Kikwete akiri tatizo la ajira kwa vijana kuwa 'bomu' linaloweza leta machafuko...

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
  • Asema lisipotatuliwa litaleta machafuko barani Afrika

RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni tatizo kubwa na kwamba lisipotafutiwa ufumbuzi wa kudumu linaweza kusababisha vurugu, machafuko na uasi wa umma, hata kwa nchi zinaoongozwa kwa misingi ya kidemokrasia, kama inavyotokea sasa katika nchi za Kiarabu.

Onyo hilo la Rais Kikwete linafanana na lile ambalo limekuwa likitolewa mara kwa mara na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, lakini, linapingana na kauli ya Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka ambaye Machi 21 mwaka huu, alimjibu Lowassa akisema, "Kitendo cha wanasiasa kuendelea kusema tatizo la ajira kwa vijana ni bomu linalosubiri kulipuka, siyo kweli."

Jana akifungua mkutano wa mwaka wa Magavana wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Jijini Arusha, Rais Kikwete alisema moja ya sababu kuu ya machafuko yanayoshuhudiwa sasa kwenye ukanda wa nchi za Kiarabu, ni matokeo ya ukosefu wa ajira kwa vijana na watu kukata tamaa.

"Siyo kweli kwamba machafuko yanayoshuhudiwa kwenye nchi za Kiarabu ni matokeo ya Serikali za nchi hizo kukaa madarakani kwa kipindi kirefu kama wengi wanavyodhani.

Ukweli ni kwamba hayo ni matokeo ya ukosefu wa ajira na watu kukata tamaa ya maisha," alisema Rais Kikwete.

Alisema bila kutafutia ufumbuzi wa haraka, tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana ambao wengi hukimbilia mijini kusaka hali bora ya maisha, hata nchi zenye kuongozwa kidemokrasia, zinaweza kukumbwa na machafuko na uasi wa umma.

Rais alitumia fursa hiyo kuishukuru Denmark kwa kutoa fedha za kusaidia Mfuko wa Ajira kwa Vijana barani Afika, akisema ni moja ya mapendekezo kadhaa yaliyotolewa na kamati maalum ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kiuchumi barani Afrika ambayo yeye na Rais wa AfDB, Dk Donald Kaberuka, walikuwa wajumbe.

Mapema Rais wa Ivory Coast, Allasane Ouattara aliyehudhuria mkutano huo aliunga mkono kauli hiyo ya Rais Kikwete kwa kusisitiza kuwa vijana lazima wawekewe mazingira mazuri na kuwezeshwa kukabiliana na kumudu changamoto za kiuchumi, kitamaduni na kiteknolojia wanazokabiliana nazo.

Source: Mwananchi
 
Tatizo kubwa, viongozi wetu wengi wanaamini siasa ni uongo!

Kabaka - Ajira siyo tatizo, JK- Ajira ni tatizo (Rais na Waziri wa serikali moja).

Ukweli ni kwamba ajira ni tatizo kubwa kwa sasa na jitihada za kutatua zinahitajika haraka, siyo tu kutambua kwamba ajira ni tatizo. Mimi nafikiri focus kubwa iwe kwenye utafutaji wa solutions za tatizo hili na siyo kujadili kama ajira ni tatizo au la maana ni kitu kilicho wazi.

Ningefurahi sana ningeona solutions alizopendekeza JK!!!
 
Hawakukutana barabarani hawa kumbuka na ajali ya kisiasa haiwezi kuwatenga ila ni upepo tu utapita.
 
tatizo la ajira kwa vijana JK ANALIJUA hata kabla hajawa rais. ndiyo maana ilani yake ya kwanza kulikuwa na ahadi ya ajira milioni moja.

KWELI, Yeye mwenyewe si alikosa ajira akaenda kugawa kadi za TANU baada ya kumaliza uchumi UDSM
 
Ni kutokana na vijana wengi kukosa ajira na kukabiliwa na maisha magumu bila kuwa na mipango mikakati ya kuwanusuru na ombwe la ajira.Swali Je WAZIRI WA AJIRA NA KAZI GAUDENCIA KABAKA BADO ANAPINGANA NA KAULI YA BOSS WAKE JK KAMA ALIVYOMPINGA LOWASSA?.

Na anatuambia nini sisi kama watanzania kwa Uongo wake?.

Source: magazeti ya leo
 
Viongozi wetu wana akili za kuku, unamkuta anadonoa/anakula mahindi unanampopoa na jiwe anakimbia mbaliii, cha ajabu anasimama na anajiuliza hivi lile jiwe nimwpigwa leo au jana au aikupigwa mimi, anarudi pale pale.

Ndo viongozi wetu
 
Alipata direct employment BOT akaitosa kwa ajili ya kukipenda chama

Wakati huo chama 'kilikuwa kinashika hatamu'. Hivyo si swala tu la 'mapenzi' bali wapi 'panalipa' zaidi. Hapa si malipo ya mshahara tu bali heshima, mamlaka, kukua kiajira na other future prospects-kwa wakati huo
 
Yule mama aliepiga mayowe wakati mamvi anatoa iyo kauli ajitokeze tena basi manake mkuu wake wa kazi kaitoa live ajira ni tatizo. Magamba at work!!wanajikaanga kwa mafuta yao wenyewe
 
Tatizo kubwa, viongozi wetu wengi wanaamini siasa ni uongo!!
Kabaka - Ajira siyo tatizo, JK- Ajira ni tatizo (Rais na Waziri wa serikali moja).
Ukweli ni kwamba ajira ni tatizo kubwa kwa sasa na jitihada za kutatua zinahitajika haraka, siyo tu kutambua kwamba ajira ni tatizo. Mimi nafikiri focus kubwa iwe kwenye utafutaji wa solutions za tatizo hili na siyo kujadili kama ajira ni tatizo au la maana ni kitu kilicho wazi. Ningefurahi sana ningeona solutions alizopendekeza JK!!!

Ajira sio tatizo lililopelekea machafuko nchi za Kiarabu. (Kabaka).

Mbona ulikuwa hujamalizia "context"?
 
Tatizo kubwa, viongozi wetu wengi wanaamini siasa ni uongo!!
Kabaka - Ajira siyo tatizo, JK- Ajira ni tatizo (Rais na Waziri wa serikali moja).
Ukweli ni kwamba ajira ni tatizo kubwa kwa sasa na jitihada za kutatua zinahitajika haraka, siyo tu kutambua kwamba ajira ni tatizo. Mimi nafikiri focus kubwa iwe kwenye utafutaji wa solutions za tatizo hili na siyo kujadili kama ajira ni tatizo au la maana ni kitu kilicho wazi. Ningefurahi sana ningeona solutions alizopendekeza JK!!!

nahis kabaka alijibu vile kuisafisha wizara yake ambayo inahusika na ajira,,,,,,political game,ila anajua kuwa ni tatizo,na kwakua alisema Lowasa alipaswa ajibu,,,,,maana hakua na sababu ya kunyamaza,hata kama kweli au si kweli,ila hata kama haupo serikalini utajua tu kuwa ajira ni tatizo kwa vijana,aidha kwa ukweli au kwa uongo
 
Yule mama aliepiga mayowe wakati mamvi anatoa iyo kauli ajitokeze tena basi manake mkuu wake wa kazi kaitoa live ajira ni tatizo. Magamba at work!!wanajikaanga kwa mafuta yao wenyewe

hivi bado yupo kwenye wizara hiyo hiyo??????
 
Hoja ya ukosefu wa ajira kwa vijana iko enzi na enzi, IWEJE IMILIKISHWE KWA LOWASA?
 
Jk asijifanananishe na nchi za kiarabu,anataka kuiaminisha Africa kuwa siku anapigwa chini tatizo ni ajira.

Kwa TZ kitakachompiga chini ufisadi,matumizi mabaya ya madaraka na unyanyasaji wa wanyonge. Hivi hapa tulipo hata kama hakuna ajira lakini tukawa tunasota wote kuanzia mkubwa mpaka mdogo kungekuwa na shida?

Leo hii wako watu wana ajira lakini hawaitaki serikali iliyoko madarakani. Iweje mtu usote miaka kazini unashindwa hata kununua bajaji halafu anatokea mtoto wa kigogo hajaanza hata kazi anamiliki malori zaid ya mia.
 
Ukiona mtawala analalamika tu bila ufumbuzi yakinifu huyo ujue hafai, unapokuwa na madaraka ya nchi cha kwanza suala la maendeleo. Namna ya kupata maendeleo ni jinsi gani utakavyotumia nguvu za vijana ktk kufanikisha hilo, kwa kuandaa misingi bora ya elimu, afya na ajira.

Ukiweza kuwawezesha vijana vyema maendeleo yatapatikana tu, zaidi ya hilo utajenga taifa la ombaomba na kulifanya kutoheshimika ktk jumuia za kimataifa.
 
Kwenye gazeti la leo, habari kuu iliopo ukurasa wa kwanza inasema: "JK akubali hoja ya Lowassa."

Ukiisoma habari yenyewe inasema kuwa Rais Kikwete amesema kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni tatizo kubwa kwa nchi za bara la Afrika.

Gazeti hili eti linataka umma wa Tanzania uamini kuwa kwa kusema hivyo, JK amekubaliana na "hoja ya Lowassa" aliyoitoa Novemba 2011 kanisani kuwa ukosefu wa ajira za vijana ni time bomb hapa nchini.

Jaribio kubwa hapa ni kuwafanya Watanzania waamini kuwa eti Lowassa ndiyo muasisi wa "hoja" hiyo kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni bomu na kuwa hakuna mwanasiasa mwingine yoyote kabla ya Lowassa aliyeweza kuona tatizo hilo. Kwa wale waliosoma taaluma ya mawasiliano ya umma, kuna mbinu moja inaitwa "agenda setting", ambapo vyombo vya habari vinatumiwa kujenga ajenda. Hii inatumiwa kwa kutoa habari za mwanasiasa wanayetaka kumjenga mara kwa mara na kuzipa habari hizi umuhimu mkubwa ili wananchi nao waaminishwe kuwa mwanasiasa huyo ni mtu muhimu nchini.

Lowassa akiwa waziri mkuu, au waziri kabla ya hapo, hakuna jambo lolote la maana alilowahi kulifanya kusaidia vijana wapate ajira. Iwaje leo akiwa nje ya serikali anajidai anawajali sana vijana? Na ile kashfa ya Richmond/Dowans aliyoisababisha yeye imepoteza ajira ngapi za vijana kwa kuchangia uhaba wa umeme nchini? Na pesa zaidi ya bilioni 200 walizolipwa Richmond/Dowans kwa njia za wizi zingetengeza ajira ngapi za vijana nchini? Kwa wasiojua, wanasiasa mbalimbali nchini, ndani na nje ya CCM, wamekuwa wakizungumzia tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana tangu enzi za serikali za Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Lowassa si muasisi wa hoja hii, bali anaidandia kujaribu kupata kuungwa mkono na vijana wa Tanzania, ikiwemo UVCCM ya chama tawala iliyopoteza mwelekeo.

Tido Mhando, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mwananchi Communications Ltd (MCL), amepewa jukumu la kujaribu kumjenga waziri mkuu wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ya Richmond, Edward Lowassa, kupitia gazeti hilo pendwa la kila siku nchini.

Kwa wasiojua, Tido Mhando aliajiriwa na Lowassa alipokuwa waziri mkuu kama mkurugenzi mkuu wa TBC1 na ni mmoja wa wahariri na waandishi wa habari nchini ambao ni wafuasi wa Lowassa.

Kwa wanaopenda "source," tetesi hizi nimezipata kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa MCL.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom