Ndugu zangu,
Nilikuwa kibaruani mpaka muda huu. Nimeingia humu JF na kupitia comments zote kwenye thread yangu ya asubuhi kuhusi nilichokiona na kukisikia kule Nyololo. Kuna waliotoa maoni yaliyojaa chuki na mashambulizi binafsi. Hakika naliona hili la chuki kutawala humu JF.
Ukweli, kuna wanaonekana kuandika maoni yao yaliyojaa chuki badala ya hoja. Wakati mwingine najiuliza; hivi hawa ni Watanzania? Maana, Watanzania hatuna hulka ya chuki za namna hii. Kuna mwingine akiliona jina langu tu anatanguliza chuki. Na kila sentesi yangu niliyoandika anatafuta ni wapi nimeteleza ili anishambulie. Kuna ambao hawaoni hata moja jema la kwangu.
Inanikumbusha kisa cha Idi Amin na mwandishi wa Kitanzania.
Inasemekama makachero wa Idi Amin walimnasa mwandishi wa Kitanzania ndani ya mpaka wa Uganda. Mwandishi yule akafikishwa mpaka kwa Idi Amin mwenyewe.
Alipofika kwa Amin, mwandishi yule wa Kitanzania akaamini kuwa amekwisha, kuwa atauawa. Idi Amin akamkaribisha kiti na soda anywe. Kisha akamwuliza; " Hivi nyinyi waandishi wa Tanzania mnaandika mabaya tu kuhusu mimi. Nikuulize, unadhani hakuna hata jambo moja zuri ambalo Idi Amin amelifanya?"
Mwandishi yule Mtanzania akajibu; " Ni mengi tu mazuri umefanya Mheshimiwa Rais!"
Idi Amin akatamka; " Kama ni hivyo, basi, rudi nyumbani Tanzania na huende ukaandike jambo moja tu zuri kuhusu Idi Amin!"
Mwandishi yule Mtanzania hakuamini masikio yake kuwa Idi Amin amemwachia huru!
Usiku Mwema.
Maggid,
Iringa.