Kijana unayejitambua kama una 1.5M fanya hii kitu utakuja kunishukuru

Papaa Gx

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
10,092
15,673
Habari zenu wakuu,

Leo nataka niandike maneno kadhaa kwa vijana wenzangu tunaojitambua. Naandika kuhusu vijana wanao jitambua namanisha wale walio na uchu wa mafanikio na wenye ndoto ama malengo makubwa hapo mbeleni panapo majaaliwa.

Hili bandiko ni chugu kwa vijana wa hovyo na wasio jielewa, maana ni hakika watapinga na kuona ni ngumu. Hapa nasema na wanaume haswa wanaojitambua na kupevuka kiakili, sio wale mabishoo uchwara.

Twende kwenye pointi sasa, kijana unae jitambua hii Tanzania yetu ni kubwa sana ni wewe tu kuamua uende wapi. Nita andika kuhusu sekta ya kilimo ambapo bado kuna fursa ila asilimia kubwa ya vijana wameona ni ujinga kuingia huko kumbe sio. Kuna wale vijana huwa wanakuja hapa na mitaji kuanzia 1.5M mpaka 5M na kuuliza wafanye biashara gani, kijana unae jitambua nakushauri ingia kwenye kilimo kwa kumanisha kweli kweli. Vijana mlio kuwa chuo na mpo mtaani tu hamuelewi mfanye nini ingia kwenye kilimo na uache malalamiko ya kukosa ajira, huna connection unataka ajira utasugua sana kwa Tanzania hii. Ni bora huo muda ujikite kwenye kilimo.

Kijana tafuta mikoa yenye uhakika wa mvua nashauri kwa mikoa hii ifuatayo, Katavi, Rukwa, Morogoro na Songea kama kuna mwingine wadau wataongezea. Katika hiyo mikoa tafuta wilaya yenye mashamba ya uhakika kisha jikite kwenye kilimo cha mahindi pekee. Kwanini mahindi, kwasababu kilimo cha mahindi hakina mambo mengi na ni rahisi kwa mtu anayeanza pia ndio zao linalolimwa kwa asilimia kubwa nchini kwetu.

Kijana hamia porini kabisa weka kambi yako huko jipe miezi tano tu, hiyo miezi sio mingi kwa mpambanaji na anae jitambua. Kodi heka tatu kisha piga kilimo cha mahindi, hiyo 1.5M inatosha kila kitu kuhudumia shamba. Yaani hapo kuanzia kukodi, kulima, kupanda, kupalilia, madawa, mbolea mpaka unavuna mazao yako. Hiyo hela ni nyingi sana kwenye kilimo cha mahindi, hiyo hela wewe unakuwepo shamba kuhakikisha kila hatua inakwenda sawia.

Kijana jiandae na msimu ujao wa kilimo cha mahindi kisha fanya hiyo project baada ya miezi mitano utakuja kunishukuru nakwambia. Vijana tumeng'ang'ania tu mjini kwa mambo yasio na msingi wowote ule kwenye maisha yetu na wakati huo muda ukituacha matokeo yake ni kulalama kila uchwao.

Kijana jikite porini huko piga kilimo chako kwa umakini na kwa kumanisha, ingia porini huko kaa miaka mitatu mpaka mitano kisha utaona matunda yake. Kijana ni ukumbuke kuwa maisha hayapo kukusubili na anaekupenda zaidi ni wewe mwenyewe, na huo ndio ukweli mchungu. Wavaa vipensi lazima wapinge!

Mkono wa Papaa Gx
 
Habari zenu wakuu,

Leo nataka niandike maneno kadhaa kwa vijana wenzangu tunaojitambua. Naandika kuhusu vijana wanao jitambua namanisha wale walio na uchu wa mafanikio na wenye ndoto ama malengo makubwa hapo mbeleni panapo majaaliwa.

Hili bandiko ni chugu kwa vijana wa hovyo na wasio jielewa, maana ni hakika watapinga na kuona ni ngumu. Hapa nasema na wanaume haswa wanaojitambua na kupevuka kiakili, sio wale mabishoo uchwara.

Twende kwenye pointi sasa, kijana unae jitambua hii Tanzania yetu ni kubwa sana ni wewe tu kuamua uende wapi. Nita andika kuhusu sekta ya kilimo ambapo bado kuna fursa ila asilimia kubwa ya vijana wameona ni ujinga kuingia huko kumbe sio. Kuna wale vijana huwa wanakuja hapa na mitaji kuanzia 1.5M mpaka 5M na kuuliza wafanye biashara gani, kijana unae jitambua nakushauri ingia kwenye kilimo kwa kumanisha kweli kweli. Vijana mlio kuwa chuo na mpo mtaani tu hamuelewi mfanye nini ingia kwenye kilimo na uache malalamiko ya kukosa ajira, huna connection unataka ajira utasugua sana kwa Tanzania hii. Ni bora huo muda ujikite kwenye kilimo.

Kijana tafuta mikoa yenye uhakika wa mvua nashauri kwa mikoa hii ifuatayo, Katavi, Rukwa, Morogoro na Songea kama kuna mwingine wadau wataongezea. Katika hiyo mikoa tafuta wilaya yenye mashamba ya uhakika kisha jikite kwenye kilimo cha mahindi pekee. Kwa nini mahindi, kwasababu kilimo cha mahindi hakina mambo mengi na ni rahisi kwa mtu anae anza pia ndio zao linalo limwa kwa asilimia kubwa nchini kwetu.

Tuna ndugu wakulima lakini ni masikini na wao ndio wanatuomba misaada sisi tusiokua wakulima. Hivi ni kweli kilimo kinalipa au propaganda tu.
 
Good idea but for to be realistic 1.5M kwenda kujichimbia mkoa ambao si mwenyeji kwa miezi mitano ni ndogo sana. Hapo hizo heka tatu kijana ambaye kazaliwa mjini sidhani kama ataweza kuzilima mwenyewe, miezi hiyo mitano atakuwa anakula nn?

So kumsaidia kijana huyu ni bora kupiga hesabu nzima pamoja na estimate ya gharama za kujikimu, vibarua..
 
Habari zenu wakuu,

Leo nataka niandike maneno kadhaa kwa vijana wenzangu tunaojitambua. Naandika kuhusu vijana wanao jitambua namanisha wale walio na uchu wa mafanikio na wenye ndoto ama malengo makubwa hapo mbeleni panapo majaaliwa.

Hili bandiko ni chugu kwa vijana wa hovyo na wasio jielewa, maana ni hakika watapinga na kuona ni ngumu. Hapa nasema na wanaume haswa wanaojitambua na kupevuka kiakili, sio wale mabishoo uchwara.

Twende kwenye pointi sasa, kijana unae jitambua hii Tanzania yetu ni kubwa sana ni wewe tu kuamua uende wapi. Nita andika kuhusu sekta ya kilimo ambapo bado kuna fursa ila asilimia kubwa ya vijana wameona ni ujinga kuingia huko kumbe sio. Kuna wale vijana huwa wanakuja hapa na mitaji kuanzia 1.5M mpaka 5M na kuuliza wafanye biashara gani, kijana unae jitambua nakushauri ingia kwenye kilimo kwa kumanisha kweli kweli. Vijana mlio kuwa chuo na mpo mtaani tu hamuelewi mfanye nini ingia kwenye kilimo na uache malalamiko ya kukosa ajira, huna connection unataka ajira utasugua sana kwa Tanzania hii. Ni bora huo muda ujikite kwenye kilimo.

Kijana tafuta mikoa yenye uhakika wa mvua nashauri kwa mikoa hii ifuatayo, Katavi, Rukwa, Morogoro na Songea kama kuna mwingine wadau wataongezea. Katika hiyo mikoa tafuta wilaya yenye mashamba ya uhakika kisha jikite kwenye kilimo cha mahindi pekee. Kwa nini mahindi, kwasababu kilimo cha mahindi hakina mambo mengi na ni rahisi kwa mtu anae anza pia ndio zao linalo limwa kwa asilimia kubwa nchini kwetu.

Kijana hamia porini kabisa weka kambi yako huko jipe miezi tano tu, hiyo miezi sio mingi kwa mpambanaji na anae jitambua. Kodi heka tatu kisha piga kilimo cha mahindi, hiyo 1.5M inatosha kila kitu kuhudumia shamba. Yaani hapo kuanzia kukodi, kulima, kupanda, kupalilia, madawa, mbolea mpaka unavuna mazao yako. Hiyo hela ni nyingi sana kwenye kilimo cha mahindi, hiyo hela wewe unakuwepo shamba kuhakikisha kila hatua inakwenda sawia.

Kijana jiandae na msimu ujao wa kilimo cha mahindi kisha fanya hiyo project baada ya miezi mitano utakuja kunishukuru nakwambia. Vijana tumeng'ang'ania tu mjini kwa mambo yasio na msingi wowote ule kwenye maisha yetu na wakati huo muda ukituacha matokeo yake ni kulalama kila uchwao.

Kijana jikite porini huko piga kilimo chako kwa umakini na kwa kumanisha, ingia porini huko kaa miaka mitatu mpaka mitano kisha utaona matunda yake. Kijana ni ukumbuke kuwa maisha hayapo kukusubili na anaekupenda zaidi ni wewe mwenyewe, na huo ndio ukweli mchungu. Wavaa vipensi lazima wapinge!

Mkono wa Papaa Gx
Andiko zuri, limekosa kusema ukweli wa changamoto dhahiri na za kiuhalisia shambani!

• Gharama halisi za usimamizi
• Upatikanaji wa nguvu kazi (iwapo msimu wa nyuma hali ya chakula iikuwa nzuri na mvua nyingi kupita kiasi)

• Sema hali halisi ya bei ya mazao baada ya kuvunwa, usafirishaji wake mpaka sokoni, ushuru, uhifadhi na uncetainities nyingine kama kuharibika, Kuibiwa kuzurumiwa, kuvamiwa etc)

• Eleza hali halisi iwapo kiwango ulichonacho kwa kazi hiyo kikawa kidogo kuliko ihalisia

N.k
 
Nimetembea maeneo mengi ni sehemu chache sana nimeona mahindi ambayo yamestawi vizuri. Watu wengi wanalima mahindi na hawapati chochote... Hiyo investment ni ndogo sana....

Maybe ungetoa mchanganuo wote wa gharama zote... Na kuzingatia huyu kijana atakuwa hafanyi kazi yoyote kwa hiyo miezi mitano isipokuwa kilimo cha mahindi...
 
Kuliko kukaa hapo sinza akilamba lips bora akaenda na hiyo 1.5m porini kuna kitu atajifunza tu na akirudi mara ya pili na ya tatu anaweza fanikiwa.
 
Mkuu upo sahihi..
Mi nimelima
2.5 ekras nimetumia 950,000/=

Niko nyanda za juu kusini
Changamoto
👉 Ufahamu wa kilimo
Vijana tumeshinda shule; means toka mdogo kujihusisha na kilimo ilikua as part time so unakosa yale maarifa sahihi ya kilimo.
👉 Mitaji: Inafika muda mahindi yanataka mbolea huna hela, yanataka palizi huna hela, so maandilizi mazuri ni muhimu ingawa kuanza kwa chochote ulichonacho ni muhimu zaidi

mwisho sijui tukivuna itakuaje kwenye ishu ya bei, maana huku mahindi yamekubali saana.

Mwisho kabisa uthubutu ni muhimu kuliko kuangalia changamoto
 
Back
Top Bottom