Kigwangalla: Serikali haiwezi kukuletea mabadiliko kwenye maisha yako, kuilaumu ni kupoteza muda tu

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
"Kosa kubwa la kwanza utakalolifanya kwenye maisha yako ni kutegemea eti Serikali itakuletea mabadiliko kwenye maisha yako, na kupoteza muda wako ukiilaumu serikali kila kukicha, na la pili ni kudhani eti waliofanikiwa ni kwa sababu ya hisani ama fursa ya kuwa kwenye serikali, wakati naanza maisha niliacha kazi ya serikali (udaktari) na kuingia mtaani, shambani, kiwandani mpaka nikaiona njia yangu" - Hamis Kigwangalla
 
wasikusanye kodi
 
Kwa hiyo kama unalima sana na barabara za kutoa mazao hakuna, una kiwanda kidogo cha kutengeneza samani za chuma na umeme wa uhakika hakuna usilalamike?. Kuna haja ya kuhoji degree zake kapataje
Kigwangala ni Daktari wa nini?
 
Kwa hiyo kama unalima sana na barabara za kutoa mazao hakuna, una kiwanda kidogo cha kutengeneza samani za chuma na umeme wa uhakika hakuna usilalamike?. Kuna haja ya kuhoji degree zake kapataje
Anajaribu kubuni theory yake,Toka kale tawala nzuri ziwe za kifalme,kiditakta,kidemokrasia Toka enzi na enzi ndizo zinafacilitate maendeleo kwa Raia wake,angalia Asia ya mbali,mashariki ya kati, na kwingineko alimradi iwe ya watu,inayofikiri vyema,inayopenda maendeleo ya watu,isiyo fisadi,isiyo na upendelelo,yenye kulinda rasilimali za asili na viongozi wa kiasi.
 
Sijui kama anajua alipata courage ya kuacha kazi baada ya kupata mtaji kutokana na kazi aliyoiacha? Sijui kama anajua Kuna watu wanatamani kupata walau kibarua ili apate mtaji wa kujiajiri na Bado mazingira ni magumu! Kwa ufupi aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa!
 
Alichozungumza ni sahihi Ila ameharibu kuzungumza Kwa lugha ya majigambo tabaka la chini ambalo limempa ubunge na ambalo ndo linalalamika amelikosea .
 
Ameandika hili katika jarida lake lake la KIgwanomics ?
Cc @kigwangallah
 
Mtu yeyote ambaye hajui kuwa maendeleo aliyonayo yanatokana na mipango ya serikali basi huyo ni mfu, ndio maana nchi zilizoendelea wao udeal na rais tu, lkn sisi huku eti mtu anaangaika na mbunge, mara diwani mara mwenyekiti wa kijiji, ujinga mtupu.
 
"Kosa kubwa la kwanza utakalolifanya kwenye maisha yako ni kutegemea eti Serikali itakuletea mabadiliko kwenye maisha yako, na kupoteza muda wako ukiilaumu serikali kila kukicha, na la pili ni kudhani eti waliofanikiwa ni kwa sababu ya hisani ama fursa ya kuwa kwenye serikali, wakati naanza maisha niliacha kazi ya serikali (udaktari) na kuingia mtaani, shambani, kiwandani mpaka nikaiona njia yangu" - Hamis Kigwangalla
Kwa hio anatuambiaje yaan turudishe kadi za Chama au?
 
Mtu yeyote ambaye hajui kuwa maendeleo aliyonayo yanatokana na mipango ya serikali basi huyo ni mfu, ndio maana nchi zilizoendelea wao udeal na rais tu, lkn sisi huku eti mtu anaangaika na mbunge, mara diwani mara mwenyekiti wa kijiji, ujinga mtupu.
Mbunge na Diwani ndio wanaotokea huku huku Shimoni Street sana sana Diwani
 
Huyo Dr akili hamna kabisa , au ni namna ya kujitetea Ili apate nafasi yabkuchaguliwa tena.
 
Back
Top Bottom