Kikwete Mbeya: Mgongano na wananchi na mwitikio wa serikali

Hellow.. is somebody in???? Nipashe na Dar leo nalo nalifungua kwa miezi mitatu kwa kuandika habari za uchochezi uchonganishi kati ya familia ya raisi na raisi mwenyewe na raisi na wananchi wake

SICKNESSS.......
 
..........mweeee....Tufwileeeee.......Chifu Mwangupuli (Kikwete) kapigwa maweeee!!!!.......aaggghh......hizi heshima za watani wangu sizitaki kabisa...........kwi kwi kwi kwi kwi
 
Mtanzania vyanzo vyako wewe vinasemaje kuhusu suala hili, hebuni tusaidie kufuatilia maana nimegonga mwamba...
 
Siifurahishwi na hili jambo hata kidogo japo linatoa message ya moja kwa moja kwa mhusika kwamba wananchi hata wale ambao tulizoea kuwaona wakishangilia hata visivyostahili kisa vinasemwa na kiongozi wa juu wa nchi wamefika mahali wanaanza kutambua.Wananchi wa kawaida wanaoishi vijijini ambao kwao kupanda kwa gharama ya maisha wanaiona kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta ya taa ambayo wanatumia katika vibatari vyao(ikumbukwe bei hii imepanda maradufu tokea kuingia kwa awamu ya JK).

Bei za pembejeo za kilimo ziko juu,hivyo kuwafanya wakulima wengi kutotumia mbolea na hivyo kufanya uzalishaji wao kuwa mdogo.

Badala ya kutumia nguvu kubwa katika kukabiliana na wananchi hawa wenye uchungu,nafikiri ilikuwa ni vyema muungwana kutuma watu wa usalama wachunguze ni nini hasa madai/matatizo ya wananchi hawa yanayopelekea wawe na chuki kiasi hicho kwa kiongozi wao wa nchi.Hiyo itamsaidia kufahamu vipaumbele vyake viwe nini kwasasa na pengine inaweza kumfanya akaahirisha ziara zake za amerika kusini na marekani anazotarajia kuzifanya hv karibuni.

Nasema hili liwe fundisho kwa viongozi wetu kwamba wananchi wa Tanzania wasasa wameamka na si wajinga tena.

Kinyamana,

Mbona majibu ya hou uchunguzi unaopendekeza ni rahisi sana? kwa nini tupoteze pesa kuchunguza kitu ambacho tunakijua?

Mishahara ni midogo, walimu wanagoma, wanafunzi wanagoma, barabara mbovu, chakula haba, umeme shida, maji shida, bei za mazao mbaya, viongozi wabovu, uzururaji, uzembe, uhujumu na ufisadi ni mkubwa katika viongozi, dawa hakuna, ajira hakuna, muafaka Zanzibar hakuna, Mafisadi wanapeta! Je niendelee?

Achukue ripoti ya Benki kuu ya kila miezi mitatu kuonyesha mambo ya uchumi. Asome ripoti ya gazeti la Economist kuhusu hali mbaya Tanzania, asome ripoti ya Transparent Index ajue ni vipi tulivyo wabovu!

Kikwete aka Mwankupuli ni kipofu wa makusudi, anajifanya hayaoni kwa kuwa yeye alidanganya watu millioni 20 kuwa atakuwa Raisi wao, kumbe yeye ni Raisi wa watu 10000 ambao ndio wananeemeka na Uraisi wake!
 
Hold on... mnakumbuka jana RPC aliniambia kuwa ana jambo "muhimu sana" anashughulikia... nilipopiga ilikuwa usiku kule nyumbani.... is this 2 + 2 ..?
 
jamani,mie nimeitafuta hii habari nimeikosa,sasa mwenye habari za kutosha tafadhali aziweke humu,au aiskani hio stori ya nipashe atuwekee humu fasta ili tuweze kutoa fair comments.

Imeandikwa gazeti la dar leo la mchana huu, search kwenye mtandao utalipata
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, akizungumza na waandishi wa habari saa 3:30 usiku Ikulu Ndogo mjini hapa, alisema waliofanya kitendo hicho ni walevi na kwamba serikali itahakikisha inachukua hatua kali dhidi yao.

Alisema kutokana na tukio hilo, ratiba ya Rais Kikwete katika ziara yake mkoani humo itabadilika na msafara wake hautatembea tena usiku.

Kuanzia sasa hivi ratiba ya msafara wa Rais kutembelea sehemu mbalimbali za mkoa itabadilishwa kwa kuanza mapema asubuhi na kurejea mapema ili kuepuka tukio kama la leo (jana) lisijirudie, alisema.

Mwakipesile alisema tayari kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kimepelekwa katika kijiji cha Kanga kusaka wahusika wa tukio hilo la aibu kuwahi kutoka katika Jamhuri ya Tanzania.

SOURCE: Nipashe

Bado wamelala hao, nyie waacheni tu waendelee kulala… kwetu sis ni vizuri zaidi. yani tukio zima la muhimu waliloliona la kutatua ni kubadili muda wa safari tuuu?????????
 
Msafara wa JK wapigwa mawe

2008-10-16 13:47:02
Na Thobias Mwanakatwe, Chunya
...........Tukio hilo la kusikitisha lilitokea katika kijiji hicho majira ya saa 7:30 usiku wakati msafara wa Rais................

....................na madaktari ambao wapo katika msafara wa Rais mara baada ya magari kuwasili katika Ikulu Ndogo ya mjini Mbeya majira ya saa 3.00 usiku.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, akizungumza na waandishi wa habari saa 3:30 usiku ................

SOURCE: Nipashe

Sielewi tukio lilitokea hasa saa ngapi. saa 1.30 usiku au saa 7.30 usiku. Saa zinanichanganya kwenye habari hii.
 
Hata kama ni walevi, lakini ujumbe umefika kuwa sasa watu wamechoka na uongozi mbove, history itamhukumu inabidi arudi kusoma historia za mapinduzi yote anzia frech revolution, Bolshevik na kuanguka Shah wa Iran, Shausheshko wa Rumania. hata kama atatumia dola namna gani, hata kama kichaka atamsaidia kumletea marine, kama wananchi wamemchoka hatakaa. Amejionea mwenyewe wananchi wa Tarime wakivyoonyeshwa kuchoshwa na ufisadi? sasa kama anataka kutafutia pa kutokea basi ni yeye aanze kwa kumuweka ndani Rotzam Aziz na Lowasa, hapo tutajua amejua nini Sita alimwambia ajaribu kuwa erious ili wananchi warudishe imani kwa serikali. Unajua hii ilikuwa kauli nzito haijawahi kutolewa na mwanasiasa yoyote aliyeko kwa serikali kumwambia raisi, ukiachia mwalimu alipoelezea udhaifu wa Mwinyi Kilimanjaro hotel. Sasa safari imeaanza hili sasa kalijua.
 
Hivi hawa wananchi nao wanafikiri nini kushambulia msafara wa Rais? Wamesahau yaliyowakuta watu wa Dujail, Iraq mwaka 1982? Kitakachotokea kwenye kijiji hicho ni collective punishment na tusipoangalia maisha ya watu wa huko will never be the same.

Hakuna kitu kibaya kama Rais akigeuka kuwa paranoid na watu wake wa Usalama wakaanza kujipendekeza kwa kuchukua summary actions. Kama tukio hili lilitokea usiku kule Chunya, there is no chance in heaven kuwa watakaokamatwa au kupigwa watakuwa ni watu wenyewe hasa isipokuwa wale ambao wataonekana ni rahisi kubebeshwa mzigo huo.

Hofu yangu ni kuwa tutaanza kuingia kwenye udikteta taratibu na hakuna atakayekuwa tayari kuuona.
 
Tanzania inakoelekea kunatisha. yaliyotokea Tarime ambako Msekwa alitishia wananchi kuwa ametumwa na Kikwete ili kuchunguza hali ya usalama kabla ya kuleta majeshi "kutuliza amani" ndiyo yatafuatia hapo.

Badala ya viongozi wetu kuhangaika kutatua matatizo ya wananchi, wao wanafikiria mbele namna watakavyo-deal na wananchi watakaochoshwa na status quo.
 
Mwanakijiji,
Umekumbusha kitu muhimu saana hapa, waandishi hili waliandike bila woga, hii ya kuadhibu kijiji chote ni lazima ikemewe kwa nguvu zote na umma wote. Wasaidizi wawakumbushe hao wanaokwenda kufanya hivyo kuna siku watafikishwa mahakamani kujibu haya. Si wameona lakini yanayowapata askari waliotumwa na Zombe? Hii si Zanzibar, kazi imeanza kusafisha uchafu
 
Tanzania inakoelekea kunatisha. yaliyotokea Tarime ambako Msekwa alitishia wananchi kuwa ametumwa na Kikwete ili kuchunguza hali ya usalama kabla ya kuleta majeshi "kutuliza amani" ndiyo yatafuatia hapo.

Badala ya viongozi wetu kuhangaika kutatua matatizo ya wananchi, wao wanafikiria mbele namna watakavyo-deal na wananchi watakaochoshwa na status quo.

hutakiwi kushangaa na kuona kama hali inatisha... hii hali zazima itokee maana inatengenezwa na wao... hakuna any other way out kama viongozi wanawahandle wananchi kwa dharau kubwa kiasi hiki
 
Inanishangaza jinsi "walevi" wanavyoweza kujipanga na kujiongoza hadi kumudu kushambulia msafara wa Rais wa nchi na kuharibu magari 12. Ajabu kubwa hii. Kila mhusika ajiangalie katika hili kuanzia wapiga mawe, wapigwa mawe, na wanaoita wenzao walevi, wote kabisa kuna tatizo kubwa hapa!
 
Mtanzania na Nsaji (wazoefu wa siasa za Mbeya) wako wapo leo? muwashauri tu hao wanakijiji wahame hicho kijiji kabisa kibakie 'abandoned village' na tutakiingiza kwenye kumbukumbu za taifa.
 
Jamani hii habari inanipa raha! naona muisome tena hapa nimeikoleza, naona tuna waandishi wa habari wchache sana kama huyu..

Msafara wa JK wapigwa mawe

2008-10-16 13:47:02
Na Thobias Mwanakatwe, Chunya


Ziara ya Rais Jakaya Kikwete mkoani Mbeya imeingia dosari baada ya wananchi wa kijiji cha Kanga wilayani Chunya kupiga mawe magari sita yaliyokuwa katika msafara wake yakiwa yamewabeba mawaziri, waandishi wa habari na viongozi waandamizi wa serikali na kusababisha baadhi yao kujeruhiwa.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea katika kijiji hicho majira ya saa 7:30 usiku wakati msafara wa Rais ukiwa njiani kuelekea Mbeya mjini ukitokea mji wa Mwakwajuni wilayani Chunya ambako Rais Kikwete alikuwa ziarani.

Miongoni mwa magari yaliyopigwa mawe ni la Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawabwa, ambalo jiwe lilipiga upande wake na kugonga `wepa`. Hata hivyo, halikuvunja kioo wala kumjeruhi Waziri huyo.

Magari mengine yaliyopigwa mawe ni la Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwatumu Mahiza, gari la Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Thomas Mwang`onda lenye namba za usajili T 894 AAY na gari namba STK 2429 lililokuwa limewabeba waandishi wa habari, ambalo limevunjwa vioo vya mlango na waandishi wawili kujeruhiwa.

Magari mengine yaliyopigwa mawe na wananchi hao ni STK 3240 na STJ 3958 linalotumiwa na Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya, katika msafara huo lilikuwa limewachukua maafisa wa serikali kutoka Ikulu.

