Elections 2010 Kikwete ampigia debe Mramba!

Ijapokuwa MRAMBA, ana kashifa kubwa ya matumizi mabaya ya uongozi, jk amempigia debe B MRAMBA, achaguliwe tena kuwa mbunge wa ROMBO, JK alikuwa anampigia debe MRAMBA, leo katika mkutano wa siasa uliofanyika katika kiwanja cha shule ya msingi mbomai kati, TARAKEA, ROMBO.
Ambapo asilimia 50 ya waliohudhuria , walikuwa wanafunzi wa shule mbalimbali hapa tarakea, kama mboma sec, nduweni sec, motamburu sec, mbomai primary, tarakea primary, na nyingine nyingi



PayGod na wana JF tunaweza pata video clip ya JK akimpigia kampeni MRAMBA na LOWASA tutengeneze advert kwenye media ili kuwaonyesha watanzania ndoa ya JK na mafisadi anaodai amewashughurikia na ana nia thabiti ya kupambana na RUSHWA?

please mwenye video clip ya Rombo na leo monduli tafadhali sana tuwekee ili tuifanyie kazi wazalendo
 
PayGod na wana JF tunaweza pata video clip ya JK akimpigia kampeni MRAMBA na LOWASA tutengeneze advert kwenye media ili kuwaonyesha watanzania ndoa ya JK na mafisadi anaodai amewashughurikia na ana nia thabiti ya kupambana na RUSHWA?

please mwenye video clip ya Rombo na leo monduli tafadhali sana tuwekee ili tuifanyie kazi wazalendo
Mkuu hili litakuwa bonge la Ad yaani Chadema wakiweza kuonyesha video clip za JK akiwapigia debe Mpamba na Lowassa inatakuwa safi sana...
 
JK+na+Mgombea+ubunge+wa+jimbo+la+Rombo+Mh.+Basil+Mramba+wakionesha+alama+ya+dola+ambayo+CCM+inatumia.jpg



Wana JF nimeona hii picha kwenye blog ya michuzi na NIMESHITUKA SANA. Hivi Mramba si anayo kesi inayoendelea mahakamani ya matumizi mabaya ya ofisi, na nina kila sababu kuamini kuwa kesi hii haikuenda mahakamani bila ya JK kutoa baraka ZAKE!! Sasa JK kumsifia Mramba na kumnadi kweli kunatoa picha gani kwa raisi wa nchi?

I am so disturbed kuona kama kweli JK anafikiri athari za matendo yake kabla haja act. Hivi kwa Judge anayesikiliza kesi ya Mramba anawekwa kwenye position gani, kama mkuu wa nchi ameshamsafisha? Je wale wanaotoa ushahidi dhidi ya Mramba si wataogopa, wengine bado wako serekalini. JK huo si utawala wa sheria, huwezi kujiassociate na mtu ambaye ana stain, hata kama stain yenyewe haijathibitishwa na mahakama kama kweli ni stain, but in public eyes ni kuwa ana stain!!!, ni kuwa amechafuka, kitendo cha serekali ya JK kumpeleka mahakamani na hata gerezani ni ishara tosha kuwa amechafuka, sasa unamandi na kumsifia mtu aliyechafuka? KWELI HUO NI UTAWALA BORA-- SHAME!!!

Hakuna nia ya dhati ya JK kuupiga vita ufisadi, na inauma kwa kuwa ni kama kuwang'ong'a wananchi huku wao wakichekeana, lol, this is a joke, tena joke ya mwaka. Chadema this is a scandal which mnaweza kuiongelea kwenye kampeni zenu na kuwaacha wananchi kuamua.



Ndugu ichondi na wana JF tunaweza pata video clip ya JK akimpigia kampeni MRAMBA na LOWASA tutengeneze advert kwenye media ili kuwaonyesha watanzania ndoa ya JK na mafisadi anaodai amewashughurikia na ana nia thabiti ya kupambana na RUSHWA?

please mwenye video clip ya Rombo na leo monduli tafadhali sana tuwekee ili tuifanyie kazi wazalendo
 
ndugu ichondi na wana jf tunaweza pata video clip ya jk akimpigia kampeni mramba na lowasa tutengeneze advert kwenye media ili kuwaonyesha watanzania ndoa ya jk na mafisadi anaodai amewashughurikia na ana nia thabiti ya kupambana na rushwa?

Please mwenye video clip ya rombo na leo monduli tafadhali sana tuwekee ili tuifanyie kazi wazalendo
nina wasiwasi na upstairs ya rais wangu ,hii imenisikitisha sana kuliko.
 
..nimesoma magazetini kwamba kesi imepangwa kuendelea kusikilizwa mpaka baada ya uchaguzi.

..JK alijigamba kwa kuwapeleka watuhumiwa wa ufisadi mahakamani. sasa JK huyohuyo anawapigia kampeni washinde uchaguzi.

..kitu cha kushangaza ni kwamba suala la JK kumpigia kampeni Mramba halijawa big deal ktk media zetu. kwenye nchi za wenzetu suala kama hili halivumiliki kabisa.
 
..nimesoma magazetini kwamba kesi imepangwa kuendelea kusikilizwa mpaka baada ya uchaguzi.

..jk alijigamba kwa kuwapeleka watuhumiwa wa ufisadi mahakamani. Sasa jk huyohuyo anawapigia kampeni washinde uchaguzi.

..kitu cha kushangaza ni kwamba suala la jk kumpigia kampeni mramba halijawa big deal ktk media zetu. Kwenye nchi za wenzetu suala kama hili halivumiliki kabisa.

wazee tusiwe tunaandika tu na kulalama inabidi tuchukue action sasa hivi nitumieni clip mimi nitai develop na kutengeneza tv advert then tuwatumie chadema walipie itv irushwe hewani, we need to tie jk with this issue, seriously hawezi kusema jangwani hiki then rombo anakwenda fanya tofauti and the guy walk free bila hata media kumulika huo udhaifu

 
Kikwete ni mtu wa ajabu anazunguka dunia nzima na hata ndani ya tzn akitamba kuwa anawashugulikia mafisadi na mifano yake mikubwa anayoitumia ni kitendo ch serikali yake kumfikisha mahakamani mramba na wenzake, leo tena mtu yuleyule aliyesema anakomesha mafisadi hakina mramba anasimama anauambia ulimwengu kumchagua mramba kuwa kiongozi wetu hii inadhiriisha wazi jinsi jk alivyomnafiki na laghai. Sasa tumuamini jk yupi anayesema ukweli, aliyesimama na kuwafikisha mahakamani mramba na wenzake akiwatuumu kwa wizi au jk aliyesimama rombo akituambia tumchague mramba kwamba ni kiongozi mzuri na imara????.
 
Naona nina wajibu kuchangia ktk Suala hili la J.K. kumpigia debe Basil Mramba. Nitangulize kusema kwamba namheshimu na kumwonea huruma sana Rais wangu Kikwete. Nikiri pia kwamba Basil Mramba ni rafiki yangu binafsi wa siku nyingi.

Kwanza, kesi ya Mramba ni ya JINAI. Kama Mramba hangekuwa na wadhamini wa kuridhisha Mahakama, ungekuta sasa ni mahabusu anaishi Keko au gereza lolote la Serikali Tanzania akingojea maamuzi juu ya kesi inayomkabili.

Pili, kesi yoyote ya jinai ni kesi ambayo Serikali inamshtaki mtuhumiwa. Serikali ni taasisi inayoongozwa na Rais, ambaye kwa wakati ule Mramba akituhumiwa ilikuwa ni Kikwete anaiongoza, na hata sasa anaiongoza hadi hapo matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba utakapoamua aendelee au asiendelee.

Tatu, nina hakika kwa mtu mashuhuri kama Mramba, na kutokana na kiasi cha fedha zinazodaiwa Serikali imepoteza kutokana na mkataba Mramba aliosaini (Shs bilioni 12), ni lazima Rais alihusika kwa karibu sana na alikubali kesi ifunguliwe dhidi ya waliohusika: yaani Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja.

Nne, kwa vile Mhe. Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM, na alifahamu Basil Mramba alikuwa amemtuhumu (akiwa Rais na kiongozi wa Serikali), angeshauri CCM isimsimamishe kugombea jimbo la Rombo. Kwa hiyo, kwa heshima na taadhima, nasema Mhe. hakutumia uwezo wake na taarifa alizokuwa nazo kupata maamuzi busara kuhusu ugombea jimbo la Rombo. Kama Kamati Kuu ya CCM ilimlazimisha Mwenyekiti wake amkubali Mramba, basi ni cham cha mafisadi kweli!!!!

Tano, hata kama Mramba alikuwa MwanaCHADEMA aliyekuwa na kesi inayomkabili mahakamani, na akapendekezwa na kura za maoni za wanaCHADEMA wa Rombo, sisi katika Kamati Kuu ya CHADEMA, hatungeidhinisha uteuzi wake aendelee na kampeni. Kwa hiyo, kwa Kamati Kuu ya CCM inayoongozwa na Mhe. Kikwete, kuidhinisha mtuhumiwa wa ufisadi agombee ubunge, inadhihirisha CCM kudhalilisha Bunge kama taasisi.

Sita, kwa Mhe. Kikwete wiki hii, kumpigia debe, Basil Mramba, mtu ambaye yeye kama Rais, amempeleka mbele ya Mahakama akimtuhumu kwa kusababisha hasara ya mabilioni ya shilingi, mali ya Serikali, inadhihirisha kutoshauriwa vizuri au yeye mwenyewe kuchanganyikiwa kwa hali ya juu.

Saba, sisi wanaCHADEMA tutaendelea kuwakumbusha wapiga kura wa Rombo kwamba Mramba ni mtuhumiwa na wasimsikilize kwani anaweza kupatikana na hatia na asiweze kuwawakilisha Bungeni. Pia sisi tusisitize kwamba Mhe. Kikwete anashauriwa vibaya au hajui hatua zinazotakiwa kuimarisha utawala bora na kwa hiyo hafai kuchaguliwa kuendelea kuwa Rais.

Mgombea wetu Dk. Willibrod SLAA apigiwe kura.

Tunamshukuru Mzee Mtei kwa kutoa somo la nguvu. Naona hali sasa iko hivi:

(1) Serikali ya Kikwete ilikuwa na ushahidi wa kutosha ndio maana ilimpeleka Mramba mahakamani. Imemwachia kwa dhamana. Kutokana na kuhofia anaweza kukimbia, ikachukua vyeti vyake vya kusafiria na kumwekea mipaka ya anakoweza kwenda.

(2) Mramba bado hajapatikana na hatia, lakini waliomshtaki, yaani Kiwete na serikali yake, waliamini ana hatia. Kwa vingine hawangempeleka mahakamani. Mwendesha mashtaka anafanya kazi chini ya uongozi wa Rais. Sijui atafanyaje sasa baada ya Rias kusema kesi ni ndogo na mshtakiwa atashinda!

(3) Rais Kiwete kusema kesi ni ndogo na mtuhumiwa atashinda ni kitu cha ajabu sana. Kwanza ni contempt of court. Pili kesi ndogo ingemweka Waziri wa zamani rumande siku zote hizo? Kesi ya jinai, inayohusu Taifa kupoteza shilingi bilioni 12 ni "ndogo" kwenye macho ya Rais Kikwete? Has he lost touch with reality?

Ni vema sana wananchi wa Rombo wakampa mgombea wa ubunge wa CHADEMA kura zao. Wamchague Slaa vile vile ili akishachukua nchi tuchunguze hata hizi kesi ndogo.
 
Back
Top Bottom