Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Watanzania,

Hivi kweli mnapenda story za udaku namna hii?.

Kila siku huwa nasema na kusisitiza anzeni kufikiri kwa kutumia ubongo wenu acheni magazeti na mitandao kuwafikiria.

Ndio maana mnalialia kila kukicha maisha magumu, hayawezi kuwa raisi kama mnaamini story ya kutunga kama hiyo hapo juu.


Mbona unapinga pinga tu??muhusika nini??mi nimesoma nimechanganya na za kwangu..sasa wewe unapingaaaaaaa tuuuuuu..point of doubt.
 
Híi michezo ipo katika kila chama ama nchi yeyote unapofika wakati wa chaguzi, lakini mwisho wa yote watu hurudi kati na kumpa nafasi aliyeshinda kugombea na kuongoza, umesahau ya Obama na H. Clinton? Mbona le wanaendesha Taifa na kila mmoja kwa nafasi yake.

Humtishi kikwete wala humtahadharishi hapa umeleta story2 ya kupokea mwaka 2012 tukiburudika.. ccm imekomaa bwana haya yote yatapita na jembe la 2015 litapatikana kwa njia hz hz lakini patabaki kuwa shwari watu wakila bata. Hata ungekuwa wewe madarakani ni lazima wangekuwepo ambao hawakukuunga mkono wakati wa mchakato, ila baada ya hapo ni kufanya nao kazi.

JK unadhani ananoma na hilo?.. Semeni na mengine yeye anajuwa kilichomgusa mpaka akagombea urais.
 
Hawa watu wa ajabu sana kila siku kujipanga kugombea madaraka kitu maendeleo kwa wananchi hakitamkwi tumechoka na thread hizi za watu wa mitandao na wenye uroho wa madaraka wakati umaskini unashambilia nchi na wanachi utafikiri kirus cha kompyuta au hiv

Uwe mtulivu, unauhakika gani imetungwa? Cha msingi fanya utafiti wa jambo hili.
 
It might be a year closing fiction!!!!! but there is some thing behind the hanging curtain!!!.....lets wait and see:shock::shock::shock::shock::shock: :poa:poa
 
Andikeni sana! KIM JONG ILL wa N. Korea atafufukia Tz ndani ya Lowasa-Next presidenti, hii haina ubishi!:eyebrows:
 
Watanzania,

Hivi kweli mnapenda story za udaku namna hii?.

Kila siku huwa nasema na kusisitiza anzeni kufikiri kwa kutumia ubongo wenu acheni magazeti na mitandao kuwafikiria.

Ndio maana mnalialia kila kukicha maisha magumu, hayawezi kuwa raisi kama mnaamini story ya kutunga kama hiyo hapo juu.

Tuletee hapa Jf waraka wa kukanusha ripoti hii hapo juu. Kama hutaweza kufanya hivyo basi we ni mnafiki usiyependa kuona ripoti za wenzako zikikubalika na kupata mashiko hapa JF.
 
Hutaki Unaacha,

Kwanza asante kwa hii. Wanabodi hii mada si ya kupuuzwa hata kidogo bali ni uthibitisho tuu 2015 ni CCM ni Edward Lowassa na mgombea Mwenza Amani Karume, Rais wa Zanzibar ni Maalim Seif, Makamo wa kwanza ni Ismail Jussa!. Waziri Mkuu wa rais Lowassa bado sijamjua ila King Maker!, nimemvulia kofia!.

Waraka huu ni uthibitisho wa sisi tunaompigia debe Lowassa tuko right.

It's very very unfortunate rais Jakaya Kikwete kwa Mtandao wa Lowassa, yeye si lolote sii chochote!. Yaani hawezi kufanya lolote it's too late now!.

Waraka huu umenipa mwanga ambao sikuufahamu kabla, ni ile siri ya muafaka walikuwepo Jussa na Maalim Seif tuu na Karume!. Taarifa za Shein kutoshinda uchaguzi wa Zanzibar nilizisikia na siku ya kutangazwa matokeo nilikuwepo Zanzibar, kwa Seif ninayemjua mimi, sikupata picha alikubalije!. Sasa nimeelewa, anaerum CUF ni Jussa sio Seif na ndio maana Hamad Rashid kuonyesha interest ya Ukatibu Mkuu ataharibu na ikibidi watammaliza!.

Wapenzi wa JK samahanini sana kuwaeleza yeye si chochote si lolote mbele ya EL kuelekea 2015 kwa sababu kama ni King Maker alimweka pale Sitta na akamng'oa na kumweka Anne!. Then JK hana option zaidi ya kumuahidi EL ikulu 2015 vinginevyo mwakani baada ya uchaguzi wa CCM, EL atamtaja yule mwenye zigo la Richmond alilombebea na kupitia Bunge, impechment process will be initiated na ikisail through that is the end of the road kwa CCM!. Ila RA ataiback up CUF na sio Chadema ndio maana Jussa ni strategic link!.

Suluhu pekee kwa JK na CCM kubaki salama ni kumteua Lowassa ili asimwage mboga!.

Kwa kweli baada ya kuzisoma powers za King Maker, nami Pasco wa JF najiandaa kukaa karibu na wafalme ili japo ninukie manukato!.

Kwa waraka huu, Lowassa ndio tayari Mgombea, Dr. Bilal ni spent force atapumzishwa!.

Kwa wasiojua politics is a dirty game, wait and see for yourself as 2015 draws near!. Kitu ambacho sijafahamu ni jee watu safi kama Dr. Shein, Nahodha na Dr. Mwinyi zamu zao zitakuwa lini kuuonja urais wa Muungano au urais wa Tanzania kwa Mzanzibari ni nehi kimoja?.

Pasco wa jf.
 
Mr President,

Ningekuwa na muda ningekueleza mengi sana. Muda wangu ni kidogo sana ndiyo maana nashindwa hata kupost mambo mengi kuhusu taifa hili hapa JF. Ninatuma post hii si kwa lengo la kukutisha. Lengo ni kukukumbusha uwe makini ili usijefanya uamuzi wa hovyo na kuliingiza taifa katika machafuko na kuharibu timetable za watanzania. Machafuko ndiyo tunayoyakwepa lakini si wewe (I have to tell you the truth because you are not my breadwinner at all).
Wow! this is powerful... yaani nasoma narudia kusoma na usoma hadi nashindwa kuelewa siasa za Bongo...Wanikumbusha Mzee Es wakati wake..

Mkuu pengine uko karibu na hawa jamaa, lakini mbona unajichanganya kumwodoa JK ktk chaguzi za mwaka 2000 wakati Rostam na Lowassa walikuwa kundi moja na JK?.. Na ilikuwaje mwaka 2005 hawa kina Lowassa wakampiga vita Mkapa waziwazi na kuwa kundi la JK ambalo walihakikisha watu wote wa Mkapa wanatelekezwa?..Haya mahusiano ya Mkapa, Lowassa na Rostam kimtandao yameanza lini haswaa maana kwa jinsi hali halisi inavyojionyesha Mkapa kavutwa tu miaka michache kuelekea 2010 baada ya kumtishia Ufisadi hasa walipochukuliwa Yona na Mramba na kuwafungulia mashtaka yasiyokwisha.. Mkapa hadi hajitokezi mbele ya kadamnasi - akizomewa nchi nzima!

Nijuavyo kimtandao hii ilikuwa mbinu nzuri sana ya kumweka Mkapa na kina Sumaye kapuni leo tunawaona wamejiunga na Mtandao huo toka uchaguzi wa mwaka 2010..Mtandao wa Lowassa sasa hivi una nguvu kubwa sana baada ya kuwavuta mtandao wa Mkapa ndani na kuwa kitu kimoja.. Hili kundi zima sidhani kama JK hayumo, bali anajua kinachoendelea na yeye ndiye rais kundi hili linamuhitaji kuliko watu wote. JK hakuwa rais kwa uchaguzi wa Chama bali alikuwa rais kwa mikakati ya mtandao ambayo ilimuondoa kwanza Malecela na Kigoda kisha wakamaliza na Salim..Muafaka ndani ya chama CCM ulikuwa kuunganisha makundi haya na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Ushauri wako nadhani unaupeleka pabaya maana JK ni jemedari wa Jeshi hilo na analindwa sidhani kama yuko hatarini bali mchezo ndio unachezwa mtu kama wewe na mimi tufahamu hivyo..JK kama rais hatakiwi kujionyesha yupo kundi nao ama ana Ubia na mtu japokuwa upo na dalili zote zipo...
 
Back
Top Bottom