Hakika vijijini ndiko kwenye kazi kubwa. Idadi kubwa ya watu walio vijijini hawana habari na mambo yanayoendelea na matatizo yanayolikabili taifa. Mkazo lazima upelekwe vijijini. Kama tunataka mabadiliko makubwa lazima kupitisha elimu ya uraia vijijini. Bila kufanya hivyo tutapata mabadiliko kidogo sana katika nchi hii.Utafiti umefanyika na matokeo ya utafiti ndiyo hayo.Sasa lawama za nini?Naamini CCM bado ina nguvu kubwa katika nchi hii na naamini kuwa JK ni maarufu kuliko wanasiasa wengine.Naamini kuwa Seif shariff huko Zanzibar ni maarufu kuliko wanasiasa wengine.Huu ni ukweli na inauma sana.
La kufanya ni kwa vyama kama Chadema na CUF kufanya kazi kubwa ya kuwafikia wananchi huko vijijini.