Kilio cha Mlalahoi: Kupanda kwa bei ya umeme wanasiasa mko wapi?

Hapo una deni la zamani, hizo fixed amount, umeme ulionunuwa ni huo 2,676.72 tu.
Ndio maana nasema lazima wewe ni mama mchawi. Watu wanazungumzia maumivu wayapatayo Watz wewe unaleta upuu.zi wako hapa. Kwa taarifa yako sio kila anayezungumzia ugumu wa maisha kuwa naye anao bali watu wanawazungumzia watu kwa ujumla wao.
 
Facts ni facts na ahsante sana kwa hilo nami umenielimisha na wala sina tatizo huko.

Sasa unalalamika nini? umeme ndio umeshapenda. Kama unaona gharama zinazidi punguza matumizi ya umeme au vumbuwa umeme wako wa rahisi au kata matumizi mengine uende sambamba na mabadiliko hayo. Njia za kufanya nyingi badala ya kukaa kulalamika bila kutafuta ufumbuzi wa tatizo kama ni tatizo.

Kulalamika lalamika inasaidia nini? halafu umeme ukikatika-katika mnalalamika, zinapotakiwa pesa za ziada muwe na umeme wa uhakika mnalalamika.

Hizo shule mlizokwenda badala ya kuwafutia ujinga zimewaongezea ujinga.
Tangu Tanzania inapata uhuru kumeshakuwa umeme wa uhakika,unajua humu javini we ni kilaza sana sijui kama unajua unachoongea,total income ya mtanzania hailingani na hizo gharama na usifikiri anazalisha kulipia umeme tu,hivi navyoandika hapa wamekata umeme alafu unadai umeme wa uhakika,watu kama nyie ni makofi tu hamjui kwa nini mnaishi,unafikiri umekuja duniani kuigiza au mkishashikwa makalio uko Lumumba mnaropoka tu,mpuuzi kweli wewe...
 
Sasa ulitaka usilipe service charge? umeshafikiria gharama za usafiri na muda ulizopunguziwa kwenda kulipia bill yako TANESCO kila mwezi?

Ukiongeza bei ya umeme tu ume disturb bajeti ya kila mlala hoi!Nchi zenye wapiga kura wanaojielewa huwezi kuwaongezea bei za nishati wakakaa kimywa kama mitanzania!Kupanda kwa gharama za nishati kumeziondoa madarakani serikali nyingi tu duniani!

Nyumbani ilikuwa inatumika elfu 8000 kwa siku lkn kuanzia juzi imepanda hadi elfu 18!Ongezeko la elfu 10 kwa siku kwenye umeme tu haikubalik(ongezeko hili ni sawa na laki 3 kwa mwezi)i!Kodi ya simu pia imeongezeka na maji yamepanda mno!CCM ni janga!

Tunashinda hapa kujadili issue za ZItto na Lowassa zisizotusaidia lolote!Tukipaza sauti zetu hawa watawala wanaogopa!Tusikubali u p u u z i huu wa kutukamua sisi ili walipie madeni ya Songas na Richmons tena aliyesabisha haya kuna vijana hata hapa JF wanamshangilia!

Mitanzania tumerogwa
 
eura walikosea wangepiga 100% unajua wakuu hakuna nchi rahisi kuongoza kama Tanzania.
kuna mama alikuwa analalamika kwenye hiace nauli zilivyopanda 400 nikasema kwa nguvu kwanini wasingefanya 1000 ili na makonda wasipate shida ya chenji,mama alinicheki kwa hasiraaa.
nikamwambia ukiambiwa andamana utakubali?

Nimeipenda hii.

seriously, wengi wetu tunaamini hii equation: maandamano=vurugu=uvunjifu wa amani.:flame:
 
Mliacha ya msingi mkajadili migogoro ya chadema hiyo ndo zawadi ya krismasi na heri ya mwaka mpya kutoka serikali ya maccm
unaoneee wanatrick hawa,kula like mkuu ngoja tuendelee kukalia msumari wa moto wa inch sita
 
Ngoja watafute hela za kuilipa richmondi maana wananchi tumelala usingizi wa pono,kila kitu tunakubali kama mateja vile..aaah tz
 
ulipata zile t shirt za bodaboda alizogawa makamba jr mwanza?
yaani mi.aisee naipenda ccm kweli mara t shirt mara kofia mara khanga mara viji hela!
Hakuna kama ccm!!

Na sasa wanatoa pikipiki...
 
Tatizo la TZ , siasa inaongoza nchi badala nchi kuongoza siasa.Muhongo alipokabidhiwa wizara alisema kuanzia leo hakuna kukatika umeme , umeme utasambazwa kwa bei nafuu , bill za umeme zitashuka na TZ nzima itawaka umeme.Ushauri wa bure kama unataka tukuelewe ni lazima ukae meza moja ili ununue mitambo ya Symbion/Richmond na Aggreko inayoiuzia umeme Tanesco kwa bei ya juu wakati Tanesco inauzia walaji kwa bei ya chini pili jaribu kuepuka makampuni /Makandarassi wanaotoa huduma TANESCO kwa sababu wamilki ni wanatanesco,wana rea na wanaeura tatu dhibiti gharama za vifaa vya ujenzi wa Lines kwa sababu ni utapeli zaidi .Nne alaaniwe SITA na MWAKYEMBE waliosababisha nchi hii ilipe faini kwa kuvunja mkataba na Richmond iliyozaa Symbioni wakati wakijua kwamba kufanya hivyo ni kuingiza nchi hii katika janga kubwa kisheria.Kwa ukaidi wao na kujitafutia umaarufu twaumia hadi wajukuu zetu wajao.Tutawalaani kwa sababu katika kamati ya Bunge iliamua mtambo huo urudishwe ulipotoka ASP ni kwanini hawakulisimamia hilo handi Mama Clintoni anakuja kuuzindua baada ya miaka miwili baadaye.Mbona mlisema chakavu na sasa ndio mkombozi wa TANESCO?Tumegundua nyie mlikuwa na ugomvi kisiasa kumbe mafahali wawili wagombanao nyika huumia
 
Yaani wadanganyika ni kama kuku wa kienyeji.....mwenzao anakamatwa na chatu wote kwa umoja wanapiga kelele kwekwe... kwekwe... kwekwe..... kwekwe....wanatimka baada ya nusu saa wanarudi pale pale kwa kuchungulia kwa jicho moja baada ya saa moja wamejazana pale pale telee..bila wasiwasi...sasa basi mwanzoni mwa mwaka 2012 ghrarama za umeme zilipandishwa wadanganyika tukaambiwa hii ni dharura kwa miezi sita tuuu!! baada ya miezi sita gharama itashuka ...ikapita miezi sita hakuna hata aliyehoji vipi kulikono mbona gharama haishuki...na jamaa zetu nao hata hawakujisumbua kurudi kutoa mrejesho nyuma ni kwanini walitoa ahadi ya uongo kwa wadanganyika!!! Very funny wakatulia tuli baadaya ya mwaka wamerudi tena gharama mara sita zaidi ya ile ya mwaka mmoja nyuma....ndio sasa watu wanaona maumivu....kwanini wakati ule baada ya miezi sita kupita hakuna hata aliyehoji mbona ile gharama haishuki!!!? Tafakari chukua hatua
 
Kabla hujaanza kuniwasha kwanza kazime umeme wako unaoulalamikia. Halafu njoo ujaribu kuniwasha, angalia nisikuwashe wewe tu. Mimi nipo kwa sasa Lumumba na Udoe Ghorofa ya tatu apartment namba 301 na 302, na ntakuwepo mpaka Jumatatu, ukichelewa karibu sana shambani kwangu Mkuranga, hapa tutakufundisha namna ya kujipatia umeme mbadala wa gharama nafuu sana.

Tuna umeme wa jua (solar), tuna umeme wa upepo (wind mill), tuna umeme wa jenereta, tuna umeme wa mavi ya ng'ombe na binaadam na taka zote za nyumbani pia tuna umeme wa TANESCO. Huu wa TANESCO kwetu ni back-up tu, na hatujautumia leo miaka miwili.

Na hivi sasa mume wangu naona anafanyia modification jenereta letu ili liwe linatumia umeme wa gongo. Anasema hii mipapai tulionayo shambani inatosha kabisa kutupatia gongo la kuendeshea jenereta la KVA 100 bila wasi wasi kwa mwaka mzima na tutafaidika kuliko kuuza mapapai, Nnajuwa baada ya siku mbili tatu atakuwa kishalimaliza kwani ni mtundu sana kwenye mambo hayo.

Njoo ujifunze njia mbadala za kujipatia umeme wa gharama nafuu na pia tutakufunda namna ya ku-save umeme.

Funny. Kwa hiyo wewe ndiye uliyevumbuwa solar, wind mills, generator, na teknolojia ya kuzalisha umeme kwa mavi ya ng'ombe na binadamu? No wonder unaishi Lumumba na Mkuranga. And are you saying bei ya umeme imepandishwa ili kuwafanya watumiaji wapunguze matumizi? Already umeme ulikuwa ghali hata kabla ya nyongeza ya sasa. Au wamepandisha bei ili kumudu gharama za uendeshaji wa Tanesco? Are these two objectives one and the same? And do you think utaendesha mashine viwandani kwa umeme wa mavi ya ng'ombe? Unaelewa athari za kuongeza bei ya umeme kwenye mfumuko wa bei ya bidhaa sokoni? Au utashauri watu wale mlo mmoja? Na kutonunua bidhaa za viwandani? And what will be the impact on the economy as a whole? Or your selfish mind doesn't enable you to see beyond your household, Lumumba, and Mkuranga? Kwamba asiyeweza kumudu gharama za umeme awashe kibatari. Shauri yao, siyo? Kwa jamii yenye watu wanaojitambua, bei kubwa ya umeme ni sababu ya kutosha kuiangusha serikali iliyoko madarakani.
 
tatizo kama tumelogwa vile kila anayetaka umeme anawazia wa tenesco baadala wa jua,mchawi wao alituweza sana

Acha hizi...hebu nipe gharama za Installation ya umeme wa jua kwa mtu mwenye matumizi ya kawaida ya nyumbani ....yani yule mwenye, fridge, Pasi , TV na Radio tuu.....tupia gharama zake hapa halafu tuangalie ni watanzania wangapi wenye kipato cha kumiliki vitu nimetaja hapo juu wanaweza kufunga umeme wa jua majumbani kwao japo ni gharama kuu maramoja...bila ya mabenki kufungua mikopo ya aina hii ni wangapi wataweza!!!!!?
 
[h=3]Tariff Categories[/h]
Domestic Low Usage Tariff (D1)This category covers domestic customers who on average have a consumption pattern for 50 kWh. The 50 kwh are subsidized by company are not subjected to service charge. Under the category any unit exceeding 50 kwh is charged a higher rate up to 283.4 kWh. In this tariff category, power is supplied at a low voltage, single phase (230 V).
General usage Tariff (T1)This segment is applicable for customers who use power for general purposes: including residential, small commercial and light industrial use, public lighting, and billboards. In this category the average consumption is more 283.4 kWh per meter reading period. Power is given at low voltage single phase (230), as well as three phase (400V).
Low voltage maximum Demand (MD) usage tariff (T2)Applicable for general use where power is metered at 400V and average consumption is more than 7,500kWh per meter reading period and demand doesn't exceed 500KVA per meter reading period.
High Voltage Maximum Demand (MD) usage tariff (T3).Applicable for general use where power is metered at 11KV and above.

Sasa hiyo fixed rate/amount ambayo haihusiani na umeme unaotumia iko wapi? Na ni shilling ngapi? Au ndiyo umeanza kuhamisha goli (which you are very good at. Btw, you are a fox.)?
 
Naona hawa jamaa wa serikali wamueamu liledeni lao wanalo daiwa na tanesko bil 400 tuwalipie kwa style hiyo, we unadhani wange wezaje kuikatalia tanesko ombi la kupandisha umeme wakati wanafahamu wazi kwamba tasisi zao zinadeni, tanesko wameamua kuitumia hiyo nafasi kujipandishia gharama za umeme kama wanavyo taka wao, usitegemee hapo serikali itapaza, sauti, na bado huo hautakuwa mwisho wa maumivu kweli tunavumilia kuwa watz lakini hatufurahii kuwa watz.
 
Funny. Kwa hiyo wewe ndiye uliyevumbuwa solar, wind mills, generator, na teknolojia ya kuzalisha umeme kwa mavi ya ng'ombe na binadamu? No wonder unaishi Lumumba na Mkuranga. And are you saying bei ya umeme imepandishwa ili kuwafanya watumiaji wapunguze matumizi? Already umeme ulikuwa ghali hata kabla ya nyongeza ya sasa. Au wamepandisha bei ili kumudu gharama za uendeshaji wa Tanesco? Are these two objectives one and the same? And do you think utaendesha mashine viwandani kwa umeme wa mavi ya ng'ombe? Unaelewa athari za kuongeza bei ya umeme kwenye mfumuko wa bei ya bidhaa sokoni? Au utashauri watu wale mlo mmoja? Na kutonunua bidhaa za viwandani? And what will be the impact on the economy as a whole? Or your selfish mind doesn't enable you to see beyond your household, Lumumba, and Mkuranga? Kwamba asiyeweza kumudu gharama za umeme awashe kibatari. Shauri yao, siyo? Kwa jamii yenye watu wanaojitambua, bei kubwa ya umeme ni sababu ya kutosha kuiangusha serikali iliyoko madarakani.

Amma katika watu finyu wewe umetia fora.

Pole sana naona shule uliokwenda imekujaza ujinga badala ya kukufungua. Ikiwa Watanzania walio wengi ndio mawazo yao namna hiyo, tuna kazi kweli kweli.

Wewe jiulize, iweje wewe ushindwe kulipa wengine waweze? ni kilema wewe si bure, tena cha akili.
 
Tangu Tanzania inapata uhuru kumeshakuwa umeme wa uhakika,unajua humu javini we ni kilaza sana sijui kama unajua unachoongea,total income ya mtanzania hailingani na hizo gharama na usifikiri anazalisha kulipia umeme tu,hivi navyoandika hapa wamekata umeme alafu unadai umeme wa uhakika,watu kama nyie ni makofi tu hamjui kwa nini mnaishi,unafikiri umekuja duniani kuigiza au mkishashikwa makalio uko Lumumba mnaropoka tu,mpuuzi kweli wewe...

Kwa mara ya kwanza tunaona Tanzania miradi ya megawati 3,000 ikiwa mbioni kutekelezwa. Kwa mara ya kwanza umeme umesambazwa kwa asimia 24 ya Watanzania. Kikwete wakati anachukuwa nchi kulikuwa giza totoroooo, au ulikuwa haupo?

Wewe unaejuwa kwanini unaishi ungelalamika? maendeleo mnayataka kuchangia hamtaki. Punguza bajeti ya gongo ununuwe umeme wacha kulalamika.

Wewe inaonesha unafikiri kuishi ni kusaidiwa na kufanyiwa tu? punguani wa ajabu wewe. Fanya, wacha kulalamika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom