Kikwete kilimo kwanza, Lowassa elimu kwanza!

Ha ha ha...!Ni kama swali la kati ya yai na kuku kipi kilianza,sort of!Binafsi nadhani either or can stimulate the growth of our economy hence better standards of living and so forth.Kwa wale wanaodai elimu kwanza,je hawaoni kuwa ubongo unategemea sana chakula?Ni wazi kwamba ili upate elimu bora ni lazima uweze kula vyema kwanza....Kama tunaweza kuji sustain kwenye uwezo wa kujilisha,then tunaweza kumove on kuprioritize elimu.

Kuna wanaodai kuwa ni lazima kuwe na elimu ambayo itatupatia uwezo kulima kilimo bora,je mnazungumzia kilimo cha individuals ama mnazungumzia large scale?Ni vyema ukawepo mpango wa namna ya kuwalisha wananchi kwa large scale agriculture ambayo itakuwa sustained kwa kutumia irrigation projects.Huwezi kumpa mwananchi elimu kwanza bila ya kujua atakula nini.

Kuchagua kuku(kilimo) ni bora kuliko kuchagua yai(elimu),matokeo ya kuchagua either or ni the same,however kuchagua yai kuna implications ambazo zinaweza zisitufikishe kule ambapo uchaguzi wa kuku(kilimo)ungetufikisha.

Mfano ukichagua kuku(kilimo)una option ya kumkeep na baadae anaweza kupata yai(elimu) na manufaa yake,ambapo utakula kwa ajili ya protein na mengine utayaacha yaangue firanga ili kuweza kuzalisha kuku wengine(more agricultural sustainable capabilities).On the other hand,kuchagua yai(elimu) kunaweza kuwa costly kama hakuna sustainable enviroments ya kuyaangua ili uweze kupata vifaranga,ambavyo itabaidi uvikuze ,hapo ni gharama kabla hata ya manufaa,kwasababu mazingira ya kulifanya yai liangue ni sawa na mazingira ya elimu bora,yanategemea chakula bora,they go hand to hand....Na kwahiyo usipokuwa na chakula bora(kuku),hata hilo yai(elimu)halitapata wa kulilalia ili liangue vifaranga.

Kwa hiyo kwa upande wangu hadi uswa huu naungana na kauli ya kilimo kwanza unless members wengine mniconvince otherwise.
 
Nami nawapinga wote wawili. Uzalendo kwanza. Lowasa si msomi? Mbona hatuoni matunda ya usomi wake zaidi ya kuuza sura na kujigeuza kiwavi. Elimu gani kwanza anazungumzia huyu mamvi? Au ndio shule za kata. Wakishajenga moyo wa uzalendo waanze na elimu ya uraia
 
Nami nawapinga wote wawili. Uzalendo kwanza. Lowasa si msomi? Mbona hatuoni matunda ya usomi wake zaidi ya kuuza sura na kujigeuza kiwavi. Elimu gani kwanza anazungumzia huyu mamvi? Au ndio shule za kata. Wakishajenga moyo wa uzalendo waanze na elimu ya uraia
Toa sababu ni kwanini unapinga idea zote kwa pamoja....?Tafadhali stay kwenye hoja,ni ushauri tu mkuu.
 
Hakuna cha kilimo kwanza wala elimu kwanza.Adui namba moja wa maendeleo ya mtanzania ni ufisadi.Ondoa ufisadi hayo mengine yataji set yenyewe
 
Jana nimeangalia kwenye TV TBC, Lowasa alikuwa anapinga initiative ya rafiki yake kuhusu kilimo kwanza, anasema yeye anaamini elimu kwanza, kilimo baadae, inawezekana akawa na point, lakini mbona hakuyasema haya alipokuwa serikalinini? make wimbo wa kilimo kwanza JK kauanzisha siku nyingi.

LOWASSA ELIMU NA MSHIKO KWANZA! Alipokuwa Waziri Mkuu alihimiza shule za kata huku akiwa busy na miradi ya Alfa na kuchukua 50% kwenye kila mradi: RICHMOND, BUZWAGI n.k. na kuwahujumu waliokataa kumpa mshiko k.m. wahindi wa magorofa ya Masaki ambao aliwaadhibu kwa kubomoa magorofa yao na leo Serikali imeamuriwa na Mahakama Kuu kuwalipa fidia wahindi hao!
 
jana nimeangalia kwenye tv tbc, lowasa alikuwa anapinga initiative ya rafiki yake kuhusu kilimo kwanza, anasema yeye anaamini elimu kwanza, kilimo baadae, inawezekana akawa na point, lakini mbona hakuyasema haya alipokuwa serikalinini? Make wimbo wa kilimo kwanza jk kauanzisha siku nyingi.

walikosea, nadhani walikuwa wanamaanisha "ufisadi kwanza"!
 
bila kisiki cha ufisadi kuondolewa hakuna hata kimoja kinaweza fanikiwa, amkeni watu, and start reading between the lines.
 
Jana nimeangalia kwenye TV TBC, Lowasa alikuwa anapinga initiative ya rafiki yake kuhusu kilimo kwanza, anasema yeye anaamini elimu kwanza, kilimo baadae, inawezekana akawa na point, lakini mbona hakuyasema haya alipokuwa serikalinini? make wimbo wa kilimo kwanza JK kauanzisha siku nyingi.

I think both are right in this one. However, it is a matter of priority per say. Hii ina maana kwamba wote hawa wawili wanasema ukweli lakini nionavyo mimi suala ni kipi kitangulie? Kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa hili letu la Tanzania ukizingatia kwamba zaidi ya 80% ya Watanzania ni wakulima ama watu wanaoishi vijijini. Kwa mantiki hiyo sehemu kubwa ya uchumi pamoja na chakula kinachotegemewa na Watanzania wapatao milioni 43 inategemea kilimo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete yuko sahihi kusisitiza kilimo. Lakini kama suala ni kipaumbele cha mambo basi Mheshimiwa Edward N. Lowassa ana alama za juu. Nasema hivi kwa sababu ni watu wenye elimu ndio wenye uwezo wa kufanya kazi ya kilimo chenye tija. Knowledge is a power that transforms lives. Therefore, it must be "elimu kwanza" ili mkulima ajue namna ya kuitumia ardhi nk na pia aweze kuzalisha mazao ya kumwongezea kipatao cha kutosha na pia endelevu.

Kwa hiyo, nakubaliana kabisa na Mhe Lowassa kwamba elimu itangulie kilimo. Unajua wamekuwepo wakulima nchini kabla na baada ya uhuru lakini kilimo hakijawahi kuwa na tija kwa sababu ya ukosefu wa elimu. Kama tutaacha mtazamo "hasi" ukweli ndio huo ama niseme kwa lugha inayotumika sasa "habari ndiyo hiyo." Kuhusu kwa nini Lowassa anasema sasa, labda niseme kila jambo lina wakati wake. Pia ikumbukwe kwamba mtu anapokuwa nje ya ulingo anaweza kuona vizuri zaidi kuliko akiwa ndani. Kama yapo yaliyo zaidi ya hayo basi nitamwachia yeye, ila katika hili la elimu kwanza nakubaliana naye.
 
Hivi hii slogan ya waha jamaa imelenga nini??? nashindwa kujua unawezaje kuhubiri kilimo hali huna wataalam wa kutosha!elimu unapiga mgongo unahubiri kilimo!ni kilimo cha namna gani kinachosemwa?cha jembe la mkono???
 
Katika kile kinachoonekana kama ni kudharau au kupuuza kauli mbiu ya waziri mkuu PINDA, WM mstaafu Edward Lowassa akizungumza na jamii ya wafugaji Ifakara mkoani Morogoro, alisema waachane na kauli mbiu ya kilimo kwanza na wawekeze kwny ELIMU. TBC.
 
Anaweza kuwa sahihi sana. Elimu itaweza kuwasaidia zaidi kuliko kuongelea kauli mbiu zisizotekelezeka. Wewe umeshashuhudia KILIMO KWANZA wapi?? Kilimo hakiendeshwi majukwaani na maofisini. Tuulize wakulima tutakuambia afadhali ya misimu iliyopita.
 
hivi watu kiswahili kwenu kigumu sana! Ni lini lowasa alistaafu? Au tutafute walimu wa kiswahili na humu? Huyu fisadi anatupa shida sana mpaka leo umeme wa elfu 50 kuwasha taa tu haumalizi hata mwezi huku miaka ya nyuma tulikuwa tunalipa elfu nane! Kama alikuwa anajua maamuzi magumu kwa nini hakumkatalia jk kuleta richmond? Tena alivunja kabisa bodi ya tenda na kuunda ya kwake ambayo iliipa kampuni ambayo hata kwenye tano bora haikuwepo.
 
Kipao mbele cha taifa kinatakiwa kuwa afya kwanza then elimu na sio kilimo kwanza, kwani bila afya uwez kulima, kusoma, kuomba miongozo bungeni n.k ~ Prof Mark Mwandosya

V
SENGEREMA
 
waache waendelee kupingana hadi kieleweke. pm anampinga rais. Mbunge anampinga pm...
 
Back
Top Bottom