hiyo ni gharama ya kila kitu ikiwa ni pamoja na pump na mafuta utaweza hudumia heka moja na vitunguu hukaa shambani miezi mitatu tuu unatoa almasi yako swafiii na mteja uakuwa hapo shambani.

Wewe unalima wapi ndugu?
 
mimi nimejaribu mbeya kusema kweli hapa makadirio ya gharama inategemeana na eneo ila mimi mpaka jana nimemaliza kupandikiza gharama niliyoitumia imekuwa ndogo sana tofauti nilivyotarajia almost nusu ya makadirio ya hapa. mungu akijalia kama mazao yakikubali mwakan najiingiza ini full walau kwa heka 50. nawashukuru sana hasa Malila for contribution.

Mchakato unakwendaje?
 
Jamani kilimo ukikipatia kinakutoa. Sasa najipanga kulima vitunguu na nikitoa naweza pilipili hoho na nyanya chungu. Wakati huo huo nafanya machakato wa kulima mananasi na mihogo Fukayosi.

Tuombeane uzima na afya njema tujikwamue wadau.
 
Naona nondo za hatari sana humu,mpaka kichwa kina waka moto.Inafariji kwa kweli kuona vijana wakichakalika na zaidi wakiungana pamoja kufanya projects mossad007, Kubota na Malila mnaonekana kuwa na uzoefu sana wa kilimo,binafsi nimependa kitendo cha kujiunga pamoja na moyo wenu wa kujitolea kutoa taarifa.

Ila nina mambo makuu mawili ambayo nafikiri yatasaidia wengi
1) humu jukwaani kumekuwa na taarifa nyingi za kilimo,mfano ni hii thread ya vitunguu.Lakini hamna sehemu ambayo mmeelezea kuhusu soko,kwa maana ya kwamba hizo sehemu mlizozitaja kuwa kitunguu kina Stawi vizuri wanunuzi huwa wanakuja mpaka shambani au inabidi kusafirisha mpaka sokoni,na soko lake lipo wapi hasa

2. Taarifa zimekuwa nyingi mno maana kila mtu anachangia kwa wakati wake,hivyo hakuna mtiririko sahihi.Mimi nilikuwa nawaomba mkuu Malila na wenzako mliojiunga pamoja na wadau wengine mfanye mpango mtengeneze thread moja ambayo itatoa details kwa mtiririko mzuri kuanzia maandalizi,kupanda,kuvuna mpaka mategemeo ya soko,na pia mnapo kutana kwenye vikao au mnapoanza project fulani mtupe taarifa.Hili linaweza kuwa ni ombi lenye usumbufu kwenu lakini mkiona lipo ndani ya uwezo wenu basi mtusaidie wadau. Mnaweza kuanzisha group la whatsap ili iwe rahisi kufikisha taarifa.

Binafsi sipo kwenye position ya kuanza kilimo kwa sasa ila taarifa ni muhimu sana kwangu maana nategemea kuingia kwenye kilimo siku za usoni kwahiyo nahitaji taarifa nyingi iwezekanyo toka kwa wazoefu
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wanajamvi habari mimi mwenzenu napenda sana kutekeleza sera hii ya kilimo kwanza je vitunguu vinaweza kustawi katka hali ya hewa ip?

Na je kilimo bora cha kisasa chaweza pelekea uzalishaji wa gunia ngapi? Na soko je......? Ni hayo
 
Kuna suali humu sajaona majibu yake na nalirudia tena kwa wadau wazoefu 'je maeneo ya Kibaha kilimo cha vitunguu kinakubali? Maji yanapatikana na ardhi yake ni ya kichanga kiasi (haituamishi maji) naomba msaada.
 
Mi ndo navuna jamani!
ImageUploadedByJamiiForums1405569763.062062.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1405569830.199511.jpg



Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Mkuu unavunia wapi? Vyangu vipo tayari hapa ruaha mbuyuni lakini soko ni majanga!

anayevuna ni LACHERO mkuu, mimi nilikuwa namuuliza swali nimeona kama alikuwa anamwagilia kwa drip. ruaha mbuyuni wanannuaje sasa hivi? au hakuna kabisa wanunuzi?
 
Last edited by a moderator:
Niko iringa mjini ila nimelima maeneo ya viwengi mbele kidogo ya chekpoint! Bei kweli ni majsnga kwa vile sina store nimeuza 2000 per kg


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Ni kweli nimetumia drip ila mvua nayo inilipiga tafu sana


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Mkuu samahani naomba kujua heka moja kwa Mang'ola kutengeneza jaruba 200 pamoja na kuipanda miche gharama inakua ngapi kwa vibarua wa hapo?

Nimethubutu mwaka huu mwezi jana nimeotesha mbegu na imeota vizur na jana tu ndo wananiambia natakiwa niandae sh 440,000 kwa vijaluba 200@1200/=(kuvitengeneza)
na 1000/=(kuotesha)so hii gharama ndiyo yenyewe kulingana na mazingira ya huko au la?

Naombeni michango yenu
 
Huenda ikiwa sawa,Kwa Moshi jaluba la 2m by 8m ni 800 kutengeza na huwa 210 kwa ekari moja na kupanda ni bei hiyo hiyo..........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom