Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 9,554
- 14,496
mnasubiri makombo sio?ndio hayo mashibuda hamkomi tu
unaandika madudu tu, potezea tu :frusty:mkuu mbona unakua kama mchawi....
mnasubiri makombo sio?ndio hayo mashibuda hamkomi tu
Ushauri wangu kwa CDM, Vijana kama hawa, waongezeeni nguvu kufikia ukombozi waliyokusudia, Mwanga kiukweli imekuwa ngome ya ccm kwa muda sasa, ila kwasasa hali imekuwa tofauti hasa kwenye kata hizi, kileo kata hii imepakana na vunjo,kivisini,jipe,kigonigoni,kwakoa, toloha,mgaogao(chadema ilipoteza hii kata kwa uzembe wa viongozi wa jimbo hapa ndipo ninapo toka na nilisimamia uchaguzi bila kulipwa wala chadema walikuwa hawajui kwamba wana mawakala)kata nyigine ni Kirya,lang'ata pamoja na ugweno, hizi kata kwasasa zimekaa kiupinzani sasa, maeneo magumu kidogo ni usangi ile siyo yote kwa kifupi tambarare imekaa vizuri kwasasa.
CHADEMA wanatembea kama kumi wakifika mahali wanasema tunaunja ngome wanapeana vikadi wanavyotembea navyo, MOVEMENT FOR CHAGAN (M4C) on cheap work. Mnakula michango yetu heti mko kazini. Wahuni wanakula visenti vya viraza
Concrete,Mkuu umeongea vizuri sana hapo juu ila kuna jambo moja ninataka kuliweka sawa zaidi kuhusu kata ya Usangi.
Kata hii ambayo mwaka 2010 nilikuwa maaneo hayo nikifanya tafiti rasmi 2 za mambo ya kisayansi na tafiti1 isiyo rasmi(Kisiasa) na haya ni baadhi ya mambo ya kisiasa niliyoyaona.
1/Kata ya Usangi ndio kata yenye ushawishi mkubwa sana kisiasa kwa eneo zima la Mwanga
(Ni kwa sababu za kihistoria tu eg. wanasiasa wakubwa karibu wote wa mwanga wametokea huko eg. Cleopa Msuya, Mzee Peter Kisumo, Asharose Migiro, Mr.Gopa, Prof.Maghembe)
2/Maendeleo makubwa ya kijamii yalifika huko mapema zaidi miaka ya 1970s (Shule, Hospitali, Umeme, Simu, Maji, Barabara, Ustaarabu wa kidini, Mahakama nk) hii ni kwa sababu ya Mzee Cleopa Msuya alikuwa waziri wa Fedha.
3/Kuna mdodoro mkubwa sana wa kimaendeleo toka mwaka 2000.
(Sababu kuu ni kustaafu siasa kwa Cleopa Msuya, mgogoro wa kidini(Lutherani))
3/Wanahamu kubwa sana ya mabadiliko ya kisiasa (Shauku yao ni kuona upinzani unakuja kuwahamasisha na kuwaunganisha kisiasa)
Hili nililiona karibu kila mahali nilipofika na kusikiliza mazungumzo yao.
4/Wanauelewa mkubwa sana wa kisiasa kwa sasa.
(Huwezi amini kata hii ambayo Mzee Cleopa Msuya na Peter Kisumo wanazaliwa, kuishi na kupewa heshima kubwa sana, mwaka 2010 kura za maoni CCM, wazee hawa kwa mara ya kwanza waliamua kutomuunga mkono Prof. Maghembe lakini wanaCCM hawa hawa waliwapinga, wakasema wao sio watoto tena na kwa makusudi kabisa wanaCCM wakamuunga mkono Prof. Maghembe japokuwa amechokwa na wengi!!)
6/Ni wafuatiliaji wazuri kwa karibu sana wa kila kitu kinachoendelea Tanzania na dunia kila siku (Kupitia redio, Tv, magazeti, Internet nk) they are very up to dated!!
7/Ni wapenzi wakubwa sana wa siasa za kimageuzi (Hawana tofauti kabisa na wananchi wa Moshi mjini na Arusha mjini) tatizo pekee walilonalo wanaamini maendeleo ni upendeleo toka serikalini.
8/Kuna mchanganyiko mkubwa zaidi wa watu kuliko kata nyingi ukiondoa eneo la mwanga mjini (eg. Kidini, kikabila, kielimu, Kirika, kikazi na kibiashara)
Mpe tusi la nguoni PAW. Chezeiya PAW wewe!Natamani kupigwa ban plz tell me the procedure:-*
Concrete,
naomba nitofautiane nad madai yako. Wapare wamefunguka toka zamani sana na maendeleo yao yamepatikana kwa kazi za kujitolea maarufu kama MSARAGAMBO. Harakati za kutafuta haki zimeanza tangu enzi za wazee wetu. Kama huna habari na hilo ulizia shauri la Shaaban Mtengeti na wenzake kupinga uchaguzi wa Chifu wa Usangi. Kesi hiyo ilikwenda mpaka kwenye kamati ya makoloni ya Umoja wa Mataifa.
Kuhusu suala la elimu, hili halikuletwa na Cleopa Msuya. Elimu ilichangamkiwa na wazee wetu tangu enzi za mkoloni. Kutokana na wananchi wa Pare District kuonekana wanapenda maendeleo, mkoloni wa Kiingereza aliamua kuanzisha a pilot program ya elimu ya watu wazima. Sasa kutokea hapo ndiyo Upare nzima ikaamka kielimu. Kabla hata ya Uhuru Wapare waliweza kuvunja rekodi kwa kuandikisha wanafunzi. wengi shule ya msingi. Suala hilo lipo ktk ripoti za Umoja wa mataifa wakati wa mkoloni. Kwa maneno mengine zoezi la UPE lilifika Upare miaka ya 40, wakati Tanzania nzima ilikuja kutekeleza zoezi hilo mwaka 1977.
Kitu kingine ambacho ni cha kipekee kwa wananchi wa Mwanga/Same ni kwamba suala la elimu lilichangamkiwa na kila mtu bila kubagua dini. Ndiyo maana unaona kwamba wasomi wa huko ni toka ktk dini zote mbili bila kubagua.
Madai kwamba maendeleo ya Mwanga au Upare yameletwa na Cleopa Msuya kwasababu alikuwa ni waziri wa fedha ni siasa chafu za majitaka.Wilaya ya Mwanga imeundwa miaka ya 1980. Kabla ya hapo Mbunge wa jimbo la Pare alikuwa Chediel Mgonja ambaye kisiasa walikuwa hawaivi na Cleopa Msuya. Mwalimu Nyerere aliwahi kufika Upare na akavutiwa sana na juhudi za wananchi wa huko katika kufanya kazi za kujitolea yaani MSARAGAMBO. Ndiyo maana Mwalimu akawaita WAPARE kuwa ni WACHINA WA TANZANIA. Msaragambo ndiyo ulioleta maendeleo katika wilaya yetu na siyo kubebwa na Mgonja, Msuya, au Kisumo.
Kuhusu Msuya vs Maghembe, "uhasimu" wao umeanza kabla ya mwaka 2000. Msuya alikuwa na mgombea wake, lakini wana CCM wa Mwanga wakaamua kumchagua Prof.Jumanne Maghembe. Uhasimu huo inaelekea haujaisha mpaka leo hii.
Mwisho, nakubaliana na maelezo yako kwamba wananchi wa Mwanga wana kiu kubwa ya mabadiliko. Kikwazo kikubwa ni kwamba vyama vya upinzani havijafanya juhudi za kutosha kujitangaza na kujitambulisha kwa wananchi wa Mwanga. Wapinzani na Watanzania toka maeneo mengine wana mtizamo hasi dhidi ya jimbo la Mwanga. Wanafikiri kwamba jimbo hilo ni ngome ya CCM na Cleopa Msuya, kitu ambacho siyo kweli.
Mbona raia wapo mbali wanaogopa kusogea karibu.
Jamani, tuwe tunatumia akili hata kidogo tu kabla ya kupost uzi hapa JF!!
nilikuna na ndoto za kua asipotokea mkomboz nitakomboa mimi ila nikajipima ubavu nikaona nitapwaya nikawa namwomba mungu amlete musa huyu atutoe kwenye makucha ya mafarao hawa
fedha za mfuko wa barabara zinafanya kuporwa kwa stayle ya ujambaz.barabara ya kijiji cha kilawen yenye km 8 imetengewa tsh mil.11 za kukwangua majani tu
najua ubabe, ujuha,ushirikina wa prf.maghembe itakupa changamoto lakni kaza mlume dalili za msiba wa wazee wahafidhina wa chama kuanguka ziko wazi na tutawaangusha sisi tukiwa na kadi zao mfukon.tunataka mabadiliko na yakija hawatazuia muda ni huu anza kusogea karibu na sis wenye jimbo.
0755445878