Kikwete akutana na uongozi wa CHADEMA Ikulu; Dr. Slaa ndani

Kususa inkwisha? mlipoteza muda mrefu sana kwa siasa za kususa susa, naona mmejifunza kuwa kususa inatumika kuwa "disadvantage" kwenu.

Slaa, nakupongeza kwa kuliona hili ingawa si matakwa yako ni matakwa ya Mwenyekiti wako na inabidi uyaheshimu na nna uhakika kuwa yupo sahihi na wewe umeshaliona baada ya kukutana na Rais wako.

Inawezekana hata aliyekuwa anasusiwa kajiuliza kwann mie ndo wananisusia so kaamua ku cool down na kukaa nao awasikilize.
 
Dr Slaa ni mtu makini sana..atakuwa ametuwakilisha vyema jana..sasa Jk na serikali yako myapuuzie hayo maoni then vijana wa kazi tuingie barabarani..
 
jigoku said:
Pasco usikatae wewe kuna kitu unajaribu kutengeneza na mwisho wa siku umeamua kujipendekeza,lakini kila mtu mwenye kutafakari kwa kina alikushangaa jinsi ulivyolishikia bango suala la kusalimiana kwa JK na Dr Slaa,sasa unataka kutuaminisha ya kwamba wewe ndio umesababisha Dr Slaa asalimiane na JK?kwani issue hapo ni nini?kuna kitu unachokitafuta na ndio maana watu wanakuona kama mzandiki,wana kuona mmbea,mimi najua unajipendekeza kwa Magamba ili utimize ndot zako.
Nikufahamishe tu ya kwamba Dr Slaa wewe ni mdogo kama Pilton,nadhani unajua udogo wa kidonge hicho,huyo ni mtu ambae wewe huwezi kwa namna yeyote iwayo ukamchafua au ukatengeza namna ya kushhusha PR yake kwa jamii.
Pole sana msukuma mwenzangu.
Msimlaumu Pasco, bado upatikanaji wa picha hii haukuwa rahisi, ama wangapi kati yenu mna access ya ikulu humu?

Naona ni bora mjadili kilichowapeleka kwasababu si kawaida kwa JK na Slaa kupeana mikono.
 
WanaJF,

Nawashukuru wote wanaofuatilia thread hii. Nawaomba kwa mara nyingine muwe na amani. Nawahakikishia hakuna wala hakutakuwa na usaliti. Chadema iko makini sana. Tunasukumwa na uzalendo na nia njema kwa Taifa letu.

Aidha kama alivyosema MMJ, tumekuwa tukisukuma mabadiliko makubwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kabla Rais hajateua Tume ya kukusanya maoni. Tulieleza wazi kuwa vinginevyo hatutashiriki mchakato wa kukusanya maoni.

Ni dhahiri busara ya kawaida inataka tupate progress ya majadiliano hayo hayo na utekelezaji wake. Katiba nzuri ndio afya na uhai wa Taifa hata kama si ufunguo wa matatizo yote yanayotusibu leo. Wakati mwafaka utakapofika tutatoa Taarifa kwa umma.

Msiwe na hofu mtuamini.

Kuna wakati najiuliza, hivi tusingekuwa na Chama makini cha Siasa ule ubabe uliozoeleka kutumika sio ndio ungetumika tena kwenye Mchakato huu? Thank God, tunacho Chadema kwa sasa. Tuko pamoja Dr. na tunasubiri taarifa
 
Kususa inkwisha? mlipoteza muda mrefu sana kwa siasa za kususa susa, naona mmejifunza kuwa kususa inatumika kuwa "disadvantage" kwenu.

Slaa, nakupongeza kwa kuliona hili ingawa si matakwa yako ni matakwa ya Mwenyekiti wako na inabidi uyaheshimu na nna uhakika kuwa yupo sahihi na wewe umeshaliona baada ya kukutana na Rais wako.

FaizaFoxy,
Si vema kupotosha wala kuingiza ushabiki katika mambo mazito. Tuko kwenye process na kinachoendelea kisitazamwe as an isolated incidence. Process hii ilianzia na wabunge wa Chadema kususia Bunge. Ni vema mtu akatafakari kwa kina kuelewa vizuri mchakato unaoendelea. Umakini, kutafakari na kuchukua hatua ndio njia pekee ya kufikia malengo makuu ya kuliokoa Taifa letu.
 
