Heshima kwenu wakuu wangu.
Wakuu naombeni maoni yenu.
Kwa mfano mtu una pesa ambazo utahitaji kuzifanyia jambo fulani miaka mitano ijayo.
Kwa kawaida watu huifadhi pesa bank ila nimefikiria nikaona kwamba say una 50,000 leo,ukiziweka bank baada ya miaka mitano hata kama zitaongezeka,zitaongezeka kidogo sana.
Pia baada ya miaka mitano kitu ambacho unaweza kukifanya kwa 50,000 leo hutaweza kukifanya kwa pesa hizo hizo miaka mitano ijayo,namaanisha thamani ya pesa yetu inapungua kwa kasi sana.
Je badala ya kuziweka 50,000 zangu bank niamue kununua viwanja katika maeneo ambayo najua wakati wowote naweza kuviuza viwanja hivyo na kupata pesa zangu.
Nimeona faida ya kuziweka pesa zangu kwenye viwanja itakua ni;
Bei ya ardhi inapanda kila siku,kama leo nitanunua kiwanja kwa elfu ishirini kwa mfano,miaka mitano ijayo naweza nikakiuza kwa elfu thelathini na tano au zaidi.
Pia nitauza kiwanja kulingana na thamani ya pesa ilivyo katika miaka hiyo.
Haya ni mawazo yangu tu ila sina utaalamu katika haya ninayofikiria,hivyo ningeomba mnaojua kwa uhakika mambo haya mniambie kama mawazo yangu ni sahihi au ninakosea.
Natanguliza shukrani.