Kikwete akutana na uongozi wa CHADEMA Ikulu; Dr. Slaa ndani

watanzania tusikubali kuporwa na wanasiasa haki yetu ya kutengeneza katiba, kwa sasa wanasiasa na vyama vyao wako front...na lengo lao ni kulinda maslahi ya vyama vyao. Kwa nini jk asikutane na wawakilishi wa wananchi, wanaharakati, wasomi na wataalamu, wanakutana wenye we na hata tofauti zao wanaziweka pembeni katika hili wanasiasa kuwa front front linaniogopesha kidogo. Kwani wanasiasa ndo wametufikisha hapa tulipo.... Wananchi tuwe makini na hawa wanasiasa ushabiki, itikadi, na mapenzi kwa vyama vyetu visiwe na nafasi katika maamuzi wakati wa kuandika katiba.la sivyo yatakuwa yaleyale, mfano hapo kuna chama ambacho kiko tayari kufuta ruzuku?? Katika katiba mpya?? Wasiturubuni wote ni wanafki wanatofautiana tu viwango

strong point!

....Inatia matumaini, labda Kikwete amegundua kwamba Katiba itakayopatikana kama itakuwa ni ile ambayo Watanzania tunaitaka atajizolea sifa kemkem si tu toka kwa Watanzania bali jumuiya ya kimataifa na hivyo kuamua kuwashirikisha CHADEMA kwa karibu mno....Labda haya ndio matunda ya mwanzo ya Ambassador Ombeni Sefue.

kwenye meza ya mazungumzo ya amani usitafute ushindi wote Jk na chadema ni washindi katika jambo hili.
 
Mambo ya ndani hayo baada ya kukutana ndani ya chama ndipo tunatoa taarifa kwa umma, si kila kilichozungumzwa kinawekwa hadharani, mengine ni ya kiutendaji zaidi, yale ya public mtayapata muda si mrefu.

Hilo la kuunganisha vyama , hiyo ndoto sahau na kuachana nayo kabisa.
Mkuu maranya, katika siasa chochote chaweza kutokea. Inaweza kuwa si kuunganisha vyama lakini kitu kingine ambacho kitakuacha mdomo wazi. Ndugu yangu usiwe mwepesi wa kula yamini namna hiyo utakuja kuiona dunia chungu pindi utakapogundua kwamba wenzako si wenzako!
 
Mkuu yaani yaliyoongelewa Ikulu mtakwenda kuyachuja na kutoa tamko? Kama kuna makubaliano yalifikiwa pale Ikulu na mkasaini (kama wakati ule) kisha kikao chenu kikayakataa itakuwaje? Hamuwaamini mliowatuma?Kwenye ujumbe ule nimemuona Mnyika nikadhani akitoka tu pale.atakwenda kuufahamisha umma nini kilijiri kwenye mkutano, kumbe itabidi asubiri mkutano mwingine ili apewe maneno ya kusema! Kaazi kweli kweli.
Sasa wakati anakwenda Ikulu aliufahamisha umma we vipi?
 
Naam, naona unazidi kufurahia kutazama picha ya Dr. Slaa akisalimiana na mkuu wa kaya, ni haki yako kwakuwa hii picha mmeitafuta sana, sasa walau mmepumua.

Mimi sijawahi kuwa na undugu na ccm, wala sikushikwa mkono na mtu kujiunga chadema, na yanayojiri chadema ninayafahamu vizuri ndio maana ninakushangaa wewe unayejidanganya kuyafahamu mambo ya chadema ambayo kwa bahati mbaya huyafahamu. Chadema haihitaji kunipenda, inahitaji mchango wangu wa hali na mali, ndio maana hadi sasa nipo kuitumikia kwa nafasi yangu. Sasa wewe unayependwa na ccm endelea kupendwa tu tutaona mustakabali wa mapenzi yenu.

Kujiunga hivi karibuni si tatizo kwakuwa bado watu wataendelea kujiunga, tatizo ni ninyi kujipatia ujira kwa kupost fyongo hapa JF. Na hili la ajira zenu za jf tunalifahamu kwa ushahidi wa maandishi, mukama ndiye aliishauri kamati kuu ya ccm kuajiri watu kuja kuitetea hapa jf, bahati mbaya sana mnaandika pumba nyingi kuliko madini, badala ya kuleta thread za kuonyesha mafanikio ya ccm kama yapo mmeishia kuandika mambo ya chadema, sasa katika hali kama hiyo unadhani tutawaacha mnamwaga fyongo na sisi tuwachekee? nope!

Hii picha ya kihistoria nimeamua kuitengenezea frame niitundike ukutani ofisini kwangu!

Wakiondoka Ikulu:
slaa-lissu-kikwete.jpg

slaa-baregu-kikwete.jpg
 
Najiuliza tena swali lingine; Mbowe alisema alipoulizwa kwamba ameongea nini na Rais akasema wana msiba hawezi kuongelea hayo masuala. Sina hakika kama msiba umeisha. Lakini kabla Mbowe hajatuambia ni nini waliongea na Rais, tunaona mkutano wa pili kati ya Rais na CDM Dr. Slaa akiwa ndani ya jumba. Je haya ndiyo majibu ya Mbowe juu ya mkutano wake usiorasmi na JK?

Hii inanikumbusha mikutano isiyo rasmi ambayo watanzania hatujapata kusikia ni nini kiliongelewa baada ya wahudhuriaji kukaa kimya na siri zao mioyoni mwao: Maalim na Nyerere, Mrema na Nyerere na sasa JK na Mbowe. Kuna mikutano mingine isiyo rasmi ambayo hatukuambiwa ni nini kilichoongelewa bali tulishuhudia tu matunda ya hiyo mikutano: Mikutano isiyo rasmi kati ya Maalim Seff na Dr. Karume tukashuhudia muafaka wa kitaifa.

WanaJF,

Nawashukuru wote wanaofuatilia thread hii. Nawaomba kwa mara nyingine muwe na amani. Nawahakikishia hakuna wala hakutakuwa na usaliti. Chadema iko makini sana. Tunasukumwa na uzalendo na nia njema kwa Taifa letu.

Aidha kama alivyosema MMJ, tumekuwa tukisukuma mabadiliko makubwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kabla Rais hajateua Tume ya kukusanya maoni. Tulieleza wazi kuwa vinginevyo hatutashiriki mchakato wa kukusanya maoni.

Ni dhahiri busara ya kawaida inataka tupate progress ya majadiliano hayo hayo na utekelezaji wake. Katiba nzuri ndio afya na uhai wa Taifa hata kama si ufunguo wa matatizo yote yanayotusibu leo. Wakati mwafaka utakapofika tutatoa Taarifa kwa umma.

Msiwe na hofu mtuamini.
 
Hivi hakuna vyama vingine mbona jk anakutana na hawa mara kwa mara..hahaaaa chezea chadema weewee..ccm mtakubali tu mwaka huu
 
Updated the 1st post, kuanzia wakati wanakutana mpaka wanaagana
Kumbe juice ilikuwepo! Halafu nimeona Dr. Safari na jamaa mwenye nguo ya bendera wakiwa wana vitambulisho, wengine hawana. ikoje?

Mbona Mabere Nyaucho Marando huwa hahudhurii hivi vikao au utetezi wake wa mafisadi unamtafuna hawezi kuwekwa front office?
 
Mambo ya ndani hayo baada ya kukutana ndani ya chama ndipo tunatoa taarifa kwa umma, si kila kilichozungumzwa kinawekwa hadharani, mengine ni ya kiutendaji zaidi, yale ya public mtayapata muda si mrefu.

Hilo la kuunganisha vyama , hiyo ndoto sahau na kuachana nayo kabisa.

utalia na kusaga meno siki ikiwadia!
 
Mkuu yaani yaliyoongelewa Ikulu mtakwenda kuyachuja na kutoa tamko? Kama kuna makubaliano yalifikiwa pale Ikulu na mkasaini (kama wakati ule) kisha kikao chenu kikayakataa itakuwaje? Hamuwaamini mliowatuma?Kwenye ujumbe ule nimemuona Mnyika nikadhani akitoka tu pale.atakwenda kuufahamisha umma nini kilijiri kwenye mkutano, kumbe itabidi asubiri mkutano mwingine ili apewe maneno ya kusema! Kaazi kweli kweli.

Najua huwezi kulielewa hili kwakuwa halifanyiki kama unavyotaka, chama ni taasisi ina vyombo vyake vya uendeshaji na utendaji. Waliokwenda ikulu ni wawakilishi wa kamati kuu lazima warudishe feedback kwa aliyewatuma.
Je unadhani zile para 2 zilizosainiwa mara ya kwanza zilifanywa kwa bahati mbaya?
Chama kinaendeshwa kwa vikao mkuu sio kwa matakwa ya Kimbunga ama Kim wa JF!
 
Baada ya kwenda ndio mtatuambia? Halafu mkuu hunaweza kutuambia Tundu Lissu, mbona anacheka sana kinachomchekesha ni nini?

Hata mimi kweli sikupata kumuona tundu akicheka kwa bashasha namna hii kabla,watu wa jikoni mlijua na hii kabla kwamba jamaa atakenua sana akifika ikulu?alipata kuwaeleza labda kwamba atatumia "strategy' ya kucheka sana?maana siku hizi kila kitu ni strategy.AU hivi vikao navyo vina posho?
 
watanzania tusikubali kuporwa na wanasiasa haki yetu ya kutengeneza katiba, kwa sasa wanasiasa na vyama vyao wako front...na lengo lao ni kulinda maslahi ya vyama vyao. Kwa nini jk asikutane na wawakilishi wa wananchi, wanaharakati, wasomi na wataalamu, wanakutana wenye we na hata tofauti zao wanaziweka pembeni katika hili wanasiasa kuwa front front linaniogopesha kidogo. Kwani wanasiasa ndo wametufikisha hapa tulipo.... Wananchi tuwe makini na hawa wanasiasa ushabiki, itikadi, na mapenzi kwa vyama vyetu visiwe na nafasi katika maamuzi wakati wa kuandika katiba.la sivyo yatakuwa yaleyale, mfano hapo kuna chama ambacho kiko tayari kufuta ruzuku?? Katika katiba mpya?? Wasiturubuni wote ni wanafki wanatofautiana tu viwango

strong point!

Ni kweli ni ilo ni kitu muhimu sana, lakini ni mapema sana kwa watu hao kuanza kuingilia hizi harakati ambazo kwa watu makini hizi ziko more political kuliko scientific and accademically.Watu hao ni makini kipindi timu timilifu ya ujenzi wa mchakato itakaposimamishwa kwa kuwa wanasiasa kazi ya ni kuinnitiate na wengine tunafuata.Tuwape muda hawa wacheze turufu yao wakitonyesha njia na kuanza kuleta madoido yao hatuchelewi kuwaambia hivyo sivyo tunavyotaka.
 
Maranya, nadhani huko CDM kuna shida kidogo. Kwa nini Slaa hakwenda Ikulu wakati ule? Kwa nini Mbowe alikutana na Rais siku mbili kabla ya viongozi wa CDM kwenda Ikulu mara ya pili muda huu wakiwa na Slaa? Slaa anawaamini wenzake? Je mara ya kwanza Slaa alisusa? Je Mbowe alienda kubembeleza ili Rais akubali kukutana nao Slaa akiwepo? Nina maswali mengi sana kichwani ila majawabu haba! Au Slaa hakukubaliana na yale makubaliano mawili?

hata kama hayo yalitokea lakini bado kitendo cha kukubali kukaa meza moja ndicho cha kishujaa/kijasiri. kwa sasa tuangalie tulipofika sio mapungufu ya huko nyuma
 
WanaJF,

Nawashukuru wote wanaofuatilia thread hii. Nawaomba kwa mara nyingine muwe na amani. Nawahakikishia hakuna wala hakutakuwa na usaliti. Chadema iko makini sana. Tunasukumwa na uzalendo na nia njema kwa Taifa letu.

Aidha kama alivyosema MMJ, tumekuwa tukisukuma mabadiliko makubwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kabla Rais hajateua Tume ya kukusanya maoni. Tulieleza wazi kuwa vinginevyo hatutashiriki mchakato wa kukusanya maoni.

Ni dhahiri busara ya kawaida inataka tupate progress ya majadiliano hayo hayo na utekelezaji wake. Katiba nzuri ndio afya na uhai wa Taifa hata kama si ufunguo wa matatizo yote yanayotusibu leo. Wakati mwafaka utakapofika tutatoa Taarifa kwa umma.

Msiwe na hofu mtuamini.
Dr. Slaa tunashukuru kwa majibu yako. Tunasubiri taarifa ila shaka yangu ipo hapo kwenye neno "wakati muafaka utakapofika tutatoa taarifa kwa umma". Sijui ni lini wakati muafaka utafika. Hilo tu. Nilikuwa nadhani ungesema kesho ama keshokutwa tutatoa taarifa kwa umma ili niishi kwa matumaini, lakini hili la wakati muafaka linaninyima raha kidogo.
 
Back
Top Bottom