Kikwete Mbeya: Mgongano na wananchi na mwitikio wa serikali

..

,..na hapo maneno rare ya busara wakati wa uchaguzi alipokuwa akilalamikia mbinu chafu za mtandawo ya SUMAYE yatatimia "ukiona mtu anatumia kalamu kuingia madarakani basi mkue kuwa akishaingia atatumia BUNDUKI kusalia madarakani....

Nadhani Mhe Sumaye alinusa hatari hii, kwa sababu ni mmoja wa majeruhi wa siasa za "Majitaka" za wanamtandao. Kwa kweli kauli hii ya busara tutaikumbuka sana sisi wapiga kura wa mwaka 2005.
For real, "What Goes Around Comes around".
 
Hivi kwa nini Rais atembee usiku?Nani anawajibika na usalama wa Rais? RC na RPC walikua wapi?
 
Ilianza JF kufichua mambo, wana forum wakatiwa ndani. Ikafuata msafara wa Mkapa kuzomewa, vijana wakatiwa ndani. Wananchi wakashikia mabango msafara wa Kikwete, wakasweka rumande. Juzi Kubenea katoboa, gazeti limefungiwa. Na sasa walevi eti wamerusha mawe, kijiji labda kitaangamizwa. Je, wananchi hapa tunajifunza nini ? Ukificha maradhi kilio kitakuumbua - Mwl. Nyerere. Bila shaka tukiogopa na kunyamaza, mawe yatapiga kelele - yangu macho for it's just a matter of time !!
 
Vyovyote vile lakini kilichotokea Huko Mbeya ni cha KULAANI.

Nikitendo cha kijinga na aibu kumpiga rais wenu mawe. Kama wanamatatizo wafuate channels zilizopo.

Na huyo mkuu wa mkoa inatakiwa ajiuzulu mara moja, ameshindwa kuwaandaa wananchi kumpokea rais vizuri.

Mie ninalaani sana kitendo hicho

siyo kitendo kizuri at all. Mkuu wa Mkoa anawajibika kutembeza Rais usiku, ajiuzulu.Angekuwa ameandaa watu wake vizuri yasingetokea
 
Lakini mawe aliyopigwa Rev. Mtikila yalihalalishwa hapa, au tofauti ni aina ya mawe yanayotumika?

wengine walihalalisha siyo mimi. Napinga uhalifu kwa jina lake. Ndio maana nilikataa kudai kuwa waliompiga ni wanachama wa Chadema kama nilivyokataa kuwa waliowapiga mapanga wananchi waliokuwa kwenye mkutano wa Chadema ni wana CCM. Wanaofanya vitendo hivyo ni wahalifu who happens to belong to a certain association...
 
Jamani kuuliza si-ujinga,tukio hilo la kupigwa mawe msafara wa Muungwana lilitokea usiku wa saa ngapi??? 1usiku,4usiku au 7usiku??.....
 
Mzee Mwanakijiji,

Confirmation niliyopata ni kwamba Sata bado yuko ndani pale polisi Kyela. Wale vijana wengine wameachiwa.

Pia aliyeniambia alitumia neno kijana wa CHADEMA anayeitwa Sata, kwahiyo hapo suala nafikiri ni zaidi ya siasa za Kyela.

Soma PM yako.
 
Habari zaidi ambazo gazeti ilizipata zinaeleza kuwa hatua ya wananchi hao kufanya uhalifu huo ilitokana na hasira ya kushindwa kumwona Rais Kikwete baada ya kumsubiri kwa muda mrefu ili apite katika kijiji hicho na ili wamweleze kero zao.

Kutokana na muda kuwa umekwenda na giza kutanda, Rais Kikwete hakuweza kusimama katika kijiji hicho, hali iliamsha hasira za watu hao ambao waliamua kukusanya mawe na kuanza kushambulia magari yaliyokuwa kwenye msafara.

Watu badala ya kujadili kiini cha tatizo wana spin tu hapa... kwa kifupi kama muda ungeruhusu Rais kusimama hapo hayo mambo ya mawe yasingekuwepo...

Hizo ngonjera nyingine sijui mapinduzi sijui nini ni kufurahisha baraza tu endeleeni simo!
 
Nikitendo cha kijinga na aibu kumpiga rais wenu mawe. Kama wanamatatizo wafuate channels zilizopo.

Na huyo mkuu wa mkoa inatakiwa ajiuzulu mara moja, ameshindwa kuwaandaa wananchi kumpokea rais vizuri.

Mkuu Fairplay,

Huwa ninaheshima sana na michango yako alyways hapa JF, lakini not this one, kwa sababu umenikumbusha siku nilipomliza Mkapa na maswali akiwa rais akakasirika na kuvunja mkutano na kukataa chakula, huku akimshambulia balozi kwa maneno kama yako kwamba eti kwa nini alitayarisha mkutano na wananchi huku akijua fika kuwa watu kama mimi ni wapinzani, mawazo kama haya ni pathetic na ni low IQ indeed!

I mean what RC has to do na mawazo ya wananchi? Hivi hatukuwaarifu mapema hapa kwamba kipigo cha Mtikila Tarime ni ujumbe mzito kwa viongozi wetu kuwa wasipowasikiliza wananchi kwa maneno na hoja watakula vipigo kama cha Mtikila? Sasa unasema kwamba RC alitakiwa kujua kuwa wananchi waliochoshwa na ufisadi watafanya nini rais asiyewachukulia hatua mafisadi na anayeruhusu kufungiwa kwa gazeti la wananchi Mwanahalisi atakapokuja kuwatembelea watafanya nini kweli inapaswa kuwa ni brainer au unahitaji kuwa professor kuelewa kuwa atapigwa mawe kama walivyofanya hawa wananchi? Are you serious au unatania mkuu?

Eti wakulaumiwa hapa ni RC are you kidding me? Yaaani ujumbe wa Tarime haujafika tu mpaka leo kuwa wananchi wamechoka na ujinga? Yaani tunawapa utabiri hapa kila siku na wanatuuliza kila siku tu-clarify tunachosema tunawafanyia kumbe yanaingia sikio moja na kutoka la pili? Sasa mkuu wangu unashangaa na kumlaumu RC? Yaani unasema kuwa tunamuona mwizi hapa anaiba tumuache maana ni tatizo la shetani sio Mungu?

Eti ajiuzulu RC? Kwa kosa gani? Kwa kosa la kutoingia vichwani mwa wananchi in advance na kujua kwamba watarusha mawe? I mean unasema tuwafukuze kazi polisi wote bongo kwa kutokujua mapema ni lini majambazi wataiba does that make a sense to you? Mimi sio a fan wa RC wa huko wala sikubaliani na mwendo wa kusua sua wa rais on mafisadi, I do not like it period, siwezi kumpiga mawe kwa hilo la mafisadi, lakini siwezi kuwa-prejudge wananchi wote wenye hasira kama yangu na ufisadi watafanya nini mbele ya mkuu wa nchi,

Tunashukuru sana kwamba rais hakuumizwa na hayo mawe, lakini nimesikia kuwa huenda waziri wa Miundo Mbinu alikula some of it, tunawapa pole sana, lakini ninaomba watafakari the message behind hayo mawe ni kwamba wananchi wamechoshwa na siasa za ujinga na zinazotabirikia kirahisi, yaani ukiona wananchi wamefikia mahali wanatabiri mapema kua Lowassa ataachiwa tu si rafiki wa rais na kweli anaachiwa kutanua hela za ufisadi za kodi ya wananchi, basi ujue kuna ujumbe mzito unakuja soon kutoka kwa hawa wananchi na this could be one of the ujumbes, yaani mawe!.

Na hata wakubwa wa dunia wanaelewa maana ya vita na ufisadi, ndio maana leo waliwaita wakuu wa gazeti moja kubwa nchini, balozi karibu nane leo ziliamua kutaka kujua hasa kilichotokea na kupelekea kufungwa kwa gazeti la wananchi Mwanahalisi, balozi kama za EU, UK, Canada, Sweeden, na Holland leo wamekutana na vigogo wa habari Dar kuwapa nafasi ya kuwaeleza wakubwa dunia kilichojiri na Mkuchika, na wamewaahidi kwamba katika hela wanazoji-commit katika ufadhili wao kwa serikali yetu, kwa mgawo huu bado hawajatoa 12%, kwa hiyo huenda wasiitoe iwapo hawataridhika na hii ishu,

Sasa mkuu Fairplay, kila mtu na nafasi yake hapa kwenye vita na mafisadi, anayerusha mawe anayeweza kuandika, anyeweza kuzuia ufadhili, I mean anything kumkosesha tembo usingizi! ni fair deal! kama sio politics! Mkuu ungana na wananchi kulilia utawala wa haki na sheria

Ahsante Mkuu!
 
Hofu yangu ni kuwa tutaanza kuingia kwenye udikteta taratibu na hakuna atakayekuwa tayari kuuona.

Tumeshaingia au tutaingia? Mifano;
mwanahalisi kutishiwa hatimae kufungiwa
polisi kurudi sokon mwanjelwa kusaka walioimba mbele ya raisi
Kubenea kuitwa polisi
mafisadi kupewa muda wa kurudisha pesa
watuhumiwa wa Richmond kupeta
watu kujifanya miungu watu nk
 
mazungumzo kati ya rc mbeya na jk ikulu ndogo baada ya tujio hili yalikuwa hivi
jk, hivi rc nini kimetokea pale kanga kjijini kwenye ule msafara?

Rc mwakipesile- mzee mkuu wangu, wale wana kijiji walikuwa na hamu ya kukuona , manake pale ndo ulipata kura 100% mwaka 2005

jk-ikawaje sasa? ndo warushe mawe?

rc- hapana mkuu wangu, wale wamechanganyikiwa, fikiria tangu ulipoamua kugombea urais 1995, hawa walikuwa na hamu ya kukuona, wakasema siku ukichaguliwa rais ukatembelea kijijini hapo watakupa zawadi ya kanga dume(kijiji cha kanga kuna kanga wengi by the way)

jk- kwa hiyo?

rc, yale mawe yaliyorushwa, kwa kimila ni ishara ya kumpokea mgeni mkuu, manake ile kusikia unakaribia tu ndo wakafurahi wakawa wanashangilia kwa kurusha maua na mawe!

kwi! kwi!
 
Kwi kwi kwikwi kwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii We Mwikimbi mbavu zangu lazima uzilipe kwi kwi kwiiiii
 
Imetolewa mara ya mwisho: 17.10.2008 0004 EAT
•
Siri yafichuka msafara wa JK kupigwa mawe

Habari Zinazoshabihiana
• Mzambia abambwa akitibiwa majeraha ya risasi kwa siri 02.09.2008 [Soma]
• Mtu, mkewe wauawa kwa kupigwa mawe 08.04.2008 [Soma]
• Kifusi chaua 2 mgodini Morogoro 19.02.2008 [Soma]

*Wanausalama wamwagwa
*Kijiji husika sasa ni hofu

Na Waandishi Wetu, Mbeya

KIU ya wananchi wa maeneo ya vijijini kutaka kuonana, kuzungumza na kumuuliza maswali Rais Jakaya Kikwete ndicho chanzo kikuu cha vurugu zilizotokea juzi ambapo baadhi ya wananchi hao walifikia hatua ya kuyarushia mawe baadhi ya magari yaliyokuwa kwenye msafara wa Rais, umebaini uchunguzi wa kina wa gazeti hili.

Majira limebaini kuwa wananchi hao waliokuwa na hasira walifikia hatua ya kuurushia mawe msafara huo, Rais akiwa ameshapita, ulipokuwa ukipita kwenye kijiji cha Kanga Mkwajuni ikiwa ni baada ya kusubiri tangu asubuhi wakiamini Rais Kikwete angesimama mahali hapo.

Hata hivyo kutokana na kuchelewa kwenye shughuli nyingine, msafara wa Rais ulipita kijijini hapo kukiwa kumeshaingia kiza na hivyo kutosimama.

Hali hiyo iliwaudhi wananchi hao kiasi cha baadhi kushindwa kudhitibi hasira zao na kuona wamekosa fursa muhimu ya kusema ambayo kwa miaka mingi hawakuwa na pa kusemea.

Ziara ya Rais Mbeya imekuwa na matukio mengi ikiwemo wafanyabiashara wa eneo la Mwanjelwa kuzuia msafara huo kwa lengo la kutaka kuzungumza naye mwanzoni tu mwa ziara yake.

Wananchi wengine pia wamekuwa wakihoji juu ya ahadi ya maisha bora kwa Rais na kutaka kumuuliza Rais mwenye ili kupata majibu.

Mzee Pambeya Kyando (90) ni kielelezo kikubwa cha wakazi wa Mkoa wa Mbeya ambao walikuwa na shauku ya kuonana na Rais na kueleza kero zao.

Licha ya uzee wake huo, alipenya kwenye kundi kubwa la wananchi wakati wa ufunguzi wa mradi mkubwa wa ujenzi wa Barabara ya Mbeya hadi Lwanjilo ili kukuta na Rais.

Pamoja na kuzuiliwa Rais Kikwete alisikia mzee huyo akilalamika na hivyo kugeuka na kutaka aruhusiwe kusalimiana naye; wakasalimiana na Rais akasikia dukuduku la mzee huyo.

Wachunguzi wa masuala ya sayansi za siasa na utawala wanasema bayana kuwa pamoja na wananchi kuwa na mitazamo tofauti ya kisiasa lakini wote wanakubaliana juu ya masuala moja muhimu; kwamba wananchi wengi wameshindwa kutatuliwa kero zao na viongozi walio nao kila siku katika kaya, vijiji, kata, wilaya na mikoa yao, hivyo kupata majibu au neno la Rais ni johari muhimu.

Habari zaidi kutoka Mbeya zinaeleza kuwa tayari maofisa usalama na Jeshi la Polisi wametumwa kwenda kijijini hapo kujua zaidi kiini cha hatua hizo za wananchi.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Bw. Zelothe Stephen amewaagiza maofisa wake kwenda kuchunguza huku kijijini hapo kukiwa kumejaa hofu. Hadi jana jioni bado hakukuwa na taarifa zozote za watu kukamatwa kuhusika na tukio hilo.

Katika hatua nyingine, Mwandishi Wetu Rashid Mkwinda anaripoti kutoka Mbeya kuwa baadhi ya wananchi wametoa maoni kuwa utaratibu wa ratiba ya ziara ya Rais Kikwete unakiuka usalama wa kiongozi huyo mkuu wa nchi kutokana na kutembezwa usiku hali iliyoruhusu msafara wake kupigwa mawe katika tukio la juzi usiku.

Wakizungumza mara baada ya taarifa ya msafara huo kupigwa mawe na watu wasiojulikana juzi, walisema miongoni mwa mambo ya hatari katika ziara hiyo ni msafara kutembea usiku.

"Safari ya kutoka Mbeya kwenda Chunya ni kilometa 75, kutoka Chunya kwenda Makongorosi hadi Mkwajuni ni kilometa 50 na kutoka Mkwajuni kurudi Mbeya ni kilometa 85, kwa hiyo ulikwenda zaidi ya kilometa 200 ziara hiyo ingeratibiwa vizuri, asingetembea usiku," alisema mkazi wa Mbalizi ambaye hakupenda kutajwa jina lake.

Alisema, hajawahi kuona msafara wa kiongozi wa nchi ukipita usiku, hususani kwa kiongozi mkuu na kwamba Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa inawajibika kwa lolote ambalo linaweza kumpata Rais katika safari yake.

"Huyu ni Rais, si mtu wa kawaida, ana watu wanaompenda na vile vile ana maadui wake wanaopinga maendeleo, jambo lolote linaweza kutokea. Kwa nini Kamati inashindwa kuratibu msafara wake?," alihoji mwananchi huyo.

Naye mkazi wa Mwanjelwa aliyejitambulisha kwa jina moja la Ambakisye, alisema anavyojua mikutano ya kiongozi yeyote wa Serikali na kisiasa, mwisho wake ni saa 12:30 jioni na baada ya hapo, mikutano husitishwa na kuendelea na itifaki zingine, ikiwamo kiongozi kupumzika.

Alisema ni vyema waratibu wa msafara wa Rais wangeweka mpango maalumu wa ziara, ili kudhibiti matukio yanayoweza kuathiri usalama wa Rais na kwamba lawama za lolote ambalo linaweza kumwathiri Rais zinatakiwa kuelekezwa kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya.

Ziara ya Rais mkoani Mbeya imekumbwa na misukosuko kadhaa kutoka maeneo mbalimbali aliyotembelea, ambapo katika siku ya pili ya ziara katika kitongoji cha Mwanjelwa, msafara wake ulisimamishwa na wafanyabiashara wa eneo hilo waliopanga mawe barabarani kwa lengo la kumzuia ili wananchi watoe kero zao.

Hata baada ya Rais kusimama na kuzungumza na wafanyabiashara hao, baadhi ya wananchi walisikika wakiendelea kuushutumu uongozi, kwa madai kuwa umekuwa ukikumbatia mafisadi na kudai kuwa ili Rais ajisafishe, anatakiwa kuwawajibisha watuhumiwa wote wa ufisadi.

Tuma kwa Rafiki Nakala inayochapika
 
Mbona hata zomea zomea nasikia inaendelea huko MBY lakini watu hawaweki wazi kabisa sijui wanaogopa kufungiwa?
Na lazima ajutie ubia wa urais.

Mkuu,

Unajua tuliposema kazomewa tulijaribu kupunguza UKALI wa maneno kwa kuwa tunamheshimu Rais wetu! Pale Mwanjelwa ilikuwa ni zaidi ya kuzomewa. Mama Salma Kikwete atakuwa anajutia kwa nini alitoka nje naye akidhani angepunguza munkari wa wazalendo. Aliyoyapata ni siri yake mwneyewe.

Msafara wa Rais ilibidi uingie 'vichochoroni' na kukwepa baadhi ya njia kule Uyole. Kuhusu waandishi kuweka wazi hilo SAHAU! Mikoani wengi wa waandishi ni 'waganga njaa' Labda hili nalo linahitaji thread yake pekee lakini ukweli ni kwamba Mikoani kuna hizi wanazoziita Press Club. Ningetegemea Press Club zingeuwa ni taasisi za kiraia kwa ajili ya kuwatetea waandishi lakini ukweli ni kwamba hizi PC ndizo zinachangia kuua fani ya Uandishi. Ungetegemea taarifa za ujio wa viongozi zingekuwa zinapelekwa kwenye Ofisi husika ya chombo cha habari na Wahariri ndio wangeweza kuteua waandishi ambao wangeongozana na msafara wa Kiongozi. Lakini wanaopelekewa taarifa rasmi huwa ni Press Club ambapo sasa hilo linakuwa ni dili kwa Kiongozi wa Press Club. Yeye ndiye anachagua ni mwandishi gani aongozane na msafara wa kiongozi. Serikali ya Mkoa wa Mbeya ilitoa nafasi tatu kwa waandishi wa habari kuongozana na ziara ya Rais. Lakini kuna 'mtu' alijitolea kutoa nafasi zingine tano ambazo angezigharamia yeye kila kitu. Unategemea habari ambazo hazimpendezi MKULU nani mwenye ubavu wa kuziripoti. Ukweli ni kwamba ziara ya MKULU wetu imekuwa na mazongezonge, labda tusubiri akina Kubenea wakirudi watatuandikia angalau kwa mtindo wa Makala.

Waandishi wengi wa huko Mikoani hawana ajira za kudumu kwenye vyombo vya habari vya Dar es Salaam, mara nyingi wanalipwa kwa habari walizoripoti na zikachapishwa au kutoka Redioni au kwenye TV. Unategemea nini wakisikia watakuwa kwenye msafara wa Rais? Huwezi amini siku hizi hata Mawaziri wanapokwenda kwenye Majimbo yao ya Uchaguzi ukiachia ziara za kiserikali wanakuwa na waandishi wao maalum.

Mbeya inatisha. Serikali ilibidi iongeze nguvu za Polisi kwa kuleta Polisi wengine kutoka nje ya Mkoa wa Mbeya. Pale Mwanjelwa hapakaliki. Anaendelea kutafutwa mchawi.

Habari zilizozagaa pale Mbeya Mjini ni kwamba Mwuungana ameahirisha Mkutano wake pale Uwanja wa Sokoine aliopanga kuhutubia kesho. Inasemekana kesho atakwenda Mwanjelwa kukabidhi Hundi ya Mkopo kutoka CRDB kwa ujenzi wa lile soko lililoungua halafu atambae zake Dar! Anyeways tusubiri habari za UHAKIKA kutoka kwa kina Mtanzania.
 
Mkuu Fairplay,

Huwa ninaheshima sana na michango yako alyways hapa JF, lakini not this one, kwa sababu umenikumbusha siku nilipomliza Mkapa na maswali akiwa rais akakasirika na kuvunja mkutano na kukataa chakula, huku akimshambulia balozi kwa maneno kama yako kwamba eti kwa nini alitayarisha mkutano na wananchi huku akijua fika kuwa watu kama mimi ni wapinzani, mawazo kama haya ni pathetic na ni low IQ indeed!

I mean what RC has to do na mawazo ya wananchi? Hivi hatukuwaarifu mapema hapa kwamba kipigo cha Mtikila Tarime ni ujumbe mzito kwa viongozi wetu kuwa wasipowasikiliza wananchi kwa maneno na hoja watakula vipigo kama cha Mtikila? Sasa unasema kwamba RC alitakiwa kujua kuwa wananchi waliochoshwa na ufisadi watafanya nini rais asiyewachukulia hatua mafisadi na anayeruhusu kufungiwa kwa gazeti la wananchi Mwanahalisi atakapokuja kuwatembelea watafanya nini kweli inapaswa kuwa ni brainer au unahitaji kuwa professor kuelewa kuwa atapigwa mawe kama walivyofanya hawa wananchi? Are you serious au unatania mkuu?

Eti wakulaumiwa hapa ni RC are you kidding me? Yaaani ujumbe wa Tarime haujafika tu mpaka leo kuwa wananchi wamechoka na ujinga? Yaani tunawapa utabiri hapa kila siku na wanatuuliza kila siku tu-clarify tunachosema tunawafanyia kumbe yanaingia sikio moja na kutoka la pili? Sasa mkuu wangu unashangaa na kumlaumu RC? Yaani unasema kuwa tunamuona mwizi hapa anaiba tumuache maana ni tatizo la shetani sio Mungu?

Eti ajiuzulu RC? Kwa kosa gani? Kwa kosa la kutoingia vichwani mwa wananchi in advance na kujua kwamba watarusha mawe? I mean unasema tuwafukuze kazi polisi wote bongo kwa kutokujua mapema ni lini majambazi wataiba does that make a sense to you? Mimi sio a fan wa RC wa huko wala sikubaliani na mwendo wa kusua sua wa rais on mafisadi, I do not like it period, siwezi kumpiga mawe kwa hilo la mafisadi, lakini siwezi kuwa-prejudge wananchi wote wenye hasira kama yangu na ufisadi watafanya nini mbele ya mkuu wa nchi,

Tunashukuru sana kwamba rais hakuumizwa na hayo mawe, lakini nimesikia kuwa huenda waziri wa Miundo Mbinu alikula some of it, tunawapa pole sana, lakini ninaomba watafakari the message behind hayo mawe ni kwamba wananchi wamechoshwa na siasa za ujinga na zinazotabirikia kirahisi, yaani ukiona wananchi wamefikia mahali wanatabiri mapema kua Lowassa ataachiwa tu si rafiki wa rais na kweli anaachiwa kutanua hela za ufisadi za kodi ya wananchi, basi ujue kuna ujumbe mzito unakuja soon kutoka kwa hawa wananchi na this could be one of the ujumbes, yaani mawe!.

Na hata wakubwa wa dunia wanaelewa maana ya vita na ufisadi, ndio maana leo waliwaita wakuu wa gazeti moja kubwa nchini, balozi karibu nane leo ziliamua kutaka kujua hasa kilichotokea na kupelekea kufungwa kwa gazeti la wananchi Mwanahalisi, balozi kama za EU, UK, Canada, Sweeden, na Holland leo wamekutana na vigogo wa habari Dar kuwapa nafasi ya kuwaeleza wakubwa dunia kilichojiri na Mkuchika, na wamewaahidi kwamba katika hela wanazoji-commit katika ufadhili wao kwa serikali yetu, kwa mgawo huu bado hawajatoa 12%, kwa hiyo huenda wasiitoe iwapo hawataridhika na hii ishu,

Sasa mkuu Fairplay, kila mtu na nafasi yake hapa kwenye vita na mafisadi, anayerusha mawe anayeweza kuandika, anyeweza kuzuia ufadhili, I mean anything kumkosesha tembo usingizi! ni fair deal! kama sio politics! Mkuu ungana na wananchi kulilia utawala wa haki na sheria

Ahsante Mkuu!

Mkuu FMES,

Heshima mbele Mkuu. Maneno yako mazito sana. Kwa kuongezea tu ni kwamba habari zilishafika mapema sana pale Mbeya kwamba ziara ya Rais kule Chunya ingepokelewa 'kimtindo'

RC Mwakipesile ilibidi atangulie Chunya siku moja kabla ili 'kusafisha mapito ya Bwana' lakini hali inaoenekana haikuwezekana. Mwakipesile alipaswa kuwa Mgeni rasmi kwenye Mhadhara wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwenye Chuo Kimoja pale jijini Mbeya lakini dakika za mwisho alituma udhuru kwamba asingeweza kuhudhuria. Mambo ni magumu sana.

Vox populi, vox dei
 
Habari zilizozagaa pale Mbeya Mjini ni kwamba Mwuungana ameahirisha Mkutano wake pale Uwanja wa Sokoine aliopanga kuhutubia kesho. Inasemekana kesho atakwenda Mwanjelwa kukabidhi Hundi ya Mkopo kutoka CRDB kwa ujenzi wa lile soko lililoungua halafu atambae zake Dar! Anyeways tusubiri habari za UHAKIKA kutoka kwa kina Mtanzania.[/QUOTE]

ni kweli kwa sasa nipo mbeya, kuna gari ya matangazo inasikika ikitangaza KUWA ATALITEMBELEA SOKO LILILOUNGUA MWANJELWA SAA TATU KAMILI, SIJASIKIA CHOCHOTE KUHUSU MKUTANO WAKE PALE SOKOINE STADIUM
 
hatimaye jk ameonja joto ya jiwe mbeya kwa kulazimika kuifuta mikutano yote iliyokuwa ifanyike leo

1, leo saa tatu asubuhi alikuwa akutane na wananchi kwenye eneo la mwanjelwa kukabidhi cheki ya kujenga soko jipya, licha ya matangazo jana kutwa nzima, leo ame-cancel mkutano huo bila kutoa sababu

2. alikuwa pia ahutubie wakazi wa mbeya katika uwanja maarufu wa sokoine, uwanja huo umekuwa unaandaliwa kwa muda wa wiki zaidi ya tatu, ikiwa ni pamoja na kuboresha miundo mbinu ya barabara nk, sasa hatahutubia tena,

badala yake jk leo atakutana na wazee wachache, na viongozi kwenye ukumbi wa mkapa unaomilikiwa na jiji la mbeya kuanzia saa sita mchana. halafu ataruka kurudi dsm

jiji la mbeya limejaa wanausalama kila kona, na watu wa mbeya wanasubiri kwa hamu jk aondoke kuepusha karaha mbalimbali za kufungwa barabara, kutanda kwa ffu kila mahali na nakadhalika.

Ziara ya jk imenikumbusha niliyopata kuona nikiwa Uganda mwanzoni mwa mwaka jana. Wakati ikulu rasmi ya rais wa Uganda ikiwa ni Entebbe kama km 25 toka kampala, yoweri museveni yeye ana ikulu mbili zaidi mojawapo ikiwa ni nakasero, na ingine Jinja. Museveni anawajibika wakati mwingine kusafiri kwa halikopta toka nakasero kwenda entebe kwa kuwa anaishi kwa wasiwasi mwingi mno. JK mbeya amekuwa na wasiwasi kama wa museveni, kulikoni mtu ambaye wana mbeya waliandama kuanzia imezu (km 17) toka mbeya (Tusi)(Tusi)(Tusi)(Tusi)karibisha wakati anakuja kwenye kampeni 2005, leo anashindwa kuwahutubia na kukutana nao? kulikoni jk?
 
Hii kuikimbia haijaa kaa sawa kwa mujibu wa ratiba si ilikuwa leo aondoke tu leo? sasa hii sensationalization kuwa jk "kuikimbia" ndio ushabiki mwenyewe huu.
 
1, leo saa tatu asubuhi alikuwa akutane na wananchi kwenye eneo la mwanjelwa kukabidhi cheki ya kujenga soko jipya, licha ya matangazo jana kutwa nzima, leo ame-cancel mkutano huo bila kutoa sababu
Amesoma alama za nyakati.
Ameelewa kuwa patakuwa hapatoshi hapo amekumbuka yale mawe.
2. alikuwa pia ahutubie wakazi wa mbeya katika uwanja maarufu wa sokoine, uwanja huo umekuwa unaandaliwa kwa muda wa wiki zaidi ya tatu, ikiwa ni pamoja na kuboresha miundo mbinu ya barabara nk, sasa hatahutubia tena,
Yawezekana maandamano ya kumpongeza yangekuwa magumu kuelekea hapo Sokoine kwani si mbali sana na Mwanjelwa kwa hiyo kabumbuluka.
Lakini yawezekana anataka kupaa ngoja tusubili.
Rais wetu kazi anayo.
 
Back
Top Bottom