Mentor
JF-Expert Member
- Oct 14, 2008
- 20,328
- 23,879
Maggid,kwanza declare interest ili usiwe unapingwa.
Kwani yeye ni mwanasiasa!??
Maggid,kwanza declare interest ili usiwe unapingwa.
Kitu cha pekee ninachokipenda kwa maggid ni kuuma na kupuliza
Well, nafahamu hizo stats peke yake hazi conclude chochote...lakini pengine zinaweza kutupa pa kuanzia? Still thinking.....Likes Received 353
Likes Given 11
==>read at 1243hrs today
Hongera kwa kumwelewa.Kwanza huyu jamaa nimnafiki.Hata kama mtu amefanya mazuri mangapi halafu leo hii mtu huyo aje amwue baba yako mzazi utakuja msifia huyo mtu hata siku moja?Lini ukaona mtu anamsifia muuaji hata kama alitenda mema mangapi.Huyu jamaa upeo ni mdogo namshangaa anapotoa mfano wa IDD AMIN na mwandishi wa habari nikapata picha alivyo.Mkuu mimi nilisoma ile thread yako ya awali kwa kweli bila chuki wala uhasama naweza kusema kuwa ilikuwa na mapungufu yake. Mle uliandika ngongera, hapakuwa na content wasomaji wako wengi walibaki watupu bila kuelewa lengo la habari ile. kwa upande mwingine msomaji wako angeweza kupata jazba baada ya kuelewa kuwa wewe ulikuwepo kwenye eneo la tukio ukiongea na watu uliosema wana uelewa wa tukio kwa upana wake kwa sababu waliliona live likitokea, na ulikuwa na nafasi ya kuwaunganisha hewani wakasikika live radioni, lakini ukaamua kutokufanya hivyo, matokeo yake unawaambia wasomaji wako waende huko ili wapate ukweli uliofichika wa tukio!!! Ni ukweli upi huo??? wewe tayari ulikuwepo, uliongea na mashuhuda kwa nini usiuseme huo ukweli???
Kwa maarifa yangu madogo niliyo nayo nilihisi wewe unatafuta namna ya kuweka "spin" kwenye tukio na hapa umeanza kwa kutaka watu waamini kuwa hivyo wanavyojua kumbe sivyo!!!
Mimi huwa sikipendi........ndio unafiki wenyewe
hahaaa mkuu read btn lines, huwa akiona hoja zimemuelemea anakwenda kulialia kwenye blog yake na facebook wakati huo akiwa amekata mguu hapa JF kwa miezi na baada ya hapo anaanza kuandika habari za kujikomba kule alipochafua ili kuwarudisha wasomaji wake... akiona watu wamesahau anarudi tena JF na baada ya muda utaona anarudia kuandika vitu vya ajabu.
Huyo ndiye maggid wa kuuma na kupuliza
Halafu anataka kulazimisha yale anayo yaamini yeye kuwa sahihi. Ukimpinga kosa
Maggid atambue kuwa mabandiko yake ni ''maoni'' tu na wala si lazima yawe ama yafanane na ''ukweli''.Na maoni yanategemeana na imani,ufahamu,elimu, matarajio,matamanio na mwelekeo wa mwandika maoni.
Atambue kuwa anatakiwa kujenga uwezo wa kuandika maoni yake huku akifikiri sawa sawa kwa kuwa yeye hamiliki ukweli.Ukweli unatafutwa nasi tunazidi kuutafuta pasipo kuchoka.Ahakikishe wanaosoma maandishi yake wanapata thamani ya pesa na muda unaotumiwa katika kutafuta na kusoma maandiko yake.
Ajue,vile vile, kuwa wapo wanaoandika ukweli hapa Tanzania na wanafahamika na kuheshimika na Watanzania.
Hata hivyo,kwa sababu za wazi watu hao wanachukiwa na kuogopwa na tabaka tawala.
Naye,aache kuchezea akili za watu.Achague sasa:kuendelea kuwa upande wa watawala ama kuwa na wananchi.
Maggid, naanza kuhisi kuwa labda wewe si mwandishi wa habari, na kama ni mwandishi wa habari basi ni aina ya wale waandishi wa habari tulio nao wengi Tanzania, ambao wanaweza kuwa waandishi wa habari wazuri tu, lakini ukweli ni kwamba hawakusomea uandishi wa habari na walisoma mambo yanayowasaidia kuwa waandishi wa habari, mfano, BA education, economics, english language nk.....Idi Amin akatamka; " Kama ni hivyo, basi, rudi nyumbani Tanzania na huende ukaandike jambo moja tu zuri kuhusu Idi Amin!"
Mwandishi yule Mtanzania hakuamini masikio yake kuwa Idi Amin amemwachia huru!
Ndugu zangu,
Nilikuwa kibaruani mpaka muda huu. Nimeingia humu JF na kupitia comments zote kwenye thread yangu ya asubuhi kuhusi nilichokiona na kukisikia kule Nyololo. Kuna waliotoa maoni yaliyojaa chuki na mashambulizi binafsi. Hakika naliona hili la chuki kutawala humu JF.
Ukweli, kuna wanaonekana kuandika maoni yao yaliyojaa chuki badala ya hoja. Wakati mwingine najiuliza; hivi hawa ni Watanzania? Maana, Watanzania hatuna hulka ya chuki za namna hii. Kuna mwingine akiliona jina langu tu anatanguliza chuki. Na kila sentesi yangu niliyoandika anatafuta ni wapi nimeteleza ili anishambulie. Kuna ambao hawaoni hata moja jema la kwangu.
Inanikumbusha kisa cha Idi Amin na mwandishi wa Kitanzania.
Inasemekama makachero wa Idi Amin walimnasa mwandishi wa Kitanzania ndani ya mpaka wa Uganda. Mwandishi yule akafikishwa mpaka kwa Idi Amin mwenyewe.
Alipofika kwa Amin, mwandishi yule wa Kitanzania akaamini kuwa amekwisha, kuwa atauawa. Idi Amin akamkaribisha kiti na soda anywe. Kisha akamwuliza; " Hivi nyinyi waandishi wa Tanzania mnaandika mabaya tu kuhusu mimi. Nikuulize, unadhani hakuna hata jambo moja zuri ambalo Idi Amin amelifanya?"
Mwandishi yule Mtanzania akajibu; " Ni mengi tu mazuri umefanya Mheshimiwa Rais!"
Idi Amin akatamka; " Kama ni hivyo, basi, rudi nyumbani Tanzania na huende ukaandike jambo moja tu zuri kuhusu Idi Amin!"
Mwandishi yule Mtanzania hakuamini masikio yake kuwa Idi Amin amemwachia huru!
Usiku Mwema.
Maggid,
Iringa.