FF kama unajuwa kusoma btn the lines unaweza kuniambia umeilewa vipi hiyo kauli hapo juu ya Dr Slaa?

Ni bora ufikishe ujumbe kwa boss kuwa umakini unahitajika kuliko kuja na vijembe peke yake.
 
Naona badala ya kushirikiana kwenye misiba tu JK&CDM wameamua kushirikiana kutatua matatizo ya watz kama kupatikana kwa people's constitution.
 
Labda umechoka wewe na familia yako! Usitusemee mkuu

Unajua punguani uwa hajijui kama yeye ni punguani,na mara nyingi anaweza akadhani anafanya mambo vizuri kuliko wengine...hivi na kweli mtu mwenye akili timamu unaweza ukasema hoja kama hii? nchi ina matatizo yafuatayo makubwa;
  1. Vyakula bei juu...
  2. ombwe la uongozi,mara posho,mara kupishana kauli nk
  3. thamani la shs kushuka
  4. migomo vyuo vikuu..
  5. Malalamiko karibia kila kada ya watu,si wanachi,wanasiasa,viongozi wa dini nk
  6. .......nk
Hivi wewe haya yote unaona sawa na unasema hujachoka? kweli punguani ni mtu wa ajabu sana....
 
Finally......!!!! huu ndio ukubwa na ukomavu wa kisiasa, luv u CDM & JK, ila JK ungemnongoneza Dr. Slaa hivi:
Kuiba kura bila kushikwa si KUIBA, halafu jioni wapeleke wakale & wakanywe kidogo, then umoja unakuwa, asanteeee CDM
 
FaizaFoxy,
Si vema kupotosha wala kuingiza ushabiki katika mambo mazito. Tuko kwenye process na kinachoendelea kisitazamwe as an isolated incidence. Process hii ilianzia na wabunge wa Chadema kususia Bunge. Ni vema mtu akatafakari kwa kina kuelewa vizuri mchakato unaoendelea. Umakini, kutafakari na kuchukua hatua ndio njia pekee ya kufikia malengo makuu ya kuliokoa Taifa letu.

Dr Slaa tunakuunga mkono.Tupo nyuma yako.
 
Msimlaumu Pasco, bado upatikanaji wa picha hii haukuwa rahisi, ama wangapi kati yenu mna access ya ikulu humu?

Naona ni bora mjadili kilichowapeleka kwasababu si kawaida kwa JK na Slaa kupeana mikono.

Mzee unachoshauri kifanyike katika hali ya kawaida ni kwamba hakiwezekani hata wewe unajua hivyo ila may be umeamua tu kuchangamsha barza maana unachokisema ni sawasawa na kujaribu kumnukuu mtu ambae amekaa kimya!can you do that?unawataka watu wajadili kilichowapeleka bila kukijua kilichowapeleka...!kila mtu hapa unasikia analia na kutojua chochote kutokana na mkutano huo,mjumbe mmoja wa kutano huo bahati nzuri kajitokeza hapa jukwaani lakini katika hali ya kusikitisha nae ameendelea kuficha waliyozungumza tukiuliza tunaambiwa tutajulishwa "wakati muafaka" ukifika!hiyo ndio hali halisi.

Labda watu waujadili mkono wa "dhahabu" wa slaa kwa jk maana vijana wanadai ulikua unasakwa kwa gharama yeyote ile hata ikiwa kwa kupanda juu ya makaburi kuupata mkono huo tulipanda bila kujali kuwajali ngugu zetu hao waliotangulia na nyumba zao hizo tulimowahifadhi,muhimu ilikua mkono wa dhahabu huo upatikane!thats our politics arena!
 
Kuna wakati najiuliza, hivi tusingekuwa na Chama makini cha Siasa ule ubabe uliozoeleka kutumika sio ndio ungetumika tena kwenye Mchakato huu? Thank God, tunacho Chadema kwa sasa. Tuko pamoja Dr. na tunasubiri taarifa

Na pia mshukuru mnae rais msikivu ama muoga vyovyote utakavoiweka,angekua mkapa "upuuzi" huu asinge ukubali abadan!nadhani wengi tunakumbukumbu nae mzee mkapa,huwa alikua hakubali kujishusha kwa wapinzani hata iweje na sikumbuki yeye kufanya kikako na wapinzani ikulu au popote pale kwa miaka kumi yote ya utawala wake,mwenye kumbukumbu hiyo atusaidie!
 
