Mkuu ni kweli kabisa unachosema ni kuwa watu hawajajua tu mim nimegusa tu kidogo mwaka jana nimeondoka na mil 3 sasa nataka mwaka huu ndiyo nizame ki kwel kwel, maana kupata gunia 100 kwa kitunguu ni kugusa halafu kuna kipind kama sasa gunia moja laki ×100 una 10milion hapo bado hujatoka tu kimaisha kwa mtaj wa 10 mil wakat wewe garama uliyotumia haizid mil 2 lakin kwa muda mfup unatengeneza faida ya mil 8 Mungu akupe nin tena. Mkuu komaa tu mim ninao mfano kuna watu walianza na mtaj wa laki kadhaa kwenye kilimo cha vitunguu lakin sasa ni matajiri wa kutupwa had unakuja kufikiria kuajiriwa hakuna dili kabisa kwa mtu anaezingatia kilimo
Dodoma moja kaka napenda nipate no yako
 
Safi sna mkuu,

Haya ndio mawazo tunataka hapa JF,

Kuna technolojia mpya na rahisi mno nimeinyaka sehemu juu ya huu ulimaji bado naimalizia resecrh yake nafikiri baada ya miezi sita itakua imekamilika nitaimwaga hapa jamvini.

Kifupi inawezekana kabisa kuchagua ukubwa wa kitunguu chako, kukuza ndani ya miezi miwili tu na kuchangua shape ya kitunguu.

Hii nikiikamilisha nitaileta hapa maana nafikiria kuteka soko lote la Comorro, Kenya na Zanzibar kwa vitunguu bora kabisa na vya bei nafuu na hakuna atakaye shindana na mie.

Mkuu no yko n pm plz
 
Kilimo cha vitunguu naona wengi wapo msibani. Teh teh teh.... Hii balaa. Naona wengine wameapa kuto lima tena.
 
Kilimo cha vitunguu naona wengi wapo msibani. Teh teh teh.... Hii balaa. Naona wengine wameapa kuto lima tena.

Naona mwaka huu umegeuka ghafla kuwa mbaya Kwa wakulima wengi wa vitunguu.

Huwezi kuamaini mtu anakuja shambani anataka anunue lumbesa ya madebe 8 Kwa elfu 40 ili hali unaona sokoni debe moja ni Tshs. 20,000 Kwa uchache. Hivyo anapata 160,000 Kwa gunia ukiondoa gharama zake za usafiri, magunia upakiaji na upakuaji anapiga si chini ya laki Kwa gunia kama faida, mbaya sana hii.

Vya kwangu nauza rejareja sasa na naanza kutafuta wenye vigenge niwapelekee, hii najua itanitoa tu. Ila kiukweli huko nilikolimia sitakaa nilime vitunguu huko tena. Gharama kubwa sana na mavuno ni kidogo.

Labda naweza kujaribu kwingineko kama Iringa au Mbeya.
 
Naona mwaka huu umegeuka ghafla kuwa mbaya Kwa wakulima wengi wa vitunguu. Huwezi kuamaini mtu anakuja shambani anataka anunue lumbesa ya madebe 8 Kwa elfu 40 ili hali unaona sokoni debe moja ni Tshs. 20,000 Kwa uchache. Hivyo anapata 160,000 Kwa gunia ukiondoa gharama zake za usafiri, magunia upakiaji na upakuaji anapiga si chini ya laki Kwa gunia kama faida, mbaya sana hii. Vya kwangu nauza rejareja sasa na naanza kutafuta wenye vigenge niwapelekee, hii najua itanitoa tu. Ila kiukweli huko nilikolimia sitakaa nilime vitunguu huko tena. Gharama kubwa sana na mavuno ni kidogo. Labda naweza kujaribu kwingineko kama Iringa au Mbeya.

Pole ndugu yangu. Mimi mwenyewe hapa nimepoteza gunia kama 47 hivi. Vitunguu nilivyovihifadhi vimeota karibu vyote. Lakini sijakata tamaa. Waliokuwa mstari wa mbele kuhamasisha watu walime vitunguu wote wametokomea pori.
 
Kilimo cha vitunguu kinahitaji maarifa sana aisee, mimi mwenyewe hapa hofu yangu ni soko, bei inatisha.
 
Pole ndugu yangu. Mimi mwenyewe hapa nimepoteza gunia kama 47 hivi. Vitunguu nilivyovihifadhi vimeota karibu vyote. Lakini sijakata tamaa. Waliokuwa mstari wa mbele kuhamasisha watu walime vitunguu wote wametokomea pori.

Aisee, pole rafiki. Vimeota sababu ya unyevu? Ulivihifadhi wapi (mkoa gani) na kwenye banda au? Vya kwangu vina karibu mwezi sasa kwenye banda. Navigeuza na kuvichambua kutoa vilivyooza. Kuanzia asubuhi nafungua mlango wa banda ambao ni mkubwa kurusuhu hewa ipite Kwa wingi ili vikauke vizuri zaidi.

Ni kweli hata mimi jamaa aliyenivutia kwenda kulima kule aliniambia ekari moja naweza vuna gunia 60 Kwa uchache na hadi 100 kama nimevitunza vizuri, kumbe wapiiiii?

Nimevitunza na nimeambulia gunia 30 Kwa eka. Sijuwi Kwa upande wako mavuno yalikuwaje Kwa ekari.
 
Aisee, pole rafiki. Vimeota sababu ya unyevu? Ulivihifadhi wapi (mkoa gani) na kwenye banda au? Vya kwangu vina karibu mwezi sasa kwenye banda. Navigeuza na kuvichambua kutoa vilivyooza. Kuanzia asubuhi nafungua mlango wa banda ambao ni mkubwa kurusuhu hewa ipite Kwa wingi ili vikauke vizuri zaidi. Ni kweli hata mimi jamaa aliyenivutia kwenda kulima kule aliniambia ekari moja naweza vuna gunia 60 Kwa uchache na hadi 100 kama nimevitunza vizuri, kumbe wapiiiii? Nimevitunza na nimeambulia gunia 30 Kwa eka. Sijuwi Kwa upande wako mavuno yalikuwaje Kwa ekari.

Hayo mavuno wanayoyasema kuyafikia ni shughuli pevu. Mimi ekari ya kwanza nilivuna kama gunia 40. Ya pili ilikuwa moja na nusu nilivuna kama 47. Nilivihifadhi kwenye chumba cha wazi. ilikuwa shughuli pevu.
 
Mimi pia nimeingia katka kilimo hiki cha vituguu na kwasasa nimemwanga mbengu na wiki ijayo ntaanza kupanda, nimeandaa heka tano hivi ambazo naanza nazo.

Kama itanilipa ntapanua zaidi ingawa garama yake ni kubwa sn, nko nakima Moshi.

Asanteni wadau kwa kututia moyo aisee
 
Hatimaye bei ya vitunguu imepanda mara dufu Dar es Salaam. Gunia sasa ni Tshs. 110,000 hadi 130,000. Mliofanikiwa kutunza kama mimi tupige pesa sasa.
 
Mkuu mwenye mtaji wa mil 1,5 anitafute mm nimfanyakazi serikalini na nipo kwa wakulima zaidi twaweza fanya kitu ni pm, nb nipo mashambani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom