Msaada juu ya mtoto nimehangaika hospitalini bila mafanikiao

Baraka sheni

JF-Expert Member
Jan 5, 2015
470
193
Poleni na majukumu.

Mwanangu ana miaezi 8 jinsia ya kike amekuwa akisumbuliwa na joto kupanda hasa kichwani na kwenye tumbo. Nilimpeleka hospitali mara 3 hospitali tofauti tofauti lakini tatizo haliishi. Vipimo walivyokuwa wakichukuwa ::

MRDT
URINE
RBG
FBP

Dokta alisema ana maambukizi kwenye damu akaandikiwa dawa na sindano dawa yakuongeza dam
kiukweli amesha maliza lakini sioni mabadiliko mtoto amekuwa kishtuka usiku hataki kula wa kunywa uji hataki.

Naimani humu kuna wazazi kama mm naombezi mawazo yenu madokta karibuni #mzizimkavu karibu upite hata
 
Malezi ya mtoto yana changamoto nyingi sana
1. Hakikisheni ndoa yenu ina Amani
2. Hakikisha mtoto Hana vipele mwilini,aweananyonya na akipewa chakula mama ahakikishe mtoto ameshiba.
3. Kutana na madaktari wawatoto atakusaidia zaidi.
4. Dawa za asili kulingana na Imani yako zitumie kama huziamini mpeleke kanisani
 
yawezekana ni madhara ya kuruka mila ikiwa ukoo wako ulikuwa strict na mila kwa watoto.

mpeleke kwa bibi au babu yake,

binafsi pamoja na kusoma mpaka masters lakini watoto lazima wavae bangili ya kiafrika, niliambiwa ndani kuna mmea unanuka sana ukiwa wazi
 
Malezi ya mtoto yana changamoto nyingi sana
1. Hakikisheni ndoa yenu ina Amani
2. Hakikisha mtoto Hana vipele mwilini,aweananyonya na akipewa chakula mama ahakikishe mtoto ameshiba.
3. Kutana na madaktari wawatoto atakusaidia zaidi.
4. Dawa za asili kulingana na Imani yako zitumie kama huziamini mpeleke kanisani
sawa mkuu nadhukuru
 
Mtoto anaharisha?
Choo chake kikoje?
Ana tapika/alitapika?
Alipata chanjo ya rota?
Ana vipele?
Ana kohoa?
Hali ya meno vipi amekwisha kuota meno mchunguze kwenye fizi zake..
Chunguza utosi Wake Umebonyea au umekuja juu?
Tatizo hili limemuanza lini?

Kuna uwezekano mkubwa akawa na Septicemia , au Tooth Eruption...

Nenda hospitali ya Mkoa au kwa daktari Aliye karibu sio Tabibu kwa ajili ya uchunguzi na matibabu

ni hatari kukaa na mtoto anayeumwa wakati huo asiyekula..
Atapata Hypoglacemia (Pungukiwa sukari) inaweza kusababisha mengine muwaishe hospitali

Baada ya kuambiwa ana maambukizi kwenye damu alipewa Dawa gani??

CC: Baraka sheni
 
Mpeleke kwa Madaktari bingwa wa watoto. Wa kwangu alinisumbua hivyo hivyo mpaka akawa kila wiki anapatwa dege dege. Ilikuwa inaogofya sana. Nilimpeleka kwa Madaktari bingwa mpaka akapona.

Pole mkuu
shukrani mkuu ila moja ya dawa ulizo tumia unaweza niambia pia hata kwa daktari ulipo enda wewe unaweza niambia pia
 
Pole mno mkuu,pls ingia kwenye google ya Red Cross children's hospital, ipo cape Town, SA,wasome vema na wasiliana nao, wakiafiki kukupa appointment, then the rest tutasaidiana InshaAllah
 
Mtoto anaharisha?
Choo chake kikoje?
Ana tapika/alitapika?
Alipata chanjo ya rota?
Ana vipele?
Ana kohoa?
Hali ya meno vipi amekwisha kuota meno mchunguze kwenye fizi zake..
Chunguza utosi Wake Umebonyea au umekuja juu?
Tatizo hili limemuanza lini?

Kuna uwezekano mkubwa akawa na Septicemia , au Toorth Eruption...

Nenda hospitali ya Mkoa au kwa daktari Aliye karibu sio Tabibu kwa ajili ya uchunguzi na matibabu

ni hatari kukaa na mtoto anayeumwa wakati huo asiyekula..
Atapata Hypoglacemia (Pungukiwa sukari) inaweza kusababisha mengine muwaishe hospitali

Baada ya kuambiwa ana maambukizi kwenye damu alipewa Dawa gani??
Maswali mazuri sana haya, bila shaka utatusaidia wengi. 🙏🏾
 
shukrani mkuu ila moja ya dawa ulizo tumia unaweza niambia pia hata kwa daktari ulipo enda wewe unaweza niambia pia
Mtoto wako anahitaji dr bingwa wa watoto. Watanzania wengi akienda hospital mara mbili tayari anakata tamaa. Badilisha hospital, nenda za uhakika. Siku hizi kuna hospital nyingi sana za vichochoronina dr wasio na utaalam mzuri. Kama uko dr ulizia kuna madaktari wa watoto wanaosifika sana.
 
Mtoto anaharisha?
Choo chake kikoje?
Ana tapika/alitapika?
Alipata chanjo ya rota?
Ana vipele?
Ana kohoa?
Hali ya meno vipi amekwisha kuota meno mchunguze kwenye fizi zake..
Chunguza utosi Wake Umebonyea au umekuja juu?
Tatizo hili limemuanza lini?
Baada ya kuambiwa ana maambukizi kwenye damu alipewa Dawa gani??
ndio anahalisha ila ameanza juzi

kuhusu kutapika ni hadi pale unapo

mlazimisha kula anakuwa kama anajitapisha maana hataki kula kabisa.

chanjo ya rota hajapata ila kwa mujibu wa kadi yake chanjo zote kapata

vipele hana
ndio anakohoa

meno yamesha ota tayari

utosi upo juu

tatizo lilimuanza tangia mwezi12*1*2024 ndio tulianza kwenda hospitali

awamu zote alikuwa akiandikiwa sindano za cethiaxone500mg od 5/7
dawa SYNEZZE
dawa HEMOVIT
 
Back
Top Bottom