Kiongozi wako wa dini hatakiwi kuunganisha ukaribu wako na MUNGU, hilo ni jukumu lako

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Kwenye safari ya kwenda mbinguni, hata mchungaji wangu simuamini. Simuamini kila mtu anayesema BWANA BWANA BWANA. Ishu ya kwenda mbinguni ipo ndefu sana. Nawakumbusheni, hao wachungaji, mashehe ni binadamu kama wewe, wanakwenda chooni, wanakula, wanakasirika, wanafanya dhambi na kadhalika.

Usimchukulie mtumishi wa Mungu ni malaika. Watu wakishikwa kwa skendo za uzinzi, wizi, fitina ama uchawi, kwangu kawaida tu. Muimba kwaya naye mwizi, mzee wa kanisa naye mchawi. Niliyaona haya yote so sishangai sana. Halafu mnashindwaga kujua kitu kimoja.

Kuna nguvu za Mungu na nguvu za giza. Mungu anakuponya, naye shetani anakuponya, ila kukuponya kwake kwa muda tu. Mchungaji anakuombea, pepo linatoka, naye mganga anakuagua jini linatoka. Braza. Muamini Mungu wako. Usifikiri mchungaji wako ni Mungu ama malaika.

Kuna siku utaamini ukisikia mtumishi wako anakula kondoo safi kabisa. Safari ya mbinguni yako peke yako. Mimi kumwamini mchungaji yeyote niliacha tangu nilipoanza kufuatilia haya mambo kiundani.

Aya mkaangalie series ya 30 COINS mjifunze kwa undani kuhusu kanisa, shetani anavyolitumia kufanikisha mambo yake na kuua watu.
 
Back
Top Bottom