Kinga dhidi ya kushtakiwa kwa Marais ni Sheria mfu

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
2,453
5,988
Ndio, Uraisi ni Wadhifa nyeti Duniani kote na Raisi anapaswa kulindwa na mfumo na Sheria za Nchi akiwa ndani na hata nje ya madaraka. Lakini swali ni Je, Kinga za kisheria wanazopewa viongozi Hawa haswa Hawa Executive Presidents, zinalinda maslahi na madudu yao, au zina Linda maslahi ya Taifa?

Mfano Ibara ya 46(3) ya Katiba ya JMT inamuwekea Kinga ya kutoshtakiwa Raisi kwa Tanzania kwa jambo lolote alilofanya akiwa madarakani. Swali Kinga hii ina maslahi gani kwa wananchi.

Raisi anaweza kufanya makosa ya kibinadamu ndio, Lakini vipi yale ya makusudi au uzembe wa wazi? Tumeona mifano mingi katika Nchi zetu haswa za Africa, ambapo matendo ya Viongozi Hawa yameleta madhara makubwa kwa Nchi zao, Bado tunaweza kusema tunahitaji Absolute Immunity from criminal liability kwa viongozi hao?

Nani asiyejua madhara yaliyoachwa na viongozi wazembe, wezi, wabadhirifu na madikteta katika Nchi za afrika? Na vipi Maraisi ambao kwa makusudi au uzembe-jinai wanasababishia Nchi kutumbukia katika mzigo madeni ya kizembe huku wao wakiendelea kunufaika na viinua mgongo na retirement benefits nono nono?

Ni vema Kinga ya kutoshtakiwa kwa Maraisi katika Katiba ijayo iwe na mipaka Ili kuleta uwajibikaji chanya kwa viongozi Hawa.
 
Back
Top Bottom