Kikwete kilimo kwanza, Lowassa elimu kwanza!

Ninapenda kuchukua fursa hii kupingana na dhana ambayo kwa mtazamo wangu haiwezi kumletea Tija mtanzania mkulima kama tutaangalia na kupokea misemo kutoka kwa wanasiasa ambao farsafa zao wameziweka kwenye kitu siyo mtu ,tutakuwa watu wa ajabu kama tutajadili kilimo kwanza na elimu kwanza bila kutanguliza mkulima kwanza amabye yeye kama yeye anahitaji kuwezeshwa na kujengewa mazingira ya kuweza kulima ikiwa ni kumpa uwezo wa kukupa na shamba lake kuwa dhamana bila mambo ya ujanja kama mpango wa kilimo kwanza ulivyo,kwa picha ya juu juu unaweza kuuona kama una tija na maendeleo makubwa kwa mtanzania wa kawaida lakini kwa undani kabisa hilo jambo halipo ni kwa baadhi tu tena wenye nafasi,na suala la elimu kwanza pia ni suala la kuangalia kwa makini kwani tayari tuna vyuo vimezalisha mabwana shamba wa kutosha na suala la elimu ya kulima sidhani kama watu wengi hawajui japokuwa msimu unabadilika kulingana na uharibifu wa tabia nchi,tukikumbuka enzi za nyerere watu walikuwa wakilima na bado kilimo kikawa ndiyo uti wa mgongo wa taifa na itaendelea kuwa hivyo kama tutawajali wakulima,katika kuwajali wakulima kwanza watu wengi watapenda kilimo na hakuna asiyejua kuwa kilimo ndiyo ukombozi wa mtanzania na mnyongeKIK​
 
Mzee wa Monduli alipowaza na kutafuta kuonyesha kuwa elimu ni kwanza halafu mengine yanafuata... Alichemsha baada ya kukuta baba mwanaasha aka mzee wa bagamoyo kaishaweka kilimo kwanza na mengine yanafuatia..... Matokeo ya form 4 yanaonyesha kuwa elimu ilitakiwa iwe kbl kumbe
 
Nimekuwa nikimsikia mara kwa mara Waziri mkuu aliyejiuzulu/aliyestaafu, mbunge wa monduli mkoani Arusha na mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje Mhe. Edward Ngoyai Lowasa (Mb), kuwa sera ya "Kilimo Kwanza" imeua elimu/mfumo wa Elimu hapa nchini, huku akijinadi kuwa yeye ni "Elimu Kwanza" hata chama chake (CCM) kinaujua msimamo wake. Hata juzi wakati akirekodiwa/akihojiwa na Swahili TV alirudia maneno hayo hayo huku akiwataka watanzania kumkumbuka, pamoja na mambo mengine, kwa kusimamia Elimu nchini (uanzishwaji na ujenzi wa shule za kata nchini - Lowasa's Secondary school). Sasa Jambo nisilolielewa hapa ni kuwa, ina maana waziri mkuu wa sasa Mhe Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb) ameua Elimu nchini? Ina maana ndani ya serikali kila kiongozi wa juu akiingia madarakani anaanzisha kitu chake au sera yake? Mfano aje kiongozi aseme mimi Miundombinu kwanza, Uvuvi kwanza, Maliasili kwanza, watoto na wanawake kwanza, Michezo kwanza n.k. Pia, ina maana huko serikalini hakuna Vipao Mbele (Priorities?), Ina maana hakuna mipango? Ina maana Five Years Development Plan (FYDP 2011-2016) ni kiini macho?. Vile vile, kama Lowasa ni Elimu kwanza na sio Kilimo kwanza, ina maana akiingia madarakani 2015 na yeye ataua Kilimo kama alivyofanya Pinda kwa kuua Elimu (kwa Logic ya Lowasa) kutokana na sera yake ya Kilimo kwanza?. Napata shida kuuelewa mfumo huu wa nchi yangu pendwa ya Tanzania. Mimi nilijua Elimu na Kilimo ni sera za CCM, hivyo kila atakayepewa nafasi ni sharti atekeleze na kusimamia alichotumwa na chama chake. Na hii inanikumbusha jamaa yangu mmoja aliniambia kuwa wakati wa Lowasa RC's na DC's waliowengi walianzisha shule zao (private) kama sio wao binafsi basi waliwashawishi ndugu na jamaa zao kuanzisha hizo private school, na hiyo ilitokana na kuwa driven na sera ya serikali iliyokuwepo wakati huo. Hivyo hivyo kipindi hiki cha pinda RC's na DC's wengi wao wamekuwa wakulima. Kwamba hakuna DC hata mmoja hasa walioko mawilayani ambaye hafanyi shughuli za kilimo ( ukulima, ufugaji hasa wa kuku na Nyuki n.k). Ikibidi katiba mpya itaje priorities za Taifa. Nawasilisha.
 
nimekuwa nikimsikia mara kwa mara waziri mkuu aliyejiuzulu/aliyestaafu, mbunge wa monduli mkoani arusha na mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje mhe. edward ngoyai lowasa (mb), kuwa sera ya "kilimo kwanza" imeua elimu/mfumo wa elimu hapa nchini, huku akijinadi kuwa yeye ni "elimu kwanza" hata chama chake (ccm) kinaujua msimamo wake. Hata juzi wakati akirekodiwa/akihojiwa na swahili tv alirudia maneno hayo hayo huku akiwataka watanzania kumkumbuka, pamoja na mambo mengine, kwa kusimamia elimu nchini (uanzishwaji na ujenzi wa shule za kata nchini - lowasa's secondary school). Sasa jambo nisilolielewa hapa ni kuwa, ina maana waziri mkuu wa sasa mhe mizengo kayanza peter pinda (mb) ameua elimu nchini? Ina maana ndani ya serikali kila kiongozi wa juu akiingia madarakani anaanzisha kitu chake au sera yake? Mfano aje kiongozi aseme mimi miundombinu kwanza, uvuvi kwanza, maliasili kwanza, watoto na wanawake kwanza, michezo kwanza n.k. Pia, ina maana huko serikalini hakuna vipao mbele (priorities?), ina maana hakuna mipango? Ina maana five years development plan (fydp 2011-2016) ni kiini macho?. Vile vile, kama lowasa ni elimu kwanza na sio kilimo kwanza, ina maana akiingia madarakani 2015 na yeye ataua kilimo kama alivyofanya pinda kwa kuua elimu (kwa logic ya lowasa) kutokana na sera yake ya kilimo kwanza?. Napata shida kuuelewa mfumo huu wa nchi yangu pendwa ya tanzania. Mimi nilijua elimu na kilimo ni sera za ccm, hivyo kila atakayepewa nafasi ni sharti atekeleze na kusimamia alichotumwa na chama chake. Na hii inanikumbusha jamaa yangu mmoja aliniambia kuwa wakati wa lowasa rc's na dc's waliowengi walianzisha shule zao (private) kama sio wao binafsi basi waliwashawishi ndugu na jamaa zao kuanzisha hizo private school, na hiyo ilitokana na kuwa driven na sera ya serikali iliyokuwepo wakati huo. Hivyo hivyo kipindi hiki cha pinda rc's na dc's wengi wao wamekuwa wakulima. Kwamba hakuna dc hata mmoja hasa walioko mawilayani ambaye hafanyi shughuli za kilimo ( ukulima, ufugaji hasa wa kuku na nyuki n.k). Ikibidi katiba mpya itaje priorities za taifa. Nawasilisha.

ccm wanajua fika kabisa vitu ambavyo watanzania wanavihitaji kama vipaumbele vyao,ila ni bahati mbaya tu hawawezi kuvifanya kwa maslahi yao binafsi.kuliko kuboresha elimu ni bora hela iliyopo waifanyie danganya toto kwa kufanya mambo rasha rasha ili zibaki hela za kula.
 
ukuta2013 siku hizi nadhani tuna mpango wa kila miaka 3, Ukiangalia hata mifumo ya H/shauri katika kuandaa bajeti wanaandaa reflection ya bajeti kwa miaka 3 na maeneo ya vipaombele yanabadilishwa kila baada ya muda huo.

hata hivyo Jinsi maendeleo yanavyoimbwa nchini na tusiyaone hali ya kuwa taifa lina wataalamu kibao tena wengi wa viongozi pia ni wataalam, Hii inaashiria moja kwa moja hawako tayari kuwaletea wananchi maendeleo makusudi.
Mf. Utakuta ujenzi wa bara bara fulani unahitaji Bilioni kadhaa lakini ukiangalia bajeti wanatoa milioni chini hata ya 100, na utaambiwa hizi ni za mwanzo kwa ajili ya upembuzi au Spot improvement n.k. Baada ya hapo yawezekana hakuna kitakachoendelea.

Pia Miradi ya umwagiliaji mingi inahitaji kati ya milioni 700 hadi Bilion na ushee lakini utakuta mradi unatengewa 30-50 milioni. Huku majukwaani wakitueleza kuwa umwagiliaji kwanza, kilimo kwanza, tuondoe njaa n.k ila miradi inakaa hadi miaka 20 haijakamilika tena hata vipande vinavyojengwa vingi ni majanga matupu.

Hili litakuwa lina tageti maalumu sio hivi hivi.
 
raisi safi ni sitta tu,uyo lowasa hela anazotoa kanisani na kwenye miskiti zinatoka wapi,na atarudishaje?tuwe makini sana
 
Hizi Hela Za Edwartwalib Na Rafiki Zake Ni Za Deal Za Masogange......
 
Urais kwa gharama yoyote hata kama ni kutofautiana na ilana ya chama chetu ,watanzania tumuunge mkono mzee wetu Samwel sita kuhusu huyu jamaa
Hapana pamoja na tuhuma zote alizonazo.
Mimi namuunga mkono kuwa ELIMU KWANZA.

Na tukumbuke yeye ndiye muanzilishi wa Shule za kata, na baada ya kuondoka shule zikabaki Ukiwa. Na mwisho wake tuna majengo bila walimu wala vifaa.
 
Lowassa, Sitta na yeyote wa CCM,including Pombe na Mwakiembe wote lao ni moja na state yao kisiasa ni moja tu,UOZO kwa taifA. Atakayetufaa ni Mgombea wa CHADEMA TU.... nguvu ya Umma kwa maslahi ya Umma. Msidanganyike kwa Ghiriba zao Mafisadi kwa rangi na aina zao. Wote hao wanachojua kuitikia ni NDIOOOOOOO hata kama ni -----.Hovyo kabisa nafuu ya choo kinaweza kuzalisha biogas. na kisha kuwa mbolea.
 
Huko nyuma kauli mbiu yetu ilikuwa kilimo ni uti wa mgongo lkn leo eti kilimo kwanza tofauti nini? Badala ya kuendesha kilimo cha kisasa, wakulima wanafyeka misitu. Tuwekeze zaidi ktk elimu halafu tutafanikiwa ktk kilimo.
 
Alipokuwa Waziri Mkuu Mhe Edward Lowassa alitilia msisitizo Elimu na ktk kipindi kifupi shule nyingi sana zilijengwa. Mradi huo ulikufa kifo cha mende mara baada ya Lowassa kujiuzulu.

Akaja Mhe Mizengo Pinda na Kilimo Kwanza. Nchi nzima imezizima kwa Kilimo Kwanza. Pembejeo zenye thamani ya mabilioni zinapelekwa kwa wakulima mashambani.

Na alipohojiwa ktk kipindi cha Dak 45 kinachorushwa hewani na ITV, Mhe Lowassa alisema, KAMA NI KILIMO KANA, BASI ELIMU NI KABLA (elimu ni Preamble)

Kwako wewe unadhani, nani kati ya hao anaona mbali?
 
Wanaomwelewa Edo ni wachache mno,mzee wetu Samwel sitta hataki kusikia habari mzuri yoyote inayomhusu Edo ,mungu tuepushe na hii laana ya wanaokataa kukubali ukweli
 
Akaja Mhe Mizengo Pinda na Kilimo Kwanza. Nchi nzima imezizima kwa Kilimo Kwanza. Pembejeo zenye thamani ya mabilioni zinapelekwa kwa wakulima mashambani.

Kwako wewe unadhani, nani kati ya hao anaona mbali?


Ndugu huu ni wizi mtupu sijkuhi kama watanzania wanjua kuwa hizi hela za Pembejeo ni za Mkopo kutoka World bank.

Hivi hata kama ingekuwa ni wewe nyumbani kwako ungewekeza kwenye Elimu au Mbolea na Mbegu za GMO kutoka kwa mabepari? Au Minjingu mbole fake isiyo na maana kw awakulima wa Tanzania.
 
Subsistance farming kamwe haiwezi kuinua uchumi wa nchi,rais alichemsha hapa.nchi zote za first world ni wachache wakulima wanafanya commercial farming
 
Back
Top Bottom