Anayosema Kigwangalla kuhusu uaminifu wa Watanzania kuna tatizo?

Motowntzjpm

Senior Member
Jun 16, 2023
118
191
Leo asb Hamisi Kigwangalla ameliamsha tena huko Instagram suala la uaminifu wa watanzania. Amehadithia alichofanyiwa na kijana aliyemuamini. Huko nyuma amewahi kuuliza WHAT IS TANZANIA'S COMPETITIVE ADVANTAGE -Akimaanisha nini ambacho tunaweza kusema hichi kinatutambulisha kitaifa.

Juzi kati I-SOKO mfumo wa kuwezesha wanawake kufanya biashara afrika mashariki imeanzishwa. Kilichojiri malalamishi kwamba watanzania hatuaminiki.

Kihehe tunasema sema we have a people problem. Tatizo ni kubwa lakini tunaogopa kulijadili kwakuwa ni kaa la moto. Au halipo

SOMA KISA HIKI KUTOKA KWA hamis Kigwangalla

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 1:

Kama ukiona elimu ni gharama, ujue haujajaribu ujinga. Vile vile, kama ukiona kutafuta utajiri ni kazi, hebu jaribu umaskini uone.

Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama umaskini. Tuliouishi umaskini tunaujua. Tukipambana nao kwa kila hali msitushangae. Mara kadhaa tushawahi kurudi nyumbani for lunch na kukuta hakuna kilichopikwa tukaishia kunywa maji na kugeuza shule, maana hata wa kumuuliza chakula kiko wapi hayupo home.

Kutajirika ni katika vitu vigumu kabisa kufanya hapa duniani. Niliwahi kujaribu kutafuta utajiri sikuufikia, nikaishia hapa nilipo! Lakini bado napambana. Si haba, WALLAH sina malalamiko yoyote yale kwa Allah, zaidi zaidi narejesha shukrani tele. Nilipotoka napajua mwenyewe.

Kwenye safari ya kutafuta maisha, kwa kuwa nilikuwa na mbio ndefu na za spidi sana, nimejifunza mengi sana. Huwa najaribu kuandika andika hapa, wenye muda husoma na pengine hujifunza.

Niliwahi kuwa nalima ekari 500 - 600 kwa msimu, nikamuamini kijana wangu mmoja mahiri, mchapakazi, mwenye dini kweli kweli, mwenye elimu na passion ya farming; pamoja na kunifaidisha na kunipa tamaa ya kuwekeza zaidi, alinipiga kweli kweli!

Nikaamini wadogo zangu damu kabisa, wakanipiga. Nikazama. 😩!

Mtaji wa zaidi ya ekari 700 ukaporomoka mpaka ekari 100/200. Wakati unaporomoka, unadaiwa na benki ulipe mkopo wa mtaji uliochukua, unadaiwa na kampuni waliokukopesha matrekta, combine harvesters, planters, unadaiwa na suppliers wa pembejeo etc. Inaendelea…

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE. Part 2!

Wakati huo huo umeshushwa cheo na unaambiwa ukajibu hoja kwa CAG za dhambi ambazo hazikuhusu. Faida moja ya cheo ni kuwa kuna mikopo bankers wanakupa kwa kukuamini tu, tena kwa simu tu. Siku kikiondoka, wadai wote wanaanza kuhaha kukudai kama hawakujui vile. Wakubwa wote hawapokei simu zako. Unabaki peke yako kama siyo wewe vile. Marafiki waliokuwa wanakusalimia kila kukicha hawapokei simu zako wala hawajibu meseji zako.

Ukiwa na roho ndogo utasema umerogwa ama utaugua ugonjwa wa akili. Ama hata utaona maisha hayana maana tena.

Wakati unajaribu kutoka, bei za mazao zinaporomoka! Vita ya Ukraine inaanza na COVID inapandisha bei za mbolea etc.

Mwaka huu bei za mazao nzuri, wanatokea kwelea kwelea 😀.

Ili kusimama kwenye maisha, muombe sana Mungu akupunguzie masomo magumu ya kupitia, aidha usihangaike sana kuimarisha misuli ya mwili ili ukivaa suti upendeze, imarisha misuli ya moyo, ubongo na roho(kama nayo ina muscles!😀) ili uweze kukabiliana na nyakati za maanguko. Siku zote jua tu kwamba, baada ya maanguko kadhaa, na kama utaweza kuinuka kila unapoanguka, na kustahimili maumivu ya kila anguko, mwangaza huja na Mungu humuinua mja wake! (Graduation hiyo sasa!)

Maisha ni Marathon. Kutajirika siyo rahisi. Lakini kwani nani alisema umaskini ni raha?

Iendelee ama iishie hapa?

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 3.

Ukitenda wema, tenda kwa watu wengi sana, muhimu ni kuwa usingoje shukran. Kwa hakika wema, ni akiba isiyooza.

Pamoja na uwepo wa watu wengi wa hovyo kwenye maisha yetu, watu ambao hawawezi kukufanyia jambo jema, zaidi zaidi wanajipanga kukuangusha na kukudhuru kila kukicha, tena hawana sababu yoyote ile, huwa wapo watu wachache wema, pengine uliwahi kuwatendea wema basi wanakumbuka ama ni watu wenye tabia ya kupenda kutenda wema tu. Wapo!

Wabaya wengi wapo lakini wema wachache pia wapo. Jitahidi uwe miongoni mwa wema.

Kwenye maisha yako jitahidi kuwatendea watu wema, bila sababu, hujui nyuma ya tabasamu la mtu aliyekuja mbele yako kuna nini anapitia!

Kuna mtu mmoja alipataga kesi ya uhujumu uchumi, sikuwahi kuwa namjua, wala hakuwa rafiki yangu, na wala namba yake ya siku sikuwa nayo.

Nikaona mambo kwenye mitandao, nikafuatilia nikaona anaonewa tu, bila sababu. Nikaingilia kati kumtetea. Siyo kwa sababu yoyote ile, bali kwa kutamani kuona anatendewa haki.

Nilipoingia nikaambiwa ni maelekezo kutoka juu. Juu kuna Rais, Makamu wake na Waziri Mkuu. Nikapiga moyo konde nikamuendea hewani bwana mkubwa; akaniuliza swali moja tu “umehongwa shilingi ngapi?” Nikamuambia Mhe. Rais, utakuwa umeshauriwa vibaya, kama unaniamini mimi mshauri wako unisikilize nikupe taarifa yangu kisha utume watu wako wafuatilie, mimi hata huyu mtu simjui na wala sijawahi kuwasiliana naye hata mara moja! Akakata simu.

Baada ya muda kidogo ukweli ulifika mezani kwa bwana mkubwa, akanipigia akasema ulisema kweli. Umenifurahisha. Yule bwana alikuja akaachiwa. Akaja akajua ushiriki wangu kwenye jambo lake. Akanishukuru sana. Akataka kunipa chochote nilikataa. Tukawa marafiki.

Siku moja baadaye kabisa, hapo nishatoka kwenye serikali, napambana na miradi yangu, hali yangu ngumu, sina kitu, naingiza kontena za kiwanda changu akajua akaniita, basi akalipia nusu ya gharama zote za kontena zangu!

Hakujua ni kiasi gani nilikuwa hoi! Usiku nilitafakari sana jambo lile hadi machozi yalinitoka. Niliswali rakaa mbili kumshukuru MUNGU…#HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 4.

Kila kitu kitapita. Hata uwe unapitia kipindi kigumu namna gani, jua tu kipindi hicho kitapita. Kama upo kwenye raha namna gani, jua tu zitaisha. Hakuna kinachodumu milele chini ya jua. Kila kitu kitapita. Kuna miamba, majabbar anidi, ilipita! Iko wapi leo hii?

Basi, maneno haya yatoshe kutunyenyekeza, kutushusha na kutukumbusha kuwa watu wema zaidi ya wabaya.
Mimi Nina kanuni moja kwenye maisha yangu; kama ni kuonewa, basi acha nionewe mimi, lakini siyo mimi nionee mtu mwingine. Kama ni kudhulumiwa, acha nidhulumiwe mimi lakini siyo mimi kumdhulumu mtu. Huwa naamini wema ni akiba isiyooza lakini ubaya ni deni lisilofutika! Ubaya utakurudia tu.

Watu kama mimi huchukuliwa kama watu imara na wagumu kweli kweli, na wenye mamlaka makubwa sana, kwamba tunaweza kufanya lolote na kumfanya mtu chochote, lakini amini nakuambia binafsi nimeonewa na kudhulumiwa mara nyingi na wengine kuliko unavyoweza kudhania.

Kuna kijana wangu mmoja, na wapo wengi, sema ntatolea mfano huyu mmoja, aliwahi kunipiga parefu sana. Kwa mara ya kwanza nililia machozi ya uchungu sana mbele ya wanangu. Na mbele ya mama yangu, nikiwa mtu mzima!

Tumelima, tumejaza stock kwenye magodown yetu na ya kukodi. Tumetazama soko tukajua bei zitapanda, tukanunua na mzigo mwingine kwa wakulima wengine tukatunza. Kwamba tutauza baadaye bei zikipanda. Biashara ya mazao siyo rocket science, ukiwa na mtaji tu, ukatunza stock siku bei zikipanda unauza kwa faida unatengeneza pesa nzuri.

Kumbe dogo ananiambia amepata mzigo wa kutosha, natuma hela, kumbe ananunua kidogo, anamhonga store keeper, wanaweka rekodi sawa, dogo anakula hela. Uko zako mjini, busy na majukumu ya serikali, unajenga nchi! Simu inaita tena baada ya siku tatu, unaambiwa kuna mkulima mwingine mkubwa anauza mzigo wake, unapiga kadhaa, unakopa hela unasukuma kwenye stock!

Kumbe unanunua Moet, VSOP etc. Dogo anafunga bar, anaagiza slay queens kutoka Dar, anawapa bata la hatari!

Dogo umempa gari, Nissan Patrol, matrekta, combine harvesters na mashine zote, na mamlaka ya kusimamia kampuni yako, basi anatukana na kuchimba mkwara kila mtu kwa jina lako! Inaendelea…#HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 5.

Anaogopwa kuliko hata unavyoogopwa wewe mwenyewe! Hakuna anayekupa taarifa na wewe uko busy na ujenzi wa Taifa!
Kumbe Taifa lako binafsi la Kigwangalla Corporation linaangamia! 😭💔

Wakati wa kulima, dogo anakupa hesabu ya kulimia ekari 400, kumbe amelima ekari 300. Ekari zako 100 amewakodishia watu wengine wanalima, halafu wewe anakuletea hesabu za mahitaji ya ekari zote 400 wakati wote - kuanzia mbegu, mashine za kulimia, kuvuruga, vibarua wa kupanda, madawa, mbolea, palizi, kuvunia, usimamizi.

Mwishoni kule anakupa hadi na idadi ya gunia alizovuna na kutunza godown. Hesabu yake na hesabu ya store keeper ziko sawa.

Bei zinaanza kupanda, wewe unachekelea unajua huu ndiyo ule mwaka wangu wa kupiga hela ndefu, ntanunua na G Wagon yangu (my dream car), ntajenga na ile lodge yangu, na zile apartments zangu! 😀. Ntalipa na madeni yangu yote ya mikopo, nitaongeza uwekezaji wangu kwenye hisa na T-bonds! Kumbe maskini unajenga zako magorofa hewani! 😭😪💔 ushapigwa!

Mtu mmoja akaniambia amekutana na ‘mdogo wangu’, yule anaitwa Kigwangalla, anayesimamia miradi yangu ya mashamba alikuwa club na warembo (ni maarufu sitowataja majina!) akampa offer! Nikashtuka.

Nikamcheki dogo, nikamuambia nimepata salamu zake. Nikaona nimtume kijana mmoja wa ofisini kwangu Dar, na mke wangu, wakakague stock. Akasikia kuwa wanakuja. Akaanza mbinu na wenzake, eti wachome godown ili kupoteza ushahidi! 💔😭😩

Anayetoa hizo taarifa ni mdada mmoja ambaye alikuwa rafiki wa mwamba, kumbe alimsikia akiongea kuhusu madumu ya petrol kumwagwa usiku kwa akili sana ili kupoteza ushahidi. Kwamba, kwanza wangetoa mpunga zaidi kutoka godown, wabakishe kidogo, halafu kwa kuwa huwa tunamwaga pumba za mpunga kwenye sakafu, wakinyunyiza petrol kidogo tu moto utakuwa mkali sana kiasi kwamba hautoweza kuzimika, kila kitu kitateketea!

Huyo dada akasikia huruma sababu alijua wizi waliokwisha kunifanyia halafu wakichoma tena hicho kidogo, wachome na godown langu, na ndani humo Kuna mashine zangu zote - trekta kubwa3, stock ya mbolea, madawa… #HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 6.

…madawa ya mimea na combine harvester, itakuwa mbaya sana! Akamuambia ndugu yangu mmoja.

Ndugu akanitafuta toka asubuhi, wapi! Siku hiyo nilikuwa Ikulu kwenye cabinet, mule hamuingii na simu. Tumetoka, naingia kwenye gari, la kwanza kuwasha simu, nakutana na meseji Lukuki! Baada ya mimi kukosekana jamaa zangu waliamua kuripoti polisi, ulinzi ukawekwa!

Nilisikia kama nimechomwa kitu moyoni. Machozi yalinitoka bila kupigwa! Bila kutoa sauti. Sitokuja kusahau.

Nilifika nyumbani nikamkuta mama yangu sebuleni, niliangua kilio kama niliyefiwa na mtoto ama mzazi. Katika ukubwa wangu, nimewahi kufikwa na mambo mengi, lakini sijawahi kulia hata siku moja. Siku hii nililia bila kujali wanangu wanatazama wala nini. Mama yangu alinikumbatia kwa nguvu na kunituliza.

Nilijiuliza sana nimemkosea nini huyu dogo? Na wenzake? Mpaka leo sijawahi kupata majibu ya maswali yangu. Vijana wa kitanzania mna la kujifunza hapa. Huyu dogo na wenzake niliwapa gari ya kutembelea, mapikipiki, mashine ambazo wakimaliza kufanya kazi kwangu wanakodisha kwa wengine wanapata hela ya kula na matanuzi (ambayo mimi siichukui), kila kijana mmoja nalipia gharama ya kuanzia kumlimia na kumtunzia shamba lake; ekari 30 (huyo mkubwa wao), ekari 15 wale wasaidizi wake wawili. Kwenye ekari 15 unapata kati ya 30 - 40m kwa mwaka. Matukio ya hivi ni mengi kwenye story za wajasiriamali wengi hapa nchini.

Vijana wanadanganyika sana na maisha ya superstars, wanataka wayaishi bila jasho. Wengine wameishia kujidhalilisha na wengine wamefikia hata kushikishwa ukuta! Kama huna kipaji mdogo wangu, usitamani maisha ya wenye navyo. Fanya kazi kwa bidii, jipe muda wa kujitafuta, na wa kutafuta nafasi yako maishani. Ukifika utakula maisha yako ya halali kabisa.

Usikubali kuingia kwenye kundi la vijana wanaotafuta ajira lakini hawataki kufanya kazi. Wala usilikurubie kundi la vijana wanaotafuta ajira ili wakapige deal! Kila kijana anataka awekwe kitengo chenye ‘michongo’! Jamani nchi haijengwi namna hiyo. Hela haitafutwi namna hiyo. Nakuhakikishia, hela ya hivyo ukiipata haitokaa. Itakimbia tu.

Kama unahisi ‘nimefika mbali’ na unatamani…#HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIBA UBORA WAKE! Part 7.

Kama unahisi ‘nimefika mbali’ na unatamani kuwa kama mimi, basi nikuambie ukweli kuwa mimi najiona ‘Muomba Allah’ tu, sijafika popote na kiukweli hata hapa padogo nilipofikia, siyo kwa madili, dhulma, ubadhirifu na wala siyo kazi rahisi. Uwe tayari kutokwa machozi, jasho na damu!

Halafu; kwenye maisha yetu pesa, vitu, vyeo havileti furaha ya kweli, na wala havina thamani ya kweli. Vitu vyote vyenye thamani ya kweli kwenye maisha huwa havishikiki na havinunuliki. Usipoteze utu na imani yako kutafuta vitu vinavyoshikika.

Swali la ‘what did I do to deserve that?’ Halijawahi kunitoka. Usiulize huyu dogo mengine ya kijamii niliyowahi kumfanyia ni mangapi? Sema sipendagi kusema wema niliofanyia watu, Ila jua tu nilim-treat kwa heshima kupindukia, harusi yake niliwekeza na kuisimamia zaidi ya nilivyofanya kwa mdogo wangu niliyemuachia ziwa la mama!

Imagine rafiki zangu walivyojitoa, hata sijawahi kuwaambia dogo alivyoninyoosha! Dan La Kairo alitoa Range Rover yake mpya Autobiography kumpa dogo akajiendesha na mkewe! Miaka mitatu tu baadaye anataka kuchoma mali yangu! Dah! #HK #Fighter #NjeYaBox Iendelee ama tuishie hapa kwa sasa?
 
Yuko sahihi, Watanzania wanao tumia akili zao binafisi kuishi wanahesabika katika watu 1000 unakuta ni 1 tu. Wengi ni ujanja ujanja wizi sana.

Kule Arusha ndio maana kampuni za Wahindi zina hadi walinzi wa Kihindi, Ogopa unakuta Getini kakaa Muhindi.
 
Kwa maana hiyo tunakubaliana na Kigwangwala kwamba tatizo lipo. Niliwahi kuenda na Aikaeli katika hooteli yake saa 2 usiku jumamosi miaka hiyo. Wataliii 130 wameingi.Tanesco imekata wanatumia mishumaa vyumba vyote ebu fikiria hartari yake amna mafuta ya jenerator. Kwa nini? Mkuu wa stores hayupo. Jikoni mishumaa kuwalisha watalii 130 wanaolipa dola mia kabla ya kukwea kilimanjaro. Mkuu mapokezi hayupo. GM hakuwepo. Yaani mamemneja wa5 wote ambao ukiacha mshahara, posho , simu , makazi na magari wote waliondoka Arusha kutanua. Wakamuacha binti pekee mapokezi.Ilibidi Aikaeli awe chef mie nikawa mapokezi mpaka saa 7 usiku huku dereva akifuata mafuta jenereta ikawashwa. Aikaeli akawa anawaza afanyeje sheria inanitaka niajiri watanzania lakini nikiwapa fursa ndio kama hivi. Sasa nini kifanyike BLACK MOVEMENT
 
Ethics ninayozungumzia hapa ni maadili. Yanaanzia nyumbani. Sio haya ya kufundishwa. Tumetengeneza jamii ambayo inaijua rushwa na kuiona ni kawaida. Pia tuna jamii ambayo usipoiba unaonekana mtu wa ajabu. Hiyo ndiyo ethics ambayo tunaizungumzia. Hatuna kabisa tuna F tena kubwa mno.
very true mkuu, tumefeli sana, angalia tu humu jukwaani mtu akileta post ya kuripoti ubadhirifu ama rushwa sehemu fulani utasikia anaambiwa ana wivu, chuki, n.k
 
Huyo dogo aliemliza kigwangala aka kigwafix anaitwa

TOMMY
Ukipita usangu mbarali wanamjua sana
Alikuwa anatembelea nissan patrol
Anapiga bata za hatari
Tumewahi zinguana pale DS makambako
Afu anajifanya mdg ake kigwangala

Alikuwa anaonea wanyonge sana
Mara apore mademu zao
Ila sisi tulimkokesha

Sijui kwa sasa kapotea wapi

Oyaa, Tommy km unasoma huu Uzi
Wambie wadau kilichokukuta pale DS hotel mpk ukakimbia ukaacha gari

Dadeeki
 
asante kuileta bandiko hili ambao hawakuwa wameiona wasome
 
Ethics ninayozungumzia hapa ni maadili. Yanaanzia nyumbani. Sio haya ya kufundishwa. Tumetengeneza jamii ambayo inaijua rushwa na kuiona ni kawaida. Pia tuna jamii ambayo usipoiba unaonekana mtu wa ajabu. Hiyo ndiyo ethics ambayo tunaizungumzia. Hatuna kabisa tuna F tena kubwa mno.
ammoshi unachosema ni sahihi -lakini mie nimeujumlisha na kuuita a people problem-wazee wetu walituambia ukiwa na vitu 3 unafanikiwa ambaovyo ni ardhi, siasa safi na rasilmali watu. Sasa Tanzania tuna madini usiseme. Tuna ardhi imelala doro afu tupo milioni 61 lakini bado tunashindwa kuwa na maisha wawastani kwa nini? Hatuoni anachosema hamisi Kigwangwala kwamba tunatatizo la watu. Tuna watu ambao kwa namna moja au nyengine waliaminishwa kwamba maisha mazuri yatatokana na kutofanya kazi-yaani fukuza mkoloni tu mengine swafi.

DeePeeWeldi imetuonyesha namna gani ubovu wa watu upo hadi ngazi ya viongozi kitaifa kwa kuwa watu ni wale wale.

Lakini zaidi tukiemdelea kuendekeza uzawa /uzalendo tutaendelea kulizwa maana kote tunakolia kuliwa wanaotunyonya ni wazawa, maana mgeni ili apate lazima afunguliwe njia na wazawa
 
Huyo dogo aliemliza kigwangala aka kigwafix anaitwa

TOMMY
Ukipita usangu mbarali wanamjua sana
Alikuwa anatembelea nissan patrol
Anapiga bata za hatari
Tumewahi zinguana pale DS makambako
Afu anajifanya mdg ake kigwangala

Alikuwa anaonea wanyonge sana
Mara apore mademu zao
Ila sisi tulimkokesha

Sijui kwa sasa kapotea wapi

Oyaa, Tommy km unasoma huu Uzi
Wambie wadau kilichokukuta pale DS hotel mpk ukakimbia ukaacha gari

Dadeeki
monopoly inc kumbe una monopoly ya violence mtu mbadi hahaha
 
Light saber yaani tunaimba kuhusu kazi, wengi vijana wanatafuta ajira lakini hawaitaki kazi....baadae ukijaribu kuwekeza unalizwa unaona kama unaonewa kumbe ulianza wewe
Yaani SASA hivi uadilifu/MTU mwenye adili Ndani yake ni WA kutafuta Kwa tochi , Inatia hofu Mkuu ni Taifa la Namna gani tunalitengeneza . Kuiamini serikali itukuzie wanetu ni kosa kubwa Zaidi ambalo linatugharimu na litatigharimu milele.

Turudi kwenye misingi yetu.

Wengine waweza kusema mwana Yule siyo mwadilifu, lakini hatuhusu atajua yeye na wazazi wake , huko mbeleni aweza Kuwa kiongozi , hatuwazi Hilo , hatuwazi Kuwa anakuwa mwenzetu katika jamii. Anaweza Kuwa ni MTU mwenye ushawishi akatumia ushawishi huo kupanda mbegu zake ...

Inatia huruma hofu na mashaka juu ya jamii tunayoitengeneza.

Siyo kusema ya kwamba Mimi ni mwadilifu Sana la hasha , lakini kuna mambo ninayafanya nafsi inanisuta lakini sina budi, Niko Rome I act as romans
 
Back
Top Bottom