Katika uandishi usiyo na chembe za ushabiki, huwa namkubali Mjengwa. Tatizo ninaloliona kwa wanajf wengi, ni kutokuamini kuwa kuna watu ambao ni neutral.
ZeMarcopolo Pili said:Kutofautiana kimtizamo si chuki ,uhasama ama uadui.Tunatofautiana kwa sababu, kila mmoja wetu, anayo itikadi yake, anao ufahamu wake,anao maslahi yake,anayo matarajio yake,anayo asili yake.Kutofautiana ni lazima kwa sababu sote,kwa wakati mmoja, hatuwezi kuwaza na kufikiri kwa namna mmoja.
Kama huo ni ukweli napenda nitofautiane na maelezo ya Ze Macopolo kuhusu utetezi wa Maggid.Nieleze kuwa mtu hapingwi kwa sababu anaonekana yupo superior dhidi ya wanaompinga.Kwa mujibu wa Ze Macopolo,sote tuliompinga Maggid tupo inferior kwake jambo ambalo si kweli hata kidogo.Kila mwananchi mwenzetu anayeweka mawazo hadharani atambue kuwa lazima watakuwepo watu watajitokeza kuhoji ukweli na usahihi wa hoja zake.Kwa kulitambue hilo,ni budi ,sote,tuweke jitihada kuusaka na kuusambaza ukweli kadiri ulivyo (absolute truth) na wala si kadiri unavyoonekana(relative truth).Tulimtaka,kwa mfano atueleze kwa nini anajibanza katika kona ya ''impartility'' katika mazingira yasiyohitaji impartiality...Kwa maelezo ya Ze Macopolo,mzizi wa tofauti za hoja za kisiasa kati ya Democtrats na Republican,USA, ni uwepo wa chama/mgombea amabaye ni inferior dhidi ya chama /mgombea superior!
Msingi wa hoja za kisiasa, ama hata zisizo za kisiasa, ni tofauti za kimsingi zinazotokana na tofauti za kimitazamo,imani,mwelekeo,falsafa,itikadi nk.Wala tofauti za hoja za kisiasa,USA, haziwezi kutokana na rangi ya Obama dhidi ya rangi ya Romney.
Kama askari wamesababisha kifo cha mwananchi mwenzetu,mwandishi ama raia yeyote anapaswa achague upande:ama awe upande wa Jeshi la Polisi ama awe upande wa raia aliyekatishwa uhai wake kinyama.Binasfi nilimtaka apangue hoja zetu kuhusu ulazima ,umuhimu na nafasi ya imparility katika tukio la Iringa na hakufanya hivyo. Isipokuwa, akatuona tuna chuki naye.Tungependa arejee hapa jamvini apangue hoja...Si kila anayepingwa anachukiwa.Wengine hatujui kuchukia wanadamu wenzetu isipokuwa ''tunachukia'' hoja.
Kwa kuwa Maggid amekuwa akiandika makala kwa muda mrefu sasa, tulimtazamia amejenga uwezo wa kuhimili maono kinzani.Inaelekea anatuona sisi tuliopinga hoja zake kama watu tunaomchukia yeye kibinafsi!Kinachopingwa ni hoja zake si yeye kama Maggid.
Is Maggid again!!?? TUMBIRI wacha nipumzike kwanza najuwa hii thread ametuanzishia sisi, lakini naapa kwa Mungu Matapeli na wanaondekeza njaa kama maggid sasa tutawashikisha adabu & i mean it.Kimbunga,
Shukrani kwa kunishtua juu ya huu mjadala. Tatizo la Maggid kama alivyosema Jmushi1 ni kutoku declare his Interest ndiyo maana huku akijidai ni mwandishi huru wakati maandishi yake yanamtafsiri yeye ni mtumwa wa naini. Akiendeleza ukaidi tutaendelea kumshindilia hoja moja baada nyingine. Na tatizo lake lingine na ukaidi wake wa kutojibu Maswali yetu Magumu yanayoelekezwa kwake. Ajifunze toka Pasco ambae ameweka wazi yupo nyuma ya Lowassa.
Kamanda Matola, karibu na wewe.
We hukunywa soda?
Mi nilikula tende na Gahwa kwa wingi.
Maggid, Tatizo lililopo nitakueleza kwa kifupi sana na hakuna
vinginevyo zaidi ya hivyo pia Tatizo hilo lipo kwa serikali na
wananchi wa kawaida ni hivi-:
TUMEKUWA TUNAPENDA KUSIKIA TUNACHOTAKA KUSIKIA
HATUPENDI KUSIKIA TUNACHOTAKIWA KUSIKIA.