peasant serious
Member
- Jan 10, 2018
- 43
- 55
Tanzania imezungukwa na maziwa makubwa yenye maji mengi kama vile ziwa Victoria , ziwa Tanganyika, Ziwa nyasa nk. Mara kwa mara viongozi wetu wamesikika wakisema tutumie maziwa haya kwa kilimo cha umwagiliaji, na wakati mwingine watu hujishangaa kwa nini maji haya hayatumiki kwa umwagiliaji.
Sina haja ya kuingilia mijadala hiyo, na kama mnavyonifahamu mimi ni mtu wa vitendo (kumbuka ile thread ya Chia Kilimo na masoko)
Kwanza kabisa tujue kuwa eneo linalofaa kwa kilimo linakuwa usawa wa juu wakati maji yako usawa wa chini (ukilinganisha na eneo la kilimo). Hivyo basi ili uweze kutumia maji hayo kwa umwagiliaji, lazima uyapandishe juu shambani. (Hii ni tofati na umwagiliaji kwa kutumia maji ya mito ambayo huwa yanatiririka kutoka juu kuelekea ziwani au baharini na hivyo unachofanya ni kuyazuia na kuyaelekeza shambani)
Hivyo basi ili uweze kuyapandisha unahitaji mashine yenye nguvu kutegemea na mwinuko toka ziwani. Hapa kuna mashine mbili zinatakiwa. Ya kwanza ni pump ya maji, na ya pili ni mashine ya kuendesha hiyo pump.
Changamoto ya kwanza unaipata hapo - ni pump ya ukubwa gani (uwezo wa kuvuta na kusukuma maji) na horse power zake ukioanisha na mashine (engine) ya kuendesha hiyo pump! Pia hapa kuna suala la mzunguko (rotation) ya engine na mzunguko wa pump Utakutana na kitu kinaitwa RPM.
Kwa sisi tunaoishi vijijini kupatata wataalamu wa mahesabu hayo ni vigumu Kwa hiyo tunategemea zaidi trial and error (kujaribu jaribu). hii husababisha gharama kubwa kwa kujikuta unanunua vifaa ambavyo ni vya bei ndogo na kumbe uwezo wake ni mdogo.
Kwa kuwa maji ni ya ziwa, lazima kukumbuka kuwa huruhusiwi kulima ndani ya mita 60 toka ziwani. Kwa hiyo lazima pump yako iweze kusukuma maji zaidi ya mita 60, na pia kama utataka kuyapandisha maji kwenye tenki la juu huko shambani, lazima ufikirie pia mwinuko wa hilo tank.
Baada ya hapo fikiria kupata mabomba sahihi, ya kuvuta maji na kuyasukuma, vinginevyo ytaishia kupasuka maana kunakuwepo mashindano ya maji (pump inasukuma maji yaende juu na yaliyoko juu yanataka kurudi (gravity); kama bomba si imara basi litapasuka au engine kama haina uwezo wa kutosha itazidiwa na kuzimika (kama gari lililoshindwa kupanda mlima) Madhara ya maji kurudi ghafla ni makubwa maana hupelekea kuharibika kwa pump ya maji.
Sehemu inakayofuata nitaonyesha nilikofikia ili mpate nafasi ya kuuliza maswali na kunipatia ushauri. Msichoke