Kinondoni: ....Eti mtu mmoja ana viwanja 99... vya nini?

sio tu kua jamaa ana viwanja vingi (94) Dar nzima, ila ktk plot iliyopimwa yenye viwanja 130, hivyo 94 kamilikishwa yeye.

Uamuzi gani basi umechuliwa wa kivitwaa hivyo viwanja na kuwamilikisha waliokosa? Nijuavyo mimi mtu mmoja anakuwa amepewa ofa ili atafute wanunuzi, akifika bei ile ofa inaenda badilishwa jina. Hii ni mbinu tuu ya kuwapiga chenga TAKUKURU.
 
Swali....Je huyo Jamaa ni MJANJA, FISADI, MSANII au apewe jina gani???
 
kwani kavunja sheria jameni?? mwacheni mwenzenu usikute anataka kujitangazia dola je???

Dada yangu, inawezekana tuna wivu kama alivyosema mchangiaji mmoja. Lakini wewe ukiomba walau viwanja viwili utapewa bila kupigishwa kwata la kijeshi ?

Swali....Je huyo Jamaa ni MJANJA, FISADI, MSANII au apewe jina gani???

Inawezekana asisistahili hata mojawapo kati ya hayo kwani huenda ni dalali. Ngoja nitafute habari yenyewe ili tujue haswa ni nani huyu mtu.
 
Dada yangu, inawezekana tuna wivu kama alivyosema mchangiaji mmoja. Lakini wewe ukiomba walau viwanja viwili utapewa bila kupigishwa kwata la kijeshi ?

nini kuomba kiwanja!!!!!!!!!!! mimi niliomba kuchapiwa hati tu miaka minne only to get gamba lenye wrong Land Office number, na sasa ni mwaka wa pili nafuatilia hiyo kitu haijabadilishwa na hayo magarasa yenyewe yamepotea na haijulikani yamepotelea wapi!!!! naomba huu mchakato na Arusha uende pia wajameni!!!!
 
Tz ni zaidi ya vile tuijuavyo na vile inavyoonekana. Tuendako kama taifa na jamii yenye mshikamano sijui ni wapi. Wenye fedha wanafanya wapendavyo maadam pesa anayo. Mtu mmoja kumiliki idadi kama hiyo ya viwanja ni hatari kwa wanyonge. Na zaidi viwanja vinavyopimwa na serikali vinapanda bei kila kukicha,huyu mwenye kipato kidogo anawekwa kwenye fungu gani?
 
Nimesikia kwenye taarifa za habari za TBC1 na dondoo za magazeti kuwa kati ya madudu ya ajabu ajabu yaliyokutwa kinondoni ni mtu mmoja anayemiliki viwanja 99! Kama ni kweli basi Watanzania tumezidi ulafi.

Ila nadhani kuna mengi zaidi. Hapa tu jiwe limesogezwa pembeni, je likigeuzwa kabisa tutakuta nini? Ndo maana naamini kuwa Tanzania inaweza tu kwenda mbele ikiwa tu kila kitu kitasambaratishwa (overhauling the system).

Hizo kawaida ndugu. Kuna mtu, anafahamika sana; yeye ana nyumba 66 na zote ziko kwenye prime areas. Hapo hapo Bongo. Alikuwa boss kwenye moja ya maeneo ya maliasili.
 
Ama kweli ukipanda bangi usitegemee kupata mchicha!

Mleta habari katuhabarisha jamani katika lile fuku fuku la maafisa ardhi kinondoni kuna ofisa fulani anamiliki viwanja 94 kati ya 130 katika eneo moja lilopimwa! Watu wanahoji kwani kavunja sheria gani?! Jamani!

Jamani wengi tunajua madhumuni ya hii miradi ya upimaji viwanja ni kuwazesha wananchi wa kawaida kumiliki viwanja kwa bei nafuu sasa akitokea afisa ardhi anajimilikisha hivyo viwanja tunasema ahaaa mtu ale kwa urefu wa kamba yake ofisini kwake!

Sasa tunapiga kelele za nini za ufisadi mkubwa wa kitaifa kama akili zetu, mawazo yetu zimesongwa na chemi chemi za ufisadi katika mizingo yetu midogo midogo tukipewa mizingo mikubwa si yale yale!

Kwa hiyo polisi ale kwa kuwabambikia wanyonge kesi za bangi?, Mwalimu asiingie darasani ili afundishe masomo ya ziada jioni?, Afisa kodi akadirie mapato kidogo kwa mfanya biashara ili apate cha juu?, Askari akodishe bunduki yake ifanyie ujambazi apate naye cha juu?, bwana mikopo naye atoe mikopo ambayo lazima apewe ten percent ama sivyo no mkopo?,

Wauza mafuta wayachakachue?, machangudoa sijui wachakachue nini? Wanachama wa vyama vya siasa wanachakachuka na IMANI ya vyama vya siasa? Wenye ndoa wanachakachuka na ma-house girls/boys au kwa wanawake au wanaume wa mabaa?

Wenye kuusaka ukubwa maofisini wachakachuke na mabosi wao au na akina kalumanzira ? Madereva na Mautingo wa madaladala hakuna LEVEL SEATING? Manesi na Madaktari wa Hospitali za serikali? Vishoka wa TANESCO?etc. etc. etc. Halafu kwenye MADHABAU wooote hawa wanamtolea MUNGU kwa kazi za mikono yao!

Ahaaaaa! Kweli Tanzania itajengwa na wenyemoyo? Au na MAFISADI Mapapa na Nyangumi kwa Kuwala Mafisadi dagaaa na Kamongo?
 
Serikali ilikuwa wapi? It is a shame.!

Is this a serious question? Yani mbwa mwitu amepewa kondoo wa kuchunga alafu simba ndo anamsimamia mbwa mwitu! Kweli kondoo wakiliwa utadhubutu kuuliza simba alikuwa wapi?hahahahaha! Get serious mate!
 
Ama kweli ukipanda bangi usitegemee kupata mchicha!

Mleta habari katuhabarisha jamani katika lile fuku fuku la maafisa ardhi kinondoni kuna ofisa fulani anamiliki viwanja 94 kati ya 130 katika eneo moja lilopimwa! Watu wanahoji kwani kavunja sheria gani?! Jamani!

Jamani wengi tunajua madhumuni ya hii miradi ya upimaji viwanja ni kuwazesha wananchi wa kawaida kumiliki viwanja kwa bei nafuu sasa akitokea afisa ardhi anajimilikisha hivyo viwanja tunasema ahaaa mtu ale kwa urefu wa kamba yake ofisini kwake!

Sasa tunapiga kelele za nini za ufisadi mkubwa wa kitaifa kama akili zetu, mawazo yetu zimesongwa na chemi chemi za ufisadi katika mizingo yetu midogo midogo tukipewa mizingo mikubwa si yale yale!

Kwa hiyo polisi ale kwa kuwabambikia wanyonge kesi za bangi?, Mwalimu asiingie darasani ili afundishe masomo ya ziada jioni?, Afisa kodi akadirie mapato kidogo kwa mfanya biashara ili apate cha juu?, Askari akodishe bunduki yake ifanyie ujambazi apate naye cha juu?, bwana mikopo naye atoe mikopo ambayo lazima apewe ten percent ama sivyo no mkopo?,

Wauza mafuta wayachakachue?, machangudoa sijui wachakachue nini? Wanachama wa vyama vya siasa wanachakachuka na IMANI ya vyama vya siasa? Wenye ndoa wanachakachuka na ma-house girls/boys au kwa wanawake au wanaume wa mabaa?

Wenye kuusaka ukubwa maofisini wachakachuke na mabosi wao au na akina kalumanzira ? Madereva na Mautingo wa madaladala hakuna LEVEL SEATING? Manesi na Madaktari wa Hospitali za serikali? Vishoka wa TANESCO?etc. etc. etc. Halafu kwenye MADHABAU wooote hawa wanamtolea MUNGU kwa kazi za mikono yao!

Ahaaaaa! Kweli Tanzania itajengwa na wenyemoyo? Au na MAFISADI Mapapa na Nyangumi kwa Kuwala Mafisadi dagaaa na Kamongo?

Mleta habari hajasema lolote kuhusu huyo mtu kuwa ofisa wa ardhi aliyejigawia viwanja mwenyewe, leteni habari kamili jamani kitu kieleweke.
 
Movie iliyokuwa inaanza-ndo imeisha PREMATURELY!!!...nadhani/naamini ilikuwa ni NGUVU YA SODA!!! Mbona hawamtaji aliyekutwa na viwanja 94??? Mwaka huu ni wa uchaguzi... Usikute ndo wamemkamatisha KAMBALE-Magesa (Mkuu wa Idara ya Ardhi Kinondoni). Kuwasimamisha KAMONGO-Hamidu Mgaya (Mkuu wa Upimaji na Ramani Kinondoni) na John Langasi (Msaidizi wa Magesa) na wale PEREGE-39 wakihamishwa mikoa mingine na DAGAA-Wapiga Chapa kupewa kazi nyingine... Je ile Movie ya MWANANYAMALA HOSPITAL imeishia wapi? Nadhani kitakachofuata Lukuvi atapewa Uwaziri/Unaibu wa Kazi,Kilimo au hata Elimu halafu afifishwe nguvu zake!!! KARIBUNI TANZANIA NCHI YA MLIMA KILIMANJARO NA ZANZIBAR...
 
Chanzo cha habari mbona hakijatoa jina la huyo jamma? Kuna woga gani au ni nini kinafichwa hapo. Tuelezwe tu bila kujiuma uma kama ni Londa au ni Makamba, au Kandoro tujue.
 
Chanzo cha habari mbona hakijatoa jina la huyo jamma? Kuna woga gani au ni nini kinafichwa hapo. Tuelezwe tu bila kujiuma uma kama ni Londa au ni Makamba, au Kandoro tujue.

Mkuu hii habari ilisomwa kwenye TV na kunukuuu magazeti. Hata hivyo nilijitahidi kupitia baadhi ya magazeti kwenye mtandao sikuweza kupata original source. Kwa hiyo hakuna woga hapo. Hata hivyo kama kuna mdau ameiona anaweza kutujulisha na tutaiweka hapa. Kama kuna jambo la kuficha bisi tusingeibandika hapa.
 
Back
Top Bottom