza idadi ya wafuasi
  6. 4 & 5 majibu sahihi?

Je, orodha ya maswali ya kumjibuTUMBIRI inaakisi ukweli wa vyombo vyetu vya habari nchini?

Nakala: Matola, Kimbunga, Narubongo, nk
 
Maggid!!
na kweli usiku mwema!!! Lol!
Mti mwema ndio upigwao mawe,
Sema kweli hata kama watu watakuchukia...
Jicho haliwezi kuwa mdomo!
 
Mkuu lakini na yenyewe ni magazeti kama yalivyo magazeti mengine na yana mlengo flani ambao si wa kupuuza na kama ulivyosema ni muhimu ku cover yote kwenye formula yako ili kupata average story. Je inapotekea Sauti Huru au MwanaHalisi yanatoka na kichwa cha Habari cha kipekee huoni kwamba average ya story itakuwa ni the same story? Je hiyo same story ni sahihi kuiita balanced news?

Naona formula yako ina Limitations / Critiques

- nadhani kuna influence ya media owners kwenye kuandika habari
- kuna intrapreneurs (journalists) within a media

"Sauti Huru au MwanaHalisi yanatoka na kichwa cha Habari cha kipekee huoni kwamba average ya story itakuwa ni the same story?" hints za majibu ya hili swali nimejaribu ku mention pale juu "-usitegemee kukuta habari nzuri za ..." mfano ukikuta same story ya vituko vya kabwela Sauti Huru na MwanaHalisi baki kuwa mtazamaji.!

- credibility ya vyombo/wanahabari wetu ---> mkuu nadhani unakumbuka chanzo cha kifo cha chacha wangwe, mwenendo wa kesi iliyomkabili deus malya na habari tulizozisoma/kusikia na kuaminishwa kupitia media zetu za tz [mimi binafsi sikuwahi kukubaliana na sababu zilizokuwa zikitolewa]. Dogo alifungwa, kukata na kushinda rufaa.. juzi juzi amekuja na ID yake halisi na kupigwa interview ya maana na kujibu maswali yote kwa kiwango cha kuniridhisha kuhusu kifo cha chacha(uzi upo humu humu JF) .. cha ajabu media zote zilikuwa zikireport vitu vya kusadikika! kwahiyo ni kweli formula yangu huwenda isitoe majibu sahihi kutokana na udhaifu wa media + wanahabari

HITIMISHO: Ni swala la msomaji mwenyewe kumuelewa mwandishi wa habari (personally) na kuelewa mlengo wa chombo cha habari. Hatupendi lakini kwa media za tz ni lazima iwe hivyo vinginevyo utapotoshwa na sijui ni watz wangapi huwa wanatafakari wanaposoma au kusikia habari
 
Ndugu zangu,

Nilikuwa kibaruani mpaka muda huu. Nimeingia humu JF na kupitia comments zote kwenye thread yangu ya asubuhi kuhusi nilichokiona na kukisikia kule Nyololo. Kuna waliotoa maoni yaliyojaa chuki na mashambulizi binafsi. Hakika naliona hili la chuki kutawala humu JF.

Ukweli, kuna wanaonekana kuandika maoni yao yaliyojaa chuki badala ya hoja. Wakati mwingine najiuliza; hivi hawa ni Watanzania? Maana, Watanzania hatuna hulka ya chuki za namna hii. Kuna mwingine akiliona jina langu tu anatanguliza chuki. Na kila sentesi yangu niliyoandika anatafuta ni wapi nimeteleza ili anishambulie. Kuna ambao hawaoni hata moja jema la kwangu.

Inanikumbusha kisa cha Idi Amin na mwandishi wa Kitanzania.

Inasemekama makachero wa Idi Amin walimnasa mwandishi wa Kitanzania ndani ya mpaka wa Uganda. Mwandishi yule akafikishwa mpaka kwa Idi Amin mwenyewe.

Alipofika kwa Amin, mwandishi yule wa Kitanzania akaamini kuwa amekwisha, kuwa atauawa. Idi Amin akamkaribisha kiti na soda anywe. Kisha akamwuliza; " Hivi nyinyi waandishi wa Tanzania mnaandika mabaya tu kuhusu mimi. Nikuulize, unadhani hakuna hata jambo moja zuri ambalo Idi Amin amelifanya?"

Mwandishi yule Mtanzania akajibu; " Ni mengi tu mazuri umefanya Mheshimiwa Rais!"

Idi Amin akatamka; " Kama ni hivyo, basi, rudi nyumbani Tanzania na huende ukaandike jambo moja tu zuri kuhusu Idi Amin!"

Mwandishi yule Mtanzania hakuamini masikio yake kuwa Idi Amin amemwachia huru!

Usiku Mwema.

Maggid,
Iringa.

Ndo nini hii sasa???

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom