Kikwete kumalizia kumsafisha Lowassa

Mkuu Mwanakijiji, Uliwahi kumshauri EL kuwa karibu na Jk na yeye ndio amefanya hivyo katika, Nakumbuka katika makala zako katika gazeti la Tanzania Daima uliyasema haya bwana, Sisi hapa Tutajua ni yapi, Tazama hata yale ambayo Makamba anayafanya kule kwa Mh Sitta?? ndio utajua kuwa hawa jamaani lao moja.
 
Busara iko wapi, post yote inatukana waziwazi. mwizi! Jambazi! nk,nk. Haya yote ni matusi kwa wenzetu ambao hawajafikishwa mahakamani na kupatikana na hatia. Tuna tofauti gani na wale waliomkamata mtuhumiwa wa wizi wa mfukoni na kumchoma moto? Nahizi tuna jaziba sana ambayo katika siasa na uendeshaji wa utawala wa sheria hairuhusiwi.

Busara itawale vinywa vyetu na vidole vyetu katika kubandika maandiko yetu hapa, kwani siku moja tutahukumiwa kwayo. Mpaka sasa hakuna fisadi tanzania kwa sababu hakuna ambaye amethibitika mbele ya sheria kuwa aliifisadi nchi yetu.

Mimi sitosema sana juu ya mwenendo mzima wa serikali ya CCM. But one day El will come up as a hero. Yapo matukio ya kutosha kuthibitisha kuwa wana CCM hatuwezi kuyashughulikia hayo.

KATAA CCM, OKOA KIZAZI CHAKO.
 
Busara iko wapi, post yote inatukana waziwazi. mwizi! Jambazi! nk,nk. Haya yote ni matusi kwa wenzetu ambao hawajafikishwa mahakamani na kupatikana na hatia. Tuna tofauti gani na wale waliomkamata mtuhumiwa wa wizi wa mfukoni na kumchoma moto? Nahizi tuna jaziba sana ambayo katika siasa na uendeshaji wa utawala wa sheria hairuhusiwi.

Busara itawale vinywa vyetu na vidole vyetu katika kubandika maandiko yetu hapa, kwani siku moja tutahukumiwa kwayo. Mpaka sasa hakuna fisadi tanzania kwa sababu hakuna ambaye amethibitika mbele ya sheria kuwa aliifisadi nchi yetu.

Mimi sitosema sana juu ya mwenendo mzima wa serikali ya CCM. But one day El will come up as a hero. Yapo matukio ya kutosha kuthibitisha kuwa wana CCM hatuwezi kuyashughulikia hayo.

KATAA CCM, OKOA KIZAZI CHAKO.

Hueleweki Mkuu!
 
Tutazunguka sana mbuyu kila siku tunazunguka pale pale.
Hawa wote ni wachafu, wote walifaidika na fedha za EPA, Richmond, Kikwete ndiye aliyetumia fedha nyingi kuliko yeyeto.Unafiki ni mkubwa kuliko chochote hapa, wote wachafu hakuna wa kumsafisha mwenzie, ila sema kwa sababu wanawaongoza mandondo ndio maana wanachezea akili za watu.
 
Hili wala halinishangazi sana JK kuamua kumsafisha EL, siasa za tanzania zimejaa unafiki! si mmemsikia Makamba eti sasa anajifanya kumsifia SS, huyu mzee hana hata aibu anayakana maneno yake mwenyewe eti wau wanajaribu kuwagombanisha na SS, hata Guninita nae sasa anamuunga mkono SS, yote hii ni baada ya kumsikia bosi wao JK kasema hana ugomvi na wanaopinga ufisadi. Unafiki! unafiki! unafiki! mtupu umejaa ndani ya CCM. aaah haya tusubiri tamthilia nyingine hii ya richmond inaanza kupoteza mvuto sasa. ndio nasema tamthilia sababu CCM wote ni wasanii.

kuna jambo hapa,baada ya kuona reaction ya umma dhid ya maamuzi ya NEC na CC juu ya SS na wabunge ant-mafisad.makamba,m/kiti wake na timu yao wamekuja na hila! Kumghilibu SS kwa kumfanyia kampen mapema ya ubunge na pengne uspika 2010.wao wanahofu kama ataamua kugombea urais hata kupitia informal reunited opposition ni wazi mgombea wao ATAANGUKIA PUA!! Maneno aliyosema makamba urambo yanareveal ghiliba hii.anawezaje kumfanyia kampen SS hali akijua muda bado,lakin yeye kama mmoja wa viongoz wanaochuja majina ya wagombea hatakiw kuwa na mgombea kabla ya mchujo wa majina lkn pia hajui wanaCCM watakaochukua fom kugombea jimbo la urambo! Wanaweza kuwepo hodari zaid ya SS! Wanamdanganya SS.na inavyoonekana AMEGHILIBIKA! ATAJUTA!! kamwe uspika ausahau!! this s teknal character assassination!! Ubunge bila uspika 2010 kwa rekodi nzr aliyoweka ni kitanzi kwake na watanzania wapenda maendeleo wote!! NAMSHAURI AACHANE KABISA NA SIFA ZA REJA REJA ANAZOPEWA SASA NA MAKAMBA! Kwa nguvu,muda na rasilimali alizowekeza kutetea mafisadi ni sawa na ngamia kupita kwny tundu la sindano makamba kuongoka ghafla bin vu kumjoin SS na timu yake.kama SS ana akili atarudisha trust yake kwa makamba na m/kiti wake na kukubal sifa uchwara anazopewa.lakin kama hana akili ATATILIA MAANANI USHAURI HUU WA BURE! Tafakari.
 
Well, vyanzo vingine vya karibu vinadokeza kuwa kambi ya EL ilishtushwa na kauli ya JK kuwa la Kagoda litashughulikiwa bila ya kujali urafiki. RA na EL hawakupendezwa na kauli hiyo. Hivyo EL akatumwa kumbipu Jk kuwa afikirie mara mbili kwani wametoka "mbali"


Kama ni kweli kama inavyoandikwa kwenye vyombo vya habari kuwa wale maodita waliogundua EPA wamerudi kukagua vitabu vya BOT kuhusu Kagoda kwa shinikizo la wafadhili ; napia kuwa kashfa ya Richmuonduli itachunguzwa tena na Takukuru ikishirikiana na wapelelezi wa kimataifa,basi nadhani sasa ukweli ndio utadhihilika kwani yale ambayo Mwakyembe alisema waliyahifadhi hawakuyaweka kwenye ripoti yao sasa yananafasi ya kuwekwa wazi. Vimemo pia ambavyo watumishi wa serikali walivificha na hawakutoa kwa tume ya bunge ,sasa nadhani vinaweza kutolewa kwani sidhani kuwa hawa civil servants wao watakubali kutolewa kafara!! Maamuzi haya hayamsaidii Lowassa na mafisadi wenzie hata punje moja ;nadhani sasa ndio wataumbuka zaidi.
 
Back
Top Bottom