Mauaji ya Tupac; P Diddy anavyofunguliwa milango ya jela

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,507
14,370
SWALI mshangao ndani ya jumuiya ya Hip Hop ulimwenguni ni je, huu ni mwanzo wa safari ya jela ya bilionea P Diddy kwa mauaji ya Tupac Shakur?

Winston Churchill, Waziri Mkuu wa zamani wa UK, alipata kusema: “The truth is incontrovertible. Malice may attack it, ignorance may deride it, but in the end, there it is.” – “Ukweli haudhibitiwi. Uovu utaushambulia, ujinga utaudhihaki, lakini mwishoni, ukweli utadhihirika.”

Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, katika kitabu “Tujisahihishe” aliandika: "Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo, adui au rafiki, wote kwake ni sawa. Ukweli una tabia ya kujilipizia kisasi ukiona unapuuzwa. Ukweli haupendi kupuuzwa.”

P Diddy, zamani Puff Daddy au Puffy, jina halisi Sean Combs, alihusishwa na kifo cha Tupac tangu siku ya kwanza. Tupac alipigwa risasi Septemba 7, 1996. Alifariki dunia Septemba 13, 1996.

Kifo cha Tupac ni simulizi iliyokosa majibu ya maswali tata. Miaka 27 imepita tangu mauaji ya rapper huyo. Hatimaye, ukungu umepungua, mawingu yanaanza kuonekana. Je, ni mwanzo wa kuiona mbingu?

Binadamu ambao wameondoa ukungu ni wawili, gangsta la kutupwa, Keffe D na mpelelezi wa zamani, Idara ya Polisi Los Angeles (LAPD), Marekani, Greg Kading. Hao ndio wamemuingiza P Diddy katikati ya crime scene ya kifo cha Tupac.

Kading, mpelelezi mkuu wa mauaji ya Tupac, Septemba 28, 2011, alitoa kitabu “Murder Rap; The Untold Story Of The Biggie Smalls And The Tupac Shakur Murder Investigations.” – “Rap ya Mauaji; Hadithi Ambayo Haijasimuliwa Upelelezi wa Mauaji ya Biggie Smalls na Tupac Shakur.”

Katika kitabu hicho, sura ya 11, Kading anasimulia kuwa kipindi cha upelelezi wa vifo vya Tupac na hasimu wake, Notorious BIG, jina la Keffe D, lilitokeza mara nyingi.

Kading pia aliandika kuhusu nadharia inayomhusu P Diddy kuwapa jukumu Keffe D na Baby Lane, kuwaua Tupac na Big Dog wa Death Row Records, Suge Knight.

Kuna kitabu “Compton Street Legend” cha Keffe D, kilichotoka Februari 15, 2019. Ndani yake Keffe anajitaja yeye na Suge kuwa ndio mashuhuda pekee waliohai wa kifo cha Tupac.

Keffe pia anajisema kuwa yeye anazo taarifa zote kuhusiana na kifo cha Notorious BIG na Tupac. Maneno hayo yanaoana na kilichoandikwa na Kading kuwa kila walipofanya upelelezi kuhusu vifo vya Pac na Biggie, jina la Keffe lilitokeza mara nyingi.

Ipo kazi ya “kisnich” ambayo Kading aliifanya kwa kumrekodi Keffe kwa siri, akikiri kuhusika na mauaji ya Tupac. Sauti hiyo ya Keffe, iliivisha jalada. Keffe alikamatwa Septemba 29, 2023. Anatarajiwa kupandishwa mahakamani Novemba 2, 2023, kujibu tuhuma za mauaji.

Kukamatwa kwa Keffe, kulimuibua Suge, ambaye yupo jela, akitumikia kifungo cha miaka 28 kwenye gereza la RJ Donovan, San Diego. Mwaka 2018, Suge alikiri kosa la kuua bila kukusudia kwa kusababisha ajali ya gari mwaka 2015 na kukimbia.

Suge, baada ya kusikia Keffe amekamatwa, alisema ameshangazwa kwa sababu gangsta huyo wa Compton, hakuwahi kukamatwa. Suge alieleza kuwa amekuwa akiviambia vyombo vya usalama kwa miaka mingi, Keffe akikamatwa na kubanwa, atasema ukweli wote kuhusu kifo cha Pac.

Wakati wa mahojiano na wapelelezi wa Idara ya Polisi Las Vegas Metropolitan (LVMPD), Keffe alifichua kuwa Diddy alimpa donge la dola milioni moja, awaue Pac na Suge. Kabla ya hapo, Keffe alipata kusema kuwa Diddy hajamalizia malipo, dola 500,000.

Habari za malipo ya dola milioni moja kutoka kwa Diddy kwa mauaji wa Pac sio story ngeni. Hata majasusi wa FBI wanayo. Shida ni moja tu; jinsi ya kuithibitisha ili kumtia hatiani Diddy.

Earl Eric Martin “Von Zip” alikuwa muuza dawa za kulevya high level aliyeunga mtandao wake kuanzia maskani kwake East Coast (New York) hadi West Coast (California). Zip anatajwa kuwa ndiye alikabidhiwa dola milioni moja na Diddy kwa ajili ya kumlipa keffe.

Wanksta wa New York, 50 Cent, aliandika Instagram kutaka sheria ichukue mkondo wake, baada ya kubainika kifo cha Pac ni mchoro wa Diddy. Kisha, 50 alisema hajawahi kumpenda Diddy kwa sababu alijua siku nyingi kuwa ndiye alihusika na kifo cha Pac.

Wimbo “Hit Em Up” wa Tupac aliowashirikisha vijana wake wa Outlawz, umetajwa na Kading kama moja ya sababu ya kifo chake. Wimbo huo, Pac aliwashambulia moja kwa moja Bay Boy Records, akiwemo Diddy na Biggie. Diddy ndiye mmiliki wa Bad Boy.

TURUDI SEPTEMBA 7

Keffe katika “Compton Street Legend”, amesimulia mithili ya movie ya uhalifu. Inasisimua zaidi unapopata picha kuwa hiyo ni real story ya kifo cha rapa aliyependwa na anayependwa sana, Tupac a.k.a Makaveli The Don.

Kabla ya simulizi ya Keffe, tuanze na ratiba ya Death Row. Septemba 7, 1996 ni siku ya pambano la boxing, ubingwa wa uzito wa juu. Main card ni Mike Tyson vs Bruce Seldon. MGM Grand Garden Arena, Las Vegas, ndio eneo la tukio.

Mchana wa siku hiyo, Tupac na mchumba wake, Kidada Jones, pamoja na Suge, waliwasili Vegas. Saa 2:30 usiku, waliketi siti za safu ya mbele. Muda mfupi baadaye Tyson na Seldon walianza ku-exchange blows. Dakika ya kwanza, sekunde ya 12, Tyson alimpeleka Seldon sakafuni kwa hook ya kushoto.

Refa Richard Steele alihesabu mpaka nane. Seldon alikuwa timamu. Pambano likaendelea. Kwa mara ya pili, Tyson alimfumua Seldon left hook, akatua sakafuni kama furushi. Seldon alijitahidi kunyanyuka. Ila hakuwa timamu. Ilimchukua Tyson dakika 1 na sekunde 49, kushinda belt ya WBA Heavyweight.

Saa 2:40 usiku, video footages zilionesha Pac na Tyson wakifurahi pamoja baada ya ushindi. Walikuwa marafiki. Walichukuliana sawa mtu mdogo wake. Tyson alikuwa kaka mkubwa wa Pac.

Ikiwa imevuka kidogo saa 2:50 usiku, Pac na Suge, waliingia eneo lenye hoteli na casino, pembeni ya arena, hapohapo MGM Grand. Tupac na Suge walijulishwa kuwa Orlando Anderson “Baby Lane”, alikuwemo casino.

Baby Lane alikuwa memba wa kundi la South Side Compton Crips. Bosi wa genge hilo ni Keffe. South Side Compton walifanya kazi kwa ukaribu na wahuni Mob Piru, Vegas.

Taarifa ya Baby Lane kuwepo casino, ilimpa jazba Tupac. Bila kuuliza, aliongoza alipokuwa Baby Lane. Suge alimfuata kwa nyuma. Pac na Suge walipomfikia Baby Lane, walimpa kichapo mfululizo.

Somewhere, Julai 1996, Baby Lane akiwa na wenzake, walimshambulia employee wa Death Row, Trevon Lane na kujaribu kumpora mkufu wake wenye kidani, walipokutana Lakewood Mall, Lakewood, California. Trevon aliripoti tukio hilo ofisini kwake.

Hivyo, Tupac na Suge, walimpa kichapo Baby Lane kulipa kisasi, vilevile kumkumbusha kuwa hapaswi kuingia 18 za big boys. Baadaye, Suge alionekana kumzuia Pac kutoendelea kumpiga Baby Lane. Ama aliona kichapo kilitosha au alikumbuka kwamba walikuwa wanacheza chess na ibilisi.

COMPTON STREET LEGEND

Katika kitabu “Compton Street Legend”, kuna sura imepewa jina “Foreshock” – “Tetemeko kubwa la ardhi.” Ndipo Keefe anasimulia mauaji ya Tupac yalivyotekelezwa.

Kwa nini Foreshock? Inawezekana ni kwa sababu baada ya mauaji hayo, athari yake ilikuwa kubwa kuliko walivyotegemea. Pengine ni majuto ya baadaye kuwa waliipeleka kaburini mapema, nyota kali ya muziki na filamu kabla ya kufilia full potential.

Siku hiyo Baby Lane alipopigwa na Pac pamoja na Suge, ilitokea pia genge zima la South Side Compton, lilikuwa Vegas. Keffe anasimulia kuwa walikwenda Vegas kwa ajili ya misosi, mitungi na ‘kuoa’ warembo. Si Tupac wala Suge aliyekuwa mawazoni mwao.

Habari za Baby Lane kupigwa, zilibadilisha siku. Mipango ya kuwasaka ikaanza. Matangazo kila kona yalishasikika wiki nzima kuwa kungekuwa na “After Fight Party” Club 662. Tupac, Suge na timu nzima ya Death Row, ingekuwepo.

Club 662, ilikuwa moja ya uwekezaji wa Suge, Vegas. Death Row team kujivinjari kiwanjani hapo, ilikuwa sawa na kuwepo home ground.

“Tunakwenda Club 662,” Keffe aliamrisha. Ndani ya kitabu hicho anasema mwenyewe kuwa msako wa vichwa vya Pac na Suge haukuwa wa kibiashara. Walimrukia mpwa wake, Baby Lane, hivyo ilikuwa vita binafsi.

Kabla ya hawajaanza safari, Keffe alijulishwa kuwa Von Zip alikuwa kwenye gari, parking, akitaka wazungumze. Keefe anasimulia, alipokwenda parking, alimkuta Zip kwenye benz (hakufafanua aina gani).

Ndani ya benz, Zip aliketi na rapa bora wa kike wa muda wote kutoka New York, Foxy Brown. Zip alitoa ishara Foxy atoke, Keffe aingie. Yalikuwa mazungumzo ya siri. Maelekezo kutoka kwa Zip kwenda kwa Keffe.

Zip alimkabidhi Keffe bastola, Glock 17, akamwambia: “Ni muda wa kupata pesa.” Keffe akaipachika bastola kiunoni kwa nyuma.

Keffe anasimulia japokuwa Zip alikuwa dealer mkubwa New York lakini mara nyingi alitimba West Coast na walishirikiana ku-handle business chafu.

“Wote ingieni kwenye magari, tunakwenda Club 662,” Keffe aliwaamrisha wanaye wa South Side Compton baada ya kumalizana na Zip.

Walifika Club 662. Walipaki magari kwenye parking za ma-VIP. Walingoja Tupac na Suge watokeze wawashambulie. Keffe anasimulia kuwa timu yake yote, kila mmoja angalau alikuwa na uzoefu wa jeraha moja la risasi. Bunduki ulikuwa mchezo wa maisha yao.

Kuua na kuuawa ni code kuu ya maisha kwa kila Mmarekani mweusi. Ndivyo anasimulia Keffe. Code hiyo inasema “niggas live, kill, and die by”. Nigga wanaishi, wanaua na wanakufa. Keffe anasema, vifo vya Pac na Biggie ni matokeo ya code hiyo.

Keffe na timu yake walisubiri parking kwa zaidi ya saa moja na nusu bila kuona chochote. Waliboeka ndani ya magari. Hakukuwa na bangi wala muziki. Keffe akaona hawawezi kuendelea kusubiri. Akatoa maagizo waondoke.

Ndinga ziliwashwa kuelekea hoteli ya Carriage House. Haipo mbali na MGM Grand. Hapo ndipo Keffe na timu yake walikodi vyumba. Barabarani walipaki kwenye duka la vinywaji. Walinunua bottles za Dom Perignon, Dom Perignon Rose na Cristal. Wahuni walihitaji kulewa.

Walipomaliza manunuzi, waliingia kwenye magari, wakaondoka. Barabarani walizuiwa na taa nyekundu. Ni makutano ya barabara za Flamingo na Koval. Keffe anasimulia kuwa wakiwa wamezuiwa na taa ya barabarani, waliona msafara wa Death Row.

Mashabiki, wengi wakiwa wanawake, walikuwa wanapaza sauti: “Tupac... Tupac... tunakupenda Tupac.” Naye Tupac aliwapa ushirikiano kwa kutoa kichwa dirishani na kuwapungia mkono.

Keffe anasema, kama si kelele hizo na Tupac asingetoa kichwa nje ya gari, wasingemwona. Sasa, baada ya hapo wakapeana ishara wamalize kazi. Walizungusha gari hadi usawa alipokaa Tupac. Mapigo manne ya risasi yalifuata. Mawili kifuani. Moja mkono wa kulia. Lingine kwenye paja.

Suge pia alijeruhiwa, ila alimudu kukimbiza gari kuondoka eneo la tukio. Polisi waliingilia kati na kuwafikisha Hospitali ya Chuo Kikuu cha Nevada Kusini. Siku sita baadaye, yaani Septemba 13, 1996, Tupac alifariki dunia.

NANI ALIMUUA TUPAC?

Tupac alikuwa kwenye gari lake jipya, BMW 750 iL toleo la mwaka 1996. Alikuwa upande wa abiria na aliyeendesha alikuwa Suge. Keffe alikuwa kwenye Cadillac. Ukiacha dereva, wengine waliokuwepo kwenye Cadillac ni Baby Lane na DeAndrae Smith “Big Dre”.

Baby Lane alikuwa wa kwanza kutuhumiwa kupiga risasi zilizomuua Tupac. Baby Lane aliuawa mwaka 1998, kabla hajafunguliwa mashitaka. Suge, mara kwa mara amekuwa akisisitiza kuwa Baby Lane hakupiga risasi. Keefe anamfahamu aliyepiga risasi.

Risasi zilitoka siti za nyuma za Cadillac ambako waliketi Baby Lane na Big Dre. Binamu wa Tupac, Yaki Kadafi ambaye alikuwa memba wa Outlawz, alikuwa gari la nyuma ya lile la Tupac. Kadafi alisema aliyepiga risasi ni Big Dre. Kadafi alifariki kwa pigo la risasi Novemba 1996. Big Dre alifariki kwa maradhi mwaka 2004.

Suge, naye ni mmoja wa watuhumiwa wa kifo cha Pac. Nadharia ya uhusika wake, ilijengwa kuanzia kwenye gari, yeye ndiye dereva, risasi alipigwa Pac peke yake. Mlinzi binafsi wa Pac, Frank Alexander “Big Frank”, alipewa jukumu la kumlinda Kidada (mchumba wa Pac). Big Frank kabla hajafa, alisema kifo cha Pac ni mpango wa Suge.

Nadharia ya pili ni kuwa Suge alilipa dola milioni moja kumtoa Pac jela mwaka 1995. Makubaliano yalikuwa Pac afanye albamu tatu na Death Row. Pac alikamilisha albamu hizo ndani ya muda mfupi, akawa anataka kuanzisha record label yake. Suge hakutaka Pac ajitegemee, kwani alikuwa akimwingizia pesa nyingi.

Diddy a.k.a Love, kama anavyojiita siku hizi. Mtoto wa mama, baba yake aliuawa na magenge ya wauza unga, akiwa na umri wa miaka miwili. Uhusika wake na kifo cha Pac, unaunganishwa na Zip, ambaye alikutana na Keffe saa chache kabla ya mauaji kutokea. Zip alifariki dunia Septemba 2012.

Tyson, amesema anaamini maneno ya Keffe ni ukweli mtupu na ametoa onyo kwa Diddy. Tyson husisitiza kuwa hujiona mwenye hatia kwa kifo cha Pac kwa sababu yeye ndiye alimshawishi kwenda Vegas, kushuhudia pambano lake. Hivyo, aliyemuua Pac ni adui yake.

Ukifuatilia sakata zima in details, unabaini kuwa FBI, NSA hadi polisi wa Los Angeles na Vegas, wanaamini Diddy ndiye mchoraji mkuu wa kifo cha Pac, ila hawana ushahidi wa moja kwa moja. Je, kukamatwa kwa Keffe na kufikishwa mahakamani, kutawezesha Love kutiwa nguvuni?

Hiki ni kipindi ambacho zile nadharia kuwa Pac aliuawa na secret society ya Illuminati, au Pac na Biggie walitangulizwa ahera na polisi, zinakufa kifo asilia. Ukweli huwa haudhibitiwi. Hata kama hakuna atakayetiwa hatiani, waliohusika na mauaji ya Pac wameshafahamika.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Diddy hauhusiki! Pac kauliwa na keffe, big dree na baby lane. Yeye pac na wenzake kilimtuma nn wampe kichapo baby lane.
 
Noma sana.
Na nani alimuu BIG? Kuna theory inasema the national of islam walimuua kulipia kifo cha 2pac. Kama una story ya kifo cha biggie ishushe mkuu
 
Nadharia zimekuwa nyingi kwenye hili tukio, ila Mimi ni miongoni mwa wanaoamini Serikali ya Marekani yenyewe hasa inahusika. Siku wakiamua kuuanika ukweli basi mambo yote yatakuwa wazi.
 
Unachosema ni kweli kwa sababu Mzungu akitaka kukuharibia atakufanyia mbinu yoyote ili akurositishe tu. Refer Bob Marley, Wacko Jacko etc
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom