Mkuu nataka kopo 10 kwanza za kujaribu. But nimekutumia meseji kwenye simu haijafika, ile namba pale juu ni sahihi?

Mbegu kwa sasa me nimeishiwa, ntaanza kuuza tena mwezi wa 11. Namba hiyo ni sahihi ila ukiona sipatikan nakua niko shamban kidogo mtandao unasumbua.
 
mkuu ninampango wakununua water pup,ila sijajua ipi ni bora na kwa garama ipi?kwa shamba la hekari 1-2.pia vipi maji yakisima chakuchimba yanaweza yakafaa..naomb unisaidie kaka.
Water pump nakushauri utafute zile za kusukwa na mafundi, huwa zinauzwa kuanzia laki 9 ila huwa ni imara na inavuta maji mengi sana, ndan ya saa moja unakua ushamwagia eneo la ekari moja. Ila hizi za madukan za laki 3 hazifai kwa kilimo serious.
 
Mbegu kwa sasa me nimeishiwa, ntaanza kuuza tena mwezi wa 11. Namba hiyo ni sahihi ila ukiona sipatikan nakua niko shamban kidogo mtandao unasumbua.

Nimekutumia pia email baada ya kuona SMS haiingii.

Pili msimu wa kilimo cha vitunguu ni kuanzia mwezi gani? Maana Nilitaka nifanye the soonest it could be.
 
Nimekutumia pia email baada ya kuona SMS haiingii.

Pili msimu wa kilimo cha vitunguu ni kuanzia mwezi gani? Maana Nilitaka nifanye the soonest it could be.

Kwa sasa umelate kaka manake tayari watu wako mashamban ma mazao wanakaribia kuanza kuvuna. Msimu mzuri ni wa kumwaga mbegu mwezi wa 3 na kuvuna wa 7
 
Kwa sasa umelate kaka manake tayari watu wako mashamban ma mazao wanakaribia kuanza kuvuna. Msimu mzuri ni wa kumwaga mbegu mwezi wa 3 na kuvuna wa 7

Ahsante sana Mkuu,

Sababu nataka kulima mwaka mzima (mzunguko), kwa sasa ni kilimo gani ndio kinaanza?
Pia una mbegu za kitunguu tu?
Huna za mazao mengine?
 
Water pump nakushauri utafute zile za kusukwa na mafundi, huwa zinauzwa kuanzia laki 9 ila huwa ni imara na inavuta maji mengi sana, ndan ya saa moja unakua ushamwagia eneo la ekari moja. Ila hizi za madukan za laki 3 hazifai kwa kilimo serious.

Nakushukuru kaka..naomba uniongeze ninakoweza kuzipata.mi niko Mbeya..samahan kw usumbufu mkuu.
 
Nakushukuru kaka..naomba uniongeze ninakoweza kuzipata.mi niko Mbeya..samahan kw usumbufu mkuu.

Ungekua uko dar ingekua rahisi kwangu kukuelekeza, ila hakuna shida nenda hata SIDO hapo mbeya watakusaidia. Unawaambia unataka pump ya inch nne na inayotumia diesel. Manake kama wananchi wanaweza isuka basi kwa sido sio tatizo kabisa.
 
Ahsante sana Mkuu,

Sababu nataka kulima mwaka mzima (mzunguko), kwa sasa ni kilimo gani ndio kinaanza?
Pia una mbegu za kitunguu tu?
Huna za mazao mengine?

Mimi najihusisha na kilimo cha vitunguu, ufugaji wa nyuki wa kisasa na nyanya F1 tu. Msaada wangu mbadala ntakupa kwa hayo mazingira mengine.
 
Ungekua uko dar ingekua rahisi kwangu kukuelekeza, ila hakuna shida nenda hata SIDO hapo mbeya watakusaidia. Unawaambia unataka pump ya inch nne na inayotumia diesel. Manake kama wananchi wanaweza isuka basi kwa sido sio tatizo kabisa.

pamoja sana kaka..Mungu akufungulie makubwa zaidi na ubarikiwe kwa moyo wako mkunjufu..
 
kitunguu kinataka mazingira ya aina gani nina shamba kubwa "marangu" na mto unaopita pembeni je mkoa huu wa kilimanjaro vitunguu vinaweza kustawi?
 
Salama mkuu, huwa navuna miezi hiyo pia ila huwa ni maalumu kwa storage na sio kuuza manake bei yake huwa ndogo sana, kwa shamba huwa gunia linarange 45 - 55. Me vitunguu vya biashara huwa napanda mwezi wa tatu na kuvuna wasaba katikati.

Ukivuna mwezi wa 10 unaweza kuvi-store hadi mwezi wa ngapi kwenye bei? Mwezi wa saba ndo bei huwa nzuri zaidi? Nimeona mwezi wa 4 Kariakoo gunia lilikuwa linauzwa Kwa 160,000.
 
Ukivuna mwezi wa 10 unaweza kuvi-store hadi mwezi wa ngapi kwenye bei? Mwezi wa saba ndo bei huwa nzuri zaidi? Nimeona mwezi wa 4 Kariakoo gunia lilikuwa linauzwa Kwa 160,000.

Ukitumia mbegu nzuri vinauwezo wa kukaa mpaka mwezi wa nne. Inamaana ivo unavoviona miezi ya nne ni stock ya kuanzia mwezi wa 10 na 11. Kwahiyo siri kubwa ya ukaaji wa kitunguu store ni mbegu nzuri kwani kitunguu kinakua na layer nyingi hivo kuweza kustahimili muda wote huo.
 
kitunguu kinataka mazingira ya aina gani nina shamba kubwa "marangu" na mto unaopita pembeni je mkoa huu wa kilimanjaro vitunguu vinaweza kustawi?

Vitunguu vinakubali maeneo mengi tu hapa nchini kwetu, kikubwa ni kuhakikisha udongo sio ule wa kuhifadhi maji kwa muda mrefu kwani ikiwa utakua unahifadhi maji mengi basi utakuta kitunguu kinanawili majani tu ila tunda lenyewe haliongezeki kitu. Kwahiyo kujibu swali lako "kitunguu kinahitaji udongo wenye rutuba, eneo linalopata jua zuri na maji ya uhakika yawepo"
 
kikubwa ni storage mimi nshalimaga mvumi, kilosa nkapata tatizo wakati navuna mvua ilikuwepo nilikuwa sijajiandaa na storage na huko hakuna magala...labda utengeneze chanja ya kuhifadhia vitungu
 
Habari ndugu zangu,

Kwa jina naitwa Joseph ni mkulima na mfanyabiashara wa vitunguu. Kitunguu ni zao lenye manufaa makubwa na kipato cha hali ya juu endapo tu utafuata maelekezo ya mtaalamu.

Dhumuni langu hapa ni kuwaletea mbegu bora kabisa za vitunguu (Red Bombay) ambazo hukupa mavuno mazuri na yenye kipato kikubwa sana.

Bei ya mbegu hizi ni tsh 30,000/= kwa kopo la lita moja(1) na tsh 600,000/= kwa ndoo ya lita ishirini.

Guarantee: Ndoo ya lita 20 ambayo ni sawa na makopo 20 ya lita moja inatosha kupanda eneo la hekari 1 (m70*m70) na kiwango cha chini cha mavuno ni gunia 100 na kiwango cha juu ni gunia 110-120 ndani ya siku 90 (3 months) toka kupanda. Gunia moja sokoni kariakoo, ilala, buguruni, temeke na mabibo kwa sasa bei ni tsh 130,000/= * gunia 100 = tshs 13,000,000/= ndani ya miezi 3.

Kama utakua na swali lolote au kutaka kujua zaidi usisite kunitafuta kwa namba zangu za simu +255655003510 au e-mail address: josephkadendulah@gmail.com

Ahsanteni sana na karibuni tujenge maisha bora kwa kila mtanzani.

ila mimi nishatumia mbegu ya red creore ya south africa....nmecheck na jamaa huko mvumi hadi lumumo bdo wanaikubali sana hiyo mbegu wasipoitumia hiyo wanatumia mbegu za kienyeji.hiyo red bombay nataka kuja ijaribu msimu ujao nione mafanikio yake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom