Kikwete Mbeya: Mgongano na wananchi na mwitikio wa serikali

Inanishangaza jinsi "walevi" wanavyoweza kujipanga na kujiongoza hadi kumudu kushambulia msafara wa Rais wa nchi na kuharibu magari 12. Ajabu kubwa hii. Kila mhusika ajiangalie katika hili kuanzia wapiga mawe, wapigwa mawe, na wanaoita wenzao walevi, wote kabisa kuna tatizo kubwa hapa!

Huyu Mwakipesile naye ni Mbumbu mzungu wa reli... anakashfu watu na akili zao kuwa ita walevi? Mbona hao walevi wasipigane wao kwa wao na hayo mawe? Ama Mwakipesile ndiye mlevi wa madaraka...? Najua wanakijiji wamepata shida na polisi lakini meseji sent..
 
Hii kitu inaweza kutumiwa pia kama mtaji wa kisiasa. Tusishangae kusikia baadae tuhuma kuwa hawa watu walitumwa na jamaa anayekusudia kugombea urais anaetokea mkoa huo. Mwakipesile hapo alipo anachekelea tu, ni kama ile ya "kichaa kapewa rungu sokoni......."
 
Mzee Mwanakijiji,

Hii habari kama ni kweli si Dr. Mwakyembe aende kuwatetea na kuwatoa hao vijana? Kama mbunge ana wajibu wa kulinda maslahi ya wapiga kura wake.

Ungewashauri waliokutumia ujumbe waufikishe pia kwa mbunge wao ili kama hana habari basi achukue hatua.

Itakuwa ni ukichaa kuwakamata vijana kwasababu tu wanalalamikia uongozi uliopo.


Mtanzania,
Hii habari kama ni kweli Dr Mwakyembe atakuwa kaishapata habari na pia atakuwa kawasaidia hao vijana kutoka.Thats all.
 


2008-10-16 13:47:02
Na Thobias Mwanakatwe, ChunyaZiara ya Rais Jakaya Kikwete mkoani Mbeya imeingia dosari baada ya wananchi wa kijiji cha Kanga wilayani Chunya kupiga mawe magari sita yaliyokuwa katika msafara wake yakiwa yamewabeba mawaziri, waandishi wa habari na viongozi waandamizi wa serikali na kusababisha baadhi yao kujeruhiwa.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea katika kijiji hicho majira ya saa 7:30 usiku wakati msafara wa Rais ukiwa njiani kuelekea Mbeya mjini ukitokea mji wa Mwakwajuni wilayani Chunya ambako Rais Kikwete alikuwa ziarani.

Miongoni mwa magari yaliyopigwa mawe ni la Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawabwa, ambalo jiwe lilipiga upande wake na kugonga `wepa`. Hata hivyo, halikuvunja kioo wala kumjeruhi Waziri huyo.

Magari mengine yaliyopigwa mawe ni la Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwatumu Mahiza, gari la Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Thomas Mwang`onda lenye namba za usajili T 894 AAY na gari namba STK 2429 lililokuwa limewabeba waandishi wa habari, ambalo limevunjwa vioo vya mlango na waandishi wawili kujeruhiwa.

Magari mengine yaliyopigwa mawe na wananchi hao ni STK 3240 na STJ 3958 linalotumiwa na Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya, katika msafara huo lilikuwa limewachukua maafisa wa serikali kutoka Ikulu.

Kutokana na tukio hilo, waandishi wawili wa magazeti ya serikali pamoja na kijana mmoja, Chipukizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wote walijeruhiwa na walipewa huduma ya kwanza na madaktari ambao wapo katika msafara wa Rais mara baada ya magari kuwasili katika Ikulu Ndogo ya mjini Mbeya majira ya saa 3.00 usiku.

Baadhi ya viongozi waliozungumza na gazeti hili katika Ikulu Ndogo, walisema kuwa wananchi waliofanya tukio hilo walikuwa wamejipanga pembeni mwa barabara na baada ya magari manne ya mwanzo kupita, ndipo mawe yalianza kuvurumishwa.

Baada ya magari hayo manne kupita, magari yaliyokuwa nyuma yalianza kuvurumishiwa mvua ya mawe na wananchi hao.

Habari zaidi ambazo gazeti ilizipata zinaeleza kuwa hatua ya wananchi hao kufanya uhalifu huo ilitokana na hasira ya kushindwa kumwona Rais Kikwete baada ya kumsubiri kwa muda mrefu ili apite katika kijiji hicho na ili wamweleze kero zao.

Kutokana na muda kuwa umekwenda na giza kutanda, Rais Kikwete hakuweza kusimama katika kijiji hicho, hali iliamsha hasira za watu hao ambao waliamua kukusanya mawe na kuanza kushambulia magari yaliyokuwa kwenye msafara.

Hata hivyo, gari la Rais Kikwete, mke wake pamoja na walinzi wake hayakuhusika katika kadhia hiyo ya aina yake inayoashiria kuporomoka kwa maadili kwa kiwango cha juu kwa wananchi kiasi cha kutokuheshimu hata msafara wa kiongozi mkuu wa nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, akizungumza na waandishi wa habari saa 3:30 usiku Ikulu Ndogo mjini hapa, alisema waliofanya kitendo hicho ni walevi na kwamba serikali itahakikisha inachukua hatua kali dhidi yao.

Alisema kutokana na tukio hilo, ratiba ya Rais Kikwete katika ziara yake mkoani humo itabadilika na msafara wake hautatembea tena usiku.

Kuanzia sasa hivi ratiba ya msafara wa Rais kutembelea sehemu mbalimbali za mkoa itabadilishwa kwa kuanza mapema asubuhi na kurejea mapema ili kuepuka tukio kama la leo (jana) lisijirudie, alisema.

Mwakipesile alisema tayari kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kimepelekwa katika kijiji cha Kanga kusaka wahusika wa tukio hilo la aibu kuwahi kutoka katika Jamhuri ya Tanzania.

Tukio hili linatokea siku tano tu baada ya msafara wa Rais Kikwete kusimamishwa mara tatu na wakazi wa mkoa huo, Oktoba 10, mwaka huu siku alipoanza ziara ya siku 10.

Katika matukio hayo yaliyoanzia Mbeya Mjini eneo la soko la Mwanjelwa, wananchi walisimama barabarani kuzuia msafara wake ili kumweleza kilio chao juu ya mafisadi kutokuadhibiwa na hali ya maisha kuzidi kuwa duni miongoni mwao.

Pia walitaka kupewa sababu za kutokuwekwa matuta barabarani hali ambayo imesababisha watoto wao wengi kugongwa na magari; wananchi hao kadhalika walitaka kujua kwa nini hawana huduma ya maji safi.

SOURCE: NIPASHE
Tuma Maoni YakoA
 
Vyovyote vile lakini kilichotokea Huko Mbeya ni cha KULAANI.

Nikitendo cha kijinga na aibu kumpiga rais wenu mawe. Kama wanamatatizo wafuate channels zilizopo.

Na huyo mkuu wa mkoa inatakiwa ajiuzulu mara moja, ameshindwa kuwaandaa wananchi kumpokea rais vizuri.

Mie ninalaani sana kitendo hicho
 
Hivi hawa wananchi nao wanafikiri nini kushambulia msafara wa Rais? Wamesahau yaliyowakuta watu wa Dujail, Iraq mwaka 1982? Kitakachotokea kwenye kijiji hicho ni collective punishment na tusipoangalia maisha ya watu wa huko will never be the same.

Hakuna kitu kibaya kama Rais akigeuka kuwa paranoid na watu wake wa Usalama wakaanza kujipendekeza kwa kuchukua summary actions. Kama tukio hili lilitokea usiku kule Chunya, there is no chance in heaven kuwa watakaokamatwa au kupigwa watakuwa ni watu wenyewe hasa isipokuwa wale ambao wataonekana ni rahisi kubebeshwa mzigo huo.

Hofu yangu ni kuwa tutaanza kuingia kwenye udikteta taratibu na hakuna atakayekuwa tayari kuuona.
..


,..na hapo maneno rare ya busara wakati wa uchaguzi alipokuwa akilalamikia mbinu chafu za mtandawo ya SUMAYE yatatimia "ukiona mtu anatumia kalamu kuingia madarakani basi mkue kuwa akishaingia atatumia BUNDUKI kusalia madarakani....
 
..


,..na hapo maneno rare ya busara wakati wa uchaguzi alipokuwa akilalamikia mbinu chafu za mtandawo ya SUMAYE yatatimia "ukiona mtu anatumia kalamu kuingia madarakani basi mkue kuwa akishaingia atatumia BUNDUKI kusalia madarakani....


Maneno mazito mkuu!!,

Mungu atuepushie tusifike huko
 
Vyovyote vile lakini kilichotokea Huko Mbeya ni cha KULAANI.

Nikitendo cha kijinga na aibu kumpiga rais wenu mawe. Kama wanamatatizo wafuate channels zilizopo.

Na huyo mkuu wa mkoa inatakiwa ajiuzulu mara moja, ameshindwa kuwaandaa wananchi kumpokea rais vizuri.

Mie ninalaani sana kitendo hicho

Unalosema ni kweli kabisa uhalifu ni uhalifu. Siyo kwa sababu aliyepigwa mawe ni Rais lakini kwa sababu ni kuingilia uhuru wa mtu mwingine kwenda anakotaka. Haiwezekani kuona kuwa kurushiwa mawe Rais ni kubwa mno kuliko watu wanaowekewa vigingi njiani na kuporwa au kushambuliwa wanapokuwa safarini.

Ni kwa sababu hiyo kitendo hiki kisionekane kuwa ni cha kisiasa bali ni uhalifu. Lakini pia ni vigumu mno kuonesha nani kafanya kitendo hicho kama hakuna picha, video n.k za kuonesha ni nani yuko responsible. Hatari yake ni kuwa na collective punishment ambapo kijiji hicho kitaadhibiwa kwa kushindwa "kuwataja" walioutupia mawe msafara wa Rais.
 
Sasa hata "Walevi" nao wanamwona muheshimiwa Rais myeyushaji, kweli mkuu wetu wa nchi ana safari pevu mbele yake.
 
Unalosema ni kweli kabisa uhalifu ni uhalifu. Siyo kwa sababu aliyepigwa mawe ni Rais lakini kwa sababu ni kuingilia uhuru wa mtu mwingine kwenda anakotaka. Haiwezekani kuona kuwa kurushiwa mawe Rais ni kubwa mno kuliko watu wanaowekewa vigingi njiani na kuporwa au kushambuliwa wanapokuwa safarini.

Ni kwa sababu hiyo kitendo hiki kisionekane kuwa ni cha kisiasa bali ni uhalifu. Lakini pia ni vigumu mno kuonesha nani kafanya kitendo hicho kama hakuna picha, video n.k za kuonesha ni nani yuko responsible. Hatari yake ni kuwa na collective punishment ambapo kijiji hicho kitaadhibiwa kwa kushindwa "kuwataja" walioutupia mawe msafara wa Rais.



Lakini mawe aliyopigwa Rev. Mtikila yalihalalishwa hapa, au tofauti ni aina ya mawe yanayotumika?
 
Mzee Mwanakijiji,

Ni kweli hao vijana wanne walikamatwa. Niliyeongea naye anathibitisha kuwaona hao vijana wakikimbizwa mchakamchaka kutoka stand ambako huyo Sata ndio ana duka kuelekea kituo cha polisi cha Kyela. Sata ndiye alikuwa mhusika mkuu, hao wengine walikuwa wapiga debe wake. Inasemekana walikamatwa kabla ya kutimiza hiyo adhma ya kupandisha mabango yao. Eti walisikika wakiongea kwenye simu kupanga huo mpango
na baada ya muda wakavamiwa na polisi.

Sijafanikiwa kujua kama bado wako ndani au wametolewa. Niliyekuwa namtafuta sikumpata, alikuwa mazoezini, nifikiri nitaweza ku confirm baadaye kidogo.

Inasikitisha sana, tunaweka ndani vijana kwakutumia haki yao ya msingi ya kuandamana kwa amani. Ukishindwa kuwaruhusu watu kutoa dukuduku zao, mwisho wake ni kupigwa mawe kama ilivyotokea Chunya.
 
Habari zaidi ambazo gazeti ilizipata zinaeleza kuwa hatua ya wananchi hao kufanya uhalifu huo ilitokana na hasira ya kushindwa kumwona Rais Kikwete baada ya kumsubiri kwa muda mrefu ili apite katika kijiji hicho na ili wamweleze kero zao. [/COLOR][/B]

Kutokana na muda kuwa umekwenda na giza kutanda, Rais Kikwete hakuweza kusimama katika kijiji hicho, hali iliamsha hasira za watu hao ambao waliamua kukusanya mawe na kuanza kushambulia magari yaliyokuwa kwenye msafara.


Kumbe kipigo hicho kinatokana na kumiss kwa sana rais wao mpendwa!!!! by the way ni nani aliyeeleza sababu hasa za kurushwa hayo mawe?
 
Mtanzania,
Hii habari kama ni kweli Dr Mwakyembe atakuwa kaishapata habari na pia atakuwa kawasaidia hao vijana kutoka.Thats all.

Nafikiri si busara kwa Dr. Mwakyembe kujihusisha moja kwa moja na hao vijana, busara hapo ni kumtumia mtu wa kati kufanya hiyo kazi. Kwa Dr. kujihusisha moja kwa moja ni kuendeleza ugomvi na Mwakipesile na hiyo inaweza kutumika kama turufu kuwa vijana wale walitumwa na Dr.
 
Vyovyote vile lakini kilichotokea Huko Mbeya ni cha KULAANI.

Nikitendo cha kijinga na aibu kumpiga rais wenu mawe. Kama wanamatatizo wafuate channels zilizopo.

Na huyo mkuu wa mkoa inatakiwa ajiuzulu mara moja, ameshindwa kuwaandaa wananchi kumpokea rais vizuri.

Mie ninalaani sana kitendo hicho

Dua la kuku!, kuna watu huwa wanawakataa wazazi wao kama hawakuwatunza au waliwatekeleza, sembuse Raisi wa nchi? mbona waliyofanya ni madogo? jamani kumbukeni wenzetu wanapigana vita, mSilisahau hili, viongozi wakijisahau na kuacha hisia na hali halisi ya wananchi iamue hatima yake ni vilio, usilaani hili rather than shangilia ukijua kama wewe unasema tu, wenzake wanatenda tu! the dont have JF na hakuna mtandao huko! ila wameamka, hata kama wamemka vibaya lakini wamemka! kama wananuka midomo na kupiga miayo ya nguvu, huku wakijinyosha basi uamkaji wao ndio huo, tunasikia sauti ya minyosho ya viungo vyao vikijibalance.Wakienda tu CHADEMA kuwaweka sawa na kuwaambia hatuendi kihivyo wataelewa, WATATUMIA NGUVU KIDOGO TU KWANI WAMESHAAMKA!, HATARI SANA KAMA WANANCHI WAKIAMKA VIBAYA SANA KAMA RWANDA BURUNDI...HAIJAWA HIVYO LETS CELEBRATE THEN .


waberoya
 
Back
Top Bottom