Kijana mwenye ndoto ya kujisomesha usiwe na haraka sana. Hiyo ada uliyojichanga izungushe kwenye biashara kwanza

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,305
Mwaka 2015 nilipata Admission ya kwenda kusoma Masters kwenye ujasiriamali pale UDSM. Nilishapokea maelekezo yote ikabakia kulipa tu ada. Nilivyojicheki nikaona hadi wakati ule nilikuwa nina pesa ya kulipa ada na gharama zingine kwa mwaka mmoja tu. Hata kama Masters sio muda mrefu bado pesa ingepelea. Baada ya tafakuri nzito nikaamua niahirishe chuo na kuwekeza pesa yote kwenye biashara. Huo ulikuwa mojawapo ya maamuzi bora kabisa niliyowahi kufanya kwenye maisha yangu.

Ninaandika huu uzi baada ya kuona vijana wengi wakikosa utulivu kwenye haya mambo ya kujisomesha. Kijana uliyemaliza form six au form four na ukawa huna msaada wowote wa kupata pesa za kwenda chuo ni bora kupambana kwanza kutengeneza hela kupitia shughuli yoyote ya halali iliyoko mbele yako badala ya kujipanikisha kutafuta ada ambayo pia hata ukiipata unaweza kujikuta unasoma kwa taabu sana. Wengine wamefikia hatua ya kuomba omba watu pesa. Ninashauri kiasi chochote utakachokipata kwenye mihangaiko yako usikimbilie kulipa ada. Chukua hicho kiasi kizungushe. Mambo yakiwa sawa utasoma baadae.

Kuna watu wanaoweza sema kwamba biashara sio ya kila mtu. Hii sio kweli. Biashara haina mwenyewe. Ni kama vile tunavyoenda shule ambako hata kama wewe ni kipanga lazima kuna wakati unafeli hata zile monthly tests. Sio kwamba utafaulu tu kirahisi. Kwenye biashara nako ni hivyohivyo. Juhudi na kujituma ndo muhimu. Sisi wote kwenye biashara ni kama wanafunzi yaani kila siku tunajifunza na kupitia mambo mengi.

Itakuwa haina maana kijana umepambana ukapata milioni 5 kisha ukaipeleka yote shule ambapo baada ya miaka mitatu unarudi mtaani kuanza upya. Hiyo 5m ungeizungusha ungekuwa mbali kwa miaka 3.

NB: Mimi naheshimu mno elimu ila pia nauchukia sana umaskini. Kwa dunia ya leo unaweza kusoma kimaskini na bado ukarudi kitaa na kuendelea kuwa maskini. Umakini unahitajika
 
Madini haya mkuu, kuna dgo ana 2M ananiulza afanye nn ndio kamalza chuo SAUT yan mm mwenyew sjui hata nmwambie nn 2M naona kdg mno kwakwel.
2m sio kidogo ukituliza akili. Miaka mitatu iliyopita niliishiwa kabisa yaani tuseme nilifilisika. Nikiwa karibia nakata tamaa kuna mtu nilikuwa namdai akanilipa Tsh 1.8m ambayo niliagizia viatu vya bei rahisi China yaani vile vya Tsh 3000 vikiwa China. Nakumbuka huo mzigo ulivyofika nilienda nao hadi mnadani.... ingawa kulikuwa na ups and downs lakini leo hii hali sio mbaya. Ni nidhamu tu ya pesa inatakiwa.
 
Back
Top Bottom