Sir R
JF-Expert Member
- Oct 23, 2009
- 2,175
- 298
Tangu kampeni zianze nimegundua kuwa JK na CCM wako mbali na watanzania, wamejaza picha kila mahali mf kuta za nyumba, nguzo za umeme, mabango makubwa.
Pamoja na jitihada hizo mvuto wao hauko kwa watu, kila mahali watu wanaizungumzia CCM na viongozi wao wanazungumziwa vibaya. Wanajitahidi kuwapakiza watu kwwenye magari lakini wapi, hakuna mvuto, wanabaki kwenye eneo la nje ya binadamu;
Upande wa pili Dr Slaa na Chadema wamejitahidi kuingia ndani ya mioyo ya watu mfano watu hujipeleka wenyewe kwenye mikutano ya Dr Slaa na chadema bila kubebwa. Hamna matangazo mengi kama ya CCM, Watu katika mikutano ya Chadema wanahamsa sana kuliko mikutano ya CCM inayotawaliwa na utarabu;
Maofisini na sehemu mbalimbali Dr Slaa ni tumaini la wengi, miaka hii kuzungumzia CCM kwa uzuri ni kama tusi, hakuna anayetaka kujadili sera CCM kwa uzuri.
CCM imekuwa kama mtu asiyeoga lakini anajitahidi kuvaa vizuri kwa nguzo za gharama kubwa, kitakachomumbua mtu huyo ni harufu mbaya.