Kikwete akiri tatizo la ajira kwa vijana kuwa 'bomu' linaloweza leta machafuko...

jamani atupishe naye walijifanya anamvuto,sasa hivi mnakula mvuto wake na uhandsome wake?inafikia kipindi natamani kama watz wote wajiunge na JF maana haya yote ni matokeo ya kofia,vilemba,kanga na tsh 10000
 
Kama anagundua Hilo Mbona mtu mmoja anapewa kazi tatu, mfano mkuu wa mkoa, mkurugenzi, mwenyekiti wa bodi na tena mbaya zaidi wengi wao ni wastafu.
Huwa anachosema hakimaanishi, achokimaanisha hakisemi wala hakitendi, na anacholkitenda ni kile asichokimaainisha
 
kila mtu hapa tanzania anajua kua vijana hawana ajira isipokua waziri wa kazi na ajira...serikali moja kauli mbili...kweli lowassa wampe urais...mambo anayosema ni ya kweli serikali inayakubali kichinichini
 
Waziri kabaka anapaswa kuuomba radhi umma maana kauli yake inapishana na ya bosi wake.
 
Yanayotokea kila kona ya nchi sio kingine bali ni lile bomu linalosemwa na mheshimiwa LOWASA kuwa ipo siku litalipuka.
Panapotokea vurugu vijana wengi hujipenyeza hapo ili kutuma ujumbe kwa serikali, mfano suala la kuchomwa kwa nyumba za viongozi wa serikali ni hasira za baadhi ya vijana kusikia na kuona familia za vigogo zikiendelea vizuri na kupata ajira bila hata kuhangaika tofauti na wao hivyo jibu pekee linalobaki ni kujiingiza pindi hiyo chansi ya vurugu inapojitokeza.
WITO:TUJISAHIHISHE KAMA TAIFA, BILA HIVYO HAKUNA TENA UMOJA WA KITAIFA
 
Yanayotokea kila kona ya nchi sio kingine bali ni lile bomu linalosemwa na mheshimiwa LOWASA kuwa ipo siku litalipuka.
Panapotokea vurugu vijana wengi hujipenyeza hapo ili kutuma ujumbe kwa serikali,mfano suala la kuchomwa kwa nyumba za viongozi wa serikali ni hasira za baadhi ya vijana kusikia na kuona familia za vigogo zikiendelea vizuri na kupata ajira bila hata kuhangaika tofauti na wao hivyo jibu pekee linalobaki ni kujiingiza pindi hiyo chansi ya vurugu inapojitokeza.
WITO:TUJISAHIHISHE KAMA TAIFA, BILA HIVYO HAKUNA TENA UMOJA WA KITAIFA

Mheshimiwa,

Hili sio bomu la Lowassa. Ni bomu la kila Mtanzania, aliyetazama elimu ikididimia kutoka Msingi mpaka Chuo Kikuu, akakaa kimya, akakubaki kudanganywa na watawala kwa propaganda za uongo na/au kuhongwa nyazifa mbamimbali na/au kwa kutishiwa kufutwa kazi, biashara kufungwa na kufilisiwa. Mtanzania yeyote aliyekubali kutumiwa kudanganya wengine kwa kutumia uwezo wake, wadhifa wake, chombo chake cha utangazaji au uandishi na kutetea uovu wa watawala amehusika moja kwa moja kulitengeneza hili bomu. Wao walijiaminishia kuwa kwa ukwasi wanaoupata kiharamu, wamewapeleke watoto wao nje ya nchi kusoma ama wamewapeleka kwenye "Academy" ili waweze kuwarithi kutawala. Hawakujua kuwa hiyo nchi ya kutawala haitakuwepo au haitatawalika kwa ujinga waliouasisi na kuupanda kwenye umma wa wa-Tanzania.

Tuna kizazi cha vijana ambacho hakina cha kupoteza kwa kufanya fujo bali wanacho cha kupata au kubahatisha kupata ikiwa fujo zao zitafanikiwa. Ndiyo sababu hawaogopi tena bunduki wala jela. Ile "Critical Mass" ya wajinga inayohitajika kuanzisha uasi imeshafikia au inafikiwa hivi karibuni.
  • Hawa ni wale wahitimu wa darasa la saba wasiochaguliwa kwenda sekondari ambao husahaulika kabisa kwenye sera cha kila chama cha siasa
  • Wahitimu wa kidato cha nne wasioendelea na kidato cha sita (halafu hawaajiriki kwa kuwa wana cheti lakini sio ujuzi wa kiwango hicho! - hata u-house-girl au house boy hawauwezi)
  • Wahitimu wa kidato cha sita wasioendelea na chuo Kikuu (Vyuo vya diploma na cheti vilishabadilishwa na kutoa shahada!)
  • Wahitimu wa Vyuo vikuu walio na shahada ya vyeti bila elimu ya Chuo kikuu - Wengi wako mijini hawana ajira kwani wanashindwa usaili wa nafasi wanazoomba.
Hawa wanahitaji mwerevu mmoja tu wa kuwalisha ujinga na kuanzisha uasi. Haya ndiyo tunayoyashuhudia sasa. Kwa taarifa yako ndugu yangu, hata wangechukua CDM 2010 mkakati wa kulitatua hili ni mgumu. Hata huyo atakayechukua nchi 2015 litamlipukia. Tukubali tusikubali, vijana wengi wasio na ajira kwa sasa hapa Tanzania hawaajiriki!

Ahsante
 
mh mween umesema ukweli tena inauma sana, kauli kuu iliyoniacha hoi ni hiyo quote from thomas paine " to argue with a person who has renounced reason is akin to administering dawa to the dead" bcoz it applies directly to CCM & mtandao wao wa kifisadi. cha zaidi hakibadiliki kitu mpaka washawishike kubadili tabia and i dont see a peaceful solution to this problem
 
Mheshimiwa,

Hawa wanahitaji mwerevu mmoja tu wa kuwalisha ujinga na kuanzisha uasi. Haya ndiyo tunayoyashuhudia sasa. Kwa taarifa yako ndugu yangu, hata wangechukua CDM 2010 mkakati wa kulitatua hili ni mgumu. Hata huyo atakayechukua nchi 2015 litamlipukia. Tukubali tusikubali, vijana wengi wasio na ajira kwa sasa hapa Tanzania hawaajiriki!

Ahsante

MWEEN, pamoja na kukupa 'LIKE' sikubaliani na wewe kwa jinsi ulivyohitimisha hoja yako. Hoja yako ni nzuri kabisa. Ni kweli, hili sio bomu la Lowassa. Lowassa ni opportunist tu - amekuwemo katika system ya utawala iliyoratibu utengenezaji wa bomu hili sasa kwa vile anataka urais anaruka kimanga na kudai kuwa ni bomu. Pia ni kweli kila mmoja wetu amechangia katika bomu hili kwa namna moja au nyingine.

Lakini ambalo sikubaliani nawe ni kwamba kuwafundisha hawa vijana kujua haki zao na kudai maisha bora ni 'kuwalisha ujinga' na pia kwamba basi huo ndio mwisho "hata huyo atakayechukua nchi 2015 litamlipukia". Hapa umekuwa pessimistic mno. Jamii kama jamii, taifa kama taifa, tukiamua tunaweza kubadilisha hii hali - uwezo tunao, sababu tunazo, ila nia ndio hatuna au kama nia ipo basi ubunifu ni zero.
 
Mheshimiwa,

Hili sio bomu la Lowassa. Ni bomu la kila Mtanzania, aliyetazama elimu ikididimia kutoka Msingi mpaka Chuo Kikuu, akakaa kimya, akakubaki kudanganywa na watawala kwa propaganda za uongo na/au kuhongwa nyazifa mbamimbali na/au kwa kutishiwa kufutwa kazi, biashara kufungwa na kufilisiwa. Mtanzania yeyote aliyekubali kutumiwa kudanganya wengine kwa kutumia uwezo wake, wadhifa wake, chombo chake cha utangazaji au uandishi na kutetea uovu wa watawala amehusika moja kwa moja kulitengeneza hili bomu. Wao walijiaminishia kuwa kwa ukwasi wanaoupata kiharamu, wamewapeleke watoto wao nje ya nchi kusoma ama wamewapeleka kwenye "Academy" ili waweze kuwarithi kutawala. Hawakujua kuwa hiyo nchi ya kutawala haitakuwepo au haitatawalika kwa ujinga waliouasisi na kuupanda kwenye umma wa wa-Tanzania.

