Kilewo Aivunja ngome ya Profesa Jumanne Maghebe Maeneo ya Usangi Mwanga Kilimanjaro

Inaleta tumaini jipya. Ila mbona hujatuonyesha umati wa watu waliokuwepo
 
Ushauri wangu kwa CDM, Vijana kama hawa, waongezeeni nguvu kufikia ukombozi waliyokusudia, Mwanga kiukweli imekuwa ngome ya ccm kwa muda sasa, ila kwasasa hali imekuwa tofauti hasa kwenye kata hizi, kileo kata hii imepakana na vunjo,kivisini,jipe,kigonigoni,kwakoa, toloha,mgaogao(chadema ilipoteza hii kata kwa uzembe wa viongozi wa jimbo hapa ndipo ninapo toka na nilisimamia uchaguzi bila kulipwa wala chadema walikuwa hawajui kwamba wana mawakala)kata nyigine ni Kirya,lang'ata pamoja na ugweno, hizi kata kwasasa zimekaa kiupinzani sasa, maeneo magumu kidogo ni usangi ile siyo yote kwa kifupi tambarare imekaa vizuri kwasasa.

Mkuu umeongea vizuri sana hapo juu ila kuna jambo moja ninataka kuliweka sawa zaidi kuhusu kata ya Usangi.

Kata hii ambayo mwaka 2010 nilikuwa maaneo hayo nikifanya tafiti rasmi 2 za mambo ya kisayansi na tafiti1 isiyo rasmi(Kisiasa) na haya ni baadhi ya mambo ya kisiasa niliyoyaona.

1/Kata ya Usangi ndio kata yenye ushawishi mkubwa sana kisiasa kwa eneo zima la Mwanga
(Ni kwa sababu za kihistoria tu eg. wanasiasa wakubwa karibu wote wa mwanga wametokea huko eg. Cleopa Msuya, Mzee Peter Kisumo, Asharose Migiro, Mr.Gopa, Prof.Maghembe)

2/Maendeleo makubwa ya kijamii yalifika huko mapema zaidi miaka ya 1970s (Shule, Hospitali, Umeme, Simu, Maji, Barabara, Ustaarabu wa kidini, Mahakama nk) hii ni kwa sababu ya Mzee Cleopa Msuya alikuwa waziri wa Fedha.

3/Kuna mdodoro mkubwa sana wa kimaendeleo toka mwaka 2000.
(Sababu kuu ni kustaafu siasa kwa Cleopa Msuya, mgogoro wa kidini(Lutherani))

3/Wanahamu kubwa sana ya mabadiliko ya kisiasa (Shauku yao ni kuona upinzani unakuja kuwahamasisha na kuwaunganisha kisiasa)
Hili nililiona karibu kila mahali nilipofika na kusikiliza mazungumzo yao.

4/Wanauelewa mkubwa sana wa kisiasa kwa sasa.
(Huwezi amini kata hii ambayo Mzee Cleopa Msuya na Peter Kisumo wanazaliwa, kuishi na kupewa heshima kubwa sana, mwaka 2010 kura za maoni CCM, wazee hawa kwa mara ya kwanza waliamua kutomuunga mkono Prof. Maghembe lakini wanaCCM hawa hawa waliwapinga, wakasema wao sio watoto tena na kwa makusudi kabisa wanaCCM wakamuunga mkono Prof. Maghembe japokuwa amechokwa na wengi!!)

6/Ni wafuatiliaji wazuri kwa karibu sana wa kila kitu kinachoendelea Tanzania na dunia kila siku (Kupitia redio, Tv, magazeti, Internet nk) they are very up to dated!!

7/Ni wapenzi wakubwa sana wa siasa za kimageuzi (Hawana tofauti kabisa na wananchi wa Moshi mjini na Arusha mjini) tatizo pekee walilonalo wanaamini maendeleo ni upendeleo toka serikalini.

8/Kuna mchanganyiko mkubwa zaidi wa watu kuliko kata nyingi ukiondoa eneo la mwanga mjini (eg. Kidini, kikabila, kielimu, Kirika, kikazi na kibiashara)
 
CHADEMA wanatembea kama kumi wakifika mahali wanasema tunaunja ngome wanapeana vikadi wanavyotembea navyo, MOVEMENT FOR CHAGAN (M4C) on cheap work. Mnakula michango yetu heti mko kazini. Wahuni wanakula visenti vya viraza

Maneno kama yako hata mkoloni aliwahi kuyasema wakati Nyerere anafanya harakati za uhuru wa Tanganyika,

Pia makaburu nao walisema hivyo hivyo wakati Nelson Mandela akipigania ukombozi wa South Africa.

Ni njia hii pia M4C wanapitia, muda na matokeo vitakupa majibu tu.

Mwenzako Nape keshasema yeye yuko tayari hata kubaki mwenyewe CCM huku akiendelea kuwavua wenzake nguo hadharani akidai ndio style ya kuwavua magamba!
 
Vyema sana mzee kachoka sana wakati serikali kama imejipanga vyema inaweza kuwalipa rejesha kadi ya Tanu nitamtwangia babu simu naye kama anayo halejeshe mapema.
 
Mkuu umeongea vizuri sana hapo juu ila kuna jambo moja ninataka kuliweka sawa zaidi kuhusu kata ya Usangi.

Kata hii ambayo mwaka 2010 nilikuwa maaneo hayo nikifanya tafiti rasmi 2 za mambo ya kisayansi na tafiti1 isiyo rasmi(Kisiasa) na haya ni baadhi ya mambo ya kisiasa niliyoyaona.

1/Kata ya Usangi ndio kata yenye ushawishi mkubwa sana kisiasa kwa eneo zima la Mwanga
(Ni kwa sababu za kihistoria tu eg. wanasiasa wakubwa karibu wote wa mwanga wametokea huko eg. Cleopa Msuya, Mzee Peter Kisumo, Asharose Migiro, Mr.Gopa, Prof.Maghembe)

2/Maendeleo makubwa ya kijamii yalifika huko mapema zaidi miaka ya 1970s (Shule, Hospitali, Umeme, Simu, Maji, Barabara, Ustaarabu wa kidini, Mahakama nk) hii ni kwa sababu ya Mzee Cleopa Msuya alikuwa waziri wa Fedha.

3/Kuna mdodoro mkubwa sana wa kimaendeleo toka mwaka 2000.
(Sababu kuu ni kustaafu siasa kwa Cleopa Msuya, mgogoro wa kidini(Lutherani))

3/Wanahamu kubwa sana ya mabadiliko ya kisiasa (Shauku yao ni kuona upinzani unakuja kuwahamasisha na kuwaunganisha kisiasa)
Hili nililiona karibu kila mahali nilipofika na kusikiliza mazungumzo yao.

4/Wanauelewa mkubwa sana wa kisiasa kwa sasa.
(Huwezi amini kata hii ambayo Mzee Cleopa Msuya na Peter Kisumo wanazaliwa, kuishi na kupewa heshima kubwa sana, mwaka 2010 kura za maoni CCM, wazee hawa kwa mara ya kwanza waliamua kutomuunga mkono Prof. Maghembe lakini wanaCCM hawa hawa waliwapinga, wakasema wao sio watoto tena na kwa makusudi kabisa wanaCCM wakamuunga mkono Prof. Maghembe japokuwa amechokwa na wengi!!)

6/Ni wafuatiliaji wazuri kwa karibu sana wa kila kitu kinachoendelea Tanzania na dunia kila siku (Kupitia redio, Tv, magazeti, Internet nk) they are very up to dated!!

7/Ni wapenzi wakubwa sana wa siasa za kimageuzi (Hawana tofauti kabisa na wananchi wa Moshi mjini na Arusha mjini) tatizo pekee walilonalo wanaamini maendeleo ni upendeleo toka serikalini.

8/Kuna mchanganyiko mkubwa zaidi wa watu kuliko kata nyingi ukiondoa eneo la mwanga mjini (eg. Kidini, kikabila, kielimu, Kirika, kikazi na kibiashara)
Concrete,

naomba nitofautiane na madai yako. Wapare wamefunguka toka zamani sana na maendeleo yao yamepatikana kwa kazi za kujitolea maarufu kama MSARAGAMBO. Harakati za kutafuta haki zimeanza tangu enzi za wazee wetu. Kama huna habari na hilo ulizia shauri la Shaaban Mtengeti na wenzake kupinga uchaguzi wa Chifu wa Usangi. Kesi hiyo ilikwenda mpaka kwenye kamati ya makoloni ya Umoja wa Mataifa.

Kuhusu suala la elimu, hili halikuletwa na Cleopa Msuya. Elimu ilichangamkiwa na wazee wetu tangu enzi za mkoloni. Kutokana na wananchi wa Pare District kuonekana wanapenda maendeleo, mkoloni wa Kiingereza aliamua kuanzisha a pilot program ya elimu ya watu wazima. Sasa kutokea hapo ndiyo Upare nzima ikaamka kielimu. Kabla hata ya Uhuru Wapare waliweza kuvunja rekodi kwa kuandikisha wanafunzi wengi shule ya msingi. Suala hilo lipo ktk ripoti za Umoja wa mataifa wakati wa mkoloni. Kwa maneno mengine zoezi la UPE lilifika Upare miaka ya 40, wakati Tanzania nzima ilikuja kutekeleza zoezi hilo mwaka 1977.

Kitu kingine ambacho ni cha kipekee kwa wananchi wa Mwanga/Same ni kwamba suala la elimu lilichangamkiwa na kila mtu bila kubagua dini. Ndiyo maana unaona kwamba wasomi wa huko ni toka ktk dini zote mbili bila kubagua.

Madai kwamba maendeleo ya Mwanga au Upare yameletwa na Cleopa Msuya kwasababu alikuwa ni waziri wa fedha ni siasa chafu za majitaka.Wilaya ya Mwanga imeundwa miaka ya 1980. Kabla ya hapo Mbunge wa jimbo la Pare alikuwa Chediel Mgonja ambaye kisiasa walikuwa hawaivi na Cleopa Msuya. Mwalimu Nyerere aliwahi kufika Upare na akavutiwa sana na juhudi za wananchi wa huko katika kufanya kazi za kujitolea yaani MSARAGAMBO. Ndiyo maana Mwalimu akawaita WAPARE kuwa ni WACHINA WA TANZANIA. Msaragambo ndiyo ulioleta maendeleo katika wilaya yetu na siyo kubebwa na Mgonja, Msuya, au Kisumo.

Kuhusu Msuya vs Maghembe, "uhasimu" wao umeanza kabla ya mwaka 2000. Msuya alikuwa na mgombea wake, lakini wana CCM wa Mwanga wakaamua kumchagua Prof.Jumanne Maghembe. Uhasimu huo inaelekea haujaisha mpaka leo hii.

Mwisho, nakubaliana na maelezo yako kwamba wananchi wa Mwanga wana kiu kubwa ya mabadiliko. Kikwazo kikubwa ni kwamba vyama vya upinzani havijafanya juhudi za kutosha kujitangaza na kujitambulisha kwa wananchi wa Mwanga. Wapinzani na Watanzania toka maeneo mengine wana mtizamo hasi dhidi ya jimbo la Mwanga. Wanafikiri kwamba jimbo hilo ni ngome ya CCM na Cleopa Msuya, kitu ambacho siyo kweli.
 
Last edited by a moderator:
Huyo mzee anayetoa kadi yake ya tanu ana
itwa kwa jina la utani MYFRIEND anaduka lake usangi,mtaa wa mombasa store,mzee machachari sana huyo
 
Concrete,

naomba nitofautiane nad madai yako. Wapare wamefunguka toka zamani sana na maendeleo yao yamepatikana kwa kazi za kujitolea maarufu kama MSARAGAMBO. Harakati za kutafuta haki zimeanza tangu enzi za wazee wetu. Kama huna habari na hilo ulizia shauri la Shaaban Mtengeti na wenzake kupinga uchaguzi wa Chifu wa Usangi. Kesi hiyo ilikwenda mpaka kwenye kamati ya makoloni ya Umoja wa Mataifa.

Kuhusu suala la elimu, hili halikuletwa na Cleopa Msuya. Elimu ilichangamkiwa na wazee wetu tangu enzi za mkoloni. Kutokana na wananchi wa Pare District kuonekana wanapenda maendeleo, mkoloni wa Kiingereza aliamua kuanzisha a pilot program ya elimu ya watu wazima. Sasa kutokea hapo ndiyo Upare nzima ikaamka kielimu. Kabla hata ya Uhuru Wapare waliweza kuvunja rekodi kwa kuandikisha wanafunzi. wengi shule ya msingi. Suala hilo lipo ktk ripoti za Umoja wa mataifa wakati wa mkoloni. Kwa maneno mengine zoezi la UPE lilifika Upare miaka ya 40, wakati Tanzania nzima ilikuja kutekeleza zoezi hilo mwaka 1977.

Kitu kingine ambacho ni cha kipekee kwa wananchi wa Mwanga/Same ni kwamba suala la elimu lilichangamkiwa na kila mtu bila kubagua dini. Ndiyo maana unaona kwamba wasomi wa huko ni toka ktk dini zote mbili bila kubagua.

Madai kwamba maendeleo ya Mwanga au Upare yameletwa na Cleopa Msuya kwasababu alikuwa ni waziri wa fedha ni siasa chafu za majitaka.Wilaya ya Mwanga imeundwa miaka ya 1980. Kabla ya hapo Mbunge wa jimbo la Pare alikuwa Chediel Mgonja ambaye kisiasa walikuwa hawaivi na Cleopa Msuya. Mwalimu Nyerere aliwahi kufika Upare na akavutiwa sana na juhudi za wananchi wa huko katika kufanya kazi za kujitolea yaani MSARAGAMBO. Ndiyo maana Mwalimu akawaita WAPARE kuwa ni WACHINA WA TANZANIA. Msaragambo ndiyo ulioleta maendeleo katika wilaya yetu na siyo kubebwa na Mgonja, Msuya, au Kisumo.

Kuhusu Msuya vs Maghembe, "uhasimu" wao umeanza kabla ya mwaka 2000. Msuya alikuwa na mgombea wake, lakini wana CCM wa Mwanga wakaamua kumchagua Prof.Jumanne Maghembe. Uhasimu huo inaelekea haujaisha mpaka leo hii.

Mwisho, nakubaliana na maelezo yako kwamba wananchi wa Mwanga wana kiu kubwa ya mabadiliko. Kikwazo kikubwa ni kwamba vyama vya upinzani havijafanya juhudi za kutosha kujitangaza na kujitambulisha kwa wananchi wa Mwanga. Wapinzani na Watanzania toka maeneo mengine wana mtizamo hasi dhidi ya jimbo la Mwanga. Wanafikiri kwamba jimbo hilo ni ngome ya CCM na Cleopa Msuya, kitu ambacho siyo kweli.

Peter kisumo na cleopa msuya walikua wanamsapoti Tadayo against magembe na ni kweli wanamchukia magembe,mimh ni kati ya mmojawapo niliyekua nasimamia oparesheni hiyo yakumng'oa magembe,ila alitumia ujanja mmoja kuingiza udini na ndipo alipomshinda tadayo.wapere wengi usangi waislamu abt 95prcnt,na ukikubalika usangi then umepita kote
 
Last edited by a moderator:
view.php
kilewo+4_o.jpg
kilewo+2.jpg
 
Mbona raia wapo mbali wanaogopa kusogea karibu.

Ndiyo staili yao ya kisasa, Vipi lakini naona Nec wameamua kula matapishi yao, siwalisema wanaohusika na kashifa za ufisadi watawaondoa, wamewaondoa? Lowassa yupo? Chenge naye vipi? Majibu tafadhali
 
kuna vijana humu kazi yenu ni kuangalia eti leo LEMA,MNYIKA,HECHE,WENJE,SUGU,MREMA, na kutoa matusi kuna wengine hamuwajui chadema nao ni tatizo saana mnaona sasa kuna huyu dogo anaitwa KILEWO kama ni mashine hii nayo ni type ya kina hao mnaowahofia eti mnajiita anti ....kaskazini huku wengine mnasahau mnatoka huko hivi mfano yule kijana anaitwa nyakarungu au saanane wa ukanda upi hao kama sikosei! eti ooh sisi ni CHADEMA ila anti kaskazini *****
 
nilikuna na ndoto za kua asipotokea mkomboz nitakomboa mimi ila nikajipima ubavu nikaona nitapwaya nikawa namwomba mungu amlete musa huyu atutoe kwenye makucha ya mafarao hawa

fedha za mfuko wa barabara zinafanya kuporwa kwa stayle ya ujambaz.barabara ya kijiji cha kilawen yenye km 8 imetengewa tsh mil.11 za kukwangua majani tu

najua ubabe, ujuha,ushirikina wa prf.maghembe itakupa changamoto lakni kaza mlume dalili za msiba wa wazee wahafidhina wa chama kuanguka ziko wazi na tutawaangusha sisi tukiwa na kadi zao mfukon.tunataka mabadiliko na yakija hawatazuia muda ni huu anza kusogea karibu na sis wenye jimbo.

0755445878
 
usiofu mkuu ukombozi upo na nina omba sana ufike
 
Back
Top Bottom