Kipindi Bora zaidi cha Television na Radio Tanzania...

Bolingo time na Zuberi Msabaha ndani ya RFA.
Mama na Mwana ndani ya RTD.
Mizengwe ndani ya ITV.
Nyimbo za Kale AZAM TV.
USWAZI ndani ya EATV.
Mieleka ITV.
 
Radio: Hizi nazo ya Radio One (Abdalah Mwaipaya na Zomboko)
Nikikosa hiki kipindi naumwa kabisa.
Pia Usiku wa Millennium ya Mtani Wambura Radio Free Africa
 
Radio.
1.Je Huu ni UNGWANA? RFA - Wambura Matani
2.Chombeza TIME - Radio 1 Stereo -Aboubakar Saqiq,Rose Chitala
3.Njia Panda - Dr Isaack Maro CLouds
4.Sintosahau - RFA Yusuph Magasha
5.Mambo Mseto - Radio One

TV.
1.Tuongee Asubuhi -Dotto Bulendu Star Tv
2.SuperTraxx - Stivie Kabuye - Star TV
3.Minzengwe - ITV - Kashi Kashi
4.House Hunters - Fine Living
5.Story - ATN
6.Bamba/Hidden Camera - Citizen/KTN
 
Mimi nakumbuka enzi hizo nasikiliza RTD fashion ya radio ilikuwa ni zile wanaita RADIO MKULIMA na brand names zake zilikuwa ni NATIONAL Panasonic ama PHILIPS. Mzazi alikuwa anainunua RTC (yale maduka ya uma).Tukirudi katika vipindi, navikumbuka sana vipindi vifuatavyo ambavyo bila shaka mdau utakubaliana na mimi vilikuwa maarufu kutokana na zile nyimbo za utangulizi kuashiria kipindi kuanza ama kumalizika.

1. Sikiliza Bwana Umeme... (Bwana Umeme) - Kile kipindi cha TANESCO cha kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya umeme.

2. Starehe na BP - Uncle Julius Nyaisanga (R.i.P) alikuwa anakimudu vyema kabisa.

3. Kahawa ni Mali - Namkumbuka sana yule mama wa kiashirio cha kipindi akitamka hayo maneno kwa rafudhi ya kichaga.

4. Jifunze Kiswahili Fasaha - sina uhakika kama nimeandika vyema tittle yake lakini kilikuwa ni kile kipindi kizuri kilichobuniwa kuhamasisha watu kuzungumza kiswahili katika harakati ya kuwaunganisha watu wa mikoani na wa Bara. Nakumbuka kiashirio chake kuna sehemu inasema.. na mikoani... ni kiswahili chatumika.....Bila kusahau vipindi kama..

5. TTCL Simu kwa Maendeleo.

6. Serikali za Mitaa.

7. Afya yako /Afya ya jamii " sikumbuki vyema title ila nakumbuka kiashiria cha kipindi ulikuwa ni wimbo mmoja anaimba Kept John Komba (R.i.P) na kundi lake wakati ule.

Ukija vipindi vya week ends

1. Club Raha leo Show.
2. Mama na Mwana namkumbuka mtangazaji Edda Sanga alikuwa anakimudu vyema kipindi na zile hadithi za "Adili na Nduguze", "Kisa cha Mfalme Juha", ile hadithi ya watoto wa mfalme wanakwenda kutafuta wachumba wa kuoa... n.k
Wakati ule radio ilikuwa na msaada mkubwa kuelimisha jamii nzima (wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara) kuhusu mambo mbali mbali na watu walikuwa wanafuatilia sana.
RTD ilikuwa kiboko. Hiyo ya watoto wa mfalme kwenda kutafuta wachumba inaitwa 'Binti chura'
 
Radio.
1.Je Huu ni UNGWANA? RFA - Wambura Matani
2.Chombeza TIME - Radio 1 Stereo -Aboubakar Saqiq,Rose Chitala
3.Njia Panda - Dr Isaack Maro CLouds
4.Sintosahau - RFA Yusuph Magasha
5.Mambo Mseto - Radio One

TV.
1.Tuongee Asubuhi -Dotto Bulendu Star Tv
2.SuperTraxx - Stivie Kabuye - Star TV
3.Minzengwe - ITV - Kashi Kashi
4.House Hunters - Fine Living
5.Story - ATN
6.Bamba/Hidden Camera - Citizen/KTN
Hapo kwenye chombeza time, Ongezea na kile cha jumapili usiku ilijulikana kama kipindi cha RAFIKI chini ya ROSE CHITALA kulikuwa na Love story hizoo!! ROSE CHITALA yupo wapi?
 
Kuna kipindi alichokua anaongoza abubakari sadik na abd radio one mida ya mchana..sikikumbuki jina

Planet bongo ya salama jabir
 
Hapo kwenye chombeza time, Ongezea na kile cha jumapili usiku ilijulikana kama kipindi cha RAFIKI chini ya ROSE CHITALA kulikuwa na Love story hizoo!! ROSE CHITALA yupo wapi?
RC Computer anaishi marekani kwa sasa!
1131096
RC COMPUTER.jpg
 
1.sitasahau ya Rfa kabla ya 2010
2.kuna kipindi nimesahau jina kilikuwa kinaanza saa 2-3 asubuhi kabla ya sitasahau pale Rfa mtangazaji akiwa rebecca mresi au Roy maganga
Daaah Rebecca mresi noma Sana angekua mdg ningekwenda kujieleza
 
Back
Top Bottom