Tuna kizazi cha vijana ambacho hakina cha kupoteza kwa kufanya fujo bali wanacho cha kupata au kubahatisha kupata ikiwa fujo zao zitafanikiwa. Ndiyo sababu hawaogopi tena bunduki wala jela. Ile "Critical Mass" ya wajinga inayohitajika kuanzisha uasi imeshafikia au inafikiwa hivi karibuni.
  • Hawa ni wale wahitimu wa darasa la saba wasiochaguliwa kwenda sekondari ambao husahaulika kabisa kwenye sera cha kila chama cha siasa
  • Wahitimu wa kidato cha nne wasioendelea na kidato cha sita (halafu hawaajiriki kwa kuwa wana cheti lakini sio ujuzi wa kiwango hicho! - hata u-house-girl au house boy hawauwezi)
  • Wahitimu wa kidato cha sita wasioendelea na chuo Kikuu (Vyuo vya diploma na cheti vilishabadilishwa na kutoa shahada!)
  • Wahitimu wa Vyuo vikuu walio na shahada ya vyeti bila elimu ya Chuo kikuu - Wengi wako mijini hawana ajira kwani wanashindwa usaili wa nafasi wanazoomba.
Hawa wanahitaji mwerevu mmoja tu wa kuwalisha ujinga na kuanzisha uasi. Haya ndiyo tunayoyashuhudia sasa. Kwa taarifa yako ndugu yangu, hata wangechukua CDM 2010 mkakati wa kulitatua hili ni mgumu. Hata huyo atakayechukua nchi 2015 litamlipukia. Tukubali tusikubali, vijana wengi wasio na ajira kwa sasa hapa Tanzania hawaajiriki!

Ahsante
Mwizi tu yule hawezi kuwa na moral authority ya kuzungumzia matatizo ya watanzania, sionaona mzee 6ta alivyomchana juzi gazeti la mwananchi?
 
Lowasa wa yule aliyejihudhulu kwa dude lake la richmond?hana maana hata kidogo huyo

Mangungo pole we Lile dude ni la Baba ridhiwani edo aliwajibika kisiasa tu ili serikali isiporomoke lakini laiti angalijua asingelijiuzulu mpaka atoke na mwenye nyumba:A S cry:
 
Ni vizuri pia ukarejea Hali ya uchumi wa Dunia unavyokwenda kwa ujumla- Mdororo wa Uchumi
 
kila mtu hapa tanzania anajua kua vijana hawana ajira isipokua waziri wa kazi na ajira...serikali moja kauli mbili...kweli lowassa wampe urais...mambo anayosema ni ya kweli serikali inayakubali kichinichini

Alipokuwa w/mkuu alishindwaje kutatua?
 
imekuwa sasa ni kama tabia na haki madereva wa bodaboda kukiuka sheria barabarani na wanapoadhibiwa hukimbilia kuvafanya vurugu na kuharibu mali za watu na serikali..ukiwaulizi wanakuambi ni people power,m4c..... na vijana hawa kwa nyakiti hizi ndio wanatumika na wanasiasa kufanya vurugu.... tumeona sehemu nyingi sana...
wito mh.jk viachie vyombo vya ulinzi vifanye kazi yake siasa iisiingilie utandaji wa vyombo hivi
 
Ni makala katika gazeti la mwananchi la leo ambapo mwandishi amechukua maoni ya vijana wengi graduates, ambapo baadhi yao wameitupia lawama serikali kwa kusababisha ukosefu wa ajira.

Lakini wapo baadhi wanaodhani kuwa ni uzembe wa graduates kutokujiajiri wenyewe. Ukitathimini maoni ya pande zote utagundua kuwa katika jamii yenye matabaka lazima kuwe na mitazamo inayokinzana huku wale wanaonufaika na mfumo uliopo wakiwalaumu wale wanaolalamikia ukosefu wa ajira.

Lakini uhalisia ni kwamba wapo baadhi ya graduates hawajawahi kukutana na ugumu wa kutafuta ajira kwa kuwa wana watu wao wanaowaandalia mazingira ya kuajiriwa.

Aidha kwa ushawishi au kwa kutumia rushwa, pia wana mitaji inayowawezesha kujiajiri, vijana wa kundi hili mara nyingi huwa wanawashambulia wenzao wanaolalamikia ukosefu wa ajira kwamba ni wazembe wasiotaka kujiajiri.

Hebu tufanye tafiti ili kubaini ni vijana wangapi wanaohitimu elimu ya juu wakiwa na mitaji ya kujiajiri na kama wengi wao wanahitimu bila kwanini tunawalaumu kwa kukosa ajira?
 
Back
Top Bottom