Elections 2010 Kikwete ampigia debe Mramba!

Eti ana kesi ndogo ... kweli jamaa msanii tuu na kiini macho. Yaani akishapata tuu uraisi kesi zote kwishnei. Kweli anadhani wananchi wajinga sana!
 
Nimepata habari kutoka Rombo Kuwa JK amesema kuwa Mramba ana kesi ndogo na atashinda hivyo wananchi wamchague !!!

Kuna maana gani kuwa na mahakama kama Rais ameshatoa hukumu tayari? Sasa kama huyo jaji akisaidiwa na vielelezo/ushahidi akiona Mramba ana HATIA, je nani hapa afukuzwe kazi??
JK, wewe pigia kampeni mafisadi wenzako, waache majaji wafanye kazi yao.
Tutashangaa siku moja JK ataibukia kutoa ramli kwenye mashindano ya MDUNDIKO au BSS......watch!!
Picha za fisadiz hapo chini.
 

Attachments

  • Mramba.jpg
    Mramba.jpg
    38.5 KB · Views: 267
  • Mramba2.jpg
    Mramba2.jpg
    86.4 KB · Views: 25
Swala la CCM kumsimamisha Mgombea ambaye ana kesi mahakamani ni makosa makubwa sana ya kisiasa. Na kila atakalosema Kiktwete lazima litakuwa na walakini kwani haiwezekani kumtetea mtu wa aiana hii kwa njia yeyote. Ilitakiwa kesi ya hawa watu imekwisha kabla hajajiandikisha kugombea na maadam CCM imempitisha, basi pengine wao wanajua zaidi ya hata mahakama.
Mkandara, mkuu wangu jana nimezungumza sana na mama mmoja ambaye alikuwa mkeleketwa asiyetaka kubadilika ili abadili msimamo na nili site mfano wa Mramba kama kielelezo cha hoja yangu mpaka akanielewa, kwani alikuwa na msimamo kuwa mafisadi wamepelekwa mahakamani. Mwisho yule mama akaniambia "Lakini wewe wasema ukweli, hivi mtu ukiwa na kesi mahakamani si unasimamishwa kazi hadi kesi iishe? mbona huyu bado yuko kwenye chama na serikalini?" niliona kaelewa nini nilikusudia na mara akageuka na kurudi upande wangu. Hiyo kura sisi M hawaipati tena. Maana hapo hapo akasema kumbe ni kweli afadhali kumpa Dr Slaa.

Lakini Hapa tu unaweza kuona jinsi sisi m walivyobugi sio? Wanacheza na akili za wananchi. Na sisi tutawakomesha.
 
“Kikwete ni rais aliyedanganywa duniani kuliko marais wote na kufanya makosa ambayo yanawatesa watanzania,” Dk Slaa.
 
Mkewe, Salma, anasema JK ni mahiri kupigana na ufisadi na rushwa, sasa sijui kama mama huyu ana high reasoning capacity!!
 
Waarabu wa Pemba hao, wanajuana kwa vilemba, JK anasema" MRAMBA NI PANGA LA ZAMANI LENYE MAKALI YALEYALE", ana maana MRAMBA NI FISADI LA ZAMANI SANA SERIKALINI NA LINAJUA JINSI YA KULA HELA ZA WALIPA KODI WA NCHI HII KWA HIO WATAENDELEZA UFISADI WAO"

Kaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaazi kweli kweli.
 
Naona nina wajibu kuchangia ktk Suala hili la J.K. kumpigia debe Basil Mramba. Nitangulize kusema kwamba namheshimu na kumwonea huruma sana Rais wangu Kikwete. Nikiri pia kwamba Basil Mramba ni rafiki yangu binafsi wa siku nyingi.

Kwanza, kesi ya Mramba ni ya JINAI. Kama Mramba hangekuwa na wadhamini wa kuridhisha Mahakama, ungekuta sasa ni mahabusu anaishi Keko au gereza lolote la Serikali Tanzania akingojea maamuzi juu ya kesi inayomkabili.

Pili, kesi yoyote ya jinai ni kesi ambayo Serikali inamshtaki mtuhumiwa. Serikali ni taasisi inayoongozwa na Rais, ambaye kwa wakati ule Mramba akituhumiwa ilikuwa ni Kikwete anaiongoza, na hata sasa anaiongoza hadi hapo matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba utakapoamua aendelee au asiendelee.

Tatu, nina hakika kwa mtu mashuhuri kama Mramba, na kutokana na kiasi cha fedha zinazodaiwa Serikali imepoteza kutokana na mkataba Mramba aliosaini (Shs bilioni 12), ni lazima Rais alihusika kwa karibu sana na alikubali kesi ifunguliwe dhidi ya waliohusika: yaani Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja.

Nne, kwa vile Mhe. Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM, na alifahamu Basil Mramba alikuwa amemtuhumu (akiwa Rais na kiongozi wa Serikali), angeshauri CCM isimsimamishe kugombea jimbo la Rombo. Kwa hiyo, kwa heshima na taadhima, nasema Mhe. hakutumia uwezo wake na taarifa alizokuwa nazo kupata maamuzi busara kuhusu ugombea jimbo la Rombo. Kama Kamati Kuu ya CCM ilimlazimisha Mwenyekiti wake amkubali Mramba, basi ni cham cha mafisadi kweli!!!!

Tano, hata kama Mramba alikuwa MwanaCHADEMA aliyekuwa na kesi inayomkabili mahakamani, na akapendekezwa na kura za maoni za wanaCHADEMA wa Rombo, sisi katika Kamati Kuu ya CHADEMA, hatungeidhinisha uteuzi wake aendelee na kampeni. Kwa hiyo, kwa Kamati Kuu ya CCM inayoongozwa na Mhe. Kikwete, kuidhinisha mtuhumiwa wa ufisadi agombee ubunge, inadhihirisha CCM kudhalilisha Bunge kama taasisi.

Sita, kwa Mhe. Kikwete wiki hii, kumpigia debe, Basil Mramba, mtu ambaye yeye kama Rais, amempeleka mbele ya Mahakama akimtuhumu kwa kusababisha hasara ya mabilioni ya shilingi, mali ya Serikali, inadhihirisha kutoshauriwa vizuri au yeye mwenyewe kuchanganyikiwa kwa hali ya juu.

Saba, sisi wanaCHADEMA tutaendelea kuwakumbusha wapiga kura wa Rombo kwamba Mramba ni mtuhumiwa na wasimsikilize kwani anaweza kupatikana na hatia na asiweze kuwawakilisha Bungeni. Pia sisi tusisitize kwamba Mhe. Kikwete anashauriwa vibaya au hajui hatua zinazotakiwa kuimarisha utawala bora na kwa hiyo hafai kuchaguliwa kuendelea kuwa Rais.

Mgombea wetu Dk. Willibrod SLAA apigiwe kura.
 
Ukiona Fisadi anadiriki kusimama jukwaani na kumpigia debe fisadi mwenzake huku akiwadanganya watu kuwa kesi aliyonayo fisadi ni ndogo, na wakati baadhi ya nyakati Fisadi akijisifia kupiga vita ufisadi kwa kuwapeleka mahakamani baadhi ya mafisadi! ujue nchi hiyo ina idadi kubwa ya mbumbumbu ndiyo maana
fisadi anapata hata watu wachache wa kumsikiliza.
 
CCM ndio walikuwa wa kwanza kusema kesi zilizoko mahakamani zisiongelewe kwenye majukweaa ya kamapeni, wakaenda mabli kwa kuwa tuhumu CHADEMA kuwa walikiuka maadili ya uchaguzi na sheria za mahakama kwa kuongelea ufisadi wa serikali siku ya uzinduzi wa kamapeni zao! sasa ajabu leo hii mgombea wao wa Urais ( ambaye pia bado ni rais) sio tu anazungumzia kesi iliyoko mahakamani bali anafika mbali pia kutoa HUKUMU kuwa Mramba ATASHINDA kesi hiyo! Sasa jaji anayesikiliza kesi hiyo ambaye ni mteuliwa wa Rais huyo huyo anawezaje kwenda kinyume na boss wake? maana tumekwisha ona huko nyuma kumbuka kesi ya mgombea binafsi, kesi ya mgomo wa walimu, pingamizi la Chademna dhidi ya Mgombea (jaji!) wa CCM!
 
Haya jamani, Kikwete amegeuka kuwa hakimu, anajua kuwa kesi ya mramba ni ndogo na atashinda tu
Loooh, this is a type of president we have now, ila ngoja tarehe 31, viziwi watasikia bandugu au mnasemaje?

Ole wa hakimu anayesikiliza hiyo kesi! kama mkuu kashasema hivyo ujue ni ujumbe tosha kuwa
1. kesi iishe kabla ya tarehe 31
2. Mshtakiwa aachiliwe

Here we go. Mtahangaika kuleta data za wezi na mafisadi wa seriakli ya CCM; KAMA CCM IISHIVYO, HAKUNA FISADI ATAFUNGWA!
 
Hii ndo inadhihirisha wazi kuwa JK yupo kwa ajili ya 'wateule' wachache..
Sasa washabiki wake wameambiwa na wasikie..watanzania wanaongelea sio wao ni hao 'wateule' ...
 
Ikiwa hadi kesho kama Jaji Mkuu hajatoa statement ya kumkemea Kikwete, basi waandishi wa habari waende kumuuliza kwa nini.
Inategemea kama ndani ya akili zao hao waandishi kuna akili za kutosha
Mostly wapo kwenye payroll ya 2010 Kikwete Press Team.
 
JK+na+Mgombea+ubunge+wa+jimbo+la+Rombo+Mh.+Basil+Mramba+wakionesha+alama+ya+dola+ambayo+CCM+inatumia.jpg



Wana JF nimeona hii picha kwenye blog ya michuzi na NIMESHITUKA SANA. Hivi Mramba si anayo kesi inayoendelea mahakamani ya matumizi mabaya ya ofisi, na nina kila sababu kuamini kuwa kesi hii haikuenda mahakamani bila ya JK kutoa baraka ZAKE!! Sasa JK kumsifia Mramba na kumnadi kweli kunatoa picha gani kwa raisi wa nchi?

I am so disturbed kuona kama kweli JK anafikiri athari za matendo yake kabla haja act. Hivi kwa Judge anayesikiliza kesi ya Mramba anawekwa kwenye position gani, kama mkuu wa nchi ameshamsafisha? Je wale wanaotoa ushahidi dhidi ya Mramba si wataogopa, wengine bado wako serekalini. JK huo si utawala wa sheria, huwezi kujiassociate na mtu ambaye ana stain, hata kama stain yenyewe haijathibitishwa na mahakama kama kweli ni stain, but in public eyes ni kuwa ana stain!!!, ni kuwa amechafuka, kitendo cha serekali ya JK kumpeleka mahakamani na hata gerezani ni ishara tosha kuwa amechafuka, sasa unamandi na kumsifia mtu aliyechafuka? KWELI HUO NI UTAWALA BORA-- SHAME!!!

Hakuna nia ya dhati ya JK kuupiga vita ufisadi, na inauma kwa kuwa ni kama kuwang'ong'a wananchi huku wao wakichekeana, lol, this is a joke, tena joke ya mwaka. Chadema this is a scandal which mnaweza kuiongelea kwenye kampeni zenu na kuwaacha wananchi kuamua.
 
Back
Top Bottom