Kilichojiri HESLB ndani ya gazeti la NIPASHE.

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,399
Wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya
juu nchini, wako
hatarini kuchelewa
kupata fedha za
mikopo kutoka
Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa
Elimu ya Juu
(HESLB) kutokana
na mchakato wa
kutoa mikopo hiyo
kuchelewa kuanza.
Hali hiyo inatokana
na vyuo hivyo
kuanza
kufunguliwa
mwishoni mwa
mwezi huu na
mwanzoni mwa
mwezi ujao.
Uchunguzi
uliofanywa na
NIPASHE umebaini
kuwa wanafunzi
katika vyuo hivyo
walioomba mikopo
toka HESLB, bado
hawajaanza
kupata hatua
ambayo imeanza
kuwapa shaka
kama wataripoti
vyuoni kwa wakati
kutokana na
kutegemea fedha
za mikopo kwa ajili
ya ada ya masomo
na mahitaji
mengine.
Kutokana na
ucheleweshaji wa
mikopo hiyo,
gazeti hili lilishudia
wanafunzi kadhaa
ambao
wamedahiliwa
kujiunga vyuo vya
elimu ya juu
mwaka huu,
wakimiminika
katika ofisi za
HESLB makao
makuu jijini Dar es
Salaam kuulizia
hatma ya mikopo
waliyoomba.
“Unavyoniona
hapa ni wiki ya
tatu nimekuwa
nikija hapa ofisi za
Bodi ya Mikopo
kuulizia kama
mikopo imeanza
kutolewa, lakini
tunaelezwa
tuendelee kusubiri
wakati vyuo
vimekaribia
kufunguliwa,”
alisema
mwanafunzi
mmoja aliyetoka
Chuo Kikuu cha
Mzumbe mkoani
Morogoro.
Hata hivyo, Afisa
mmoja wa HESLB,
aliyejitambulisha
kwa jina moja la
Venelanda, alisema
mchakato wa
kuandaa mikopo
ya wanafunzi bado
unaendelea na
kwamba zoezi hilo
linachukua muda
kidogo kutokana
na mikopo hadi
kukamilika kwake
hupitia maeneo
mengi.
Venelanda ambaye
hata hivyo,
hakutoa jibu la
moja kwa moja
kama mikopo kwa
wanafunzi hao
itaanza kutolewa
lini, alisema HESLB
itahakikisha
mikopo hiyo
inatolewa kwa
wanafunzi hao
kabla ya
kufunguliwa vyuo
hivyo.
Mkuu wa Idara ya
Habari Wizara ya
Fedha, Ingiahedi
Mduma, alipoulizwa
na gazeti hili kama
fedha za mikopo
kwa wanafunzi
wa elimu ya juu
zimeshapelekwa
HESLB, alisema
suala hilo waulizwe
Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya
Ufundi.
“Bajeti
ikishapitishwa
bungeni,
kinachobakia ni
kwa wizara husika
kushughulikia
mipango yake,
hivyo hata suala la
fedha za mikopo
ya wanafunzi wa
vyuo vikuu wenye
majibu ni Wizara ya
Elimu na Mafunzo
ya Ufundi,” alisema
Mduma.
Naibu Waziri wa
Elimu na Mafunzo
ya Ufundi, Phillipo
Mulugo, alipoulizwa
na NIPASHE,
alisema kimsingi
mikopo bado
haijaanza
kutolewa kwa
wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya
juu na kufafanua
kuwa kuanzia wiki
hii wizara yake
itaangalia
uwezekano wa
kushughulikia
suala hilo ili
wahusika wapewe
mikopo hiyo.
Rais wa Serikali ya
Wanafunzi wa
Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam
(Daruso),
Bhokombe Itembe,
alisema wanafunzi
wa mwaka wa
kwanza
wanatarajia
kuripoti chuoni
hapo Oktoba Mosi,
mwaka huu.
Alisema wiki
iliyopita uongozi
wa chuo na
Daruso, walitaka
kupanga vyumba
katika hosteli kwa
ajili ya wanafunzi,
lakini zoezi hilo
lilishindikana kwa
sababu bado
haijafahamika
idadi ya wanafunzi
wa mwaka wa
kwanza
watakaoripoti
chuoni hapo.
Itembe alisema
tatizo la
kuchelewa kwa
mikopo linatokana
na sababu kadhaa,
ikiwemo
kutokuwepo kwa
ushirikiano kati ya
HESLB na Tume ya
Vyuo Vikuu
Tanzania (TCU).
“Mwanafunzi
anapodahiliwa bila
TCU kumuamulia
ataenda chuo gani,
huwezi kwenda na
wakati huo huo
bila HESLB
kukupatia mkopo,
vile vile huwezi
kwenda chuoni,”
alisema Itembe.
Rais wa Chuo Kikuu
cha Usimamizi wa
Fedha IFM, Michael
Chazy, alisema
chuo hicho
kitafunguliwa
Oktoba 8, mwaka
huu na kwamba
hadi sasa bado
wanafunzi
wanaoendelea na
wale wa mwaka
wa kwanza
hawajaanza
kupatiwa mikopo.
Naye Rais wa Chuo
Kikuu cha Dodoma
(Udom), Paul
Yunge, alisema
suala la mikopo
katika chuo lina
utata hasa kwa
wanafunzi
wanaoanza
mwaka wa kwanza
ambapo baadhi
yao wamejaza
fomu vibaya na
hivyo taasisi
husika
zinashughulikia
tatizo hilo.
Rais wa Chuo Kikuu
cha Mzumbe, Amos
Chakushemeire,
alisema utoaji wa
mikopo hauridhishi
kabisa katika chuo
hicho ambapo
wanafunzi
walioanza muhula
Julai, mwaka huu,
wamelipwa robo
ya mkopo wakati
kiasi kingine cha
mkopo
hawajalipwa hadi
sasa, hali ambayo
imesababisha
ukata mkubwa
kwa wanafunzi.
“Chuo chetu ni
tofauti na vingine,
kina mihula mitatu,
wanafunzi
walioanza muhula
wa Julai
hawajalipwa
sehemu nyingine,.
Hivi karibuni
uongozi wa chuo
ulilazimika
kuwakopesha Sh.
50,000 wanachuo
hao ili kuwatuliza
wasigome,”
alisema
Chakushemeire.
Rais wa Chuo cha
Ustawi wa Jamii,
Frank Nkinda,
alisema mikopo ni
changamoto
kubwa katika chuo
hicho ambapo
wanafunzi wa
mwaka wa kwanza
hawajapata
mikopo hadi sasa.
Alisema kutokana
na hali hiyo, hivi
karibu Mwenyekiti
wa HESLB alifika
chuoni hapo
kuzungumza na
uongozi, serikali ya
wanafunzi na
wanachuo ambapo
alitoa ahadi kutoa
mikopo kwa
wanafunzi wa
mwaka wa kwanza
katika mwaka huu
wa 2012/2013.
Mwaka jana
serikali kupitia
Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi
ilitangaza
utaratibu mpya wa
utoaji wa mikopo
ambapo badala ya
fedha hizo
kutolewa kwa
waombaji na
HESLB, sasa fedha
hizo zinapelekwa
vyuoni ambako
menejimenti za
vyuo zinawajibika
kuzisimamia na
kuwapa waombaji.
Hatua hiyo ilifikiwa
ili kurahisisha
mchakato wa
kuwapatia fedha
waombaji na pia
kuepusha
usumbufu kwa
HESLB kutokana
na wanafunzi
kutoka vyuoni
kuvamia ofisi hizo
kwa lengo la
kushinikiza
wapewe fedha.
Taarifa iliyotolewa
na HESLB na TCU
Agosti 10 na 12,
mwaka huu ilieleza
kuwa zaidi ya
wanafunzi 3,074
walioomba mikopo
ya elimu ya juu
kwa mwaka
2012/13,
wameenguliwa
katika maombi yao
kutokana na
dosari mbalimbali.
Taarifa hiyo
ilieleza kuwa
HESLB pekee
iliorodhesha zaidi
ya wanafunzi
2,649 ambao
ilibaini kuwa na
mapungufu
kadhaa katika
maombi yao ya
kupewa mikopo.
Miongoni mwa
makosa ama
dosari ambazo
HESLB ilizibaini
kwa walioenguliwa
ni pamoja na
kukosekana kwa
vyeti vya kuzaliwa
kwa muombaji,
sahihi ya
mdhamini/
muombaji,
kukosekana kwa
picha ndogo ya
muombaji/
mdhamini,
kukosekana kwa
sahihi za viongozi
wa serikali za
mitaa/vijiji kwa
waombaji na
nyaraka nyingine
muhimu kwa
waombaji.
Kwa upande wake
TCU, iliwaengua
jumla ya waombaji
425 kwa dosari na
makosa
mbalimbali.
Miongoni mwa
dosari ambazo
zilitajwa na TCU ni
pamoja na baadhi
yao kukosea
namba za vyeti
vya masomo kwa
vidato vya nne na
tano, miaka ya
kumaliza masomo,
mawasiliano sahihi
kwa muombaji
pamoja na
uchaguzi wa
masomo.
Hata hivyo, taasisi
hizo mbili zimetoa
muda kwa
walioenguliwa
sasa kutokana na
dosari hizo
kurekebisha na
kutuma tena
maombi yao
kupitia mitandao
kwa mujibu wa
maelekezo
waliyotoa.
Kwa mwaka huu
wa fedha 2012/13,
serikali
imeiongezea fedha
HESLB kwa
kuitengea Sh.
bilioni 326 kwa
wanafunzi 98,772.
Mwaka jana,
serikali iliitengea
HESLB Sh.
91,722,783,264
kwa ajili ya mikopo
ya wanafunzi wa
elimu ya juu.
Ucheleweshaji wa
fedha za mikopo
kwa wanafunzi wa
elimu ya juu
umekuwa
ukisababisha
wafanye migomo,
vurugu na
maandamano mara
kwa mara
kushinikiza
walipwe.
 
thanks alot mkuu....sasa cjui yule jamaa(nimekimbiaccm) aliyesema leo mkopo unatoka tena saa6 alikua anaota au vipi......
 
mwaka jana bilion 91, huku mwaka huu bilion 326, halafu bado watu wakose mkopo? Mh, hii nchi balaa
 
Kila chuo nadhani kina utaratibu wake. Vipi wewe Msafwa wa Swaya ipi? Ile ya kule juu airport?
Bila shaka mkuu ile ile ya mbeya vijijin mlimani nimepata chuo lakn mkopo ndo hvyo iv nimeulizia ili nijiandae kama mkopo utachelewa kutoka hata kwenda chuo nitachelewa asante best kwa kunijuza?
 
unajua hizi taasisi yaani HELSB na TCU zinashindwa kuwa na mikakati au mbinu za kiutendaji
maana hadi inakuwa hivi ni jibu tosha
kwamba hazifanyi kazi kulingana na wakati au kujari huduma/mahitaji kwa wateja (wanafunzi walioomba mkopo).
pia chelewa chelewa hii inasababishaa mianya ya rushwa pamoja na urasimu
ingekuwa busara watoe fedha kwa hao ambao tayari wapo ktk orodha ya kupata mikopo na ambao bado wasubiri
majina yao yatakapo kuwa tayari..
tatizo ni kutokuwa na mpango kazi unaenda na muda kulingana na mahitaji ya washika dau ( vyuo na wanafunzi) pitatizo jingine ni kutokuwa na mawasiliano mazuri kati ya HESLB, TCU na Vyuo husika.
suluhisho ni kuwa na tarehe ya kutoa majina ya waliopata mkopo mapema inayoendana na mahitaji ya watu hata kama
hata kama waliomba kwa wakati tofauti au wataanza masomo tarehe zikiwa tofauti.
 
nimeshangazwa na kauli ya rais wng wa mzumbe,eti wametutuliza tusigome kwa sh 50000/,hajui hali halisi ya hapa chuo nadhan,na hili linazid kusibitisha udhaifu wa serikali yako Amon pamoja na mawazir wk weng wenye uwezo mdo kitendaj na hata kifikra...hali bado tete b back chuo..
 
Kwa kweli inaumiza sana na sijajua kwanini HESLB, TCU na vyuo hawana ushirikiano, kwani ingewekwa Tarehe au mda ambao vyuo vinatakiwa kufungua isiwe kabla ya na baada ya alafu wakati huo huo nao tcu wana akikisha wana allocated wanafunzi kabla ya na sio baada ya na kwa bodi ya mikopo vivyo hivyo kabla ya na sio baada ya hapo tutenda na nina uhakika itakuwa safi sana kwa wanafunzi hasa wa mwaka wa kwanza kwani ndio wanaoathirika zaid ya michakapo hii ya Kuwa Allocated vyuoni, Vyuo kufunguliwa na Upewaji wa Mikopo.
 
Back
Top Bottom