BAK fani yangu inanitaka niwe impartial. Tatizo langu ni watu wa upande fulani wametamalaki mpaka kufikia kiwango cha kujiona jf ni jukwaa lao na yoyote akiukosoa upande wao au viongozi wao, watamshukia kwa nguvu zote kuwa katumwa, analipwa with all sort of names!.

Nilishajifunza kitu kutokana na ukosoaji wa Chadema, nashukuru mimi uvumilivu wangu bado ni mkubwa.
Hiyo link uliyo iweka ndio nimemchafua Dr. Slaa?!. Haya nimekubali sasa turudi kwenye mada Mkuu BAK!.

Hahahahahah lol! kwanza ulisema umesoma literature sidhani kama kusoma kwako literature kunakupa ruhusa ya kuja hapa jamvini na kuzuga watu. Waliosoma literature hapa jamvini wapo wengi tu. Fani yako kama inakufanya uwe impartial basi naona huitendei haki kabisa fani yako maana mara nyingi sana hapa jamvini umeikandamiza CHADEMA na hata kumpigia debe fisadi Lowassa waziwasi, sijui mwenzetu unakiona kipi toka kwa Lowassa hadi umfagilie kiasi hicho, labda utapata muda siku utueleze. Amekuwa madarakani miaka chungu nzima lakini sidhani kama unaweza kupinpoint chochote kile alichowahi kukifanya akiwa madarakani kwa maslahi ya Tanzania na Watanzania zaidi ya kujikusanyia utajiri kupitia migongo ya walipa kodi wa Tanzania.

Wiki chache zilizopita kulikuwa na mjadala kwenye TV nadhani ulihusu katiba mpya na wewe ukamtwanga swali Tundu Lissu (kama sikosei) swali ambalo lililenga kumuadhiri. Pia katika kumzodoa kwako Dr Slaa ungeweza kabisa kuandika Kikwete kamkacha Dr Slaa katika mazishi ya Regia maana hata Kikwete bila shaka alimuona Dr Slaa katika mazishi yale na angeweza kabisa kumfuata kwa nia ya kumsalimia kama akgekuwa na nia ya kufanya hivyo, lakini hakuuona umuhimu wa kufanya hivyo. Basi na wewe ulipoliona hilo ukaona umejipatia nafasi nyingine ya kumpiga dongo Dr Slaa kwamba kamkacha Kikwete mazishini.

Usijifiche nyuma ya pazia la eti "nimesoma literature" au "Fani yangu inanitaka niwe impartial." Ukiona mashambulizi yanazidi dhidi yako hapa jamvini unataka kuzuga watu kwamba umesoma literature au fani yako inakutaka uwe impartial lakini kwa taarifa yako tumeshakushtukia kwamba wewe unacheza kwenye kambi zote mbili huku ukiwa umeegemea zaidi upande wa Magamba tena unafanya hivyo kwa maslahi yako zaidi badala ya maslahi ya Tanzania na Watanzania. Bado ni mapema mno Mkuu kuweza kuchagua bega ama la magamba kupitia mgombea wako Lowassa au la CHADEMA nakuomba ufanye maamuzi haraka badala ya kutaka kuendelea kuzuga watu hapa jamvini.

Jumapili njema Mkuu.
 
Mtu huwezi kuwa jikoni halafu uwe mtu wa kusubiri makombo. Ukiwa jikoni unaweza kushiba kwa kuonaja tu. Tusidanganyane hapa, walio jikoni ni hao tunaowana hapa kwenye picha. Jamaa anajifariji kwa 'kurumagia' ugali kwa halufu au picha ya samaki.

msimbishie sana jamaa yangu,labda na yeye ni mmoja wa hao mnajuaje na hapa wengi wetu hatutumii majina yetu,may be mnabishana na freeman mbowe mwenyewe who knows?yeye kawaambia yuko jikoni so that anaweza kuwa ni mbowe pia lakini amekuja kivingine hapa!
 
Kim, naona sasa umeishiwa hoja unaanza kujichekesha chekesha. Mimi ni ''Traditionalist'' huwa sidanganywi na vicheko vya kichina!
Btw, nimealikwa na mafilili kuja hapo mtaa wa lumumba., nikifika nitakutafuta ili nikujulie hali. Kwa hii inflation ya 19.82% sidhani kama hali yako ni mujalab!

Nashukuru baada ya kuwaona viongozi wako wameanza kuelewa namna ya kufanya siasa za kistaarabu hasa baada ya kuwaona wamekaa na rais kwenye makochi wakinywa mvinyo na kucheeeeka na wewe umebadilisha ile style yako ya kufanya siasa hapa ndani,maana sijasikia tena ukiniita "mchumba",haya ni maendeleo makubwa,nimejaribu kuitafuta ile post yako ya jana uliyoniita hivyo kwa mara ya mwisho ambayo kama utakumbuka sikuijibu niliipotezea lakini sijaiona, naona mods walikudharau wakaamua kuifuta,ili ilitosha kuwadhihirishia mods na wastaarab wengine wanojua siasa wewe ni mwanasiasa wa aina gani ya siasa-SIASA ZA MAJI TAKA!ulijidharirisha sana kwa post ile na bahati mbaya uliiharibia mpaka chadema maana watu wanaamini kweli uko jikoni!
 
Na pia mshukuru mnae rais msikivu ama muoga vyovyote utakavoiweka,angekua mkapa "upuuzi" huu asinge ukubali abadan!nadhani wengi tunakumbukumbu nae mzee mkapa,huwa alikua hakubali kujishusha kwa wapinzani hata iweje na sikumbuki yeye kufanya kikako na wapinzani ikulu au popote pale kwa miaka kumi yote ya utawala wake,mwenye kumbukumbu hiyo atusaidie!
Mkapa aliweza kwa mazingira yale.temper ya nchi inalazimisha maridhiano.hali si nzuri mkuu hakuna jinsi.
 
FaizaFoxy,
Si vema kupotosha wala kuingiza ushabiki katika mambo mazito. Tuko kwenye process na kinachoendelea kisitazamwe as an isolated incidence. Process hii ilianzia na wabunge wa Chadema kususia Bunge. Ni vema mtu akatafakari kwa kina kuelewa vizuri mchakato unaoendelea. Umakini, kutafakari na kuchukua hatua ndio njia pekee ya kufikia malengo makuu ya kuliokoa Taifa letu.

Tunashukuru Dr Kwa maelezo yako makini na nakupongeza sana kwa kujumuika nasi hapa jamvini. Tulikuwa naye Bi Regia lakini kwa bahati mbaya Mungu hakupenda tuendelee naye, yeye alimpenda zaidi.

Pole pia kwa kumpoteza mpiganaji wako mahiri . Tunajua katika huu mchakato wa kuelekea katiba mpya mengi ya mapendekezo yenu yatapata nafasi kwani yana kila ujazo wa nguvu za hoja. Ujazo na uzito ambao bila ya shaka ndio unaopelekea mchakato wa vikao vya kukutana na rais kuendelea. Hilo hatuna shaka nalo. Mimi ninalo jambo dogo sana la binafsi, ambalo ningependa wewe mwenyewe uliweke wazi.

Kumekuwa na mada nyingi ambazo kwa namna moja ama nyingine watu wamekuwa wakidai kuwa, umekuwa na kinyongo na rais tangu wakati ule baada ya uchaguzi mkuu uliopita na, kumekuwa na madai kuwa huwa ukikwepa kukutana naye. Unasemaje kuhusu madai hayo? Ili mijadala hiyo ambayo si muhimu sana kwa hali ilivyo sasa, ife kabisa.

Mwisho; utaratibu wa kumface moja kwa moja rais na kufanya majadiliano naye moja kwa moja ni mzuri sana kwani tuna mashaka washauri wake ama watendaji wake wa chini huwa wakimpotosha katika mambo mengi. Mfano ni katika muswada huu wa katiba mpya ambao mpaka sasa unagonga vichwa vya watanzania walio wengi.

Kwanini basi kusiwe na mpango wa kundelea kumtembelea mara kwa mara kwa ajili ya kujadiliana mambo mengine pia yanayohusu mustakabali wa Taifa kama vile kupanda kwa gharama za maisha kupita kiasi, kuporomoka kwa uchumi kunakokuja kwa kasi, ufisadi na nk? Hii itasaidia kumkumbusha kuwa, meli anayotarajia kuiendesha kama nahodha imekwama mchangani katikati ya jangwa huku abiria, yaani wananchi tukisubiri kusafiri.
 
Back
Top Bottom