Pus dawa za kuulia wadudu waharibifu! sina uhakika ni shiling ngapi!

Pia gharama za kumwagilia (Mashine ya kumwagilia) au mtu wa kumwagilia hasa kama utalima wakati wa kiangazi
Watu wa kungoa vitunguu na kukata majani yake pale vitunguu vinapokuwa tayari.

Na gharama nyingine ndogo ndogo za hapa na pale

Kwa hiyo ukiwa na at least million moja unaweza kulima bila usumbufu!
 
Aisee hongera sana mossad007.
Mimi binafsi nalima kitunguu ndo nimeanza mwaka huu 2015 maeneo ya mtandika ndani huko kuna kijiji kinaitwa nyanzwa. Evaluation uliyoitoa ipo sahihi kabisa. binafsi nimekutana na changamoto kama. umbali maana kutoka barabarani mpaka huko kijijini ni kama 45km. na hamna usafiri reliable. lipo tuu gari la kijiji ambalo huondoka saa 11 asubuhi kijijini na hurudi saa 11 jioni.
pia ni sehem ambayo hamna network wala umeme wa tanesco.
pia nafanya remote monitoring ivyo kwa huo umbali usimamizi sio mkubwa sana ila nashukuru MUNGU nina watu wa kuaminika katika hili. cha muhimu tuu ni umakini wa kitunguu mwanzo mpaka mwisho.
Plan yangu ni kusogea barabarani msim ujao maana maeneo kama ruaha mbuyuni mashamba hayapo mbali na barabara kiasi ambacho inakuwa rahisi kufanya usimamizi.
ndugu yangu massod007 naomba uni PM nipate namba yako kwa msaada zaidi.
pia mwenye kufaham wapi kinalimwa kitunguu swaumu anitaarifu.
thanks much

Hi mkuu.. ardhi ilifanikiwa kukupatia mavuno?? Nijongee tuwe pamoja
 
Je ni mtaji kiasi gani wafaa kuanza biashara ya kununua na kuuza vitunguu, wenye experience please
 
Wakuu hongereni kwa jitihada zenu za kupambana na maisha na michango mnayotoa kwenye hili jukwaa...je kuna mtu anayefanya kilimo cha vitunguu kwa maeneo ya karibu Dodoma mjini..kama yupo basi tujuzane ili nipate furusa ya kufahamu ni maeneo gani yaliyo karibu na dodoma mjini hiki kilimo cha vitunguu kinafanyika..

Ahsanteni.
 
Habari zenu wadau nahitaji kuanzisha mradi wa kulima vitunguu swaumu.... naweza kuzipata wapi mbegu za vitunguu swaumu maana nimehangaika sanaa kuzitafta katka maduka ya pembejeo lakin nimeambulia patupu nahtaji msaada wenu wana jamvi
 
Habarini, nililima kitunguu msimu wa mvua 2014/15 nilikumbana na changamoto ya pacha nyingi nilipanda red creole pia dawa ya magugu haikunisaidia. Mwenye uzoefu naomba msaada
 
Nimeipenda hii topic nitaifanyia kazi kwa eneo nilipo nione majibu yake. Ahsante kwa mliochangia - Joseph ahsante kwa mchango wako
 
mossad007 naomba uni PM namba yako. mimi binafsi nililima Nyanzwa msimu huu ulioisha. nimejifunza mengi na kupata changamoto nyingi sana. kwa sasa plan ni kulima tena lakini nataka nisogee barabarani. wiki iliyopita nilienda kufanya survey ruaha mbuyuni , msosa na kware. nilipapenda sana kware ila sikubahatika kupata eneo kwa sasa. nilianza kidogo ila nina mpango wa ku expand zaid na zaid.
 
Milioni moja?
Inategemea unalimia wapi?
Inategemea umwagiliaji kwa pampu au mifereji au mvua
Uzoefu wangu huku Kilosa huu:
Mbegu lita 7 kwa ekari @ 25,000/= jumla 175,000/=
Kuandaa kitalu 20,000/=
Kusia mbegu 10,000/=
kutunza kitalu 30,000/=
kukodi shamba 100,000/=
kufyeka shamba 48,000/=
kukatua udongo 64,000/=
kulainisha udongo 48,000/=
kutengeneza majaruba 25,000/=
kupandikiza 160,000/=
dawa ya kuua magugu 40,000/=
palizi mara mbili 100,000/=
Mbolea mifuko mitatu 210,000/=
Mtu wa kuweka mbolea mara mbili 10,000/=
madawa kuua wadudu na magonjwa 50,000/=
mpiga dawa wiki kumi 50,000/=
kung'oa 50,000/=
kukata vitunguu gunia mia 200,000/=
usafiri 100,000/=
chanja kukodi 100,0000
umwagiliaji petrol 2500 x lita 5 x wiki 10 = 125,000/=
mtu wa kumwagilia 5000 x wiki 10 = 50,000
JUMLA KUU = 1,855,000/=

Kwa wastani ni mil 2
 
Kama wewe ni mkulima na unafanya kilimo jiunge nasi wakulima wenzako 0717269137


kama kawaida yako kuacha contacts kila mahali ukiombwa kuadd watu unapozi nyingi sikupendi hata kidogo unarudisha nyuma watanzania wenzako
 
Milioni moja?
Inategemea unalimia wapi?
Inategemea umwagiliaji kwa pampu au mifereji au mvua
Uzoefu wangu huku Kilosa huu:
Mbegu lita 7 kwa ekari @ 25,000/= jumla 175,000/=
Kuandaa kitalu 20,000/=
Kusia mbegu 10,000/=
kutunza kitalu 30,000/=
kukodi shamba 100,000/=
kufyeka shamba 48,000/=
kukatua udongo 64,000/=
kulainisha udongo 48,000/=
kutengeneza majaruba 25,000/=
kupandikiza 160,000/=
dawa ya kuua magugu 40,000/=
palizi mara mbili 100,000/=
Mbolea mifuko mitatu 210,000/=
Mtu wa kuweka mbolea mara mbili 10,000/=
madawa kuua wadudu na magonjwa 50,000/=
mpiga dawa wiki kumi 50,000/=
kung'oa 50,000/=
kukata vitunguu gunia mia 200,000/=
usafiri 100,000/=
chanja kukodi 100,0000
umwagiliaji petrol 2500 x lita 5 x wiki 10 = 125,000/=
mtu wa kumwagilia 5000 x wiki 10 = 50,000
JUMLA KUU = 1,855,000/=

Kwa wastani ni mil 2
Mkuu kubota,je hii petrol unamwagilia vipi?na je muda muafaka kulima kwa kilo na ni miezi gani na vinachukua muda gani kukomaa??ahsante
 
Milioni moja?
Inategemea unalimia wapi?
Inategemea umwagiliaji kwa pampu au mifereji au mvua
Uzoefu wangu huku Kilosa huu:
Mbegu lita 7 kwa ekari @ 25,000/= jumla 175,000/=
Kuandaa kitalu 20,000/=
Kusia mbegu 10,000/=
kutunza kitalu 30,000/=
kukodi shamba 100,000/=
kufyeka shamba 48,000/=
kukatua udongo 64,000/=
kulainisha udongo 48,000/=
kutengeneza majaruba 25,000/=
kupandikiza 160,000/=
dawa ya kuua magugu 40,000/=
palizi mara mbili 100,000/=
Mbolea mifuko mitatu 210,000/=
Mtu wa kuweka mbolea mara mbili 10,000/=
madawa kuua wadudu na magonjwa 50,000/=
mpiga dawa wiki kumi 50,000/=
kung'oa 50,000/=
kukata vitunguu gunia mia 200,000/=
usafiri 100,000/=
chanja kukodi 100,0000
umwagiliaji petrol 2500 x lita 5 x wiki 10 = 125,000/=
mtu wa kumwagilia 5000 x wiki 10 = 50,000
JUMLA KUU = 1,855,000/=

Kwa wastani ni mil 2

Duh kumbe shughuli ipo. Hujaweka usafiri wako wakwenda shambani mpaka mavuno
Na ukifqnikiwa unapata she ngapi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom