Nini hasa kilisababisha vurugu za Mwembechai mwaka 1998?

ESCORT 1

JF-Expert Member
Dec 7, 2015
1,267
2,519
Wakuu wa jukwaa,

Leo ningeomba tukumbushane, ni nini hasa kilisababisha vurugu za mwembechai mwaka 1998? Wakina nani walikuwa nyuma ya tukio lile? Wangapi walipoteza maisha? Je kuna askari ambao walichukuliwa hatua yoyote kutokana na vurugu zile?

Ahsanteni.

MAONI YA WADAU

Image15.jpg

Mwembechai killings followed a similar pattern. Father Camillius Lwambano of the Mburahati parish claimed that he passed at Mwembechai mosque and heard Muslims ridiculing Jesus Christ. It was later established, after the police had opened fire and killed at least four unarmed Muslims and maimed several others, that this claim by Father Lwambano was, after all, a sheer fabrication. As I am writing this book,almost two years after the killings, our government has yet to form a team to probe the killings despite repeated requests from many concerned Tanzanians across the religious divide.

I do not know if there is any serious observer of Tanzania’s political history who can deny the commitment and sacrifice of Tanzanians to the freedom fighters of Mozambique, Angola, Zimbabwe, Namibia, South Africa, and even beyond Africa. In this regard Tanzania has indeed provided a shining example to the rest of the world, and has deservedly won the respect and admiration of many countries. That admirable aspect of our national history is not the focus of the present study. My interest here is to encourage my fellow country men and women to have the courage to confront the odious side of our political history.

A political history of religious discrimination against Muslims. The unstated but effective policy of marginalising Muslims in education, employment and political appointments is not of recent origin. It began and was firmly entrenched during the twenty five years of Mwalimu Nyerere’s political rule. And I believe unless
this problem is openly addressed Tanzania may also find itself engulfed in civil strife.

Multiple interpretations of the problem
On the political future of our country many Tanzanians irrespective of their religious affiliation

Kilichosababisha mwembechai kinuke mwaka 1998.
Ingawa nilikuwa mdogo, lakn kiasi nilikuwa na uelewa wa kuangalia taarifa ya habari na kusimulia kwa ufupi nini kimeelezwa.

Ikumbukwe kuwa mwaka 1998 vuguvugu la vurugu la udini lilitaka kuitawala Tanzania na Afrika mashariki na dunia kwa ujumla kwa kujithibishia kuwa dini IPI ni bora na ina nguvu kiasi gani.

Ni kipindi ambacho dini moja ilikuwa inamikutano ya kutafuta waumini kwa kuita mihadhara ya hoja na kualika msemaji kutoka dini nyingine kubishana kwa hoja. Mihadhara hii ilifanyika sana karibu kila kiwanja cha wazi kilichopo karibu na nyumba ya ibada maeneo km mwananyamala...magomeni...manzese ...kigogo...kinondoni mtambani nk n jambo LA kawaida kukuta mihadhara ya dini na kina Dr sule wakihutubia kipindi hicho.

Ikumbukwe pia ni kipindi hikihiki cha mwaka 1998 ndicho kulizuga propaganda nyingi sana za udini hata ikafika mahali ndani ya sehemu ya nyumba ya ibada kunakuwa na mawaidha ya kuhubiriana kuwa dini Fulani INA viongozi wengi serikalini kuliko sisi kwahyo wanatutawala na hatuna maamuzi katika nchi yetu.

Mwaka 1998 kama ulikuwa na akili timamu ndio kipindi ambacho kila nyumba ya ibada nilikuwa na mafunzo ya karate kwa vijana wa dini kwa lengo LA kujilinda. Self defence ukiniuliza walikuwa wanajilinda nini ? Sina jibu.

Na ndio mwaka huo kulikuwa waliibuka viongozi wa dini wenye ushawishi mkubwa kwenye mimbari..kwa Tanzania na Afrika mashariki. Watu km shekh Rogo kule Mombasa...kulikuwa na connection na shekh mmoja alikuwa Mwanza kwa Tanzania na wengne walikuwa visiwani.

Serikali kwakuona hatari ya mbele ikapiga BAN mihadhara yoyote ya dini. Hapo ajenda za ajabuajabu zukapita kupitia nyumba za ibada kuwa wanatunyanyasa umma.

Na mengne meng ambayo huwezi kuandika hapa kwa usalama wa nchi na kuibua tena hasira za wafia dini na kuchafua nchi. Naishia hapa kwa machache baada ya upande mmoja kushindana serikali ya Ben kipindi hicho.

Mauaji ya Mwembechai yalikuwa ni kilele cha kilio cha waislamu juu ya ubaguzi dhidi yao wa siri na dhahiri katika nyanja nyingi hususan elimu na ajira serikalini, Serikali ya Mwalimu haikufanya vya kutosha kubridge gap kati ya Wakiristo waliokuwa na advantage kielimu toka wakati wa mkoloni.

Hata shule za Kanisa ambazo Nyerere alitaifisha kwa hoja kwamba Watanzania wote wasome haikusaidia kwa sababu gepu la kielimu liliendelea. Na badala ya Nyerere kujenga shule mpya nyingi yeye alitaifisha zilizokuwepo ambazo bado ziliendelea kuwa chache na ndiyo maana watoto walikuwa wakifaulu primary school hawachaguliwi kutokana na uhaba wa shule za Sekondari.

Viwango na idadi ya waislamu chuo kikuu ilikuwa ni ndogo sana na serikali ya Nyerere na ya Mwinyi ambayo iliendelea kuwa under watch kali ya Nyerere kama Mwenyekiti wa CCM hadi mwaka 1990 haikuweza kuaddress tatizo hili.

Mkapa alivyoingia madarakani alikuta tatizo hili limefikia peak, mihadhara ilikuwa ni sehemu mojawapo tu ya waislamu kufikisha grievences zao kwa serikali.

Mkapa akaona atoe kile chuo cha TANESCO morogoro kuwapa waislamu ili kupunguza gepu na kilio hiki cga waislamu kuwa marginalized kwenye elimu.

Alipoingia JK akafanya kazi nzuri sana ya kujenga shule za kata kila nchi, kwa hiyo waislamu wakaweza nao kuaoma kwa wingi na pia JK akapandisha hadhi vyuo vya advanced diploma na kuvifanya vitoe digrii kwa hiyo katika mazingira haya huwezi kuwabagua tena waislamu.

Katika ishu ya teuzi, Kikwete alijirahidi kuteua teua na waislamu kwa wingi kidogo ijapokuwa wakiristo overall waliendelea kuwa wengi.

Alipoingia Magufuli, amejaribu kurudisga nyuma mafanikio haya ya kubalance demography za taifa katika utumishi wa serikali.Teuzi za Magufuli zinanuka Udini.

Proportiaonally ukiangalia idadi ya ma RAS, MaDAS, Wakuu wa wilaya, Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Mashirika ya Umma, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wenyeviti wa Bodi Waislamu ni wachache mno kulinganisha na proprtion yao katika hii nchi.

Kitila mkumbo kabla hajaenda CCM aliandika makala juu ya hili akasema ni muhimu kwa kiongozi kubalance demography za kitaifa ktk utumishi wa serikali.
Magufuli aishukuru sana BAKWATA na Sheikh mkuu, hawa wamekuwa kama nguzo yake kuu katika kutuliza munkari wa waislamu, lakini kiukweli lazima ukweli usemwe Teuzi za serikali y awamu ya tano zinanuka udini.

Na kama akishinda uchaguzi ujao akaendeleza teuzi za hivi basi ajue matatizo mengi ya utawala wake kupigwa vita sababu mojawapo ni yeye kushindwa kubalance force za demography kwenye watu wa kumsaidia kazi. Akimarginalize watu ajue pindi anapohitaji force za kumuunga mkono anaweza asizipate na kibaya zaidi inajenga chuki kali kwa wananchi ambao wanahisi wanatengwa

Pia Soma

Sehemu ya mazungumo ya Mheshimiwa Kitwana Kondo (MB) kuhusu mauaji ya Mwembechai

JUZI tarehe 21 ya mwezi huu, niliwaambia ya kwamba mimi ni mwanachama wa CCM, na kiongozi wa CCM,
na nina wajibu mimi wa kufuata maagizo na maelekezo yote ya CCM. Niliwaambia pia ya kwamba nina wajibu
mimi wa kutetea maamuzi ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi.

Lakini nilisema pia kwamba pia nina wajibu wa kuishauri serikali yangu pale ninapoona inafanya makosa.
Wajibu huu mie ninao.

Nililolisema na ninalisema tena leo ni kwamba serikali imekuwa Insensitive kwa mambo yanayowahusu
Waislamu na mambo mengine. Na kwa kuwa serikali inakuwa insensitive Waislamu wanatafsiri ile insensivity
ya serikali kuwa bila shaka serikali haiwapendi.

Siku ile nilitoa mfano wa kuingia Msikitini Polisi wa serikali walikuwa hawana sababu ya kuingia Msikitini.

Lakini lile limetokea na ghasia ambazo serikali yenyewe ili contribute (ilichangia). Kabla ya siku ile polisi
wamekuwa wakiwakamata Masheikh majumbani kwao kimya kimya.

Kama serikali ingekuwa inataka kumkamata Magezi wangeweza kumkamata Magezi nyumbani kwake.

Lakini serikali katika busara zake iliona Magezi imkamate Msikitini baada ya swala ya Alasiri pale mahala
pamejaa watu. Huku ikijua kwamba Magezi ana wafuasi wake.

Kwanini isimkamate Magezi asubuhi nyumbani kwake? Kwanini isimkamate Magezi usiku nyumbani kwake?
Wakaamua kumkamata pale. Kitendo kile ndicho kilicholeta rabsha ya tarehe 12.

Watu walipozidiwa nguvu wakakimbilia ndani ya Msikiti. Msikiti ule una wanawake ambao hawakuwahi
kutoka.

Sasa mimi bado narudia kwamba kama serikali ingetaka ingeweza kuuzingira ule Msikiti wale wangetoka tu. Ni
insensitivity yao ya kusema potelea mbali (kwanza) kwanini wangoje mpaka saa nane za usiku, wakavunja
mlango ambao mpaka leo haujatengenezwa wakaingia ndani. Walishawakatia umeme na nini. Wakavunja
Msikiti wakaingia ndani. Na si hivyo tu, wakawakamata, wakawapiga wale wanawake wakawapiga. Na
wakawamwagia unga ambao unawasha. Mimi nilizungumza na wale wanawake wanaeleza mambo hayo.

Sasa mimi nasema hilo linaonyesha insensivity ya serikali.

Na imefanya kosa kuwashitaki wale Waislamu wa Mwembechai kwa kusema Yesu si Mungu. Au kusema Yesu
si mwana wa Mungu au kusema Yesu hakusulubiwa. Imefanya kosa kubwa kuwashitaki wale. Kwa kusema
maneno ambayo ndiyo anayoyaamini miaka yote. Kila mahali palipo na Uislamu maneno hayo yapo.

Sasa naambiwa habari ya mahakama. Mimi sisemi habari ya mahakama. Nasema habari ya serikali. Mahakama
inapelekewa kesi. Sasa kesi ya kusema Yesu si Mungu haikutoka kwenye mahakama.

Haya yametoka nje, polisi ndio waliomshitaki mtu huyu kwa kusema Yesu si Mungu. Serikali ambayo haina
dini!

Mwaka 1996 walimamatwa vijana wawili Lushoto. Walikuwa Msikitini wanatoa mawaidha wakasema Yesu si
Mungu. Wakangojewa nje walipokuwa wanakwenda sokoni wakakamatwa. Wakashitakiwa kwa kosa, kwa
kashfa ya dini nyingine. Dini gani nyingine?

Kashfa yenyewe ni nini wamesema Yesu si Mungu. Na hivi juzi juzi, mambo ndio hayo hayo.

Sasa mimi nasema serikali inafanya kosa kubwa, serikali isiyokuwa na dini inafanya kosa kuwashitaki watu
kwa sababu ya imani yao.

Hivi karibuni Muadhama Kadinali Pengo amesema kwenye Kiti Moto ya kwamba kwa Muislamu kusema Yesu
si Mungu si kashfa. Kwasababu ndio imani yake. Na amesema mimi yaani yeye Kadinali Pengo naamini ya
kwamba Mtume Muhammad si Mtume wa mwisho. Hivyo ndivyo imani yangu. Si kashfa kwa dini yoyote.

Si hivyo tu, juzi kwenye gazeti la Dar Leo ... kuna maneno Maaskofu wamuunga mkono K.K. Hawa ni Maaskofu
wa Kanisa la Protestant, na wao wanasema kwa Muislamu kusema Yesu si Mungu si kashfa. Na kwa Mkristo
kusema Yesu Mungu si kashfa.

Haya ni maneno ambayo yamesemwa na Mabishops, sasa ikiwa dini yenyewe inayosemwa ni kashfa ni dini ya
Kikristo, Wakristo wenyewe wanasema si kashfa. Sasa serikali inasema kashfa kwa dini nyingine, dini gani?

Sasa mimi nilichowaomba mnisaidie siku ile ni kuiomba serikali ifute count hii. Serikali kusema lakini kesi iko
mahakamani si kweli. Serikali bado ina uwezo wa kwenda mahakamani na kusema tunafuta count hii.

Kuwashitaki kwasababu wanasema maneno yaliyoko ndani ya Qur’an ndio kusema serikali inaona Qur’an ni
kitabu cha uchochezi.

Unapomshitaki mtu mahakamani kwa uchochezi kwa kusema maneno yaliyo ndani ya Qur’an, lazima useme na
kitabu chenyewe ni kitabu cha uchochezi.

Sasa ninachosema mimi kwa bahati mbaya hawa kina Bwana walioshtakiwa kwa count hii moja wamepata
conviction maana yake, mahakama itakuwa inasema kitabu hiki ni kitabu cha uchochezi.

Swali langu mimi, serikali itaifungia Qur’an? Serikali wataifungia dini ya Kiislamu? Huo ndio woga wangu
mimi ... hiki kitabu ni kitabu cha uchochezi inabidi kifungiwe. Hawawezi kuwaambia Waislamu semeni yote
lakini haya Yesi si Mungu msiseme. Sasa hii ndio hatari ninayoiona mimi.

Kesi ikiwa mahakamani , pale mwenye uwezo ni hakimu. Lakini hakimu anapima ushahidi uliokuwa pale. Hawa
watu wasema wanastahili kupata dhamana. Hawa watu wanaumwa, wagonjwa. Jana gazeti moja limesema
Magezi kadhoofu kabisa. Yule Bwana Kamishna amesema Magezi anatibiwa jela. Na wengine.

Kuna mzee moja Musa Katembo ana umri wa miaka themanini. Basi hata nyie watu wa magazeti hamna huruma,
mtu wa miaka themanini! Siku hizi mahakama inasema hata mtu aliyeshitakiwa kwa kuua anaweza kupata
dhamana. Itakuwa huyu mzee wa miaka themanini, atafanya nini huyu akipata dhamana.

Sasa mie kuishauri serikali kwamba jamani hawa watu wamekaa zaidi ya miezi mitatu ndani. Ndani kule kuna
adha wamekuwa wagonjwa. Mmoja kesha kufa.

Sasa kusema aah alikuja ndani mgonjwa. Sasa kwanini msimpeleke hospitali! Sasa huenda akafa mmoja, mmoja
mmoja na dhana ipo. Dhana ipo kwamba serikali inafurahia hivyo; kwamba wafe mmoja mmoja. Sasa dhana
can be wrong. Na dhana usiitie kwenye sheria.

Kesi ikiwa mahakamani , pale mwenye uwezo ni hakimu. Lakini hakimu anapima ushahidi uliokuwa pale. Hawa
watu wasema wanastahili kupata dhamana. Hawa watu wanaumwa, wagonjwa. Jana gazeti moja limesema
Magezi kadhoofu kabisa. Yule Bwana Kamishna amesema Magezi anatibiwa jela. Na wengine.

Kuna mzee moja Musa Katembo ana umri wa miaka themanini. Basi hata nyie watu wa magazeti hamna huruma,
mtu wa miaka themanini! Siku hizi mahakama inasema hata mtu aliyeshitakiwa kwa kuua anaweza kupata
dhamana. Itakuwa huyu mzee wa miaka themanini, atafanya nini huyu akipata dhamana.

Sasa mie kuishauri serikali kwamba jamani hawa watu wamekaa zaidi ya miezi mitatu ndani. Ndani kule kuna
adha wamekuwa wagonjwa. Mmoja kesha kufa.

Sasa kusema aah alikuja ndani mgonjwa. Sasa kwanini msimpeleke hospitali! Sasa huenda akafa mmoja, mmoja
mmoja na dhana ipo. Dhana ipo kwamba serikali inafurahia hivyo; kwamba wafe mmoja mmoja. Sasa dhana
can be wrong. Na dhana usiitie kwenye sheria.

Sasa isisemwe maneno ya kwamba mahakama ndio inayowaweka. Si kweli. Mahakama inaamua baada ya
kuambiwa. Waliokuwa wakipinga dhamana siku zote ni serikali. Sasa wakati ule walikuwa wazima afadhali,
sasa wagonjwa. Kwahiyo, serikali isibabaishe hapa ikasema oh kesi ipo mahakamani.

Viongozi wangu baadhi wanasema kuwa mimi natafuta umaarufu. Mimi sitafuti umaarufu. Mimi maarufu. Mimi
sitafuti umaarufu. Mimi tayari maarufu. Kwahiyo, si kweli kwamba mimi natafuta umaarufu.

Mimi nimeanza ubunge 1965. Na tokea nimeanza ubunge sijagombea nafasi yoyote mimi nikashindwa. Yoyote.
Sasa umaarufu unakuaje.

Nimegombea ubunge mara nne nimeshinda mara zote nne. Nimegombea udiwani mara tatu nimeshinda mara zote
tatu. Nimegombea ubunge juzi juzi, nimeshinda. Nimegombea ujumbe wa kamati ya siasa ya mkoa juzi juzi
nimeshinda. Sasa umaarufu unakuwaje. Mie sitafuti umaarufu.
 
Japo nilikua mdogo kama miaka 4 hivi lakini sitasahau yale mabomu ya machozi asee tulipata tabu sana wakazi wa Manzese hilo tukio hadi leo lipo kichwani. Ikapelekea mzee kujenga fasta vyumba viwili Tabata Kisukuru tukahamia ingawa kulikua bado porini kweli kweli.

Sijui sababu ilikua nini dah.
 
Ilikuaje mkuu??
RPC alikuwa Alfred Gewe,hata mimi ningependa Kufahamu ukweli,Serikali ilidai Kuna baadhi ya nchi zilikuwa zinawapa mafunzo wahuni wa chama fulani,wengine wakidai kuna viongozi wa dini na serikali wanachochea chinichini kwa manufaa ya kisiasa,ukweli usiopingika ni kwamba walikula shaba live ndani ya msikiti na idadi ya wafu kufichwa,muhenga yeyote mwenye details zaidi aziteme.
 
nakumbuka Sheikh Ponds kipindi hicho alikuwa anacheza karate...aliwadhibiti wale mapoti Kwa kung-fu

walipozidiwa Kwa kung-fu za wale maustazi, wakakimbia na kwenda kuita Kaka zao..

eee bhanaa wee.! acha kabisa..

hadi sisimizi walikuwa hawakatishi Eneo hilo nao walikuwa wanapigwa;ndege WA angani nao walikuwa wanapigwa risasi live wakikatisha..

kile kikosi kilikuwa hatari Kama Barcelona ya Guardiola.! Hakuna huruma
 
Wakuu wa jukwaa,

Leo ningeomba tukumbushane, ni nini hasa kilisababisha vurugu za mwembechai mwaka 1998? Wakina nani walikuwa nyuma ya tukio lile? Wangapi walipoteza maisha? Je kuna askari ambao walichukuliwa hatua yoyote kutokana na vurugu zile?

Ahsanteni. Kama hujui kama pita kimya kimya tu
Ninachokumbuka ni kutapakaa kwa Yeboyebo zilizokosa wenyewe magomeni nzima.......fanya fujo uone si wa kuchezea!
 
Wakuu wa jukwaa,

Leo ningeomba tukumbushane, ni nini hasa kilisababisha vurugu za mwembechai mwaka 1998? Wakina nani walikuwa nyuma ya tukio lile? Wangapi walipoteza maisha? Je kuna askari ambao walichukuliwa hatua yoyote kutokana na vurugu zile?

Ahsanteni. Kama hujui kama pita kimya kimya tu
Nia yako nini?
Na pili Raisi wa Wakati huo ni mstaafu unaweza kwenda kumuuliza kama askari ndio waliokuwa na makosa au waliosababisha hizo vurugu n.k
Au una lako Jambo ndio maana unataka kumchokoa "pweza"
 
Ndani ya tukio hili niliwaona live polisi wa vituo vidogo vya polisi pale friends Corner,Tandale,CCM Manzese,Manzese mpakani wakivikimbia vituo vyao baada ya raia kuvivamia na kuwaachia waliopo ndani ya vituo hivyo na kuchoma makaratasi,kuchoma moto magari yenye namba za serikali ila walishindwa kukivamia kituo cha polisi pale urafiki,polisi walikilinda,kiza kilipoingia maeneo ya manzese wahuni wakaanza kula kula,FFU walikuwa wanaishia Morogoro road wakiingia ndani wanakutana mawe na kukimbia
Nalog off
 
Sikumbuki exactly but kilichoshangaza waliokamatwa walikutwa wakristo wengi sana

So mostly inaonesha kulikuwa na kilio tu cha watu kudai uhuru wa kuandamana
na uhuru wa kupinga hiki au kile...

Msikiti wa mwembechai ulitumika tu kwa raia wengine kujiunga kwenye madai hayo
 
Back
Top Bottom