Kuna maeneo nchini miaka nenda rudi miundombinu ni mibovu, mamlaka hazioni? Mpaka maafa yatokee ndio wachukue hatua?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Kuna maeneo nchini yana miundombinu mobuvu miaka na miaka lakini serikali wala haichukui hatua. Unakuta barabara mbovu, madaraja yamebomoka nk, lakini ni kama hakuna anayeoona!

Ni kwamba wanasubiri maafa yatokee ndio wachukue hatua? Wanasubiri mpaka watu wafe ndio wachukulie malalamiko ya wananchi kwa uzito?

Mfano ni hili daraja linalounganisha mkoa wa Dar na Pwani eneo la Kibaha, hapa ni Kidimu B, daraja hili limevunjika zaidi muda mrefu zaidi ya miaka minne, kama unavyoona watoto wanavyovuka kwenda shule, fikiria wazee, wagonjwa na wajawazito wanavukaje eneo hili? Mtu amepata tatizo linahitaji uangalizi wa haraka si anakufa kabla hajafika upande mwingine? Serikali ipo kweli?

 
Kuna changamoto nyingi kibaha na hata mbunge toka uchaguzi hatujawahi kumuona
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom