Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
JK: Bila safari za nje tungekufa njaa
Na Joseph Mwendapole
* Asema hawezi kubakia Ikulu akimtazama Salma
* Anataka akumbukwe kwa kujenga barabara, maji
Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili katika Jimbo la Sikonge, mkoani Tabora kuhutubia mkutano wa kampeni jana.(Picha: Khalfan Said).
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amewashangaa watu wanaobeza safari zake za nje na kusema kuwa bila kwenda nje kuomba kwa wahisani huenda Watanzania wengi wangekufa kwa njaa.
Aliyasema hayo katika jimbo la Urambo Magharibi na Mashariki akiwanadi wagombea wa ubunge katika majimbo hayo, Samuel Sitta na Profesa Juma Kapuya.
Ninapokwenda nje nakwenda kwa malengo. Siende tu. Siwezi kukaa Ikulu jijini Dar es Salaam, kuangalia uzuri wa mke wangu Salma hapana lazima nikutane na watu huko huko waliko, alisema na kuongeza:
Ziara zangu zina manufaa makubwa sana, hivi nikikaa pale Ikulu nikamwambia mke wangu 'Mama Salma umependeza sana' huenda wengine mngeshakufa kwa njaa, mimi bila kwenda nje Wajapani wangeijuaje wilaya ya Kaliua? alihoji.
Katika mikutano hiyo iliyofurika watu, alisema anapokwenda nje ya nchi anakutana na watu mbalimbali mashuhuri na matajiri ambao wamekuwa wakiisaidia Tanzania katika nyanja mbalimbali kama elimu, afya na miundombinu.
Kuna wakati nilikwenda Marekani nikakutana na rafiki yangu akasema wewe kwako si unatatizo la malaria, nikamweleza ndiyo akasema atanikutanisha na mtu atakayenisaidi na kumaliza tatizo ... kweli akanikutanisha naye na akanunua vyandarua vyenye thamani ya Dola milioni 78, alisema.
Alisema vyandarua hivyo, milioni 14 vitaanza kugawiwa na hadi Desemba mwaka huu zoezi la kuvigawa litakamilika.
Alisema hata vyandarua vilivyotolewa bure kwa watoto ilikuwa ahadi ya Rais mstaafu wa Marekani, George W. Bush, ahadi iliyotekelezwa na Rais wa sasa wa nchi hiyo, Barrack Obama.
Kwa upande wake Sitta alimwomba Rais Kikwete fedha zilizotengwa kwa ajili ya barabara za Urambo zisihamishwe ombi ambalo Kikwete alilikubali.
Sitta alimmwagia sifa Kikwete kuwa alilelewa vyama na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, na kwamba kila aliyemwona alijua angefika hapo alipofika na kuwataka wananchi kumpa ushindi wa kishindo.
Sitta alijisifu kuwa ni chuma cha pua na kwamba anakaribia kustaafu siasa na kuwataka wananchi kumchagua pamoja na madiwani.
Katika hatua nyingine, Kikwete, amesema iwapo atachaguliwa tena kwa miaka mitano ijayo, anataka atakapostaafu Watanzania wamkumbuke kwa kutatua kero ya maji, elimu na barabara.
Kadhalika, alisema Watanzania wasitishwe na wanasiasa wanaohubiri kuwa damu itamwagika.
Aliyasema hayo katika tarafa ya Kaliua jimbo la Urambo Magharibi, mkoani Tabora.
Alisema katika miaka mitano ijayo ataelekeza nguvu kubwa kutatua kero ya maji maeneo mbalimbali nchini ili atakapostaafu akumbukwe kwa hilo.
Rais Kikwete alisema serikali imejitahidi kufanya mambo makubwa katika elimu kwa miaka mitano iliyopita na kwamba zamu hii miaka mitano nguvu kubwa itakuwa kuwapatia wananchi maji ya uhakika.
Kama ambavyo Watanzania watakavyoikumbuka serikali yangu ya miaka mitano iliyopita katika elimu nataka awamu hii wanikumbuke kwa kuwapa maji watu waseme tulikuwa na tatizo la maji, lakini Rais Kikwete alitutatulia, alisema.
Alifafanua kwamba serikali imechimba visima, lakini havitoshi hivyo itachimba vingine 15 kwa kuanzia wilaya ya Urambo na vingine vitaendelea kuchimbwa hadi kero ya maji iishe. Pia, alisema serikali ya Japan imeahidi kufikisha maji katika wilaya mbalimbali mkoani Tabora.
Aliwaomba wananchi wa Urambo Magharibi wamchague Profesa Kapuya, kwani amekuwa na msaada mkubwa kwake tangu mwaka 2005.
CHANZO: NIPASHE