kwenye website ya kenyan seed wameweka hizi taarifa. inawezekana watu mavuno yanatofautiana sababu ya aina ya kitunguu unacholima. pia mtu anaweza sema kalima eka kumbe nusu. eka hauwezi kuipima kwa macho hata siku moja. nina 2.2 acres nataka nijaribu hiki kilimo mwezi wa saba.
Variety
Planting spacing (cm)
Maturity in days
Average yield/acre in kg
Ideal climate
Special attributes
Red Passion F1​
30 x 10/ 30 x 5​
120​
25,000​
Cool and wet​

  • Deep red hybrid onion
  • Very good drying and keeping quality
  • Tolerant to pink rot diseases
  • Produce good onions
  • Uniform maturity
  • Easy manage
  • Can store for upto 6 months
Red Creole​
30 x 10/ 30 x 5​
150-180​
10,000​
Warm and hot​

  • Attractive shaped red onion
  • Good storage qualities
  • Tolerant to Pink rot disease
  • Easy to manage
Bombay Red​
30 x 10/30 x 5​
120-150​
6,000-7,000​
Warm and hot​

  • Globular shaped deep red onion
  • Provides good grade onions
  • Dries well
  • Widely grown
Texas Grano​
30 x 10/30 x 5​
150​
12,000​
Cool and warm​

  • The ideal ‘grano’ type onion
  • Straw coloured outer skin and white inner flesh
  • Mild tasting. Ideal for salads
  • Easy to grow and widely adapted
 
hiyo red passion f1 inaonekana ni noma. wanasema average kwa acre ni kilo 25,000! wakati red bombay ni kilo 7,000 na creole 10,000.
 
kiukweli waliokuwa wanatushawishi kulima niwaongo, ni vigumu kupata hizo gunia 100 wastan ni gunia 40. pia nimeamin wengi wao nahisi niwafanyakaz wa maeneo hayo kwa hiyo wanakuwa wanakupiga kwenye mbegu. mimi mwaka jana nimejaribu ila nilikuwa tofauti na wenzangu mimi nilinunua lita moja tu za mbegu. kiukweli ni mbegu nyingi sana kwa ufupi wasiozijua ni vimbegu vyenyewe ni saiz ya mbegu ya nyanya . na baada ya kuzihudumia nilifanikiwa kupanda zote na chache zilibaki, pia sikutaka kubana sana kama wengi wetu wanavyoshauri humu eti size ya kiberiti.
kuhusu dawa mara nyingi nilipulizia dawa ya kuzuia wadudu tu tena mara moja kwa wiki kopo nilikuwa nanunua buku tano mpaka navuna nilitumia kopo kumi ambayo total ilikuwa 50000.
mbolea kwetu huku zipo za kununua mchanganyiko ila mimi nilinunua mfuko mmoja mmoja kwa kila mbolea na bei zake kwa mbeya ni
urea 48000
can48000
npk nilikuwa nanunua ya unga inauzwa 5000 na kila baada ya siku 14
sa 45000
uchumi haukuwa mzuri sikununua dap
kuandaa kitalu mpaka kupandikiza jumla ya matumizi ilikuwa35000 na mimk mwenyewe nilikuwa nashiriki.
nilivuna jumla gunia25 kwa eka moja.
NILICHOJIFUNZA
watu wanadanywa kuhusiana mbegu hivo wanajikuta wananunua mbegu nyingi na kumwaga shamban. hata wakati wakupandikiza vitunguu vinabanwa sana hivyo mbegu nyingi inakufa au mkulima anajikuta anapata vitunguu vidogovidogo vingi sana badala ya vile vya wastan. pia mbolea inatakiwa iwekwe kila baada ya siku ishirini na moja na ingependeza upandikize kwa mstari hata wakat wa kumwaga mbolea ufuatishe mstari badala ya kumwaga ovy sabab ukimwaga onyo wakati wakumwagilia mbolea inaweza sombwa na kujikuta ni sehem moja ndo imenawili tena kwa muono wangu ni vyema kupitisha mstari wa kishimo pembeni ya mstari wa vitunguu na uksha mwaga ufukie.
kwa ushauri wangu ni vyema kama ndo unaanza ushiriki mwenye kwa usaidiz wa wafanyakazi kuna uongo mwingi sana unaenezwa ambao ndo unawaliza wengi humu. mtu anakwambia unahukika wa kuvuna gunia 100. wadau gunia linalozungumzwa hapa sio kilo mia ni debe nane ambalo si chini ya kg 130 sasa hata ukiingia kenyanseed.com hizo mbegu za red bombay na redcreole wamekadilia kg 10000 per hectare ambazo ni acre 2.5 pia kitunguu kwa jinsi nilivoona ukijitoa mwenyewe kwa usimamizi mzuri hupaswi kufikisha gharama ya milion. pia tusikariri maeneo mfano lumuma wenyeji washakuwa matapeli wanapokuona mgeni wenyewe wanachofikiria ni kukukamua tu. pamoja na kuwa bei haikuwa nzuri lakini nashukuru gharama yangu ilirudi na faida pia. twenden shamban lakini kabla ya yote tutafute information bila kukurupuka. love you all. sikuwahi kulima ila mwaka huu mungu bariki ntalima kila kitu mpaka nyanya
jamaa wamekadiria 10,000kg kwa ekari na si hekta. utaona kwa gunia za 100kg gunia 100 zinafika. kumbuka hiyo ni average.
 
unapanga kulimia wapi mkuu?
 
Aisee hongera sana mossad007.
Mimi binafsi nalima kitunguu ndo nimeanza mwaka huu 2015 maeneo ya mtandika ndani huko kuna kijiji kinaitwa nyanzwa.

Evaluation uliyoitoa ipo sahihi kabisa. binafsi nimekutana na changamoto kama. umbali maana kutoka barabarani mpaka huko kijijini ni kama 45km. na hamna usafiri reliable. lipo tuu gari la kijiji ambalo huondoka saa 11 asubuhi kijijini na hurudi saa 11 jioni.

pia ni sehem ambayo hamna network wala umeme wa tanesco.
pia nafanya remote monitoring ivyo kwa huo umbali usimamizi sio mkubwa sana ila nashukuru MUNGU nina watu wa kuaminika katika hili. cha muhimu tuu ni umakini wa kitunguu mwanzo mpaka mwisho.

Plan yangu ni kusogea barabarani msim ujao maana maeneo kama ruaha mbuyuni mashamba hayapo mbali na barabara kiasi ambacho inakuwa rahisi kufanya usimamizi.
ndugu yangu massod007 naomba uni PM nipate namba yako kwa msaada zaidi.

pia mwenye kufaham wapi kinalimwa kitunguu swaumu anitaarifu.
thanks much
 
Nimesoma views na mimi nimefaidika sana. shukrani wote.

Mimi pia nipo dar heb malila naomba uni PM nijue mnakutana wapi na lini.
Vile vile natafuta sehemu wanazolima vitunguu swaumu nikafanye survey. mimi binafsi pia nalima vitunguu maji maeneo ya mtandika mbele ya Aljazeera. kijiji kinaitwa NYANZWA.

tatizo sema ni mbali na barabarani ila kitunguu kinatoka vizuri tuu na kule.
 
wakuu najua mada ni vitunguu, ila nahitaji msaada kuhusu kilimo cha matango, mwenye experience ama ushauri naomba tuongee nambari 0717584992, nataka kulima Mlandizi, Pwani.
 
Kama wewe ni mkulima na unafanya kilimo jiunge nasi wakulima wenzako 0717269137 whatsapp
 
Ungekua uko dar ingekua rahisi kwangu kukuelekeza, ila hakuna shida nenda hata SIDO hapo mbeya watakusaidia. Unawaambia unataka pump ya inch nne na inayotumia diesel. Manake kama wananchi wanaweza isuka basi kwa sido sio tatizo kabisa.
Mkuu niko DSM nazipata wapi pump za kusukwa
 
Wakuu habarini! nipo Dar kwa yeyote mwenye kufahamu wanapouza pembejeo za kilimo kama vile madawa,mbolea n.k kwa bei ya jumla.
 
Naomba kujuzwa gharama za kilimo cha vitunguu kwa heka moja wadau, kwa Iringa na Kilimanjaro

Nawasilisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom