Kikwete azidi kun'gara Duniani!

mtu wa pwani amenikumbusha story moja,huko kwetu alikuwepo jamaa
mmoja,tajiri kupitia kwenye mifugo yake pamoja na mashamba makubwa aliyokuwa nayo.pindi alipouza mazao yake nakupata pesa,alihakikisha akinunua suti za gharama kubwa,na kinachofuatia ni kwenda baa,akiwa baa ataanza kumuita kila anayepita njiani njoo unywe tani yako rafiki yangu.watu watamzuguka na kuanza kumsifia.jamaa alikuwa anajulikana kwa jina la kalunguyeye.kila mtu utamsikia kalunguyeye una pesa,tajiri nchi nzima n.k.wakati hayo yakifanyika nyumbani kwake familia inapata taabu,njaa kwa kwenda mbele,watoto hawana karo,na matumizi mbali mbali kwa ujumla.kusifiwa kwa king`wendu nje ya nchi,wakati wananchi wanakufa kwa umaskini Hospitali hakuna chanjo,bei za bidhaa kama chakula na cement inazidi kupaa
yeye akiendelea kuwakumbatia mafisadi na wala rushwa,vinamsaidia nini mwananchi aliyempa kura kwa kumuamini?na kwanini asisifiwe wakati hizo nchi zinanufaika kwa kujichotea madini kupitia mikataba yenye masharti nafuu,kujisombea magogo bwerere n.k?
HAKUNA MTANZANIA ANAYETAKA KUSIFIWA NJE.TUNATAKA KUJENGA UCHUMI IMARA ILI KUONDOA UMASKINI.
 
hapa ndipo patamu. mzungu akisema hakuna demokrasia tanzania, serikali inaiba kura, mzungu kasema kweli eeeh?, ila akija kusema sasa serikali inajitahidi rais anajitutumia, hapa kasema uongo duh !!!!

nyie wenye majibu yenu mkononi mna mambo kweli nyie
 
Mtu wa Pwani,

Kwa hiyo unataka kusema kuwa hiyo habari ameandika mzungu, na kwa kutumia mantiki yako mzungu hakosei, hivyo tusihoji, najaribu tu kukufahamu vizuri umekusudia nini hasa maalim?
 
JK atakuwa judged kwa sifa atakazopewa na Watanzania. Haya mambo ya Wazungu, tuwaachie watoe sifa kwa viongozi wao.

Hawa jamaa hata siku moja hawakuwahi kumpa sifa Nyerere mpaka alivyofariki. Pia kuna mifano ya kumsifia Mkapa wakati jamaa ni fisadi. Huko nyuma walikuwa wanawasifia watu kama akina Maboutu huku wananchota mabilioni ya fedha.

For JK the jury is still out and it is now time for him to start delivering on his promises.
 
Yaani mzungu kutaka kupiga picha na JK ndio inafanya tuone kwamba JK anafanya vizuri, huu ni uzuzu au nini? Acheni hizo. Hata Idd Amin enzi zake kila alipoenda alipaparikiwa sana na wazungu. Nakumbuka baada ya kuwafukuza wahindi alienda Ufaransa na wazungu walijipanga barabara kutaka kumuona Amin. Wazungu hawahawa wakija kwetu huwa wanakimbilia kupiga picha na wamasai wa kijijini ili warudi na picha zenye migorore!

Sasa kwa wazungu kumshangilia JK ni sawa; lazima wataka kujua huyu mtu anayewapa ardhi na madini kirahisi namna hii ni nani hasa?! Sasa hao waholanzi wale hawana time kabisa na viongozi wao wa kisiasa, wala hakauna mwenye mukari wa kwenda kuwasikiliza maana kila wanachofanya wanajua wanatekeleza wajibu wao na hakuna sababu ya kumsifia mtu anayetekeleza wajibu wake. Sasa ndio mnataka kuniambia wazungu wa Uholanzi wanaridhika na utawala na utendaji wa JK kuliko wa waziri mkuu wao, kama sio unafiki ni nini?

Msidanganyike ndugu zangu, wazungu wanapenda kutuchora, mawazo yao ni yaleyale ya James Watson. Kama sisi hatujaridhika na utendaji wa JK kwa kuona, kugusa, kusikia na kunusa, iweje tushawishiwe na waholanzi wanaolilia kanga za CCM zenye picha za JK? Msitufanye watu hapa tuanze kukubaliana na mawazo ya James Watson! Tena ni aibu kwa Profesa mzima Msola kuwaambia watu etu wazungu walikuwa wanapigania kumuona JK, huu ni utoto na ulimbukeni wa ajabu!
 
heshima yenu wakuu;

Hivi nani wa kusema serikali inawajibika, na wajibu ni nini? kada mpinzani, tutasema umefail mtihani, kama hukujibu kama nilivyokuelekeza ufanye.

kama uko darasa la pili na nikakupa swali la 1-2, ukaweka haiwezekani, nitakupa mia kwa mia sababu ni mimi niliyekufundisha hivyo. ila Mwl. wa darasa la saba akisema amekosa sababu jibu lake ni -1, tutakataa sababu mimi nilimfundisha kama alivyojibu.

kama uko darasa la tano, swali hilohilo nikakuwekea na ukasema haiwezekani, nitakukata sababu sivyo tulivyokubaliana darasani ufanye, hata huyo Mwl. wa darasa la kwanza atasema haiwezekaninitampinga.

sasa wapendwa, darasani tulimpa mambo ya kufanya huyu muungwana akiwa anatafuta urais. kashindwa na ameweza machache, sasa wa kutoa maksi ni sisi watanzania tuliomweka pale au wazungu ambao wakati huo hawakuwa darasani wakati huo.

ni upumbavu sisi kutunga mtihani alafu marking skim atuandalie mwingine. ni upumbavu nioe, alafu masharti ya namna ya kuishi na mwanamke anipangie dume jingine toka pembeni.

SISI NDIO TUNAOJUA KAZI TULIOMPA MUUNGWANA AMEFANYA NA TUMPE MARKS NGAPI. PIA SISI NDIO TUTAKAO SEMA AMESHINDA AU LA! WAKATI HUO TUTAKAPOORODHESHA TATHMINI.

Mazuri anayofanya ni part of his obligation. hata jambazi ingawa anakuwa kafanya mambo mazuri tu, anapendwa na watu kiasi gani, kosa moja tu linampeleka jela. refer Babu seya na wanao

Mbona wanamtandao walikuwa wakichafulia majina ya wengine bila kukumbuka mazuri waliokuwa wameyafanya? toa boriti kwanza kwenye jicho lako ndipo utakapo taka toa la mwenzio. kumbe mkuki kwa nguruwe kwa binadamu ni chungu.
 
Nionavyo mimi. Wengi wamesifia TZ kwa sababu ya watu wake waungwana, wazungu waliosifia hawakufurahishwa sana na maendeleo yaliyopatikana ndani ya kipindi cha JK bali wamewapenda waTz kama WaTZ kwa tabia zao.

Tusiseme kana kwamba sio watanzania, kwani nyie wenzetu mnaishi wapi?hamuoni hali tuliyonayo? Huduma gani tunaweza kuja kumuonyesha huyo mzungu anayesifia kuwa imeboreka? shule wanazonadi wakati watoto wao hawasomi humo? hospitali wakati wao wanatibiwa nje?barabara wakati wao wanaruka na ndege?maji au tuseme nini?zingekuwa nzuri basi zingewavutia na wao kuzitumia lakini huduma hizo zimeachwa kwa walala hoi kwa sababu ni huduma mbovu zisizofaa kwa binadamu, wao kama binadamu wanazipata nje.

Tunaambiwa makusanyo ya TRA yameongezeka, sasa mwananchi wa kawaida atajuaje kama yameongezeka wakati hakuna mabadiliko katika maisha yake?angalia nyumba zao ni zilezile tangu wakati wa nyerere, barabara ni zilezile, Huduma za afya ni zilezile, elimu watoto wanakaa chini na waalimu wanaoletwa kwenye mashule ni wale wale kwa mtindo wa upe kama wakati wa nyerere.

Hatuna chuki na JK, tunampenda na ndio maana tunajaribu kuonyesha mapungufu ili tusadiane kuyaondoa. Akiyaondoa tutamsifia sana tena sana kama tulivyofanya tukimtumaini wakati wa uchaguzi na tukamuwezesha kushinda kwa kishindo.

Mnaosema eti watu wanachuki naye, ni nyie hao hao wabaya wake ambao mnampaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kudai kuwa maisha yameboreka wakati nyie wenyewe hata nauli ya dalala hamnayo hahahahaha! pia mnasikia kilio cha watanzania dhidi ya serikali yake lakini mnaenda kumwambia eti Mhe. watu wanafurahia matunda ya kazi yako ili aendelee kufanya anayoyafanya hatimaye mumwangushe. Hatutaki kumwangusha tunamtupia kijiwe kidogo akiwa karibu na simba ili simba huyo asituone au asishituke na kumdhuru Mhe, bali aondoke taratibu bila kudhurika. Hatutasita kusema hili ni hovyo na hili limefanyika vizuri. Sipendi unafiki.
 
Yaani mzungu kutaka kupiga picha na JK ndio inafanya tuone kwamba JK anafanya vizuri, huu ni uzuzu au nini? Acheni hizo. Hata Idd Amin enzi zake kila alipoenda alipaparikiwa sana na wazungu. Nakumbuka baada ya kuwafukuza wahindi alienda Ufaransa na wazungu walijipanga barabara kutaka kumuona Amin. Wazungu hawahawa wakija kwetu huwa wanakimbilia kupiga picha na wamasai wa kijijini ili warudi na picha zenye migorore!

Sasa kwa wazungu kumshangilia JK ni sawa; lazima wataka kujua huyu mtu anayewapa ardhi na madini kirahisi namna hii ni nani hasa?! Sasa hao waholanzi wale hawana time kabisa na viongozi wao wa kisiasa, wala hakauna mwenye mukari wa kwenda kuwasikiliza maana kila wanachofanya wanajua wanatekeleza wajibu wao na hakuna sababu ya kumsifia mtu anayetekeleza wajibu wake. Sasa ndio mnataka kuniambia wazungu wa Uholanzi wanaridhika na utawala na utendaji wa JK kuliko wa waziri mkuu wao, kama sio unafiki ni nini?

Msidanganyike ndugu zangu, wazungu wanapenda kutuchora, mawazo yao ni yaleyale ya James Watson. Kama sisi hatujaridhika na utendaji wa JK kwa kuona, kugusa, kusikia na kunusa, iweje tushawishiwe na waholanzi wanaolilia kanga za CCM zenye picha za JK? Msitufanye watu hapa tuanze kukubaliana na mawazo ya James Watson! Tena ni aibu kwa Profesa mzima Msola kuwaambia watu etu wazungu walikuwa wanapigania kumuona JK, huu ni utoto na ulimbukeni wa ajabu!

Heshima yako mkuu,
Naungana nawe,sijawahi kuona katika dunia hii kuna mtu anajisifia kupigwa picha,huo ni ulimbukeni,eti wanamng'aninia kupiga naye picha,what a hell,kwani yeye ni superstar?Kwanza nani anayeijua Tanzania na Kikwete,huu ni ujinga kabisa,wazungu siku zote wanazungumza mabaya tu kuhusu Africa katika media zao,sasa Kingwendu yeye ni nani hadi wamng'aninie,toeni pumba zenu hapa.
 
Kweli its a white man's world... haya someni poem hii mpunguze jazba

living in this white man's world
is not that hard to do
you'll get along just perfectly
as long as you're white too

but if by chance your skin is black,
and your mind and soul as well
a constant struggle will exist
and make your life here hell!

the white man creates all the laws..
his books are in our schools...
the ruling class, the master race...
the white man makes the rules

the path the black man follows here,..
the white man sets the flow...
we've had a triumph here and there,...
but progress has been slow...

our leaders he eliminates,...
our families he destroys!
drugs, war, hatred, poverty...
are tactics he employs

for centuries the white man has
in every way he could
convinced the world that black is bad
and only white is good

and sadly he has beat us down
his persistence stole our will
divided, brainwashed and confused
each other now we kill

a judgment day will surely come
a sight blacks long to see
because it seems that only God
can set Black people free

Copyright Feb 1991 Stop & Think Poetry
By Steven Taylor
Published: 4/19/2005
 
Alaaa kumbe JK anaweza kuonana na watu wanaoishi ughaibuni, nilidhani ameiahirisha maana jamaa wa kutoka kwa George William Bush, walileta makasheshe hapa!!!

Alijua atakutana na Mwanakijiji HUKO USA,na atamuuliza maswali ambayo atashindwa kuyajibu na yataathiri credibility yake,zaidi ya hapo VOA walikuwa wamempania kumtwanga maswali ya nguvu baada ya kuonekana mdahalo wa hapa ulitawaliwa na wingu zito katika kuuliza maswali.
 
Ni kweli ni mapema mno ku-judge performance ya Kikwete, hata hivyo sikubaliani na yalisemwa na Mlaki ( Mume wa Rita) na Msolwa kuhusu masifa ya hao wazungu. Kwangu ni upuuzi kama alivyosema Kitila mambo ya kupiga picha, khanga za kampeni, urafiki wa Kapuya na Bilal ni vitu visivyo na tija yeyote ktk ustawi wa Mtanzania.

Kuhusu Elimu ni kweli toka kuingia Kikwete kuna some development hususan kwa wanaojiunga na shule za sekondari. Hata hivyo nakubali pia kuna matatizo ya walimu, vifaa nk lakini ukweli unabaki kuwa walau tumesogea kidogo, na wahusika watie mkazo sasa kwenye hayo mapungufu, Roma haikujengwa siku moja kama tumepata over 1000 sekondari ndani ya mwaka mmoja basi hayo ya maabara na vifaa yanawezekana pia.

Kama nilivyo tangulia kusema awali kwangu bado ni mapema kutoa tathmini ya utendaji wa Kikwete
 
Mwache Ang'ae Dunia,hata Mpaka Aling'aa Dunia,kumbe Tapeli Kama Yeye Hakuna,katukamuaaaaaa Kuna Zilikuwa Zinakwenda Ktk Anna Na Benjamini,leo Mambo Hadharani,butiku Hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,sema Sema Mwana,chukua Tano Babu Butiku.kikwete Ziiiiiiiiiiiiiii,hatutaki Ang'ae Nje Tunataka Atung'arishe Watanzania!!!!!!!!!kung'aa Kwake Kwa Sura Yake Na Mataifa Ya Nje Hatutaki,maana Hakutusaidiiiii!!!!
 
Kama nilivyo tangulia kusema awali kwangu bado ni mapema kutoa tathmini ya utendaji wa Kikwete

Miaka miwili na nusu ni kipindi tosha kabisa kutathmini juu ya utendaji wa jamaa aliyekaa madarakani. Yeye na timu yake hawana vision yoyote ni wababaishaji tu. Kutoa ahadi wakati wa kampeni na kuzitimiza wakati unapokuwa madarakani ni vitu viwili tofauti. Sidhani kama kipindi kilichobaki kabla ya uchaguzi wa 2010 kutakuwa na ahueni yoyote, bali usanii ndio utazidi kuongezeka. Kumbuka nyota njema.......
 
Miaka miwili na nusu ni kipindi tosha kabisa kutathmini juu ya utendaji wa jamaa aliyekaa madarakani. Yeye na timu yake hawana vision yoyote ni wababaishaji tu. Kutoa ahadi wakati wa kampeni na kuzitimiza wakati unapokuwa madarakani ni vitu viwili tofauti. Sidhani kama kipindi kilichobaki kabla ya uchaguzi wa 2010 kutakuwa na ahueni yoyote, bali usanii ndio utazidi kuongezeka. Kumbuka nyota njema.......
mkandara keshaanza kukusanya data,tusubirie atatoaka na jibu gani
 
Kama alivyosema mwana JF hapo juu, watu ukiwaandalia hafla watasema nini kibaya kuhusu wewe (at least to your face)? Sote tunajua jinso wazungu walivyo wanafiki. Kama JK anataka ajue kung'ara kwake kwa ukweli, basi aandae hafla hapa nyumbani na aone jinsi tutavyomchambua!

Tumwache a-vacation huko nje weeeee, akichoka basi tunamsubiri hapa hapa nyumbani. Eti anang'ara....pleeeez!

But all in all, I don't hate JK....I am simply ashamed that he's my president! He's weak and Indecisive1
 
Kikwete, Tanzania wavutia nje

Habari Zinazoshabihiana
• Mwaka mmoja madarakani...Rais Kikwete kutoa tathmini leo 21.12.2006 [Soma]
• Kikwete, Salma wamkuna mke wa Rais Bush 30.07.2007 [Soma]
• Lumbanga awa Balozi Umoja wa Mataifa 02.02.2006 [Soma]

Na Godfrey Lutego, Paris

WAKATI nchini Tanzania baadhi ya watu na hasa wa vyama vya upinzani wakimdhihaki na kumpaka matope Rais Jakaya Kikwete, Wazungu na watu wa mataifa mengine wa Ulaya, Marekani, Afrika na nchi za Pasifiki na Karibeani, wamevutiwa naye na kumwona kama alama ya kiongozi wa Afrika kwa vitendo vyake, mwelekeo na anavyoendeleza heshima ya Tanzania tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere.

Hayo yalibainishwa hapa juzi usiku na watu mbalimbali walioshiriki hafla iliyoandaliwa na Tanzania baada ya mchana Rais Kikwete kuhutubia mkutano wa 36 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwenye makao makuu yake mjini hapa.

Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH), Bw. Theophilus Mlaki na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, Profesa Peter Msolla ambao taasisi zao ziliandaa hafla hiyo, walisema walikuwa na kazi ya ziada kuwatuliza watu wa nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya waliofurika kwenye moja ya kumbi za UNESCO juzi usiku kwa hafla hiyo fupi, waliokuwa na shauku ya kumwona Rais Kikwete kwa karibu, baada ya kuvutiwa naye na hasa kwa hotuba nzuri aliyoitoa alipohutubia mkutano wa 34 wa UNESCO.

"Sasa tunaweza kupumua. Yaani ilikuwa kazi kuwatuliza watu. Ilibidi tuhangaike kuwauliza wasaidizi wake kama anakuja au la, kwani watu walikuwa na shauku ya kumwona," mmoja wa viongozi wa Wizara ya Elimu, Bw. Oliver Mhaiki aliwambia waandishi wa habari baada ya Rais Kikwete kuingia ukumbini na kufanya watu wachangamke, kila mmoja akisalimiana naye kwa kushikana mikono na kupiga naye picha kuonesha walivyovutiwa naye kutokana na uwezo mkubwa wa uongozi aliouonesha katika Afrika hadi sasa.

Naye Bw. Mlaki alisema Tanzania na Rais wake, imejizolea sifa kubwa zaidi kwa ilivyoandaa mambo yake katika mkutano wa mwaka huu wa UNESCO kiasi cha Wazungu kuona fahari na wengine kutangaza ukumbini pale kuwa nao ni Watanzania mmoja akiwa ni Bw. hubert Gijzen, raia wa Uholanzi ambaye sasa ni Mkurugenzi na Mwakilishi wa UNESCO Jakarta, Indonesia.
Mzungu huyo alisema aliwahi kuishi Tanzania miaka minne ya 90 akifundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Fizikia na rafiki zake, Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya.

"Nchi ni watu si miti. Tanzania ni nchi bwana. Watu wake wakarimu. Nimetembea nchi nyingi duniani lakini Tanzania ni ya pekee. Watu wake ni wakarimu sana. Niliwahi kuishi Mikocheni. Nitakuja tena Tanzania kesho, " Mzungu huyo aliwaambia waandishi wa habari waliokuwa kwenye ziara ya Rais Kikwete, akiungwa mkono na mwanamke mwingine wa kizungu ambaye ameolewa na Mtanzania.

Mwanamke huyo awali alihangaika kumtafuta Rais Kikwete apige naye picha alipoingia ukumbini na baadaye alisema alivutiwa sana naye mwaka juzi wakati wa kampeni na aliposhinda, alisema alitamani siku moja amwone kwa karibu, hivyo juzi alifurahi.

"Wakati wa kampeni nilikuwa naishi kisiwani Mayote na nilikuja Dar es Salaam. Nakumbuka kampeni zilisimama, kwa sababu ya msiba wa mgombea mwenza wa urais wa CHADEMA. Nilipata khanga ya 'Chagua CCM' yenye picha yake lakini sijui iko wapi ningependa nipate nyingine ya CCM. Naipenda CCM," aliwaambia waandishi na kusema ingewezekana, angekuwa mwanachama wa CCM.

Mbali ya Wazungu hao na wengine waliofurahishwa na hotuba ya Rais Kikwete iliyozungumzia mwelekeo wa Tanzania katika elimu na utamaduni na umuhimu na haja ya taasisi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa (UN) na mashirika yake kama UNESCO kuzidi kusaidia jitihada za Serikali kuboresha elimu na huduma nyingine za jamii ukiwamo utamaduni, wengine walifurahishwa na jinsi Watanzania walivyokuwa wakicheza muziki wa taarab uliporomoshwa na kikundi cha Daruwesh Sound kinachomilikiwa na msanii wa zamani wa kundi la East Africa Melody, Bw. Mohammed Ahmed Daruwesh, Mzanzibari aliyeweka makazi yake Paris akisema anatafuta maisha huku.

Watu wa mataifa mengine ya Afrika ya Senegali, Mali, Uganda, Kenya, Afrika Kusini wengine wakiwa na bendera za nchi zao, waliujaza ukumbi ambako hafla ya Tanzania ilifanyikia na kuufanya uchangamke zaidi na wengi wakionekana kupiga picha na kuzungumza na Rais Kikwete kwa muda mrefu, kabla hajapiga picha na wasanii wa taarab na kuondoka.

Bw. Mlaki alisema wamekuwa katika mkutano wa UNESCO kama wataalamu wa mambo ya elimu na sayansi na teknolojia yeye na wenzake wa ujumbe wa Tanzania na wamekuwa wakiulizwa sana kuhusu habari za Rais Kikwete na anavyofuata nyayo za Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na kuendelea kusikika na kusikilizwa na mataifa ya nje na kuwa msemaji wa mataifa mengi ya Afrika.

Awali Rais Kikwete aliwashangaa Watanzania wanaoitukana nchi yao kwa kuwaambia Watanzania wanaoishi Roma, Italia, kuwa wasidhani Wazungu huwa wanawaona wana akili nyingi wanapoikandia nchi yao, bali wakiwapa kisogo huwa wanawang'ong'a kwa kuisema vibaya nchi yao wakati wao, Wazungu wanaiona ni nzuri na wanalilia kuja kuiona.

Aliwaambia Watanzania kuwa wale wanaowaambia Wazungu nchi zao za Afrika ni mbaya wanajitukanisha, kwani Wazungu hao hao baadaye huja kuzungumza na viongozi wa Serikali zao na kuzipa misaada, jambo linaloonesha kuwa wanawaheshimu na kuwaona kuwa nchi yao na uongozi wake unafaa.

Rais Kikwete alisema, Watanzania walioko nje ya nchi hawana budi kuipenda nchi yao na kuisaidia ipige hatua zaidi za maendeleo kwa kuleta wawekezaji, kampuni na asasi kuwekezea katika miradi mbalimbali ambayo wao wanaweza kuwa wabia na Serikali itawasaidia

Rais Kikwete jana jioni alitarajiwa kuzungumza na watanzania wanaoishi Ufaransa na leo anatarajiwa kurejea nyumbani.

Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete amemteua Bw. Michael Mwanda, kuwa Katibu Mkuu Ikulu.

Uteuzi huo kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Bw. Phillemon Luhanjo kwa vyombo vya habari jana, unajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bibi Rose Lugembe, ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.

Taarifa hiyo ilisema uteuzi huo wa Bw. Mwanda ambaye kabla alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu unaanza rasmi leo.

http://www.dailynews-tsn.com/habarileo/index.php

Hakuna haja ya kusoma magazeti ya serikali pumba tupu..
huyu si muandishi aliliye somea kazi yake ,amesomea mialiko ya kusafiri na rais na kumsifia mimi nilikuwa kwenye kampani walikuwa wanaandika mambo ya ziada tu kila mahali wakienda, hatav picha wanachangua ile inayo onyesha kuna watu wengi kumbe siyo, nikuyasusia magazeti ya serikali yote au usiamini kilicho andikwa ndani.
stori nzima ni wazungu kweli mweusi na wazungu basi tena hata wazungu vichaa kwetu ni wanamaana jamani hajui kuna wazungu na vizungu?
 
Kwanza hodi .nawasalimia nyote sina zaidi kwani nipo na kasi mpya na ari mpya na mwamko mpya.
Nikianza kuchoma nasema waswahili tuna msemo usemao Ngoma kila ikizidi sauti basi ndipo inapokaribia kupasuka ,kama mmekita macho yenu kwa Mh.Kikwete basi mtaona kuna kitu kimeanza kuchomoza na si kingine ila ni kitumbo au kitambi bila ya shaka ulaji umeanza kumzoea.
Nina haraka.
 
nyie hamuamini mpaka muone kila kitu kiko safi kwa dakika moja.
Lowassa keshasema wakishindwa kutekeleza ahadi basi 2010 ndio mwaka wa kuwakatili kiaina.

ila nnaamini wanatekeleza kivitendo na wasio makengeza wanaona.

hata hiyo waaandishi kuandika kwa uhuru ni maendeleo. wananchi kujadili na kuhoji karibu mambo mengi ya wananchi ni maendeleo.

au mpaka niazime kauli ya Rais wangu Mh Amani "dogo hiloooo"
 
Kwanza hodi .nawasalimia nyote sina zaidi kwani nipo na kasi mpya na ari mpya na mwamko mpya.
Nikianza kuchoma nasema waswahili tuna msemo usemao Ngoma kila ikizidi sauti basi ndipo inapokaribia kupasuka ,kama mmekita macho yenu kwa Mh.Kikwete basi mtaona kuna kitu kimeanza kuchomoza na si kingine ila ni kitumbo au kitambi bila ya shaka ulaji umeanza kumzoea.
Nina haraka.

Mwiba,
Karibu jamvini,ili tuwachome hivyo vitambi vyao.
Ikulu kuna mafuta mengi pale,hukuona mzee Mkapa,nusura apasuke.
 
Back
Top Bottom