Kutokana na tukio hilo, waandishi wawili wa magazeti ya serikali pamoja na kijana mmoja, Chipukizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wote walijeruhiwa na walipewa huduma ya kwanza na madaktari ambao wapo katika msafara wa Rais mara baada ya magari kuwasili katika Ikulu Ndogo ya mjini Mbeya majira ya saa 3.00 usiku.

Baadhi ya viongozi waliozungumza na gazeti hili katika Ikulu Ndogo, walisema kuwa wananchi waliofanya tukio hilo walikuwa wamejipanga pembeni mwa barabara na baada ya magari manne ya mwanzo kupita, ndipo mawe yalianza kuvurumishwa.

Baada ya magari hayo manne kupita, magari yaliyokuwa nyuma yalianza kuvurumishiwa mvua ya mawe na wananchi hao.

Habari zaidi ambazo gazeti ilizipata zinaeleza kuwa hatua ya wananchi hao kufanya uhalifu huo ilitokana na hasira ya kushindwa kumwona Rais Kikwete baada ya kumsubiri kwa muda mrefu ili apite katika kijiji hicho na ili wamweleze kero zao.

Kutokana na muda kuwa umekwenda na giza kutanda, Rais Kikwete hakuweza kusimama katika kijiji hicho, hali iliamsha hasira za watu hao ambao waliamua kukusanya mawe na kuanza kushambulia magari yaliyokuwa kwenye msafara.

Hata hivyo, gari la Rais Kikwete, mke wake pamoja na walinzi wake hayakuhusika katika kadhia hiyo ya aina yake inayoashiria kuporomoka kwa maadili kwa kiwango cha juu kwa wananchi kiasi cha kutokuheshimu hata msafara wa kiongozi mkuu wa nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, akizungumza na waandishi wa habari saa 3:30 usiku Ikulu Ndogo mjini hapa, alisema waliofanya kitendo hicho ni walevi na kwamba serikali itahakikisha inachukua hatua kali dhidi yao.

Alisema kutokana na tukio hilo, ratiba ya Rais Kikwete katika ziara yake mkoani humo itabadilika na msafara wake hautatembea tena usiku.

Kuanzia sasa hivi ratiba ya msafara wa Rais kutembelea sehemu mbalimbali za mkoa itabadilishwa kwa kuanza mapema asubuhi na kurejea mapema ili kuepuka tukio kama la leo (jana) lisijirudie, alisema.

Mwakipesile alisema tayari kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kimepelekwa katika kijiji cha Kanga kusaka wahusika wa tukio hilo la aibu kuwahi kutoka katika Jamhuri ya Tanzania.

Tukio hili linatokea siku tano tu baada ya msafara wa Rais Kikwete kusimamishwa mara tatu na wakazi wa mkoa huo, Oktoba 10, mwaka huu siku alipoanza ziara ya siku 10.

Katika matukio hayo yaliyoanzia Mbeya Mjini eneo la soko la Mwanjelwa, wananchi walisimama barabarani kuzuia msafara wake ili kumweleza kilio chao juu ya mafisadi kutokuadhibiwa na hali ya maisha kuzidi kuwa duni miongoni mwao.

Pia walitaka kupewa sababu za kutokuwekwa matuta barabarani hali ambayo imesababisha watoto wao wengi kugongwa na magari; wananchi hao kadhalika walitaka kujua kwa nini hawana huduma ya maji safi.

SWALI: Je wananchi hawa wangekuwa na silaha za moto,JK angepona kweli naona, hivi? siyo kweli tunaongozwa na Rais ambaye watanzania wengi wameshamuua mawazoni mwao? wamekosa tu uwezo au chansi?
waberoya
 
Inanishangaza jinsi "walevi" wanavyoweza kujipanga na kujiongoza hadi kumudu kushambulia msafara wa Rais wa nchi na kuharibu magari 12. Ajabu kubwa hii. Kila mhusika ajiangalie katika hili kuanzia wapiga mawe, wapigwa mawe, na wanaoita wenzao walevi, wote kabisa kuna tatizo kubwa hapa!

Hapo ni 'WALEVI' tu muziki mnene hivi... sasa subiria ya wananchi 'SOBER'
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom